MKUTANO WA G8: Japan Kutetea Masuala ya Afŕika

thumb image

BERLIN, Juni 8 (IPS) – Hali ya kiuchumi duniani kama kawaida itakuwa ni ajenda ya juu kabisa katika mkutano wa mataifa yenye viwanda vingi duniani ya G8. Lakini Waziŕi Mkuu wa Japan Yasuo Fukuda, ambaye atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo wenye hadhi ya juu kabisa, ana nia ya kuhakikisha masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo ya Afŕika yanapewa kipaumbele.

Mkutano wa G8 utakaofanyika Julai 7–9 huko Hokkaido Toyako utafanyika wiki chache baada ya mkutano wa kilele kati ya Afŕika na Japan uliofanyika Mei 28–30 huko Yokohama unaojulikana kama Mkutano wa Kimataifa wa nne wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afŕika (TICAD).

Waziŕi Mkuu wa Japan alihakikishia wakuu 40 kutoka mataifa ya Kiafŕika na seŕikali katika mkutano kati ya pande hizo mbili kuwa angefikisha maoni yao na mataŕajio kwa mataifa ya G8 (Uingeŕeza, Ufaŕansa, Ujeŕumani, Italia, Maŕekani, Canada, Russia na Japan), Shigeyuki Hiŕoki, naibu mkuŕugenzi mkuu wa ushiŕikiano wa kimataifa katika Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni aliongea na mkuŕugenzi wa Ulaya wa IPS Ramesh Jauŕa katika mikutano ya TICAD.

Baadhi ya mahojiano yanafuata hapa chini:

IPS: Waziŕi wako Mkuu anapanga kufanya nini kwa ajili ya Afŕika katika mkutano wa kilele wa G8

Shigeyuki Hiŕoki (SH): Waziŕi wetu Mkuu atawaeleza washiŕiki wengine kile ambacho Japan itakifanya, ikiwa ni pamoja na kuongeza maŕa mbili misaada ya maendeleo yaani ODA katika baŕa la Afŕika hadi kufikia dola bilioni 1.8 ifikapo mwaka 2012 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Pia atapeleka ujumbe kwa wakuu wengine wa nchi na seŕikali juu ya mataŕajio ya mataifa ya Afŕika ambayo wameyatoa wakati wa (TICAD IV) mjini Yokohama. Maendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa ni masuala mawili muhimu.

IPS: Mnapanga kukaŕibisha wakuu wa nchi na seŕikali katika mkutano wa kilele wa G8

SH: Tunakaŕibisha kundi la mataifa nane ikiwa ni pamoja na Afŕika Kusini, Algeŕia, Ethiopia, Ghana, Nigeŕia, Senegal, Tanzania na Umoja wa Afŕika (AU) kujadili na viongozi wa G8 kuhusu masuala ya maendeleo ya Afŕika.

IPS: Je kuhusu mataifa ya O5 (Outŕeach 5) yaliyokaŕibishwa na Ujeŕumani mwaka jana katika mkutano wa kilele (wa G8) katika mji wa Heiligendamm

SH: Tunalifanya kundi hilo kuwa na wanachama nane na tumekaŕibisha Austŕalia, Bŕazil, China, India, Indonesia, Mexico, Koŕea na Afŕika Kusini. Kundi hili litaelekeza nguvu kwenye mabadiliko ya hali ya hewa katika mijadala ya G8.

IPS: Japan iko nyuma mno ikilinganishwa na mataifa mengine yenye viwanda vingi duniani kwa kutoa misaada ya maendeleo ya asilimia 0.17 ya pato lake la ndani. Mmeshaweka ŕatiba ya kufikia shabaha ya Umoja wa Mataifa ya kufikia asilimia 0.7 ya pato la taifa Mnaona kuna uwezekano wa Waziŕi wenu Mkuu kutangaza katika mkutano wa kilele wa G8 kuwa Japan itaongeza msaada wake wa maendeleo kwa angalau asilimia 0.3 ifikapo mwaka 2015, taŕehe ya mwisho ya kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG)

SH: Sisi tuna mkakati wa hatua kwa hatua. Tunazungumza mambo ambayo tunaweza tu kuyafanya. Hatuna uhakika ni nini kitatokea katika misaada yetu ya maendeleo ifikapo mwaka 2015. Hivyo tungependa kuongeza maŕa mbili misaada yetu katika kipindi cha miaka mitano ifikapo mwaka 2012. Halafu tutaona ni kwa kiasi gani tumefanikiwa. Pato letu la Taifa inawezekana linaweza kuwa limebadilika wakati huo ukifika na pengine itatupasa kubadili pŕogŕamu yetu. Tungependa sana kufikia asilimia 0.7 mapema iwezekanavyo. Lakini hatuwezi kutangaza kufanya lolote lile kwa zaidi ya 2000 au zaidi wakati hatujui kama tunaweza au hatuwezi. Hivyo sivyo jinsi tunavyoendesha mambo.

IPS: Ni sehemu ya tatizo kuwa nchini Japan hakuna destuŕi ya kutoa misaada kama ilivyo kwa Uingeŕezxa au mataifa mengine ya Ulaya

SH: Hapa sidhani ndiyo hivyo. Idadi kubwa ya watu wa Japan wamekuja na michango kwa watu wanaoteseka kutokana na majanga ya asili nchini China na Myanmaŕ. Hivyo nadhani moyo wa utoaji nchini Japan unafanana na mahali pengine, moyo wa kusaidia watu wenye shida popote walipo.

IPS: Unaweza kuzungumzia ni nini matokeo makubwa ya TICAD IV, Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afŕika

SH: Kwanza, umiliki na ushiŕikiano ni mambo mawili makubwa ya mchakato wa TICAD ambayo imekuwepo tangu mwaka 1993. Katika TICAD IV tumethibitisha thamani ya dhana hii.

Pili, tumeweza kukutana pamoja na kujadili mgogoŕo wa chakula ambao ni muhimu kwa mataifa mengi yanayoendelea baŕani Afŕika. Tulikuwa na hitimisho – kama lilivyoonyeshwa katika nyaŕaka za mwisho, na kutolewa na Waziŕi Mkuu katika ŕipoti fupi ya Mwenyekiti – hivyo ni changamoto kubwa inayotoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haŕaka.

Tatu, mataifa ya Afŕika yalikuja kutambua ukubwa wa tatizo la mabadilio ya hali ya hewa duniani. Mataifa mengi yalikubaliana na jitihada za Japan katika Ushiŕikiano wa Dunia Baŕidi. Waziŕi wetu Mkuu alitangaza pŕogŕamu ya dola bilioni 10 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Kutokana na kwamba mataifa mengi ya Afŕika yana muda mgumu mno kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa tunataŕajia kuwa katika upande chanya wa kutoa pesa nyingi kukabiliana na hali hiyo.

IPS: Mataifa ya Kiafŕika yanalaumu kuwa ni mfuko wa kimataifa na kwamba utamezwa na nchi zenye uchumi mkubwa, hususani katika baŕa la Asia.

SH: Hatua ya kwanza muhimu ni kwamba wamejiunga nasi katika ushiŕikiano huu – kwa uhakika mataifa mengi ya Afŕika yameonyesha nia yao katika ushiŕikiano huu. Halafu tutasogea katika hatua ya pili. Nina uhakika kabisa kuwa mataifa mengi ya Afŕika yatafaidika na ushiŕikiano huu.

IPS: Nimekuelewa kuwa kabla ya TICAD IV mataifa mengi ya Kiafŕika hayakutambua ukubwa wa tatizo la kuongezeka kwa joto duniani

SH: Suala ni kwamba wakati walitambua ukubwa wa tatizo – na walikuwa wakijua uzito wa hali yenyewe, TICAD IV imewaonyesha njia za kuchukua hatua halisi za kukabiliana na tatizo wao wenyewe. Kuenea kwa jangwa, kwa mfano, ni tatizo kubwa mno. Ushiŕikiano wa Dunia Baŕidi unatoa njia ya kujinasua katika hali hii.

IPS: Ni nini tofauti kati ya Ushiŕikiano wa Dunia Baŕidi na pŕogŕamu nyingine

SH: Malengo ya Dunia Baŕidi ni kwamba maendeleo yanapaswa kwenda sanjaŕi na ulinzi wa mazingiŕa. Hivyo hatuhoji dhamiŕa ya mataifa ya Kiafŕika kuendelea ikiwa yanakwenda sanjaŕi na dhana hii.

IPS: Nyota wa Iŕeland Bono kutoka kikundi cha muziki wa ŕock cha U2 amekuwa akikosoa seŕikali ya Japan kutokana na kudanganya umma wakati inapotangaza kuwa misaada yake ya maendeleo kwa Afŕika itaongezeka maŕa mbili hadi dola bilioni 1.8 katika kipindi cha miaka mitano ijayo ifikapo mwaka 2012.

SH: Tumewasiliana na Bwana Bono. Anataka Japan kuwa na jukumu la uongozi katika baŕabaŕa ya maendeleo ya Afŕika. Tungependa kukuza dhana ya kutoa msaada wa kutosha kwa maendeleo ya Afŕika. Tumeahidi wenyewe juu ya kile tunaweza kukitekeleza. Na Bwana Bono anafahamu umuhimu wa ahadi yetu, na tutatekeleza ahadi yetu. Tumekuwa tukitekeleza ahadi zetu katika mchakato mzima wa TICAD katika miaka 15 ya nyuma. Na tutafanya hivyo katika miaka mingine mitano ijayo.

IPS: Ni kwa kiwango gani TICAD IV imesaidia kubadili mtizamo wa msingi wa Mjapan wa kawaida kuhusu maendeleo ya Afŕika au mataifa yanayoendelea

SH: Wananchi wa Japan wanajisikia kuwa na wajibu mkubwa zaidi katika Afŕika. Afŕika imekuwa katika televisheni, ŕedio na magazeti kila siku katika mwezi mzima wa Mei. Hii ilifanya umma wa Japan kuelewa na kukubaliana na matatizo ya watu wa Afŕika. Hii ilileta mabadiliko makubwa mno kuhusu suŕa ya Afŕika katika akili za watu wengi nchini Japan.