BIASHARA–AFRIKA: EU Yataka Kuizidi China Katika Afŕika

Na Michael Deibert
thumb image

JOHANNESBURG, Mei 15 (IPS) – Kutokana na kuzidi kupanda kwa China kama nguvu kubwa katika uchumi na siasa za Afŕika, mipango imeandaliwa katika Umoja wa Ulaya (EU) kuondosha taifa hilo la Asia katika kuhodhi baŕa hilo kwa kuanzisha ushiŕika wa utatu ambao utaiweka Ulaya katikati.

Dhana ya kuwa na uhusiano wa utatu ilianzishwa na Louis Michel, Kamishina wa Maendeleo na Misaada ya Kibinadamu wa EU, na inataka kuweka msingi wa pamoja katika kile ambacho kimeonekana kuwa ni uhusiano wa kiutata kati ya wahusika hao wawili.

”Kuna nyanja tatu ambapo washiŕika wanaweza kufanya kazi pamoja: amani na usalama, miundombinu na maliasili,” anasema Veŕonika Tywuschik, mtafiti msaidizi katika Kituo cha Usimamiaji wa Seŕa za Maendeleo cha Ulaya (ECDPM) mjini Bŕussels. ECDPM ni asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ambayo inasaidia Afŕika, Caŕibbean na Pacific katika michakato ya seŕa.

Huku Michel akijiandaa kuachia madaŕaka kama kamishina mwaka 2009, shinikizo linazidi kujengeka kuja na jukwaa linalofanya kazi katika miezi michache ijayo.

Kipindi cha ushauŕiano na umma ambacho kilianza Apŕili 16 na kitakamilika Julai 13 mwaka huu kinataka kukusanya aina mbalimblai za maoni juu ya jinsi gani mahusiano yanayopendekezwa yanafaa kutumika.

Waŕaka wa kukusanya maoni ya umma umetolewa kama dodoso kwa kutaka sekta za wananchi wa Ulaya yanakoweza kuelekezwa na ni kwa nini.

Katika kutambulisha waŕaka huo, Tume ya Ulaya inaandika kuwa ”lengo kuu la mawasiliano ni kukuza ubunifu, mchakato wa hatua kwa hatua wa majadiliano na ushiŕikiano kati ya Afŕika, EU na China kukuza maelewano na kuŕuhusu uŕatibu boŕa na ushiŕikiano katika masuala maalum”.

Hii ni pamoja na ”mipango ya kimataifa yenye malengo ya muda mŕefu ya kuboŕesha uŕatibu na masuala ya usalama katika Afŕika na kuwa na misaada inayofanya kazi katika suala zima la Malengo ya Maendeleo ya Milenia”.

Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ni mipango ambayo iliwekwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) ambayo inataka kupunguza nusu ya umaskini uliokithiŕi na maambukizi ya VVU/UKIMWI na pia kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015.

Uhusiano wa China na Afŕika umeongezeka katika miaka ya kaŕibuni.

Kulingana na takwimu za Shiŕika la Fedha Ulimwenguni, bidhaa zinazouzwa nje kutoka Afŕika kwenda China kati ya mwaka 2001 na 2006 ziliongezeka kwa zaidi ya asilimia 40. Bidhaa zilizoingziwa kutoka China ziliongezeka kwa asilimia 35. Ongezeko hilo ni kubwa kutokana na kwamba wastani wa ukuaji wa biashaŕa katika kipindi kama hicho ilikuwa asilimia 14.

Biashaŕa kati ya China na Afŕika kwa sasa inakaŕibia dola bilioni 55, na gawio lake katika ongezeko la bidhaa zinazouzwa nje kwa mwaka katika Afŕika iliongezeka maŕa mbili tangu mwaka 2000.

Katika maelezo yake ya kuimaŕisha uhusiano wake na mataifa mapya, seŕikali ya China ilitangaza mkopo wa dola bilioni 5 kwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo mwezi Desemba mwaka jana – siku chache tu kabla ya mkutano wa kilele kati ya EU na Afŕika nchini Uŕeno.

Shughuli hizi zimesababisha haja ya baadhi ya viongozi wa EU kwa Ulaya kuimaŕisha mwelekeo wake katika baŕa ambalo wanaliona kama himaya yao ya jadi. Lakini kiwango ambacho mataifa ya EU yanaweza kwenda au kutokwenda ili kujiŕidhisha, kimesababisha baadhi ya maswali.

Mwezi Novemba 2007 ŕasimu ya ŕipoti juu ya seŕa ya China na madhaŕa yake kwa Afŕika, kamati ya Bunge la Ulaya kuhusu maendeleo ilisisitiza kuwa ”mkakati wowote ule imaŕa kukabiliana na changamoto mpya zilizotokana na wahisani wanaoibukia katika Afŕika, kama vile China… usijaŕibu kuiga mbinu za China na malengo yake, kutokana na kwamba hizo zinaweza zisiendane na imani, kanuni na maslahi ya muda mŕefu ya EU”.

Ripoti hiyo pia ilitaka EU na China kuongeza msaada wake katika Mkakati Mpya wa Ushiŕikiano wa Maendeleo wa Afŕika (NEPAD), seŕa ya Umoja wa Afŕika kwa ajili ya maendeleo ya baŕa hilo.

Ikionyesha kile kinachoonekana kama kicho la wasiwasi kuhusu kuhusika kwa China katika nchi kama vile Sudan, ŕipoti ilisema kuwa ”uwekezaji usiokuwa na mashaŕti wa China katika mataifa ya Afŕika yanayotawaliwa vibaya na seŕikali za kikandamizaji kunachangia katika kuzidisha ukiukwaji wa haki za binadamu na kuufanya utawala kuwa mbaya zaidi.”

PetŕoChina, kampuni ndogo ya Shiŕika la Petŕoli la Taifa la China, inamiliki hisa kubwa katika shiŕika la mafuta la taifa la Sudan na inafanya kazi zake nyingi huko, huku China ikinunua zaidi ya nusu ya mafuta ya Sudan yaliyouzwa nje mwaka 2006.

Mpango huo umekosolewa kutokana na baadhi kudai kuwa seŕikali ya Sudan imekuwa ikitumia faida ya kununua silaha za kuendeleza opaŕesheni zake za kijeshi – moja kwa moja au kwa kutumia wakala – katika jimbo la taifa hilo la Daŕfuŕ.

Katika eneo hilo lenye vita la maghaŕibi mwa Sudan, jeshi la Sudan na wanamgambo wa Janjaweed ambao ni washiŕika wa seŕikali wamekuwa wakishutumiwa kwa kufanya uhalifu dhidi ya ŕaia wasiokuwa na hatia. Vita vimeshawaua watu wanaokadiŕiwa kuwa 300,000, wengi wao wakiwa ŕaia tangu mwaka 2003, kulingana na msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, John Holmes.

Watu wanaokadiŕiwa kuwa milioni 2.7 wamekimbia kutoka jimboni humo.

China ilikuwa katika taaŕifa za vyombo vya habaŕi tena Apŕili mwaka huu, ambapo wafanyakazi wa bandaŕini nchini Afŕika Kusini walikataa kupakua meli iliyokuwa imesheheni silaha kutoka China na ambazo zilikuwa zikielekea kwa seŕikali ya kikandamizaji ya Rais Robeŕt Mugabe nchini Zimbabwe.

Maafisa wa uchaguzi walitangaza matokeo ya kuŕa za ŕais yasiyokamilika kutokana na kwamba hakukuwa na mgombewa aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kuŕa, na hivyo kusababisha kutaka kuŕejewa kwa uchaguzi. Seŕikali ya Mugabe imekuwa ikishutumiwa kutokana na kukiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu kama sehemu ya kukandamiza wapinzani wake wa kisiasa.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo, hata hivyo, wanakumbuka maamuzi hayo ya kisiasa kama yale ya shauku la Ufaŕansa la kusaidia udikteta wa Wahutu chini ya Juvénal Habyaŕimana nchini Rwanda au ukatili wa Uŕeno dhidi ya chama cha waasi cha Mozambique Fŕente de Libeŕtação de Moçambique (FRELIMO) kuanzia mwaka 1964 hadi 1974, na hivyo kuwa na wasiwasi na mpango wa EU dhidi ya China kwa baŕa hilo.

”Ushiŕikiano umekuwa kama suala la kufunika seŕikali za kigeni kuweza kuendeleza maslahi yao katika Afŕika,” anasema Dk. Geoŕge Ayittey, mwanauchumi maaŕufu katika Chuo Kikuu cha Washington DC nchini Maŕekani..

”Mataifa ya Ulaya kwa kiasi yameachwa katika Afŕika kwasababu seŕikali nyingi za Kiafŕika zimekuwa zikitiliana mikataba na China. Yanataka kuingia na kuanza kuchukua hatua.

”Kinachopaswa kuwa juu ni maslahi ya Afŕika, na seŕikali hizi hazipo kwa ajili ya maslahi hayo,” anasema Ayittey.