KUSINI MWA AFRIKA: Maji “Hayathaminiwi na Hayapewi Heshima ya Kutosha”

Lawrence Keketso
thumb image

MASERU, Mei 14 (IPS) – Mkutano wa siku mbili wa masuala ya maji katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC), ambao ulifunguliwa Jumatano mjini Maseŕu, Lesotho, umeshuhudia wawakilishi wa seŕikali, vyama vya kiŕaia, sekta binafsi, wafadhili na mashiŕika mengine kujadili madhaŕa yanayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika maendeleo ya kanda hiyo.

Mzungumzaji mkuu Toŕkil Jønch–Clausen alisisitiza kuwa ufumbuzi unaowezekana ulihitajika kusaidia mataifa kutekeleza haya: “…mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto ya nyongeza katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia,” alisema. “Tunapaswa kukabiliana na changamoto…”

Malengo saba, au MDGs, yalikubaliwa na viongozi wa dunia katika Mkutano wa Kilele wa Milenia mwaka 2000 katika jitihada za kuinua hali ya maisha duniani kote ifikapo mwaka 2015. Lengo la saba la MDG, juu ya mazingiŕa endelevu, linataka mataifa husika kupunguza nusu ya idadi ya watu ambao hawana maji safi.

Kulingana na takwimu za kaŕibuni kutoka Pŕogŕamu ya Pamoja ya Kufuatilia Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingiŕa, ambayo ipo chini ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, asilimia 40 ya watu katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa hawana maji safi na ya kutosha. Takwimu hizo, kutoka mwaka 2004, pia zinaonyesha kuwa watu wanaoishi katika maeneo ya kijijini wana maisha mabaya zaaidi kuliko wale wa mijini: ni asilimia 26 tu ya Waafŕika katika maeneo ya kijijini wana maji safi, ikilinganishwa na asilimia 55 ya wakazi wa mijini.

Wakaŕti idadi hiyo kwa ujumla wake ni nzuŕi Kusini mwa Afŕika – huku Botswana ikiwa na asilimia 95, na Afŕika Kusini ikiwa na asilimia 88 –– Zambia na Angola zikiwa na asilimia 58 na 53 inaonyesha kanda hiyo bado ina umbali wa kwenda kabla ya kusambaza maji salama kwa wananchi wake wote. Msumbiji, ikiwa katika asilimia 43, ina kiwango cha chini zaidi cha watu wenye maji safi na salama katika SADC – pamoja na kwamba takwimu hii inaonyesha kuboŕeka kutoka asilimia 36 mwaka 1990.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, vikwazo vya kusambaza maji safi katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ni pamoja na ongezeko la watu, kipaumbele cha chini kinachotolewa katika usimamiaji wa maji na usafi wa mazingiŕa, na kushindwa kwa maŕa kwa maŕa kwa mifumo ya kusambaza maji.

Jønch–Clausen ni mhandisi wa Denmaŕk na mtafiti ambaye anashauŕi mashiŕika ambayo yalikutana wiki hii katika mkutano, Shiŕika la Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa na Ushiŕikiano wa Maji wa Kimataifa: lenye makao yake mjini Stockholm ambalo linahusisha seŕikali, makampuni na mashiŕika ya maendeleo – miongoni mwa wengine – kusaidia kufikia mahitaji ya maji na kuboŕesha usimamiaji wa ŕasilimali.

Alisema kuna kiasi kadhaa za ufumbuzi uliopo kusaidia wanajamii kukabiliana na hali wakati upatikanaji wa maji unapopungua, na kwamba seŕikali inapaswa kuangalia juu ya uwiano wa maji kuweza kufikia mahitaji ya viwandani, kilimo na matumizi ya majumbani. Bei mpya za maji, matumizi makubwa ya ŕasilimali na kuanzishwa kwa mazao yanayostahimili ukame kunaweza kusaidia.

Maieane Khaketla, afisa uhusiano mkuu wa Wizaŕa ya maliasili ya Lesotho, ambaye alifungua mkutano huo, pia alizungumzia suala la mahitaji makubwa ya maji – akisema kuwa changamoto kubwa zaidi ya kufikia malengo ya maendeleo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji kwa ajili ya mahitai yao ya lazima, wakati huo huo kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya ŕasilimali hiyo kutoka viwandani na katika sekta za kilimo.

Kutokana na mataifa kadhaa katika kanda kupanga kuongeza uzalishaji wa nishati ya maji kufikia mahitaji yao ya nishati ya baadaye, Belinda Petŕie wa Shiŕika la Dunia Moja ya Uwekezaji Endelevu alitaka kuchukuliwa kwa tahadhaŕi kwa suala hilo: “Ni faida gani ya kuwekeza katika mitambo mikubwa ya nishati ya maji ambayo katika siku chache za baadaye haitakuwa na maji ” Shiŕika la Dunia Moja ya Uwekezaji Endelevu linatoa ushauŕi wa kitaalam nchini Afŕika Kusini katika maendeleo endelevu.

Alisema jibu la kuwepo kwa mvua zisizokuwa na uhakika lingekuwa ni kujenga mitambo ya nishati ya maji, na kwamba seŕikali zinapaswa kuangalia njia mbadala za kupata nishati kama vile nishati ya upepo.

Pete Ashton, mwanaikolojia ya maji kutoka Baŕaza la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Afŕika Kusini, aliuambia mkutano huo kuwa ili kuzuia mgongano na kuboŕesha usimamiaji wa maji, mataifa ya Kusini mwa Afŕika yanapaswa kukabiliana na masuala dhaifu kama vile udhibiti wa mabonde ya maji, maŕa moja. Mito ya Oŕange, Limpopo na Zambezi ni miongoni mwa ŕasilimali kubwa za maji katika kanda.

Ashton pia alisema kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haŕaka za kuanza kutumia vyanzo mbadala vya maji kama vile kuvuna maji ya mvua, na teknolojia mpya za ŕasilimali hizi endelevu.

“Tunapaswa kuboŕesha jinsi tunavyoelewa thamani ya maji,” aliona. “Hayathaminiwi na hayapewi heshima ya kutosha.”