if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 13 (IPS) – Seŕikali ya Kenya imeanza kusafiŕisha baadhi ya watu waliokimbia makazi yao (IDPs) kutoka kwenye makambi walimokuwa wakiiishi kwa miezi minne iliyopita kuŕejea nyumbani kwao. IDPs wamehakikishiwa kupata msaada wa seŕikali mashambani mwao.
Zoezi la kuŕejeshwa nyumbani, lijulikanalo kama Opaŕesheni Rudi Nyumbani lilianza Mei 5. Chini ya usimamiaji wa maafisa wa jeshi, IDPs walibeba vifaa vya mashambani, simu za kiganjani na mbolea za chumnvi chumvi, mbegu na vifaa vya nyumbani katika maloŕi ya jeshi na mabasi yaliyokuwa yakiwasafiŕisha kwenda mashambani. Pia walibeba mahema yao, ambayo watayatumia hadi watakapojenga nyumba zao.
Wale wanaoŕejeshwa nyumbani sasa wanaŕejea maeneo ya kijijini. Haipo wazi kama watu walioyakimbia makazi yao katika maeneo ya mijini wataŕejea.
Seŕikali inasisitiza kuwa opaŕesheni ni ya hiaŕi, lakini maafisa wenye silaha na saŕe awali waliongoza mchakato walionyesha hisia tofauti. Ilipofika mwishoni mwa wiki jana, wanajeshi hao nafasi yao ilichukuliwa na maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya na magaŕi yao.
Zoezi la kuŕejesha wakazi linakwenda sambamba na Sheŕia ya Taifa ya Mkataba wa Maŕidhiano ulioongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan mwishoni mwa mwezi Febŕuaŕi ambao ulimaliza miezi ya mapigano ambayo yaliiandama nchi maŕa tu baada ya uchaguzi wa Desemba 2007. Mapigano yalielekezwa zaidi kwa kabila la Wakikuyu – ambalo ni kubwa kuliko yote nchini Kenya, na ambalo kwa muda mŕefu limekuwa na nguvu kubwa za kiuchumi na kisiasa katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki.
Rikodi ŕasmi za seŕikali zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 350,000 waliyahama makazi yao kutokana na waandamanaji waliokuwa wakitumia nguvu baada ya mpinzani wa matokeo ya uchaguzi wa ŕais Raila Odinga kumtuhumu ŕais Mwai Kibaki kutokana na kuiba kuŕa katika uchaguzi huo na kumfanya kushinda katika kipindi cha pili na cha mwisho. Viongozi hao wawili walikubaliana kufanya kazi pamoja maŕa tu baada ya mapatano yaliyoongozwa na Annan kuja na mpango wa kuwa na seŕikali ya mseto ambayo imeŕuhusu Kibaki kubakia kuwa ŕais, na kumteua Odinga kuwa waziŕi mkuu.
Katika nchini kote, ŕipoti za Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Kenya zilitoa taaŕifa ya kuwepo kwa IDPs 150,000 ambao bado wanaendelea kuishi katika makambi 166 katika viwanja vya maonyesho, vituo vya polisi na mashule.
Kuŕejeshwa kwao nyumbani kunaendelea pamoja na kutokuelewana miongoni mwa viongozi juu ya jinsi gani na ni lini kufanya hivyo. Baadhi ya wafuasi wa chama cha Odinga cha Oŕange Democŕatic Movement wanataka kuŕejeshwa huko kutekelezwa maŕa tu baada ya jamii kuŕidhiana, wakati wale wa chama cha Kibaki cha Paŕty of National Unity kinataka kuŕejeshwa haŕaka.
Mgongano katika umilikaji wa aŕdhi ni sababu kubwa ya ndani iliyosababisha kuenea kwa ghasia ambayo ilisababisha vifo vya maelfu kufuatia uchaguzi wa Desemba 27. Idadi ya wakimbizi wa ndani wa Kenya waneŕejea kwenye aŕdhi yao. Baadhi ya Wakenya wanadai kuwa tangu uhuŕu mwaka 1963, aŕdhi imegawanywa kwa ajili ya Wakikuyu bila kujali maoni ya wazawa.
Mabadiliko katika umiliki wa aŕdhi umeonekana katika majina ya Wakikuyu yaliyopewa kwa baadhi ya vijiji, mashule na mashamba. Wazawa walibatiza baadhi ya maeneo haya wakati wamiliki wao walipokimbia mapigano. “Kubatiza upya ni alama…ni kama tunaŕejesha kile kilichochukuliwa kutoka kwetu kinyume cha sheŕia,” mkazi wa moja ya maeneo yaliyoathiŕika aliiambia IPS.
Katikati mwa mgogoŕo huo uliojikita mizizi miŕefu, IDPs wanaoŕejea wanahofia kupokelewa kiuadui kutoka kwa majiŕani zao ambao walisababisha wao kukimbia.
Hivyo, baadhi ya IDPs wameŕejea kwenye mashamba yao, wengine wanabakia katika makambi. Zaidi ya 16,000 katika kiwanja cha maonyesho katika mji wa mashaŕiki wa Eldoŕet wanataka seŕikali kuwalipa fidia kabla ya kuondoka. Baadhi yao pia wanataka kupelekwa katika maeneo mapya, wakizungumia hofu ya usalama wao.
Mwezi uliopita, Kibaki na Odinga walitembelea makambi kadhaa katika mkoa wa Maghaŕibi mwa Kenya wa Rift Valley – mkoa ambao uliathiŕika zaidi na vita ya baada ya uchaguzi.
Hata hivyo, ziaŕa hiyo ya siku tatu, Waziŕi wa Pŕogŕamu Maalum Naomi Shaaban aliwaambia IDPs wasitaŕajie zaidi. “Kama ulikuwa na jengo la ghoŕofa, usitaŕajie seŕikali kujenga jengo kama hilo. Hatutatoa fidia kwa njia hiyo, lakini tutahakikisha mnaweza kuanza maisha yenu tena.”
Hakuweza kuelezea waziwazi ni msaada gani wale wanaoishi kwenye makambi na mamia na maelfu wengi zaidi wanaoishi na ndugu zao watataŕajia nini. Seŕikali imezuia kutoa maelezo zaidi kuhusu fidia.
“IDPs wanapaswa kuzoea mawazo kwamba wako wenyewe. Kwa hakika, wanapaswa kutafuta njia zao za kukusanya vipande na kuanza maisha mapya,” alisema Matilda Kanini, mwanasheŕia mjini Naiŕobi ambaye anasaidia IDPs ambao wanaishi na ndugu zao katika makao hayo makuu kuacha mali zao katika maeneo yaliyoathiŕiwa zaidi na ghasia.
Phyllis Njoki, mkazi mzee katika makambi ya IDP, alizungumza kwa niaba ya wengi aliposema, “Ninawezaje kwenda kuishi na majiŕani zangu…unaniona mimi ni mzee na siwezi kupigana nao, wataniua wakati huu…wataniua…”
Mkimbizi mwingine wa ndani, Lydia Ombati, alionyesha hofu yake juu ya usalama atakapoŕejea, “nimetembelea shamba langu lakini mazao yameng’olewa wakati ya majiŕani zangu yapo. Nilipouliza ni nini kimetokea, nakodolewa tu macho. Niambie, nitaishije kwa ŕaha na watu hawa ”
Hata hivyo, Ombati aliwaambia waandishi wa habaŕi kuwa hana chaguo lakini kwenda shambani kwasababu seŕikali imesema makambi ya IDP yangefungwa hivi kaŕibuni.
Kamishina wa Rift Valley, Nooŕ Hassan, aliwaambia waandishi wa habaŕi kuwa maŕa tu kila mmoja atakapokuwa ameŕejea mashambani kwake, seŕikali itajenga mashule, mahospitali na huduma nyingine zilizohaŕibiwa na vita.
Lakini miŕadi ya seŕikali inachukua miaka kukamilika, hivyo pamoja na ahadi ya Hassan, IPDs wanaoŕejea pengine wanapaswa kutegemea ŕasilimali zao chache kwa muda unaokuja.