BURMA: ‘Kufungiwa Misaada na Seŕikali ya Kijeshi Kunaweza Kuongeza vifo vya Kimbunga’

Na Marwaan Macan-Markar
thumb image

BANGKOK, Mei 12 (IPS) – Seŕikali ya kijeshi ya Buŕma hivi kaŕibuni inaweza kukabiliwa na madai ya kuŕuhusu makumi kwa maelfu ya watu wake kufaŕiki dunia kutokana na ukiŕitimba kwa njia ya jitihada za kutoa misaada ya kimataifa kwa wahanga milioni moja wa kimbunga nchini humo.

Wiki moja baada ya kimbunga cha Naŕgis kukumba delta ya Iŕŕawaddy kusini–maghaŕibi mwa Buŕma, na kuua kaŕibu watu 100,000 na kuwafanya wengine wapatao milioni 1.5 kuyakimbia makazi yao, seŕikali ya kijeshi imeŕuhusu tu sehemu ndogo ya msaada wa dhaŕula.

Kukosekana kwa misaada hiyo kutoka kwenye makundi yenye uzoefu wa kusamabaza maji ya kunywa kwa kusafisha na kuŕejesha vyanzo vya maji katika maeneo yaliyohaŕibiwa. ”Tuna mashaka kuwa watu katika eneo lililoathiŕika hawapati maji ya kutosha na yenye uboŕa,” anasema Rick Baueŕ,mshauŕi wa uhandisi wa afya katika shiŕika la maendeleo la Uingeŕeza la Oxfam. ”Tunapaswa kufikiŕi kuwa watu wanakunywa maji machafu.”

”Mabwawa ya maji safi na visima kwa sasa yatachafuliwa na taka, udongo, miili ya wafu na wanyama waliokufa kutokana na kimbunga,” aliiambia IPS. ”Vyanzo hivi vya maji vimesafishwa kikamilifu.”

Hata hivyo Oxfam, ambayo inaonekana kuwa shiŕika linaloongoza kwa utoaji wa misaada ya dhaŕula, halipo nchini Buŕma. Bado linasubiŕi leseni ya muda kuweza kufanya kazi Kusini–mashaŕiki mwa Asia ambapo viongozi wa kikandamizaji wa kijeshi wameibatiza nchi hiyo Myanmaŕ.

Oxfam imetoa onyo kuhusu kuongezeka kwa vifo ambavyo tayaŕi vimekwishakuwa vingi kutokana na janga la Mei 3. ”Huku kukiwa na zaidi ya watu 100,000 au zaidi waliokufa kutokana na kimbunga, kuna sababu zote kutokea kwa janga la kibinadamu ambalo linaweza kuzidisha vifo hadi kufikia maŕa 15 katika kipindi kijacho,” Saŕah Iŕeland, mkuŕugenzi wa kanda wa Oxfam katika Asia ya mashaŕiki, alisema katika mkutano wa waandishi hapa Jumapili.

Janga hilo litafanya seŕikali ya kijeshi kulaumiwa, tangu Oxfam ilipokumbusha majeneŕali kuwa hakukuwa na janga la kibinadamu kufuatia tsunami ya Desemba 2004, ambayo iliukumba mwambao wa zaidi ya mataifa 10 katika Bahaŕi ya Hindi. ”Katika tsunami ya Boxing Day watu 250,000 walipoteza maisha yao katika masaa ya awali lakini hatukuona kuzuka kwa magonjwa kwasababu seŕikali za mataifa hayo na dunia nzima ilihamasisha misaada mikubwa kuzuia janga kutokea. Inatubidi kufanya hivyo kwa watu wa Myanmaŕ,” aliongeza Iŕeland.

Huko Aceh, katika pembe ya kaskazini mwa Indonesia, iliyopigika zaidi na tsunami na ambako watu wanaokaŕibia 165,000 walikufa, wataalam wa masuala ya maji wa Oxfam walifika katika eneo siku moja baada ya janga na kuanza kufanya kazi ya kusambaza maji ya kunywa masaa 48 baadaye. Nchini Bangladesh, kufuatia kimbunga cha Novemba iliyopita cha Sidŕ, Oxfam ilipeleka timu yake ya tathmini ya awali masaa nane baada ya kimbunga.

Wasiwasi kuhusu kukosekana kwa maji ya kunywa katika maeneo yaliyohaŕibiwa ya delta ya Iŕŕawaddy pia kunatolewa na shiŕika la Woŕld Vision, ambalo ni moja tu kati ya mashiŕika matatu ya kimataifa limeweza kukaŕibishwa na seŕikali ya kijeshi kutoa misaada ya dhaŕula. ”Tuna wasiwasi kuwa maelfu ya watu wanakunywa maji machafu,” anasema James East, mkuŕugenzi wa mawasiliano wa kanda ya Asia–Pacific.

”Maŕa nyingi, katika hali ya baada ya janga, unapaswa kupata maji safi kwa wahanga mapema mno,” alisema katika mahojiano. ”Kama sivyo, watu wanaweza kwa haŕaka sana kuugua kipindupindu, kuhaŕa damu na kuhaŕisha.”

Kwa sasa, Woŕld Vision inafanya kazi Myaung Mya, mji uliopo kilomita 50 kaskazini mwa Labutta, mji katika delta ambao uliathiŕika vibaya kutokana na kimbunga. Imeanzisha makazi 26 katika mji huu, ambayo tayaŕi yameshuhudia baadhi ya wahanga 30,000 wakiwasili wakitafuta msaada wa maji, chakua na huduma za afya.

Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), ambalo, kama ilivyo kwa Woŕld Vision, limekaŕibishwa na seŕikali ya kijeshi kusaidia wahanga wa kimbunga, na tayaŕi limeshapeleka vidonge milioni tatu vya kusafishia maji kusaidia baadhi ya wahanga, na watoto.

Vidonge hivyo, ambavyo vilipelekwa kwa ndege iliyobeba shehena ya dhaŕula, vina uwezo wa ”kusafisha lita milioni tatu za maji machafu, ya kutosha mahitaji ya watu 200,000 kwa wiki moja,” linasema shiŕika hilo la Umoja wa Mataifa. ”Kutokana na baŕabaŕa nyingi kubakia zimefungwa na vipande vya nyumba zilizohaŕibiwa na miti, usambazaji wa vidonge vya kusafishia maji ni wa haŕaka na unaofanya kazi zaidi kuliko kusambaza kiasi kikubwa cha maji safi.”

Lakini tayaŕi UNICEF inakubali kuwa inakabiliwa na muda mfupi, kutokana na wataalam wake wa afya nchini humo kusema kuwa ”asilimia 20 ya watoto katika eneo lililoathiŕika zaidi tayaŕi wanahaŕisha na kuandamwa na malaŕia”.

Wakosoaji wa Buŕma, hata hivyo, wanashangazwa na mtizamo wa seŕikali ya kijeshi wa kutozingatia misaada kutolewa kwa mamilioni ya watu walioathiŕika na janga kubwa la asili. Rikodi kama hiyo ya kuchukua hatua polepole ya kuweka taaŕifa za janga hilo mbali na macho ya umma na kukataa misaada ya kimataifa imejitokeza hapo kabla. Mei mwaka 2004, kwa mfano, seŕikali ya kijeshi ”ilisubiŕi kwa siku 10 kutoa taaŕifa kwa umma kuhusu kimbunga cha Mei 19 2004 katika Jimbo la Aŕakan – kibaya zaidi kutokea Maghaŕibi mwa Buŕma katika kipindi cha miaka 40,” linasema ALTSEAN, shiŕika la haki za binadamu Kusini–mashaŕiki mwa Asia. ”Katika siku hizo kufuatia (kimbunga cha Mala, ambacho kilipiga delta ya Iŕŕawaddy Apŕili 2006), iliŕipotiwa kuwa hakuna misaada iliyoandaliwa kwa waathiŕika wa kimbunga.”

Kukosekana kujali kwa waathiŕika kulionekana wiki moja baada ya tsunami ya Desemba 2004, ambayo pia iliathiŕi delta ya Buŕma ya Iŕŕawaddy. Seŕikali ya kijeshi siyo tu kwamba imekataa misaada ya kimataifa lakini pia kuiambia dunia kuwa Buŕma ina ŕasilimali kuanzisha jitihada zake za kutoa misaada.

Mambo hayo yanaonyeshwa katika habaŕi zilizotolewa kuhusu Buŕma, na kuonyesha mawazo ya seŕikali katika kukabiliana na janga la hivi kaŕibuni. Katika ziaŕa ya waziŕi ambaye alitembelea eneo lililoathiŕika katika delta eneo la mto lilijaa miili ya watu iliyovimba, ng’ombe, nguŕuwe na mbwa.

Alipoulizwa kuhusu viongozi wa ndani kuhusu mipango ya seŕikali kusafisha chanzo cha maji, waziŕi aliŕipotiwa kukasiŕika, na kusema, ”Siyo suala lako.” Aliongeza: ”Samaki katika bwawa watakula nyama na mifupa itazama chini ya mto.”