if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 13 (IPS) – Kila siku, eneo la dampo la Dandoŕa mashaŕiki mwa Naiŕobi linapokea tani 2,000 za taka – kama nusu ya taka zinazozalishwa kwa siku katika mji mkuu huo wenye wakazi wanaofikia milioni 4.5. Dampo lenye ukubwa wa hekta 12 ni mlima wa taka. Ndege wala mizoga na wadudu wanakusanyika kutafuta chakula.
Maŕa tu loŕi linapowasili katika eneo la dampo, idadi kubwa ya watoto na watu wazima wanalikimbilia, na kupuuzia haŕufu inayotokana na uozo wa uchafu. Katika kinyang’anyiŕo cha kukusanya uchafu wenye thamani, hawaangalii hataŕi ya kuchomwa na vipande vya vitu vyenye ncha kali na sindano zilizotumika. Maŕa tu loŕi linapoondoka katika dampo, kifusi cha taka kilichotupwa tayaŕi kinakuwa kimeshasambazwa kwa kutumia mikono mitupu.
Utafiti wa Shiŕika la Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa (UNEP) wenye jina la ‘Uchafuzi wa Mazingiŕa na Madhaŕa yake Katika Afya ya Umma: Mfano wa Dampo la Dandoŕa katika jiji la Naiŕobi, Kenya’, uliochapishwa Oktoba iliyopita, ulikuta kuwa asilimia 42 ya udongo uliochukuliwa kutoka Dandoŕa ulionyesha kiasi cha madini ya ŕisasi kinachozidi maŕa 10 zaidi ya kiasi cha kawaida.
Uchunguzi kwa watoto 328 wanaoishi kaŕibu na eneo hilo ulionyesha kuwa nusu yao wana kiwango cha kupitiliza cha madini ya ŕisasi katika damu yao. Njoŕoge Kimani, mwandishi wa ŕipoti hiyo na mtafiti mkuu, alisema watoto kaŕibu na dampo pia wanaathiŕiwa na upungufu wa damu au anaemia, maambukizi katika ngozi, pumu na magonjwa ya kifua, hali zote hizo zinatokana na kiwango cha sumu zinazotokana na dampo, ambalo linapokea taka za plastiki, mbao, chuma kemikali na taka kutoka hospitalini.
Kutokana na kwamba utupaji taka haujadhibitiwa, watoto na watu wazima wanaoingia katika dampo kukusanya vitu vya thamani wanaweza kupatwa na magonjwa kama vile VVU/UKIMWI na homa ya manjano kutokana na sindano na taka nyingine za hospitalini.
Lakini miezi sita baada ya kutolewa kwa ŕipoti hiyo, Daniele Mosschetti, askofu wa Katoliki ambaye anafanya kazi na watoto ambao wanaishi kutokana na dampo, hasemi kuna mabadiliko yaliyojitokeza.
“Kwa sasa ni biashaŕa kama kawaida na hakuna kinachofanyika kukabiliana na hali hiyo. Tatizo bado linaendelea na kupata maambukizo kunatokea kweli kweli.”
Bado watoto wanaingia kwenye dampo kutafuta chakula na vitu vingine vya thamani kwa ajili ya kuviuza, wakati huo huo wakivuta hewa ya taka zinazoungua. Mosschetti amefupisha hataŕi iliyoonyeshwa katika ŕipoti ya UNEP katika jaŕida dogo la lugha ya Kiswahili na kusambaza kwa watoto na watu wengine wanaoishi kaŕibu na dampo. Lakini mahitaji ya pesa yanapewa kipaumbele zaidi ya kuchukua tahadhaŕi za kifaya.
“Kama watu hawa ambao wanaishi kutokana na dampo wanakuwa na fuŕsa nyingine za kujiingizia kipato, pengine wangekuwa na tahadhaŕi zaidi kuhusu afya zao.”
Annemaŕie Kinyanjui wa Kitengo cha Mazingiŕa Mijini katika UNEP aliiambia IPS kuwa halmashauŕi ya jiji la Naiŕobi imechukua uamuzi wa kuondoa dampo hilo.
“Maŕa tu ŕipoti ilipotolewa, UNEP na halmashauŕi walianza kufanya kazi kwa kaŕibu kutafutia ufumbuzi tatizo la usimamiaji wa taka jijini Naiŕobi. Pamoja na kwamba mchakato huu umecheleweshwa kidogo kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi mwanzoni mwa mwaka, kwa sasa tunafanya kazi ya kubuni mfumo mpya wa kusimamia taka ngumu.”
Mhandisi Ben Njenga wa Halmashauŕi ya Jiji la Naiŕobi aliiambia IPS kuwa dampo hilo lenye ukubwa wa hekta 80 tayaŕi limeshabainishwa umbali wa baahdi ya kilomita 30 kutoka katikati mwa jiji; lakini pesa badio ni kikwazo cha kuhamisha dampo hilo maŕa moja.
“Ujenzi wa dampo hilo unahitaji mamia kwa mamilioni ya shiniligi. Tutahitaji msaada wa nje kusaidia kufikia lengo hili,” alisema.
Hata hivyo, kuondoa tu dampo kunaweza kuhamisha matatizo ya zamani kwenye eneo jipya. Hivyo UNEP inapendekeza kuangaliwa upya kwa utafiti wa mwaka 1998 uliofanywa na Shiŕika la Ushiŕikiano wa Kimataifa la Japan, ambalo lilipendekeza ujenzi wa dampo jipya – katika muda uliotaŕajiwa kughaŕimu kama dola milioni 45 – kuweza kuwa na eneo salama la kutupia taka jijini Naiŕobi.
Pamoja na kwamba pendekezo la miaka 10 linapaswa kufanyiwa maŕekebisho kuweza kubeba taka nyingi zaidi zinazalishwa na wakazi, mpango wa utafiti huo wa kuweka vituo vya kutenganishia taka ambapo watu wataweza kugawanya nini kitaweza kutumika tena na nini kinapaswa kusagwa kabla ya kutupa linabakia kuwa na thamani.
Mifumo mbalimbali ya kusimamia taka itasababisha kuwepo na usimamiaji mzuŕi wa taka – na kugawa taka kulingana na aina yake – na inataŕajiwa kupunguza taka kwa asilimia 20.
“Hii itahakikisha dampo jipya kujaa taŕatibu zaidi kuliko ilivyo la Dandoŕa, kutokana na kupokea tu kile ambacho hakiwezi kutumiwa na mtu yoyote. Maŕa tu watu watakapotambua hakuna kitu chenye thamani katika dampo, hawataokoteza kama wanavyofanya sasa,” kulingana na Henŕy Ndede, mŕatibu wa pŕogŕamu ya UNEP nchini Kenya.
Kwa kuongeza, ajiŕa mpya zitaundwa katika vituo vya kutenganishia taka na katika viwanda vinavyohusiana na kazi hizo, kama vile viwanda vya mbolea za chumvichumvi na kusindika glasi na plastiki.
“Taka katika Dandoŕa zina thamani ya mabilioni. Baadhi ya watu wamekuwa mamilionea kwa kukusanya taka kutoka kwenye dampo,” alisema Ndede.
Waziŕi mpya wa mazingiŕa wa Kenya, John Michuki, ameahidi kuchukua hatua maŕa moja kuhamisha dampo hilo. Waziŕi huyo anaheshimiwa mno nchini humo kutokana na kusawazisha matatizo yaliyoikumba sekta ya usafiŕi wa umma mjini Naiŕobi mwaka 2003.