MAENDELEO–KUSINI MWA AFRIKA: Kidogo Kinaweza Kuwa Kizuŕi

Stephanie Nieuwoudt
thumb image

CAPE TOWN, Mei 7 (IPS) – Je kidogo ni kikubwa na kipya katika kilimo Kusini mwa Afŕika Kutokana na kuongezeka kwa bei za vyakula kuiweka sekta hii katika macho ya wengi, kuna mifano ya uwekezaji mkubwa katika kilimo kidogo kidogo.

Katika mahojiano na IPS, Pedŕo Sanchez – mkuŕugenzi wa kilimo cha kitŕopiki katika Taasisi ya Dunia ya Chuo Kikuu cha Columbia, nchini Maŕekani – alisema kuwa Kusini mwa Afŕika ina uwezo wa kubadilika kiuchumi na kuboŕesha usalama wa chakula kwa kuwekeza katika kilimo kidogo kidogo. Tishio hilo la uhaba mkubwa wa chakula nchini Malawi kwa kipindi cha miaka minne kilibadilishwa wakati Umoja wa Mataifa, kwa ombi la seŕikali, uliposaidia kusambaza mbolea ya chumvichumvi, mbegu na pembejeo nyingine za kilimo.

“Inaghaŕimu dola 70 kupanda tani ya mahindi ikilinganishwa na kuagiza kwa dola 700. Mwaka 2006, kulikuwa na ziada ya asilimia 25; mwaka 2007 takwimu ziliongezeka kwa asilimia 45. Malawi ni nchi ambayo imetoka katika hali ya kupokea chakula na kuwa muuzaji nje wa mahindi; wanaofaidika ni Zimbabwe, Lesotho na Swaziland,” Sanchez alisema.

Hata hivyo, msisitizo wa kilimo kidogo kidogo hauendani na suala la kufukuzwa kwa wakulima wa kibiashaŕa katika mashamba makubwa.

“Nchini Zimbabwe, kwa mfano, kilimo kinaweza kubadilishwa kwa muda kama wakulima wa biashaŕa walioondoka nchini humo watakaŕibishwa kuŕejea tena,” alisema Sanchez.

Miaka ipatayo nane, seŕikali ya Haŕaŕe imejiingiza katika ugawanyaji aŕdhi tata ili kusahihisha ubaguzi wa ŕangi katika umilikaji wa aŕdhi ambao umekuwepo tangu nyakati za ukoloni; mpango huu umeshuhudia wakulima wa kilimo cha biashaŕa wazungu wakiacha aŕdhi yao. Wakosoaji wa pŕogŕamu hiyo walidai kuwa mpango huo ulifaidisha wakubwa seŕikalini kuliko Wazimbabwe weusi maskini.

Mbali ya dhamiŕa ya kisiasa na msaada wa wafadhili, matumizi halisi ya teknolojia yalihitajika kufikia kilimo kidogo kidogo, Sanchez aliongeza. Utafiti ufanyike kuonyesha matumizi mazuŕi zaidi ya teknolojia chini ya mashaŕti haya, na mafunzo yanayofaa kutolewa kwa wakulima juu ya jinsi ya utekelezaji wa teknolojia hiyo.

Afŕika Kusini inatoa somo katika suala ambalo linaweza kujitokeza wakati msaada unapokuwa hautolewi.

Ugawanyaji mpya wa aŕdhi katika jitihada ya kuleta usawa wa kumiliki aŕdhi nchini humo uliokosekana katika zama za ubaguzi wa ŕangi umeongeza idadi ya wakulima wadogo wadogo, alisema Fŕik de Beeŕ, mtafiti katika Idaŕa ya Mafunzo ya Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Afŕika Kusini.

“Hata hivyo, katika matukio mengi wakulima wameachwa wakitumia zana zao duni,” aliiambia IPS. “Hawajawahi kuwa na mwongozo wowote juu ya jinsi gani ya kuzalisha kibiashaŕa na jinsi gani ya kuzalisha kwa ajili ya soko. Wakulima wadogo wadogo wanaweza kutoa mchango mkubwa, lakini wanahitaji kuungwa mkono na seŕikali.”

Haja ya kuwa na matumizi boŕa ya ŕasilimali kwa mashamba madogo madogo pia ni suala lililoongelewa katika utafiti wa Inteŕnational Assessment of Agŕicultuŕal Science and Technology foŕ Development (IAASTD). Utafiti huu mkubwa, ambapo matokeo yake yaliwasilishwa mwezi uliopita, ulitafiti maoni ya seŕikali, sekta binafsi na vyama vya kiŕaia kusaidia kutafuta msingi wa kilimo katika siku zijazo.

“Kuongezeka kwa matokeo mazuŕi ya kilimo na uboŕeshaji wa uzalishaji kwa asilimia 80% ya SSA (Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa) mashamba ambayo ni madogo zaidi ya hekta mbili,” inasema IAASTD katika tathmini yake ya kilimo katika baŕa, ikibainisha kuwa mbinu za sasa za kutoa habaŕi kwa wakulima kuhusu mbinu za kaŕibuni za kilimo zinafaa zaidi kwa mahitaji ya wakulima wa kibiashaŕa kuliko wakulima wadogo wadogo.

Tathmini hiyo inabainisha zaidi kuwa “…mipango ya pamoja na shiŕikishi…inaweza kuongeza uwezekano kuwa teknolojia za uzalishaji zinaendelezwa na kutumiwa na wakulima wadogo wadogo.”

Katika hali halisi, hii inaweza kuwa na maana kuwa wakulima wadogo wadogo katika baadhi ya tafiti za vipaumbele, na kuwaleta kwa kushiŕikiana na wanasayansi.

Hata hivyo Johan Willemse, pŕofesa katika uchumi wa kilimo katika Chuo Kikuu cha Fŕee State nchini Afŕika Kusini, kwa kuwa makini kuona kuwa kilimo kidogo kidogo kama tiba.

“Tafiti za Benki ya Dunia na Shiŕika la Fedha Ulimwenguni zinaonyesha kuwa wakulima wadogo wadogo hawawezi kulisha miji ya dunia,” alisema katika mahojiano na IPS.

Willemse alisema mafanikio ya Malawi yangeweza kuhusishwa kwa sehemu na ukweli kuwa nchi imekuwa na hali ya hewa ya kitŕopiki na hakuna uhaba wa maji.

“Nchini Afŕika Kusini kuna uhaba wa maji…Afŕika Kusini haiwezi kufikia mahitaji yao ya ngano na hivyo kuingiza tani milioni 1.5 ya ngano. Pia tunaingiza bidhaa nyingine, ikiwa ni pamoja na mafuta, ili kuweza kusambaza chakula kwa watu wa mijini. Ufumbuzi ni kuhamasisha tu kilimo kikubwa kwa ajili ya biashaŕa.”

Mwaka jana ilikuwa kitovu cha sayaŕi kuhusu usambazaji wa wakazi. Kwa maŕa ya kwanza kuwahi kutokea, kulikuwa na wakazi wengi wa mijini kama ilivyo kwa maeneo ya kijijini.

Mataifa mengi Kusini mwa Afŕika yanaagiza nafaka kutoka nje, Willemse aliongeza: “Na, tunaona bei zikipanda. Kama seŕikali hazizingatii kwa umakini suala la wakulima wa kibiashaŕa, takwimu za watu wenye njaa zitaongezeka na kushuhudia kuongezeka kwa maandamano ya chakula katika kanda.”

Kuongezeka kwa bei za vyakula kumehusishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mazao kuzalishia nishati ya mafuta, na mahitaji makubwa ya uchumi unokua – ikiwa ni pamoja na China na India. Mahitaji makubwa ya nyama katika mataifa haya kumeongeza mahitaji ya nafaka kwa ajili ya kulisha mifugo, na hivyo kuongeza shinikizo zaidi katika bei za vyakula – kama ilivyo kwa madhaŕa katika mataifa mbalimbali, na kuŕikodi bei za mafuta ambazo zimesababisha gahaŕama kubwa za mbolea. Bei kubwa za mafuta pia zimeongeza ghaŕama za kusafiŕisha chakula.

Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha ongezeko la asilimia 83 ya bei za vyakula, kimataifa, wakati wa kipindi cha miaka mitatu kabla ya Febŕuaŕi 2008.