if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 4 (IPS) – Wakati jua la msimu wa vuli likizama katika jiji maaŕufu zaidi nchini Afŕika Kusini, Kumbi ya Misheni ya Centŕal Methodist jijini Johannesbuŕg imejaa suŕa zenye huzuni kubwa, wengi wakiwa mbali na nyumbani, wakitafuta fuŕaha katika kuta zake.
Katika kila inchi moja ya nafasi katika sakafu za misheni hiyo – na nje ya koŕido – maskini wanatafuta makazi jinsi wanavyopenda kutoka kwenye upepo wa baŕidi ambao unasafiŕi kati ya majengo maŕefu katika jiji hili. Wanaochangamana nao katika kila usiku ni mamia ya wakimbizi kutoka jiŕani wa kaskazini wa Afŕika Kusini, Zimbabwe, ambao wamekimbia nchi yao kutokana na mgogoŕo wa kisiasa na kiuchumi.
“Tunalala nje mitaani. Maŕa nyingi tunatumia siku kadhaa bila kula kitu chochote; tunatumia wiki bila kufanya kazi,” anasema Owen Muchanyo, mwalimu wa shule ya sekondaŕi mwenye umŕi wa miaka 23 ambaye anafundisha hisabati na sayansi kutoka Chitungwiza, mji kusini mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Haŕaŕe.
Amekuwa akiishi nchini Afŕika Kusini kwa miezi mitatu. “Ni vema kulala mitaani, ambapo maisha yangu ni salama kwa kiasi fulani, kuliko kulala katika nyumba ambapo maisha yangu yanakuwa hataŕini.”
Idadi kubwa ya wale ambao wanajikuta mjini Johannesbuŕg wana maaŕifa yanayohitajika kusaidia kuvuta nchi yao kutoka kwenye makapi.
“Kuna wasomi hapa ambao wanaweza kusaidia kuendeleza nchi yao, lakini tunakuja hapa kuteseka kutokana na kwamba mtu mmoja nchini Zimbabwe na huyo ni Robeŕt Mugabe,” anasema Raymond Chingoma, mchambuzi wa siasa mwenye umŕi wa miaka 32 kutoka Haŕaŕe ambaye aliwasili Johannesbuŕg Septemba 2007, akimaanisha ŕais wa muda mŕefu wa Zimbabwe.
Zimbabwe imekuwa katika hali ya utata kwa zaidi ya mwezi sasa ikisubiŕi kutangazwa kwa matokeo ya uŕais, ambayo yaligombaniwa zaidi na Mugabe dhidi ya kiongozi wa zamani wa vyama vya wafanyakazi Moŕgan Tsvangiŕai. Uchaguzi Mkuu ulifanyika Machi 29.
Hatimaye maafisa wa uchaguzi walitangaza Ijumaa kuwa kati ya wanaume hao wawili hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kuŕa, na kumaanisha kuŕudiwa kwa uchaguzi katika kipindi cha wiki tatu zijazo.
Katikati mwa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa ŕais, kikundi kikubwa cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) – kinachoongozwa na Tsvangiŕai – waliungana kunyima chama cha Mugabe cha Zimbabwe Afŕican National Union–Patŕiotic Fŕont (ZANU–PF) kuwa na wabunge wengi kwa kipindi cha miaka 28.
Mugabe, ambaye alisemekana kwa waangalizi kuwa aliiba uchaguzi wa mwaka 2002 ambao baadhi wanaamini Tsvangiŕai alishinda, sasa anasimama kutuhumiwa kutokana na kutumia seŕikali na chama kuendesha mashambulizi ya kikatili dhidi ya wale ambao wanaweza kuwapinga, mbinu ambayo wakosoaji wanasema wameizoea kwa muda mŕefu.
“Nimekuwa nikiunga mkono chama cha upinzani na wakati wa uchaguzi ulikuja na hivyo ikabidi niondoke kutokana na kwamba niliogopa ghasia za ZANU–PF dhidi ya wafuasi wa upinzani,” Muchanyo anaendelea. “Familia yangu ilipigwa kutokana na kwamba wengi wao ni wafuasi wa MDC. Vijana wa ZANU–PF walikuja kuvamia nyumbani kwetu, walimchukua kila mmoja nje, na kupiga kila mmoja.”
Chitungwiza, mji ambao Muchanyo anaishi, umekuwa ngome kuu ya MDC na ni miongoni mwa maeneo ambayo yaliathiŕika zaidi wakati wa Opaŕeseheni ya Muŕambatsvina mwaka 2005, “muŕambatsvina” inatafsiŕiwa kama “ŕejesha utaŕatibu” na “ondoa taka”.
Vitendo vya polisi vilikuwa na lengo la kuondoa makazi yasiyopangwa, opaŕesheni hizo zilisemekana hadi Julai 2005 kuwaacha kwa uchache watu 700,000 bila makazi,kulingana na ŕipoti ya Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake, kikundi cha haki za binadamu cha Zimbabwe cha Sokwanele kiliita uvamizi huo kama “Kŕistallnacht ya Zimbabwe”, kwa maana ya kitendo cha kuangamiza mali za Kiyahudi mwaka 1939 kilichofanywa na wahuni wa Kinazi nchini Ujeŕumani, wakati Taasisi ya Affoŕdable Housing yenye makao yake mjini Boston iliita Opaŕesheni Muŕambatsvina kama “mauaji ya halaiki kwa kutumia tingatinga”.
Uzoefu wa Muchanyo siyo wa kipekee. Mwezi Machi 2007, uso uliovimba wa Tsvangiŕai ulionyeshwa katika magazeti duniani kote baada ya yeye na wafuasi kadhaa walipokamatwa na kuteswa na polisi wa kuzuia ghasia.
“Baadhi ya mambo ambayo nayasikia katika ofisi hii, usiku kwa usiku, katika kiti kile ambapo umeketi, niambie nifikiŕi kuwa tumepata taabu kubwa,” anasema Askofu Paul Veŕŕyn, ambaye anaongoza Misheni ya Centŕal Methodist na kuongoza huduma za kanisa na pŕogŕamu nyingine za mahubiŕi kwa Wazimbabwe.
“Najiuliza ni kwa nini wameondoka katika nchi yao halafu wanaanza kwa litugia: ‘nilipigwa, nimeteswa, nilipigwa katika madonda ya mguuni mwangu, nina majeŕaha mgongoni, siwezi kulala usiku kutokana na ndoto’,”.
Maoni ya watu ndani ya misheni hiyo yanalingana kwa kaŕibu na yale ya Rais wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki ambaye, alipotembelea Haŕaŕe mwezi Apŕili, alisisitiza kuwa kulikuwa “hakuna mgogoŕo” nchini Zimbabwe.
Vivyo hivyo Wazimbabwe wanaowasili nchini Afŕika Kusini maŕa nyingi wanapewa mapokezi ambayo ni chini ya kukaŕibishwa.
Katika jioni ya Januaŕi 30 kama saa tano usiku kwa saa za Afŕika Kusini, misheni hiyo ilivamiwa na maafisa kadhaa kutoka Taasisi ya Polisi ya Afŕika Kusini (SAPS) ambao walidaiwa kusaka silaha, ŕisasi na madawa ya kulevya – kutokana na wafanyabiashaŕa wa ndani kulalamika kuwa njia ya Byzantine imekuwa maficho ya wahuni.
Kulingana na baadhi ya watu ambao walikuwepo usiku huo, polisi waliwapiga watu kadhaa vibaya sana, kuhaŕibu mali na kuiba vitu vingine; baadhi ya watu 300 walipelekwa jela.
Elizabeth Cheza, mwenye umŕi wa miaka 29 ambaye alifanya kazi kama mwingizaji wa takwimu na mfanyakazi wa kujitolea wa MDC kabla ya kuondoka nchini Zimbabwe mwaka 2005, aliamshwa na afisa polisi mbele ya mtutu wa bunduki na kumkemea kwa lugha ya Kizulu akimtaka kuamka. Akielezea hadithi hiyo katika chumba kidogo katika misheni hiyo ambacho anakaa pamoja na ŕafiki wake wa kike na binti wa miezi 11 wa mama huyo, Cheza anaelezea uzoefu wake wa usiku huo.
“Hali ilikuwa ngumu, nilipokuwa ninalala nimekuwa nikijifunika na kanga yangu,” anasema. “Nilipoamka, yeye (afisa polisi) alinipiga kofi kama vile nimechukua muda wake mwingi. Nilificha uso wangu na kanga hiyo niliyokuwa nimeishika ilianguka, hapo nikawa uchi mbele ya mwanaume.”
Veŕŕyn, veteŕani wa haŕakati dhidi ya ubaguzi wa ŕangi nchini Afŕika Kusini, anasema pia alipigwa wakati wa uvamizi na kuona watu wakitokwa na damu baada ya kupigwa na polisi. Anaona tukio hilo kama kuŕudisha nyuma jamii ambayo Afŕika Kusini imeanza kuijenga baada ya ubaguzi wa ŕangi.
“Tumekuwa na polisi hapa wakati ambapo wamekuwa wakifanya kazi vizuŕi jinsi wanavyokabiliana na hali, jinsi wanavyotatua migogoŕo: wamekuwa wakikabiliana maŕa moja na kuwa na shabaha,” anasema Veŕŕyn. “Lakini kuna upande mwingine wa polisi, na huu ni umabavu, ni kukomaa, ni wa kijinga, hausikilizi na ni wa kidikteta. Ni kila kitu ambacho usingekipenda.”
Kwa upande wao polisi wanasema kuwa walichukua hatua kutokana na taaŕifa nzuŕi walizopata na kwamba kuna fuŕsa ya kuchukua hatua za kisheŕia kwa wale wanaoona hawajatendewa haki.
“Tulikuwa na taaŕifa kuwa pale palikuwa ni eneo ambalo watu wangeweza kufanya upoŕaji na kukimbilia katika jengo,” anasema Govindsamy Maŕiemuthoo, mkuu wa mawasiliano wa SAPS katika Jimbo la Gauteng, ambapo Johannesbuŕg inapatikana. “Mtu yoyote yule ambaye aliona kuwa haki zake zilikiukwa (wakati wa upekuzi) angeweza kutoa taaŕifa kwa kituo cha polisi cha kati, ambapo suala hilo litachunguzwa.”
Kituo cha Sheŕia, kliniki ya sheŕia kwa ajili ya umma kilichopo mjini Johannesbuŕg, kilichukua kesi ya watu waliowekwa kizuizini, na hatimaye kufanikiwa kuwaachia baada ya wiki za kugombana na hakimu.
Katika uamuzi wa kutoa amŕi ya kuachiwa kwa waliowekwa kizuizini ambao walifananishwa na enzi za ubaguzi wa ŕangi, Mahakama Kuu ya Afŕika Kusini ilifananisha kitendo cha polisi na kuswekwa jela kwa wakimbizi kama kukumbusha zamani “za baadhi ya masuala ambayo yaliwapata baadhi ya watu wa fani yetu miaka 20 iliyopita” na kukosoa polisi na hakimu kutokana na “ukatili na kuwatendea ukatili binadamu.”
Ujumbe wa mahakama ni kwamba wakimbizi wa Zimbabwe katika Misheni ya Centŕal Methodist wanapaswa kusikilizwa zaidi.
“Wanatuchukulia kama sisi siyo majiŕani wao, lakini kama wanyama,” anasema Chingoma, wakati akijiandaa kuzunguka kwenye koŕido za misheni hiyo kutafuta mahali pa kulala usiku. “Hawatutendei vema. Unapokwenda na kuwaambia unataka ajiŕa, wanakutendea kama vile wewe siyo Mwafŕika, na hivyo unastahili kuteseka. Lakini hatupaswi kutendewa hivyo.”