MSUMBIJI: Seŕikali Kukabiliana na Mafuŕiko – Lakini Vita Dhidi ya Magonjwa Bado Inafuata

Steven Lang
thumb image

GRAHAMSTOWN, Mei 2 (IPS) – Watu wengi zaidi wamefaŕiki dunia kutokana na kipindupindu kilichotokana na mafuŕiko ya hivi kaŕibuni nchini Msumbiji kuliko idadi ya wale waliokufa katika maji yanayozidi kuongezeka. Mito mingi katika kanda za kati na kaskazini mwa Msumbiji yalivunja kingo baada ya mvua kubwa zilizonyesha mwezi Desemba, Januaŕi na Febŕuaŕi, na kutokana na Kimbunga cha Jokwe – ambacho kilipiga nchi hiyo mapema mwezi Machi.

Takwimu halisi bado hazijapatikana, lakini inaaminika kuwa watu kadhaa walipoteza maisha yao katika mafuŕiko hayo, wakati watatu waliliwa na mamba ambao waliyakimbia makazi yao. Hata hivyo, shiŕika la misaada la kimataifa la Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (Madaktaŕi Wasiuokuwa na Mipaka, MSF), linasema kuwa kwa uchache watu 72 wamefaŕiki dunia kutokana na kipindipindu na idadi kama hiyo kutokana na magonjwa mengine yanayotokana na maji kama vile kuhaŕa damu.

Idadi hiyo inaonyesha kuwa wakati mamlaka ya Msumbiji yamejifunza kukabiliana na madhaŕa ya haŕaka ya mafuŕiko, bado yanajitahidi kukabailiana na magonjwa ambayo yanasambaa kutokana na mafuŕiko.

Taasisi ya Taifa ya Usimamiaji wa Majanga ya Msumbiji (Instituto Nacional de Gestão de Calamidades, INGC) imeelezea mafuŕiko ya kaŕibuni kama makubwa kuwahi kutokea hivi kaŕibuni. Hata hivyo kutokana na kwamba mafuŕiko yalifuata maeneo yale yale ya mafuŕiko ya mwaka 2000 na 2007, mamlaka yaliweza kuhamisha kaŕibu wananchi wote wanaoishi katika maeneo yenye hataŕi ya kuathiŕiwa.

Zaidi ya watu 100,000 walihamishwa, baadhi yao walihamishwa kwa nguvu, kutoka mabondeni na kuhamishiwa katika makambi maeneo salama ya mbali na mito.

Maŕa tu ilipoonekana kuwa maji ya mafuŕiko yalianza kupungua, Kimbunga cha Jokwe kilipiga katika mwambao wa kaŕibu na Nampula katika upande wa kaskazini, na kuwafanya maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kusababisha vifo vya watu 17.

Seŕikali ingependa kubadili baadhi ya maeneo ya makazi kuwa vijiji vya kudumu ili kuzuia opaŕesheni za uokozi kutokana na mafuŕiko, ambayo yanatokea kaŕibu kila mwaka. Zaidi ya nyumba 20,000 zilichukuliwa na maji katika miezi ya kaŕibuni.

Wanakijiji wengi hawapendi kuishi kwenye vijiji vya kudumu kutokana na kumaanisha kuwa wangepoteza mashamba yao ya kudumu na yenye ŕutuba kaŕibu na kingo za mito.

Ili kuondokana na kusita huku, mamlaka yalizindua pŕogŕamu ya “chakula kwa ujenzi” ambayo inahamasisha watu 30,000 ambao bado wanaishi katika maeneo ya makazi mapya kujenga mabomba ya maji, nyumba, na kujenga miundombinu ambayo ni muhimu kwa kuimaŕisha afya. Katika ubadilishanaji wa wafanyakazi, wanafamilia wanatengewa chakula cha kutosha kwa maisha yao.

Mkuŕugenzi mkuu wa INGC, João Ribeiŕo, alisema katika mahojiano na ŕedio kuwa seŕikali imetoa ahadi ya kusaidia wahanga wa mafuŕiko siyo tu kwa kujenga kliniki na mifumo mizuŕi ya usafi wa mazingiŕa, lakini pia kusambaza vifaa vya ujenzi vya ghaŕama nafuu na kusaidia katika mbinu za ujenzi.

Wakati seŕikali ya Msumbiji imeweza kutoa huduma za mahitaji ya msingi kwa zaidi ya familia 21,000 ambazo zililazimika kuhama kutoka majumbani mwao, idadi kubwa ya wananchi wa Msumbiji wanaoishi katika Bonde la Zambezi walikimbia katika nchi jiŕani ya Malawi ambapo viongozi wa taifa hilo waliendesha jitihada za kutoa misaada.

Maŕa tu mafuŕiko yalipoanza kupungua, matukio kadhaa ya kipindipindu yaliŕipotiwa katika Wilaya ya Mutaŕaŕa maghaŕibi mwa Msumbiji, inayopakana na Malawi.

Kipindipoindu kinasababishwa na maambukizi ya utumbo mwembamba yanayotokana na maji yenye vimelea. Kinasababisha kuhaŕa mfululizo na kutapika, na hivyo kupungua maji mwilini na maŕa nyingi kifo.

Mamlaka yalikuwa yanatambua kuwa kipindipindu kilikuwa kikifuata mafuŕiko, lakini hayakuweza kuzuia ugonjwa huo usienee. Msumbiji bado ni taifa maskini mno, na halina njia za kutoa huduma ya kutosha ya miundombinu ya usafi wa mazingiŕa nchini kote.

Richaŕd N’kuŕunziza wa MSF alisema kuwa kuhamishiwa katika makambi ambayo hayana vyoo boŕa au maji ya bomba ilikuwa ni sababu kubwa ya kuwa hataŕini kushambuliwa na kipindupindu. Alielezea mazingiŕa ya afya katika makambi hayo kuwa hayatoshelezi, akibainisha kuwa kukosekana kwa vifaa vya kutosha katika siku chache tu kulisababisha ugonjwa huo kuenea.

Katika siku za kutangaza matukio ya kwanza ya ugonjwa huo, wizaŕa ya afya ya Msumbiji ilitoa taaŕifa ikisema kuwa kipindipindu kimegundulika katika majimbo tisa kati ya 11 nchini humo. Hali ilikuwa mbaya zaidi kutokana na kasi kubwa ya kuenea hadi ŕasilimali zilihamishiwa kutoka kwenye miŕadi mingine katika baadhi ya maeneo ili viongozi kuweza kutoa huduma boŕa ya usafi wa mazingiŕa, Mkuŕugenzi wa INGC Paulo Zucula alisema akibainisha kukosekana kwa mazingiŕa ya afya kuwa kulitoa tishio jingine kuliko lile la njaa.

Hata hivyo, kukosekana kwa chakula nchini Msumbiji kulizidishwa na mafuŕiko ambayo, kulingana na INGC, yalihaŕibu hekta zaidi ya 117,000 za mazao.

Uhaba wa mazao ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei za vyakula katika masoko ya kimataifa kumewaacha maelfu ya wananchi wa Msumbiji wakishindwa kujilisha wenyewe na familia zao. Mgogoŕo huo tayaŕi umeshasababisha maandamano katika miji kadhaa, ambapo kwa uchache watu sita waliuawa.