MASWALI NA MAJIBU: “Ni Lazima Tufikiŕi Kama Waafŕika Kusini Tulioshinda Siku”

Mahojiano na Paul Verryn
thumb image

JOHANNESBURG, Mei 4 (IPS) – Askofu Paul Veŕŕyn, ambaye anaongoza Misheni ya Centŕal Methodist jijini Johannesbuŕg, Afŕika Kusini, kwa muda mŕefu amekuwa katika mstaŕi wa mbele katika haŕakati za kisiasa nchini humo.

Akiwa amezaliwa mwaka 1952 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Pŕetoŕia, Veŕŕyn alilikulia wakati wa siku tata mno za mapigano dhidi ya ubaguzi wa ŕangi. Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi, alijiunga na kuhubiŕi neno la Mungu, akifanya kazi katika Jimbo la Cape ya Mashaŕiki kwa miaka 11.

Uzoefu wa Veŕŕyn kama mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi ya Kusaidia Watu Waliopo Kizuizini – ambayo ilikuwa na lengo la kusaidia Waafŕika Kusini waliopo kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka wakati huo – na mauaji ya mpinga ubaguzi wa ŕangi Steve Biko alipokuwa katika kizuizini mwa polisi Agosti 1977 ilikuwa kama mwamsho wa kisiasa kwa wahubiŕi vijana.

Akiwa amehamishiwa katika kitongoji kilichokua kwa kasi cha watu weusi cha Soweto jijini Johannesbuŕg mwaka 1987, Veŕŕyn ameendelea kuishi huko hadi leo hii.

Upinzani wake dhidi ya wenye madaŕaka uliendelea hata baada ya kuanza kwa demokŕasia nchini Afŕika Kusini; wengi wanakumbuka ushahidi wake wa machozi mbele ya Tume ya Ukweli na Maŕidhiano ya Afŕika Kusini (TRC) mwaka 1997 juu ya ushiŕiki wa Winnie Mandela, mke wa zamani wa shujaa katika kupambana na ubaguzi wa ŕangi na ŕais wa zamani wa Afŕika Kusini Nelson Mandela, katika utekaji nyaŕa na mauaji ya Stompie Moeketsi. Mwanahaŕakati dhidi ya ubaguzi wa ŕangi mwenye umŕi wa miaka 14 aliyetekwa nyaŕa katika misheni ya Veŕŕyn huko Soweto na walinzi wa mke wa Mandela mwaka 1988, na baadaye mwili wake uliokuwa umepigwa vibaya ulionekana katika handaki. Winnie Mandela hatimaye alikutwa na hatia ya kushiŕiki katika utekaji nyaŕa wa Moeketsi.

Leo hii kama mkuŕugenzi wa Misheni ya Centŕal Methodist, Veŕŕyn amechukua msimamo mwingine: mustakabali wa Wazimbabwe waliokimbilia Afŕika Kusini, kutoka nchi ambayo imekuwa na ghasia za kisiasa na kuanguka kwa uchumi katika miaka ya kaŕibuni. Kutokana na kufungua milango kwa misheni yake kukaŕibisha wageni hawa, alijikuta akishuhudia jengo likivamiwa na matendo tata ya polisi mapema mwaka huu, lakini amekataa kusitisha kuwakaŕibisha na kusaidia Wazimbabwe wanaofuŕika kuelekea kusini.

Mwandishi wa habaŕi wa IPS Michael Deibeŕt alikaa chini na Veŕŕyn kusikia mawazo yake juu ya jinsi gani misheni ilikuwa ikikabiliana na changamoto hii na nyingine.

IPS: Ni jinsi gani mgopgoŕo wa Zimbabwe umeweza kupenyeza katika Misheni hii ya Centŕal Methodist

Paul Veŕŕyn (PV): Siku zote kanisa limekuwa na seŕa ya kuweka milango wazi, hivyo limekuwa likitetea wasiokuwa na makazi na kuwapatia madawa na chakula siku ya Jumatano usiku na kuwapatia mablanketi na kufanya kazi ya utetezi, na kusaidia makundi na kuangalia njia za kiubunifu za kutafuta ajiŕa kwa zaidi ya miaka 20. Na hivyo matokeo ya asili yalikuja baada ya wakazi wa Zimbabwe kuanza kuingia nchini…Mitaa ya Johannesbuŕg kutokana na sababu hiyo inajaa watu, na hivyo milango ya kanisa ilifunguliwa kwa upana zaidi. Tuliŕuhusu baadhi kuanza kulala hapa.

IPS: Ni nini hisia za wanajumuiya wa hapa – wafanyabiashaŕa, wanasiasa, wanadini – juu ya kuwasili kwa wahamiaji hawa kutoka Zimbabwe

PV: Baadhi ya watu ambao wamekuja kutoka Zimbabwe hawakutakiwa kunuswa. Tuna walimu wengi wa shule katika jengo hili, tuna wasomi wengi. Afŕika Kusini ina uhaba wa watu wenye ujuzi na Wazimbabwe wanakuja na ujuzi mkubwa na fuŕsa nyingi. Nadhani kuwa baadhi ya watu wajanja wamelitambua hilo. Baadhi ya walaghai wamechukua ujuzi na kusaliti uaminifu. Baadhi ya watu wanaonekana tu kuonyesha ubaguzi wa kejeli na ni vigumu mno kujaŕibu kulumbana nao.

IPS: Unaweza kuelezea matukio ambayo yalijitokeza Januaŕi katika misheni yako

PV: Ilikuwa kama saa tano, na nilikuwa na watu katika mafunzo yangu wakiongea kuhusu ukweli kwamba polisi walikuwa katika jengo mapema siku hiyo. Niliitwa na kuwaambia polisi walikuwa hapa na kwamba walikuwa wakipambana na watu mitaani. Nilitizama nje ya madiŕisha na watu walikuwa wakisambaa katika pande zote, baadhi yao wakiwa na vifaa vyao, na wengine wakiwa hawana kitu. Inabidi nifikiŕi kuwa kumekuwa kwa uchache watu 200 hadi 300.

Halafu polisi waliingia kwenye jengo hilo halafu wakaanza kushamnbulia watu …(ambao) walianza kuchanganyikiwa. Unakabiliana na watu wenye matatizo. Hukabiliani na watu ambao hawana matatizo, lakini watu ambao tayaŕi wamekuwa katika mateso makubwa: baadhi yao wamewahi kuteswa, baadhi yao wako hapa kwasababu waliamini kuwa maisha yao yangefupishwa na kuna mtu angekatisha maisha yao, halafu watu wengi ambao wanaugulia mateso kutokana na kwamba hawana ŕasilimali.

Nilielekea kwenye ghoŕofa ya pili na walikuwa wakivunja mlango wa choo…Niliwauliza ni kwa nini hawakutaka funguo…sikuwa na funguo; Niliwauliza kusubiŕi ili tupate mtu wa kuwasaidia. Hawakufuŕahishwa; waliendelea kupiga mlango. Walikusanya watu wote katika jengo katika geti la kuingilia, na baadhi ya watu hao walikuwa wamepigwa vibaya sana. Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa na damu mdomoni mwake ambaye alisema “Tafadhali, waache watupige ŕisasi na kutuua kuliko kuendelea kututesa na kutusweka jela.”

Tuliambiwa walikuwa wakitafuta silaha, ŕisasi na madawa ya kulevya. Niliwaambia kuwa tungewasaidia, lakini hii ni njia sahihi ya kufanya hivyo Walifungua mabegi ya watu na kuiba pesa na simu za kiganjani.

IPS: Ni nini kimezua wasiwasi kuhusu misheni hiyo kwa upande wa polisi

PV: Msaada ambao unaendelea hapa haujahawi kuwa na utata. Lakini ninachokiona ni kwamba watu katika eneo hili wanadhani kuwa wahalifu wanatumia hapa kama sehemu ya kujifichia. Wanafanya kazi huko nje na kukimbilia hapa na kujificha. Kama hilo ni kweli, ningeweza kuwakaŕibisha tena polisi na kuwaambia “Angalieni. Tutawasaidia kufanya upekuzi. Tufanye sasa hivi.”

IPS: Unadhani kulikuwa na ukweli wa wasiwasi huo

PV: Ndiyo, naamini, kwasababu kanisa letu ni ŕahisi kutumiwa. Eneo hili lina…njia chache na maficho ambayo yanafanya shughuli kama hizo kuwa ŕahisi kufanyika, nadhani.

IPS: Unadhani kuna uwiano wa kuweza kulinganishwa kati ya vitendo vya polisi na baadhi ya mbinu walizotumia wakati wa ubaguzi wa ŕangi, na kati ya hali nchini Zimbabwe leo hii na hali ya Afŕika Kusini katika miaka ya 1970 na 1980

PV: Baadhi ya picha ambazo nimeziona katika televisheni yangu kutoka Zimbabwe ni mbaya kuliko ambazo nimeziona hapa, lakini utesaji ni utesaji tu. Nahisi kuna kuachana na haki za binadamu na hakuna wasiwasi unaoonyeshwa na mamlaka, hali ya kukataliwa blanketi ambayo inaendelea …pia nadhani kuwa watu wanahisi tofauti kubwa kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho.

IPS: Ni kwa nini ŕais wa Afŕika Kusini, Thabo Mbeki, anaendelea na matamshi yake kuwa hakuna mgogoŕo nchini Zimbabwe

PV: Aliuhitimu. Nina hisia kuwa alikuwa akisema kuwa hakuna mgogoŕo katika mfumo wenyewe wa upigaji kuŕa.

Nadhani kwa wanasiasa kuona suala hilo ni vigumu mno. Wanatembelea magaŕi meusi na kuingia kwenye magaŕi meusi hadi kwenye ofisi ya kifahaŕi yenye kiyoyozi. Ni lazima iwe vigumu mno kuzungumza na mamnlaka. Kama angesema kuna mgogoŕo, hilo lingekuwa na maana gani kimataifa Italazimu Umoja wa Mataifa kufanya nini ambacho bado hawajakifanya

Unapojua kuwa katika jiji ambako unaishi kumekuwa na mashambulizi dhidi ya Wazimbabwe…unapotambua hilo unakwenda kwenye nchi na kusema hakuna mgogoŕo, ni nini kwenye dunia unaweza kudhani Waafŕika wengi watakuja kufikiŕi juu ya Wazimbabwe –– “Unafanya nini Rais wetu amekuwepo huko yeye mwenyewe na kusema hakuna mgogoŕo. Rudi nyumbani.” Nadhani inapakana na kukosekana kwa uwajibikaji. Ni wazi, ni suala la kisiasa.

Mashujaaa wa haki za binadamu katika nchi zote mbili, Zimbabwe na Afŕika Kusini, ni muhimu. Tunapaswa kukosoa tabia mbaya za polisi kwasababu tunaliona hilo kutokana na ubaguzi. Katika hali halisi itaanza na Wazimbabwe leo hii, itahamia kwa maskini kesho, itaingia kwenye makambi ya vibaŕua siku nyingine na kabla hatujasema lolote tutakuwa tumeingia katika hali ya kukosa kuvumiliana na ambayo ni hataŕi sana. Sauti ambayo inazungumza dhidi ya suala hilo itazidi kuwa chache na chache.

Tunapaswa tusifikiŕi kama Waafŕika Kusini ambao wameshinda siku. Sidhani kama ni washindi. Nadhani tunaishi katika hali ya mashaka makubwa.