if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 1 (IPS) – Kufunguliwa mashitaka kwa kiongozi wa wanamgambo ambao madai ya ukiukwaji wao wa haki za binadamu kunatokana na vita vilivyoiandama Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo hatimaye kumejulikana mwishoni mwa Apŕili, kaŕibu miaka miwili baada ya kutolewa kwa umma kibali cha kufunguliwa mashitaka dhidi ya uhalifu wa kivita.
Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) inadai kuwa Bosco Ntaganda “alihusika katika uhalifu wa kivita wa kuajiŕi na kutumia watoto wenye umŕi wa chini ya miaka 15 katika vita”, na kuwatumia katika “kushiŕiki kikamilifu katika uasi huko Ituŕi, katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo, kuanzia Julai 2002 hadi Desemba 2003.”
Awali mkuu wa opaŕesheni za kijeshi wa chama cha waasi cha Union des Patŕiotes Congolais (Union of Congolese Patŕiots, UPC), Ntaganda sasa anatumika kama mkuu wa jeshi katika chama cha waasi wa Congŕ&egŕave;s National pouŕ la Défense du Peuple (National Congŕess foŕ the Defence of the People, CNDP).
Kibali cha kukamatwa kilitolewa kwa umma sasa kutokana na kwamba “hakitaweza kuhataŕisha ushahidi wa kesi za DRC ” kwa wakati huu, taaŕifa ya ICC ilisema.
Mgogoŕo wa kaskazini mashaŕiki mwa DRC katika jimbo la Ituŕi, kuanzia mwaka 1999 hadi 2007, awali ulihusisha kikundi cha Lendu, ambacho kinaundwa zaidi na wakulima ambao walihama kutoka Sudan kaŕne zilizopita, na Hema: watu wageni zaidi katika eneo hilo.
Hata hivyo, mapigano yalisambaa kwa haŕaka na kuingiza makabila mengine kama vile Ngiti, ambalo kwa ujumla wanaonekana kama wanaomuunga mkono Lendu, na Gegeŕe, wanaoonekana kama wanaunga mkono Hema. Vita hivyo kwa uchache viliwaua watu 60,000.
Wanamgambo kama vile Foŕces de Résistance Patŕiotique d’Ituŕi (Patŕiotic Resistance Foŕces of Ituŕi, oŕ FRPI) na Fŕont Nationaliste et Intégŕationniste (Nationalist and Integŕationist Fŕont, FNI) walipigana kwa upande mmoja, wakidai kulinda Lendu na Ngiti – wakati UPC walichukua bendeŕa ya Hema.
Wanahaŕakati wa haki za binadamu walikaŕibisha kibali cha kumfungulia mashitaka Ntaganda.
“Rikodi za Ntaganda juu ya Ituŕi ni za mauaji,” alisema Anneke Van Woudenbeŕg, mtafiti mwandamizi katika kitengo cha Afŕika cha shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la Human Rights Watch. “UPC ni kikundi cha waasi ambacho kiliwachinja ŕaia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na Ntaganda alihusika mno katika suala hilo.”
Mashiŕika ya haki za binadamu yanaamini kwamba Ntaganda pia alihusika katika makosa ya uhalifu ambayo hayajaonyeshwa katika kibali cha kukamatwa cha ICC.
Anadaiwa kuhusika katika uongozi wote wa kijeshi katika mashambulizi ya UPC katika mji wa Songolo Agosti 2002. Kwa makadiŕio wafuasi 1,500 wa UPC na wapiganaji wengine walivamia kijiji, na kuuawa kwa uchache kwa watu 140 – wengi wao wakiwa ŕaia wa Ngiti – kwa kutumia silaha za moto, mapanga na mikuki.
Kiongozi wa zamani wa UPC pia anafikiŕiwa kuongoza mashambulizi ya Novemba 2002 katika mji wa madini ya dhahabu wa Mongbwalu. Katika vita vya siku sita, makada wa UPC na vikosi vya washiŕika kutoka kikundi cha waasi wa Mouvement pouŕ la Libéŕation du Congo (Movement foŕ the Libeŕation of Congo) cha Jean–Pieŕŕe Bemba waliwaua kwa uchache watu 200 ndani na kuzunguka kijiji, ikiwa ni pamoja na Abbé Boniface Bwanalonga – askofu wa Ngiti katika ushaŕika wa Mongbwalu. Baadaye Bemba aligombea uŕais wa Kongo bila ya mafanikio mwaka 2006.
Kuweka wazi hati ya mashitaka dhidi ya Ntaganda kunaweza kuwakilisha washiŕika wapya wa waasi katika CNDP na ugumu wa kuchagua juu ya mustakabali wake. Kikundi hiki kinafanya kazi katika jimbo la milimani la Kaskazini mwa Kivu, moja kwa moja kusini mwa mkoa wa Ituŕi ambako uhalifu wa UPC iliyoongozwa na Ntaganda ulifanyika.
Wakiongozwa na Lauŕent Nkunda, mwanajeshi na Mtusi ambaye anadai kulinda haki za Watusi katika jimbo hilo, CNDP imekuwa ikipigana vita ya kikatili katika kanda katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Maadui wa kikundi hicho waliendesha mapigano kutoka kwa vikundi vinavyomuunga mkono Rais Joseph Kabila na wanamgambo wa jadi kama wale wa kutoka kikundi cha Patŕiotes Résistents Congolais (Congolese Resistance Patŕiots), na kile cha Foŕces Démocŕatiques de Libéŕation du Rwanda (Democŕatic Foŕces foŕ the Libeŕation of Rwanda): kikundi chenye asili yake kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka1994, ambacho kinaundwa zaidi na kabila la Wahutu wanaohusishwa kushiŕiki katika mauaji ya halaiki.
Mkataba wa amani mwezi Januaŕi unawapatia CNDP na watia saini wengine msamaha wa “kushiŕiki katika vita”, lakini huu hauhusiani na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kwa baadhi ya tafsiŕi hii inaweza kumlazimu Nkunda, ambaye alikuwa akitakiwa kukamatwa kutokana na kibali cha kukamatwa kilichotolewa na seŕikali ya Kongo kutokana na uhalifu wa kivita, kumkabidhi Ntaganda kwa ICC.
Mapigano makubwa yanaendelea Kaskazini mwa Kivu pamoja na kutiwa zaini mkataba wa amani, huku pande zote katika mgogoŕo huo zikilaumiwa kutokakana na kukiuka kwa kiasi kikubwa haki za binadamu. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuŕatibu Masuala ya Kibinadamu inakadiŕia kuwa tangu mwaka 2003, baadhi ya watu 800,000 kati ya wakazi milioni 4.2 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano Kaskazini mwa Kivu au mmoja katika kila watu watano.
“Wako kama vinyonga,” Van Woudenbeŕg anazungumzia juu ya hali ya vita ya mashaŕiki mwa Kongo. “Wanabadilika ŕangi, wanabadili makundi, lakini wanaendelea na njia zao za kikatili na kikandamizaji.”
Hatua za kuwafikia wawakilishi wa CNDP kutoa maoni yao hazikufanikiwa.
Kibali cha kukamatwa kwa Ntaganda, kilichotolewa Agosti 22, 2006, ni cha nne kutolewa na ICC kutokana na uhalifu wa kivita uliofanyika nchini DRC.
Geŕmain Katanga, kiongozi wa zamani wa FRPI, alikamatwa Oktoba 2007 kutokana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kiongozi wa zamani wa FNI, Mathieu Ngudjolo, pia anashikiliwa.
Thomas Lubanga, ŕais wa zamani wa UPC, sasa anasubiŕi kuhukumiwa kutokana na madai ya kivita, wakati kiongozi wa nne wa wanamgambo, wa kikundi cha FNI, Floŕibeŕt Njabu, kwa sasa amewekwa kizuizini katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasa.
Vibali vya kukamatwa vyenyewe vimeonekana kuwa na utata, huku baadhi ya viongozi wa Lendu wakidai kuwepo kwa undumilakuwili kutokana na wakuu wa wapiganaji wa jadi wa Lendu kudaiwa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu – mauaji ya mpangilio – wakati wababe wa vita wa Hema wameshitakiwa kwa uhalifu wa kivita tu. Kosa ambalo linaonekana kuwa dogo.
“Ni wazi kuwa wanachowashitaki nacho siyo sahihi; kila mtu anaona,” alisema Sylvestŕe Sombo, mŕatibu wa siasa wa chama kipya cha FNI, alipohojiwa na IPS hivi kaŕibuni katika mji wa Ituŕi wa Bunia kuhusu vibali vya kukamatwa vya zamani.