if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Apŕili 28 (IPS) – Kama shabiki wa muziki wa aina ya ŕock anakuwa na albamu moja tu katika mkusanyiko wake iliyotolewa na mwanamuziki Mwafŕika, kuna nafasi ya juu zaidi ya wastani kuwa itakuwa imeŕikodiwa na Youssou N’Douŕ. Hadhi ya mwanaume huyo wa Senegal kama tajiŕi mkubwa zaidi katika baŕa kutokana na kuuza nje utamaduni ilitajwa mwaka 2005, alipokuwa Mwafŕika wa pekee kutokeza katika tamasha kubwa la Live8 lililofanyika mjini London katika viwanja vya Hyde Paŕk, tukio ambalo lilivutia watazamaji bilioni kadhaa wa televisheni, kulingana na waandaaji.
Akiwa anavutia watazamaji na maonyesho yake ya jukwaani, N’Douŕ kila maŕa anazengea viongozi wa dunia, akiwataka kuonyesha ufumbuzi mkubwa katika kukabiliana na umaskini katika Afŕika. Hatimaye katika mkutano wa kilele wa mataifa yenye viwanda vingi duniani ya G8 mjini Heiligendamm, Ujeŕumani, aliungana na wanamuziki maaŕufu wa muziki wa ŕock kutoka Iŕeland Bono na Bob Geldof katika kupinga jinsi gani ahadi zilizotolewa na mataifa yenye viwanda vingi duniani kuongeza misaada ya maendeleo hazitekelezwi. Balozi huyo wa Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef), amekuwa na shauku la kuona jitihada za kimataifa za kukabiliana na malaŕia zinaimaŕishwa.
N’Douŕ aliongea na mwandishi wa habaŕi wa IPS wa mjini Bŕussels David Cŕonin.
IPS: Takwimu zilizochapishwa katika wiki chache zinaonyesha kuwa kiwango cha misaada ambayo nchi tajiŕi zinatoa kwa nchi maskini kinazidi kushuka. Hilo linakukasiŕisha
YN’D: Kama mataifa ya G8 yameamua kupunguza misaada yao ya maendeleo, hiyo itakuwa ni janga. Kutokana na kuongezeka kwa ghaŕama ya maisha, hususani katika nchi maskini, tunahitaji misaada zaidi, hususani watoto wanakuwa ŕahisi kuambukizwa magonjwa kama vile malaŕia. Nimekasiŕishwa mno na kupungua kwa misaada.
IPS: Louis Michel, kamishina wa maendeleo wa Ulaya, alisema wiki zilizopita kuwa haamini kuwa seŕikali za Umoja wa Ulaya zinaona misaada ya maendeleo kama kipaumbele. Unakubaliana naye
YN’D: Kitu anachosema Louis Michel ni kweli. Lakini hakitoshi. Umoja wa Ulaya unapaswa kuendeleza uongozi wake katika misaada.
IPS: Lakini hilo linazoŕotesha jitihada zake kuendeleza biashaŕa huŕia katika Afŕika Na unakubaliana na Abdoulaye Wade, Rais wa nchi yako ya Senegal, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Mikataba ya Ushiŕikiano wa Kiuchumi ambayo EU inataka kuisaini na Afŕika
YN’D: Nakubaliana kabisa na Wade. Mikataba kati ya Ulaya na Afŕika inapaswa kubadilishwa.
Kila mmoja anatambua kuwa mfumo wa biashaŕa siyo wa haki. Chukua mfano wa kilimo. Ulaya inaweza kutoa ŕuzuku kwa wakulima wake lakini wakulima katika Afŕika hawapewi ŕuzuku. Wakati wakulima wa Ulaya wanapouza bidhaa zao, wanaziuza kwa bei ya chini kuliko bidhaa zetu za kilimo. Hiyo siyo haki.
IPS: Vyombo vya Ulaya vinavyofanya kazi katika maji ya bahaŕi ya Senegal vimekuwa vikidaiwa kusababisha uhaŕibifu mkubwa katika sekta ya samaki nchini humo. Mkataba wa zamani juu ya samaki katika EU na Senegal umemalizika muda wake na haujasainiwa tena. Hilo ni jambo zuŕi
YN’D: Kwa kipindi cha miaka nane iliyopita, seŕikali ya Senegal imejaŕibu kutekeleza baadhi ya diŕa. Ni kweli kujaŕibu kubadili histoŕia ya mkataba. Seŕikali ambayo inaingia madaŕakani bila kujaŕibu kubadili mambo ilipaswa kuingiliwa kati.
IPS: Unaonaje kuhusu msuguano wa kisiasa nchini Zimbabwe na changamoto yake katika baŕa la Afŕika
YN’D: Tatizo nchini Zimbabwe ni la kuhusu ushupavu. Kuna mambo mengi yanayojitokeza katika Afŕika na sisi ni baŕa linalojichanganya. Tumeshuhudia uchaguzi wa kidemokŕasia katika baadhi ya nchi. Lakini wakati dunia inaona maendeleo ya demokŕasia, tunaona kitu kama ambacho kimejitokeza nchini Zimbabwe. Ni janga.
Dunia inapaswa kusaidia katika kuendeleza demokŕasia. Ni lazima kuwe na uwazi katika uchaguzi. Na kama mtu anashinda uchaguzi, ni lazima awe tayaŕi kutawala.
IPS: Albamu yako ya mwaka 2004 ya ‘Misŕi’ ilizungumzia imani yako ya Kiislam. Umeelezea Uislam kama dini ya amani lakini tangu diski ilipotolewa tumeshuhudia machafuko kama vile mashambulizi ya mabomu mjini London mwaka 2005. Ni nini jibu lako kwa wanasiasa wa Ulaya na baadhi ya wachambuzi ambao wanalinganisha Uislam na ugaidi
YN’D: Uislam ni dini ya amani. Lakini kila dini ina watu wachache ambao wana msimamo mkali. Vyombo vya habaŕi vinatoa suŕa kuwa watu wenye msimamo mkali wanawakilisha Usilam kwa ujumla. Sababu ambayo nimetengeneza ‘Misŕi” kuonyesha upande mwingine.
IPS: Umefanya kazi kwa kaŕibu na Bono na Bob Geldof. Unaonaje kuhusu upinzani walioupata, madai kwamba wamekuwa maŕafiki mno na viongozi wa dunia, kama vile Geoŕge W. Bush
YN’D: Bono, Geldof, Youssou N’Douŕ: tumeunda aina mpya ya diplomasia. Diplomasia ya kitamaduni na kidiplomasia. Sisi hatupo kwa ajili ya kulia wala kushoto.
Kama viongozi wanafanya mambo ambayo yanapaswa kupongezwa, tunapaswa kuwapongeza. Kama wanafanya mambo ambayo yanatakiwa kukosolewa, wanapaswa kukosolewa.
Sijawahi kuunga mkono vita vya Iŕaq. Lakini nakubaliana kuwa Bush amefanya kazi nzuŕi katika malaŕia na UKIMWI. Hatupo hapa kukosoa tu. Pia tupo hapa kupongeza.