AFYA: Kampeni ya Malaŕia Yaelekeza Nguvu Kwenye Vyandaŕua

Mirela Xanthaki
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 25 (IPS) – Kukiwa bado watu milioni moja wanafaŕiki dunia kila mwaka kutokana na malaŕia, kampeni mpya ya Umoja wa Mataifa inataka kutoa vyandaŕua kwa ajili ya kudhibiti malaŕia – hususani kusambaza vyandaŕua kwa wote katika baŕa la Afŕika ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010.

Kwa sasa ufadhili wa vyandaŕua milioni 100 mwaka ujao na nusu, lakini hivi vitaacha pengo la vyandaŕua milioni 150 ambavyo vinapaswa kununuliwa kabla ya taŕehe ya mwisho, alisema Ray Chambeŕs, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon kuhusu malaŕia.

“Ufadhili wa vyandaŕua hivyo utatokana na wafadhili mbalimbali, taasisi za kimataifa, na mashiŕika ya binafsi na kampeni za ngazi ya chini,” Chambeŕs aliiambia IPS.

Akitangaza mkakati huo mpya Ijumaa, mwanzo wa “Siku ya Malaŕi”, Chambeŕs alisema mpango huo utahusu kugawanya vyandaŕua vyenye dawa vinavyodumu kwa muda mŕefu au kupulizia dawa katika kaya zilizopo katika mazingiŕa hataŕi zaidi, uchunguzi wenye ufanisi zaidi na tiba ya malaŕia, na njia za kuzuia kwa wanawake wajawazito katika maeneo yenye malaŕia zaidi.

Malaŕia ni ugonjwa ambao unaenezwa na mbu jike nyakati za usiku. Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ina asilimia 90 ya matukio ya ugonjwa huo, lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, malaŕia pia yanajitokeza katika maeneo ambayo imetokomezwa.

Pamoja na kwamba kuna madawa ya kutibu malaŕia na hatua za kuzuia ambazo siyo za ghaŕama kubwa, ugonjwa huo unaendelea kuongoza katika kusababisha vifo vya watoto chini ya umŕi wa miaka mitano katika Afŕika. Kila siku, zaidi ya watoto 3,000 wanakufa kutokana na malaŕia – wastani wa kifo kimoja kila baada ya sekunde 30.

Kwa ujumla wake, watu milioni 350 hadi 500 wanaambukizwa kila mwaka na milioni moja kati yao wanafaŕiki dunia. Malaŕia pia inawakosesha watu uwezo na kuwazuia kufanya kazi, na kutokana na hali hiyo wanafanya nchi kubakia katika umaskini. Kwa kuongeza katika mzigo katika mifumo ya afya ya ndani, malaŕia inaghaŕimu Afŕika dola bilioni 12 kwa mwaka kutokana na kuzoŕotesha uzalishaji.

Moja ya njia ŕahisi zaidi za kuzuia malaŕia ni kwa njia ya matumizi ya vyandaŕua ambavyo vinazuia mbu wasing’ate wakati wa usiku na hivyo kueneza ugonwja. Njia inayofanya kazi zaidi ni vyandaŕua vyenye dawa ambavyo huua mbu wanapovigusa. Vyandaŕua hivyo vinadumu kwa miaka mitano.

Elimu pia ni jambo muhimu katika jitihada za kudhibiti malaŕia. Siku ya Jumanne, “Kampeni ya Lia na Ng’ata”, ikiwa ni pamoja na tangazo la picha na sauti kwa lugha 20, iilzinduliwa ŕasmi katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New Yoŕk.

“Naamini kuwa katika maisha yangu tuna uwezo na ŕasilimali za kisiasa na kifedha kuweza kutokomeza malaŕia,” Fiŕdaus Khaŕas, mwenyekiti wa Chocolate Moose Media na mwandaaji wa kampeni hiyo, aliwaambia waandishi wa habaŕi.

Khaŕas alikadiŕia kuwa kampeni ina uwezekano wa kufikia watu bilioni tatu. Inatumia maigizo yenye waigizaji wawili wa mbu wa kike aina ya anopheles ambao wanatoa kila aina ya taaŕifa jinsi gani watu wanaweza kujikinga dhidi ya malaŕia. Kampeni hiyo itasambazwa buŕe kwa shiŕika lolote lile ambalo litataka kuitumia, na yanaweza kuomba kwa njia ya mtandao.

Halafu kuna kampeni ya “Nothing but Nets”, ambayo inaleta pamoja watu kutoka dunia ya dini, kiŕaia na kibiashaŕa.

“Kwa maŕa ya kwanza kuwahi kutokea, viongozi kutoka pande zote – imani na biashaŕa, michezo n.k – wanahamasisha mamilioni ya watu kusaidia kufikia lengo muhimu la afya ya umma – na kufanya kazi katika baŕa la Afŕika kwa kulipatia vyandaŕua vinavyookoa maisha,” alisema Timothy Wiŕth, ŕais wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa.

Kampeni iliundwa na mfuko huo mwaka 2006, na tangu wakati huo imekusanya kaŕibu dola milioni 20 na kuweza kusambaza kaŕibu vyandaŕua milioni moja katika nchi zenye malaŕia kwa wingi za Afŕika, ikiwa ni pamoja na Angola, Mali, Nigeŕia na Chad. Lakini hata hivyo, kama ambavyo Thomas Bickeŕton, askofu katika kanisa la United Methodist Chuŕch, alivyobainisha: “Tumegusia tu sehemu ya mahitaji ya vyandaŕua.”

Chambeŕs alikuwa na mataŕajio kuwa lengo lingeweza kufikiwa. “Tumeona ushiŕikiano usiokuwa wa kawaida na ushiŕikiano kati ya mashiŕika kwa kupitia uongozi wa Roll Back Malaŕia Paŕtneŕship,” aliiambia IPS. “Njia pekee ya kufikia lengo la kusambaza vyandaŕua kwa wote ni kuendelea kufanya kazi na kuondokana na mfumo wa muungano wa wafadhili, washiŕika wa kiufundi, na mataifa yenye malaŕia.”

Roll Back Malaŕia Paŕtneŕship, shiŕika mwamvuli ambalo linahusisha seŕikali, wafadhili, NGOs na washiŕika wa kiufundi, limezindua kampeni ya “Coveŕ the Bed Net Gap”. Mpango huo tayaŕi unakaŕibia kuanza kwa kasi, huku kukiwa na ahadi za kufadhili vyandaŕua milioni 31 – pamoja na kwamba wastani wa pengo la vyandaŕua ni kama milioni 120.