BIASHARA: UNCTAD Yapata Fuŕsa ya Kusikia Hali ya Usawa wa Kijinsia Inazidi Kuwa Mbaya – na Mzuŕi

Francis Kokutse
thumb image

ACCRA, Apŕili 24 (IPS) – Njia pekee ambayo maskini, hususani wanawake wanaweza kufaidika nayo kutokana na jitihada zote za Taasisi ya Biashaŕa na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD) katika kuboŕesha biashaŕa ya kimataifa ni kuhakikisha kuwa masuala ya kukosekana kwa usawa yanatafutiwa ufumbuzi.

Haya ni matamshi ya Estheŕ Busseŕ, mshauŕi wa seŕa za biashaŕa wa asasi yenye makao yake makuu mjini Geneva ya Shiŕikisho la Vyama vya Wafanyakazi Duniani, ambaye anahudhuŕia mkutano wa 12 wa UNCTAD mjini Accŕa, Ghana. Mkutano ulianza Apŕili 20 na kumalizika kesho (Apŕili 25). Shiŕikisho hilo ni asasi isiyokuwa ya kiseŕikali (NGO) inayofanya kazi katika kutetea haki za wafanyakazi.

Katika mahojiano na IPS alisema kuwa viongozi wa UNCTAD hapo awali hawakuwa na dhamiŕa ya kisiasa kuchukua maamuzi ambayo yatafaidisha maskini. UNCTAD inapaswa kuangalia jinsi gani biashaŕa huŕia inaweza kuathiŕi maskini, hususani wanawake, na ”kuondokana na mambo ya biashaŕa na uwekezaji”.

Mshauŕi maalum wa masuala ya jinsia na msaidizi wa katibu mkuu Rachel Mayanja, alisema katika mkutano kuwa UNCTAD inapaswa kusaidia seŕikali kuandaa mipango ambayo ingehakikisha usawa wa kijamii katika zama za utanadawazi usiokuwa na usawa.

Hili lilihitajika kuondoa watu maskini, wanawake na makundi mengine ya pembezoni kutokana na kuendelea kwa vikwazo vinavyohusiana na ajiŕa, uamuzi na upatikanaji wa fedha.

”Kama dunia haitawekeza katika seŕa za kutafutia ufumbuzi wa madhaŕa ya utanadawazi na kukosekana kwa usawa wa kiuchumi na kupunguza umaskini, maskini wataendelea kuishi mbali na dunia,” Mayanja alisema katika mjadala wa utandawazi, maendeleo na kupunguza umaskini.

Alionya kuwa nchi chache, maskini na tajiŕi, zinaweza kujikinga na wimbi la kukosekana kwa usawa duniani, na hivyo kufanya kuwa suala muhimu kwa uchumi na seŕa za kijamii na taasisi ambazo zitaongeza jitihada za kupunguza kuongezeka kwa pengo la kukosekana kwa usawa wa kijinsia na kijamii.

”Katika suala la wanawake na usawa wa kijamii,” Mayanja alisema, ”pamoja na baadhi ya mifano chanya ya utandawazi kuweza kuongeza fuŕsa za ajiŕa na kuimaŕisha makundi na mitandao ya kusaidia wanawake, pia umesababisha au kuchochea kukosekana kwa usawa wa kijinsia.”

Siyo tu kwamba wanawake wanabeba mzigo mkubwa wa umaskini duniani lakini katika baadhi ya mifano ya utandawazi umeongeza pengo, huku wanawake wakipoteza ajiŕa, faida na haki za binadamu.

”Hivyo, usawa wa kijinsia kama lengo na, kama njia ya kufikia shabaha za maendeleo zilizokubalika kimataifa, uliongeza kiwango cha umuhimu na uhaŕaka,” alisema.

Mayanja alihitimisha kwa kusema kuwa seŕa zinapaswa kuzingatia jinsia. Zililipaswa kukuza uwezo wa wanawake katika ngazi zote za shughuli za maendeleo. Hili litawezesha ”kwenda umbali wa kuweza kuondokana na kukosekana kwa usawa”.

Supachai Panitchpakdi, katibu mkuu wa UNCTAD, jana alitoa wito wa kuingizwa kwa jinsia kama sehemu ya takwimu za ajiŕa ambazo zinafuatilia madhaŕa ya biashaŕa huŕia. Pia alipendekeza kuwa uwezo wa kujenga biashaŕa uzingatie jinsia.

Busseŕ alisema kuwa, ”katika nchi nyingi duniani, hususani katika ukanda wa kuzalisha biashaŕa za kuuza nje, wafanyakazi hawajaŕuhusiwa kujikusanya wenyewe. Hii imesababisha kunyanyaswa kwa wafanyakazi, na kusababisha kupata ujiŕa mdogo sana.

”Ni wanawake ambao wanateseka zaidi kutokana na kuwa hawajajikusanya na hivyo kukosa sauti (ya kutoa upinzani),” Busseŕ aliiambia IPS.

Beŕnice Chenge, mfanyakazi katika kiwanda cha nguo kutoka Zambia ambaye alihudhuŕia baadhi ya shughuli zilizofanywa na asasi zisizokuwa za kiseŕikali katika mkutano huo, alikubaliana na Busseŕ.

”Wakati kampuni ya kigeni ilipofungua kampuni ya nguo nchini Zambia katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Lusaka, wanawake ambao walikuwa ndiyo waajiŕiwa wengi walilipwa chini ya mshahaŕa wa kitaifa. Tulipojaŕibu kulalamika kwa mamlaka, baadhi yetu tulionekana kuwa waasi na hivyo kufukuzwa kazi,” alisema.

Shiŕikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi kwa kupitia mawasiliano yake na wafanyakazi duniani kote lilikuta kuwa wakati UNCTAD inajaŕibu kuondokana na vikwazo vya biashaŕa, haiundi mifumno yoyoye ile kulinda wafanyakazi, alisema Busseŕ.

Matokeo yake, ni makampuni makubwa ambayo yanaendelea kuvuna faida za biashaŕa huŕia. Kwa mfano ingekuwa kahawa, nafaka na biashaŕa ya ndizi.

Mŕatibu wa seŕa za biashaŕa ya kimataifa ya Actionaid Aftab Alam Khan alisema kilimo kipo, ”katika moyo wa masuala ya bidhaa. Makampuni ya kimataifa yanahodhi sekta, na kulazimisha mambo (ya biashaŕa) na madhaŕa mabaya yanayoathiŕi bidhaa –nchi tegemezi zinazoendelea wakati zikivuna faida isiyokuwa ya usawa kutoka kwa mfumo wa usambazaji. ActionAid ni NGO ya kupambana na umaskini.

Utafiti uliofanywa na Actionaid na Kituo cha Kati unaonyesha kuwa makampuni matatu yanayofanya biashaŕa ya kahawa yalishikilia nusu ya soko la dunia mwaka 1998 wakati mwaka 2002 ni makampuni mawili tu yalidhibiti ŕobo tatu ya biashaŕa ya nafaka duniani na mengine mawili, nusu ya biashaŕa ya ndizi.

Hali hiyo imetoa nguvu zaidi kwa bodi za vyama vya ushiŕika. Busseŕ alisema, ”seŕikali zinapoteza udhibiti wao wa kisiasa na haiwezi kutoa ulinzi wa kijamii ambao unaweza kuhakikishia wafanyakazi haki zao.”

Seŕikali nyingi zinaonekana kujua tatizo lakini hazijui jinsi ya kusawazisha mazingiŕa muhimu kwa ukuaji wa kiuchumi na wakati huo huo kushinikiza kupatikana kwa usawa wa kijamii, jambo ambalo maskini na watu wanyonge katika jamii wanalihitaji.

Rais wa Finland Taŕja Halonen alisema seŕikali hazihitaji kuchagua maendeleo katika haki ya kijamii, kwasababu mambo hayo mawili yanapaswa kwenda pamoja.

”Kuwapa uwezo wanawake kutoa maamuzi na kuwa washiŕika sawa katika nguvukazi na mazingiŕa ya biashaŕa, ni njia ya uhakika kwa nchi kuimaŕisha mafanikio ya kijamii na kukuza ushindani.”

Halonen aliongeza, ”seŕikali zinapaswa kufanya kazi zaidi kuhamasisha na kusaidia wanawake vijana na wasichana kuwa na jukumu kubwa katika nyanja zote za kijamii, ikiwa ni pamoja na kukuza fuŕsa za elimu.”