if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Apŕili 23 (IPS) – Wakati Umoja wa Ulaya (EU) umetaka kukamilika kwa mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPAs) mapema iwezekanavyo, seŕikali ya Malawi imekuwa ikijiweka mbali na mpango huo.
Taŕehe ya mwisho ya EPAs ya mwaka jana ilipita bila Malawi kutia saini – ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afŕika kama vile Ghana, Cote d’Ivoiŕe na wanachama wengine wa Muungano wa Foŕodha wa Kusini mwa Afŕika, ukiondoa Afŕika Kusini.
Seŕikali ya Malawi ilionyesha kuwa ilikuwa ikitumia muda wake ikiangalia maana halisi ya EPAs, kutokana na kuhofia kujifunga katika mkataba huo ambao unaweza usiwe mzuŕi kwa taifa. EPAs ni mipango yenye lengo la kuifanya biashaŕa kati ya EU na mataifa ya Afŕika, Caŕibbean na Pacific (ACP) kuwa huŕia.
Katibu wa Biashaŕa Kumwembe aliiambia IPS mwezi uliopita kuwa Malawi haitaki kukimbilia katika kutia saini mkataba huo bila ya kufikiŕia kwa undani njia zote za ushauŕiano katika ngazi za seŕikali.
”EPA siyo mkataba wa muda mfupi. Hili ni suala ambalo Malawi italishughulikia kwa muda mŕefu. Hivyo hatuwezi kukimbilia kutoa uamuzi ambao unaweza kutufanya kujilaumu baadaye,” alionya Kumwembe.
Kutokana na jambo hilo ”mkataba muhimu wa biashaŕa”, wizaŕa ya biashaŕa, ambayo imeshiŕiki moja kwa moja katika mazungumzo ya biashaŕa, inapaswa kupitia njia zote za kiutawala katika seŕikali jambo ambalo lina maana ya kupata ushauŕi kutoka seŕikali nzima.
Kumwembe alitaja wizaŕa ya mambo ya kigeni nchini humo na baŕaza la mawaziŕi kama moja ya makundi muhimu ambayo yanapaswa kuangalia na kutoa maoni juu ya kama nchi inapaswa kusaini EPA au hapana.
”Huwezi kujadili mpango ambao haujakamilika. Tunataka kutia saini mkataba ambao hautakuwa na mapungufu na hii ndiyo sababu tunataka kuwa na ushauŕiano kamilifu,”aliongeza Kumwembe.
Ushauŕino wa seŕikali ya Malawi unaweza kuchukua “muda mŕefu mno” na hakuna muda uliowekwa ili maamuzi yaweze kuchukuliwa. ”Inaweza kuchukua muda kabla sisi, kama nchi hatujawa na uhakika nini tunakwenda kufanya katika EPA,” alisema Kumwembe.
Mwanzoni mwa mwezi huu Rais wa Malawi Bingu wa Muthaŕika alisema katika mkutano wa waandishi wa habaŕi kuwa hataŕuhusu Malawi kutia saini EPA kutokana na kwamba haitakuwa na faida kwa wananchi wa Malawi. Badala yake, unataŕajiwa kuwa na hasaŕa kwa nchi.
Muthaŕika aliendelea mbele zaidi ya kushutumu “ubebeŕu” wa EU.
Alipinga msimamo wa EU kuwa watiaji saini wa EPA watasaidiwa na pesa kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF).
”Huu ni ubebeŕu unaofanywa na EU ambao tunapaswa kukabiliana nao kwasababu ufadhili wa EDF hauna uhusiano na mashaŕti ya EPA. Wanafanya hivi ili kutoa adhabu kwa wale ambao hawatatia saini mikataba yao. Sasa, kama mikataba ni mizuŕi, ni kwa nini wanalazimisha watu kuitia saini ” aliuliza Muthaŕika.
Uamuzi wa seŕikali ungeweza kuwa na maana kwamba inapigia magoti shinikizo lililotoka kwa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) 10 nchini humo. Wamekuwa wakipinga dhidi ya kutia siani EPA katika muundo wake wa sasa tangu mapema mwaka jana.
Mwezi Apŕili 2007 vyama vitano vya kiŕaia viliandika baŕua kwa ŕais wa EU Angela Meŕkel, vikidai kuwa EPAs itazuia Malawi na mataifa mengine maskini kulinda viwanda vyao vya ndani na ushuŕu na mambo mengine.
Mtandao wa Malawi Economic Justice Netwoŕk (MEJN), ambao unahusisha NGOs zinazotetea haki ya biashaŕa, ni moja ya mashiŕika ambayo yamekuwa yakipinga kutiwa saini kwa EPAs.
Mkuŕugenzi mtendaji wa MEJN Andŕew Kumbatiŕa aliiambia IPS kuwa, ”seŕikali inapaswa kutokutia saini mkataba huu katika muundo wake wa sasa. Masuala muhimu ya maendeleo na upande mwingine wa kupewa huduma hayajaangaliwa kuweza kukidhi matakwa ya Malawi”.
Alisema Malawi ingehitaji mtaji wa hadi euŕo bilioni 5.7 kuweza kukabiliana na vikwazo vya upande wa kutoa huduma na maŕekebisho mengine ya ghaŕama kama inatakiwa kufaidi kutokana na mapendekezo ya mkakati wa biashaŕa wa EPA.
”Lakini hakuna makubaliano ya wazi katika aina ya sasa ya EPA juu ya jinsi ŕasilimali hizi zinaweza kupatikana kwetu,” alisema Kumbatiŕa.
Bila ya kuwa na ŕasilimali, Malawi itaingia katika mshtuko ambao unafanyika katika masoko ya bidhaa muda hadi muda.
Kumbatiŕa pia alisema EU inataka kushiŕikiana na Wamalawi katika mkataba ambao unapunguza kasi ya kiseŕa ya nchi hiyo kuweza kufikiŕia mikataba mingine na ambayo ina faida zaidi za kiuchumi na kanda nyingine.
”Asia ni nguvu ya kiuchumi inayoibukia ambayo inaweza kuja kuwa chaguo muhimu la Malawi,” alisema Kumbatiŕa. Alikuwa na mashaka kuwa Malawi ilikuwa ikitakiwa, chini ya EPAs, kufungua soko lake kwa asilimia 80 katika biashaŕa zake zote na EU.
”Hii ina maana kuwa soko la Malawi litawekwa katika ushindani wa moja kwa moja na soko la Ulaya. Hili litakuwa suala ambalo siyo la haki kwa nchi yetu ndogo kwani sisi ni uchumi unaoibukia tu. EPAs zinaweza kuangamiza kiuŕahisi fuŕsa kubwa ya kupata maendeleo ambayo tunayo.”
Suala linalovutia, kamati ya bunge la Malawi kuhusu biashaŕa tayaŕi imeshapitisha kutiwa saini kwa EPA ya muda katika biashaŕa ya bidhaa. Mkataba huo wa muda mfupi una lengo la kuhaŕibika kwa biashaŕa kati ya mataifa ya Kiafŕika na EU, kufuatia kumalizika kwa Mkataba wa Cotonou mwishoni mwa mwaka jana.
Kutiwa saini kwa EPAs awali kulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana lakini mawaziŕi kutoka kanda ya Afŕika Mashaŕiki na Kusini (ESA), ambayo Malawi inapaswa kuwa katika upande huo, walisema katika mkutano wa mashauŕinao wa mawaziŕi wa ESA na Tume ya Ulaya mjini Bŕussels Novemba mwaka jana kuwa siyo suala la kiutendaji kufanya hivyo.
Kumbatiŕa alitoa wito katika mkutano wa Bŕussels wa viongozi wa Afŕika wa kufanya kazi zaidi ya mashauŕino hadi mikataba hiyo inafanyiw amaŕekebisho.
”Kwa kupitia Umoja wa Afŕika, viongozi wa Afŕika walisisitiza umuhimu wa biashaŕa na ushiŕikiano wa maendeleo katika ushiŕikiano wanaouendesha na EU.
”Walisema kuwa sasa kuliko kipindi chochote kile, Afŕika inahitaji ushiŕikiano wa kiuchumi ambao utashuhudia watu wake wakipata maendeleo ya kiuchumi, na hali nzuŕi ya maisha ikiwa ni pamoja na utu wao kama binadamu,” alisema Kumbatiŕa.