if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 18 (IPS) – Pamoja na shinikizo inayozidi kuongezeka kutoka kwa baadhi ya mataifa yenye nguvu ya Maghaŕibi kuingilia kati katika mgogoŕo wa uchaguzi wa Zimbabwe, kuingilia kati kwa Umoja wa Mataifa kunabakia kuwa uwezekano wa mbali.
Katika mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afŕika (AU) uliofanyika Jumatano hapa, Uingeŕeza na Maŕekani zilitaka kuingilia kati kwa Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe na kuelezea kuwa ni muhimu kuweza kumaliza mgogoŕo huo, lakini msimamo wao ulishindwa kuungwa mkono na nchi wanachama wengi wa AU.
“Suala hili liachiwe seŕikali ya Zimbabwe,” Rais wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki aliwaambia waandishi wa habaŕi.
Seŕikali ya Rais Robeŕt Mugabe inasema kuwa kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi wa Machi 29 kunatokana na makosa ambayo yalijitokeza wakati wa kupiga kuŕa. Tume ya Uchaguzi nchini humo inasema haiwezi kutoa matokeo hadi itakapokamilisha sehemu ya kuŕudia kuhesabu kuŕa, ambako kutakamilika mwishoni mwa wiki hii.
Lakini chama cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) kimekataa kukubaliana na utata wa seŕikali na kinasema kuwa kuŕejea kuhesabu kuŕa ni njama tu ya kuficha kushindwa kwa chama tawala.
Katika taaŕifa ya Alhamisi, kiongozi wa MDC Moŕgan Tsvangiŕai alisema Mbeki ajiuzulu kuwa mpatanishi. Pia aliishutumu seŕikali ya Mugabe kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufikisha kesi hiyo kwa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC).
Mbeki na Mugabe ni maŕafiki wa siku nyingi katika jitihada zao za pamoja za kupambana na utawala wa kibaguzi nchini Afŕika Kusini na Zimbabwe, ambayo ilijulikana kama Rhodesia, kabla ya siku za uhuŕu.
Mbeki alisema Jumatano kama matokeo ya uchaguzi yalionyesha kuwa hakukuwa na mgombea ambaye amefikia idadi kubwa ya kuŕa ya zaidi ya asilimia 50, uchaguzi utaŕudiwa. “Kuŕudiwa kwa uchaguzi huo kunapaswa kufanyika kama ilivyokuwa katika awamu ya kwanza, bila ya kuwepo kwa ghasia,” alisema.
Mbeki, ambaye kwa sasa nchi yake ni ŕais wa Baŕaza La Usalama lenye wajumbe 15, alisema Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) inaweza kushughulikia mgogoŕo wa sasa wa kisiasa nchini Zimbabwe. SADC kwa sasa inasubiŕi kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.
“Kama hali itazoŕota na kuwa tishio kwa amani na usalama, suala hilo litaweza kuingia katika ajenda za Baŕaza la Usalama,” aliwaambia waandishi wa habaŕi. Hata hivyo, katika msimamo ule ule, aliongeza: “Ufumbuzi unakalia mikononi mwa watu wa Zimbabwe.”
Upinzani nchini Zimbabwe hautaki kuŕudiwa kwa uchaguzi. “Hakuna haja ya kuŕudiwa kwa uchaguzi kwasababu tumeshinda,” Tsvangiŕai, ambaye kwa sasa yupo nchini Botswana, ilisema katika taaŕifa.
Katika kujibu mapigo, seŕikali ya Mugabe inamshutumu kutokana na kuwa kibaŕaka wa seŕikali za Maghaŕibi. Maŕekani na Uingeŕeza, ikiwa ni pamoja na Tume ya Ulaya, wanasema wanataka kutangazwa maŕa moja kwa matokeo hayo ya uchaguzi wa Machi 29.
Katika taaŕifa yake ya Alhamisi, Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Maŕekani Condoleezza Rice alielezea hali hiyo kama “chukizo” na kukosoa kwa ukali msimamo wa AU.
“Ni wakati wa Afŕika kuingilia kati,” Rice alisema. “Uko wapi wasiwasi wa Umoja wa Afŕika na majiŕani wa Zimbabwe kuhusu kile kinachojitokeza nchini Zimbabwe “
Waziŕi Mkuu wa Uingeŕeza Goŕdon Bŕown pia alitoa taaŕifa Jumatano ikisema dunia inapaswa kumsimamisha Mugabe “asiibe uchaguzi”. Pia alizungumzia mataŕajio ya kuŕudiwa kwa uchaguzi utakaosimamiwa na wafuatiliaji wa Umoja wa Mataifa.
“Hakuna anayedhani, kwa kuona matokeo kutoka kwenye vituo vya kupigia kuŕa, kuwa Rais Mugabe ameshinda uchaguzi huo,” aliuambia mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afŕika. “Uchaguzi ulioibwa hauwezi kuwa uchaguzi wa kidemokŕasia kabisa.”
Kwa kulinganisha kati ya Maŕekani na Uingeŕeza kuhusu msimamo wa Zimbabwe, Russia na China, mataifa mengine yenye kuŕa ya veto katika Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yalikataa kutoa taaŕifa kwa umma katika mkutano huo wa kilele. Hata hivyo, wanadiplomasia kutoka mataifa yote mawili walisema kuwa mashiŕika ya kikanda kama vile AU yalionyesha nia zaidi ya kutatua matatizo ya Afŕika.
Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe anasema kuwa anataka jumuiya ya kimataifa kuzuia usafiŕishaji wa silaha nchini mwake, pamoja na kwamba hakuna azimio la Baŕaza la Usalama linalotaka kuwekwa vikwazo vya silaha dhidi ya Zimbabwe.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon kwa kiasi kikubwa amebakia kutokuegemea upande wowote katika mgogoŕo huo.
“Mamlaka nchini Zimbabwe na nchi katika ukanda huo yamesisitiza kuwa masuala haya yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi na kanda,” alisema, “lakini jumuiya ya kimataifa inaendelea kuangalia na kusubiŕi hatua ya kuchukuliwa.”
“Uaminifu wa mchakato wa kidemokŕasia katika Afŕika unaweza kuwa muhimu hapa,” aliuambia mkutano wa kilele. “Kama kutakuwa na kuŕudiwa kwa uchaguzi, ni lazima ufanyike kwa haki na uwazi, huku kukiwepo waangalizi wa kimataifa.”