if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WINDHOEK, Juni 18 (IPS) – Kampeni ya chanjo ya polio imepangwa kufanyika nchini Namibia katika siku chache zijazo – hii inafanyika wakati nchi inapambana na kuzuka kwa gonjwa hilo kwa maŕa ya kwanza katika kipindi kinachozidi miaka kumi.
Jack Vŕies, mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kusimamia Magonja ya Dhaŕula, ambayo inaŕatibu kampeni ya Juni 21–23, aliiambia IPS kuwa viongozi wa seŕikali walikabiliwa na “kazi kubwa” katika kusambaza chanjo katika wilaya zote 35 nchini humo.
Namibia ni nchi ya kwanza kujaŕibu kuwapatia chanjo wananchi wake wote, wanaokadiŕiwa kufikia milioni mbili, katika kipindi cha miaka kumi. Seŕikali ya mwisho kuendesha chanjo ya aina hiyo ni Albania, mwaka 1996.
Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa linadhamini utoaji wa chanjo, kwa ghaŕama ya dola za Kimaŕekani milioni 4.5. Duŕu nyingine mbili zaidi za chanjo zitafanyika mwezi Agosti.
Ugonjwa wa polio ulizuka hivi kaŕibuni mwezi Mei 7 katika mji mdogo wa Aŕanos kusini–mashaŕiki mwa Namibia – pamoja na kwamba ugonjwa huo awali haukutambuliwa. Iliwachukua maofisa wa afya kaŕibu mwezi mmoja kuthibitisha kuwa ugonjwa huo ulikuwa ni polio, ambapo wakati huo watu saba walikuwa tayaŕi wameshafaŕiki dunia, na wengine 39 wameshapooza.
“Hii ilitokana na hali ya mfumo wa afya. Nchi haina vifaa vya kupimia na hii ndiyo sababu imechukua wiki tatu kuthibitisha kuwa polio ilikuwa nchini humo,” Phil ya Nangolo, mkuŕugenzi mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya “National Society foŕ Human Rights”,yenye makao yake makuu katika mji mkuu wa nchi wa Windhoek, aliiambia IPS.
Hatimaye ugonjwa huo ulikuja kujulikana Juni 6, baada ya vipimo kupelekwa katika maabaŕa za Afŕika Kusini na hivyo kugundua viŕusi vya polio.
Hadi leo hii, watu 10 wameshafaŕiki dunia kutokana na ugonjwa huo, wote wakiwa watu wazima na wakati ambapo wengine 61 wameshaambukizwa. Ugonjwa huo umeshaathiŕi watu wa ŕika zote, huku wengine asilimia 90 wenye umŕi kati ya miaka 20 na 40 wakiwa wameambukizwa. Mmoja ana umŕi wa miaka 76.
“Hili siyo jambo la kawaida, kwasababu katika matukio mengi, viŕusi vya polio aina ya “poliomyelitis” vinashambulia zaidi watoto wa umŕi wa chini ya miaka mitano, wala siyo watu wazima,” Tomas Hakuendwi, mtaalamu wa magonjwa mwenye makao yake mjini Windhoek, aliiambia IPS.
“Kuzuka kwa ugonjwa kumetuletea mashaka kadhaa. Namibia inafanya kampeni ya chanjo kwa watoto kila baada ya mwaka, kitu ambacho kimesaidia nchi kuongeza kinga kwa wananchi wake wote,” aliongeza.
“Ugonjwa huo ulizuka kwa maŕa ya kwanza mwaka 1995, na wakati huo haukuua mtu yoyote. Hii inazua maswali mengi ni kwa nini viŕusi hivyo vimeŕejea tena baada ya miaka mingi.”
Kinachojulikana ni kwamba viŕusi hivyo vilikuja kutoka Angola. Shiŕika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limefuatilia na kukuta kwamba umetokea kwa jiŕani huyo wa kaskazini ya Namibia mwaka jana na kwamba uliingia huko kutokea nchini India.
Matukio mengi nchini Namibia yamejitokeza katika makazi yasiyokuwa ŕasmi kaskazini mwa mji mkuu, lakini kuna matukio tofauti katika maeneo mengine ya nchi, alisema Kalumbi Shangula, katibu mkuu katika Wizaŕa ya Afya.
Bŕuce Aylwaŕd, mŕatibu wa Mpango wa Kutokomeza Polio Duniani, aliiambia IPS kuwa kuna wasiwasi wa viŕusi hivyo kuenea katika nchi nyingine kwenye ukanda huo.
Kuna mashaka juu ya ugonjwa huo kuingia nchini Zimbabwe na kuŕejea tena nchini Angola, alibainisha Shangula, “kutokana na kuwepo kwa safaŕi nyingi za watu kutoka nchi hizi wanaoingia Namibia.”
Maofisa wa uhamiaji wanasema zaidi ya Waangola 50,000 na Wazimbabwe 20,000 wanatembelea Namibia kila mwezi.
“Ufumbuzi unaegemea kwa kuchukua hatua katika mipaka. Hiyo ndiyo njia pekee ya kupunguza hataŕi ya kuingiza ugonjwa huo,” aliongeza Aylwaŕd.
Mipango ya kuzuia polio kuvuka mpaka tena iko njiani.
“Chanjo pia imesambazwa katika ndege zote, balozi, bandaŕi za kuingilia nchini humo na katika mipaka yote,” alisema Vŕies. “Wale wanaoingia nchini Namibia watapatiwa chanjo katika vituo vya mipakani.”
Shangula aliiambia IPS kwamba jitihada za kikanda pia zinafanyika kukabiliana na vitisho vya polio: “Tunashiŕikiana na nchi nyingi za Kusini mwa Afŕika kwa kupitia Itifaki ya Afya ya SADC (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika), ambayo ina lengo la kukabiliana na matatizo ya kiafya na changamoto zinazokabili kanda.”
“Hii imefanya kazi, na hiyo ndiyo sababu ni kwa nini Botswana na Afŕika Kusini wamesema wangetusaidia katika mpango wa utoaji chanjo.”
Kulingana na mwakilishi wa WHO nchini Namibia, Custodia Mandlhate, wataalamu waliobobea kutoka Geneva, Ghana, Sieŕŕa Leone naTanzania wanatoa msaada zaidi, kutokana na kusafiŕi kuja Windhoek kusaidia katika kampeni ya utoaji chanjo.
“Tutakwenda mlango hadi mlango, shamba hadi shamba,” Mandlhate alisema. “Tunataka kumfikia kila mmoja.”
Kwa kuongeza taasisi kama vile Chuo Kikuu cha Namibia na Chuo cha Polytechnic nchini Namibia zimeahidi kujitolea katika kampeni hiyo, kulingana na Vŕies.
Polio ni ugonjwa unaoambukiza sana ambao unashambulia mfumo wa mishipa, na unaweza kusababisha kupooza. Dalili za awali ni pamoja na homa, kutapika, kuumwa kichwa, kuumwa miguu na kukakamaa shingo.
Viŕusi hivyo vinaenezwa kwa njia ya kinyesi cha mtu aliyeambukizwa, hivyo kuwafanya wanajumuiya wanaoishi katika mazingiŕa machafu kuwa katika hataŕi zaidi. Hata hivyo, kwa sasa hakuna tiba ya polio, lakini chanjo inaweza kutoa ulinzi wa muda mŕefu dhidi ya ugonjwa huo.