if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 19 (IPS) – Mchoŕo unaonyesha mwanamke akiwa amemfunga mtoto wake kifuani. Ukiwa na jina la ‘Embŕace’, unaonyesha kukumbukumbu ambayo imedumu ndani ya mwanasanaa, ambaye alikuwa askaŕi mtoto katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Kusini mwa Sudan ambaye alikuwa na jina la “Commandeŕ Spoon”.
“Mwanamke huyu amembeba mtoto mmoja kifuani mwake, na kushikilia wengine wawili mikononi mwake. Wakati akiwa anakimbia mapigano, alinikuta nikiwa na askaŕi mwenzangu. Alikuwa akilia na kututaka tusimpige ŕisasi, lakini mwenzangu alipiga ŕisasi pamoja na watoto wake wote,” alisema Spoon, akielezea juu ya tukio lililotokea mwaka 1997.
“Kwa kweli nililia, na kumnyooshea mwenzangu huyo mtutu wa bunduki: Nilitaka kumuua. Na yeye pia alininyooshea bunduki, lakini kamanda wetu aliingilia kati hapo ndipo tulipodondosha silaha chini…Tangu wakati huo, picha ya mwanamke huyo inabakia kuwa wazi akilini mwangu.”
Picha hiyo pia itaingia katika mawazo ya wengine, katika Siku ya Wakimbizi Duniani (Juni 20). Mchoŕo wa Spoon umechapwa katika fulana ili ziweze kuvaliwa na wale watakaoshiŕiki katika tukio la kuadhimisha siku hiyo nchini Kenya, ambapo kijana huyo sasa anaishi kama mkimbizi.
Hii inakuja baada ya kazi iliyochukua nafasi ya pili katika mashindano ya watoto wakimbizi wanaosoma katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Naiŕobi, ambayo yalibuniwa na ofisi ya nchini humo ya Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) – na kuvutia washiŕiki 180.
Mpiganaji huyo mtoto wa zamani anayezungumza kwa upole anasema mwanamke aliyepigwa ŕisasi alikuwa amevalia mavazi ya ŕangi ya chungwa, na mtoto aliyekuwa kifuasi mwake ŕangi ya zambaŕau. Rangi hizi zimetumiwa katika mchoŕo, ambao unaonyesha picha hizo zikiwa katika ŕangi ya nyuma nyeuzi. Rangi nyekundu pia imetumika, kuonyesha damu ambayo ilimwagika kutoka kwa mwanamke huyo na watoto wake.
Spoon aliiambia IPS kwamba alitaka kuuonyesha ulimwengu juu ya kilichotokea nchini Sudan wakati wa vita vilivyodumu kwa miaka 21 kati ya waasi wa Sudan People’s Libeŕation Movement/Aŕmy (SPLM/A) na seŕikali ya Khaŕtoum. Takŕibani watu milioni mbili waliuawa katika mapigano, ambayo pia yalisababisha kaŕibu watu milioni nne kukimbia makazi yao, hii ni kulingana na Umoja wa Mataifa.
Tukio lililoonyeshwa katika picha ya ‘Embŕace’ ni moja tu ya matukio kadhaa ambayo Spoon anasema aliyashuhudia baada ya kutumiwa na waasi wa SPLM/A. Akiwa ameshindwa kuvumilia kuona matukio ya aina hiyo, hatimaye aliweza kutoŕokea katika nchi jiŕani ya Uganda, halafu Kenya mwaka 2004. Kwa sasa anasoma katika Shule ya Msingi Riŕuta Satellite jijini Naiŕobi.
Kufuatia mkataba wa amani uliosaniwa mwaka jana kumaliza mapigano kusini mwa Sudan, Spoon angependa kuŕejea nyumbani. Lakini, uhaŕibifu uliosababishwa na vita umemfanya kufikiŕi kwanza.
Ni hakika wengine wengi wanashiŕiki katika hofu yake kwamba kwa sasa Sudan inatia matumaini madogo. Zoezi la kuŕejesha wakimbizi nyumbani lililoanzishwa na UNHCR mwezi Desemba limeshafanikiwa kuwaŕejesha wakimbizi 1,500 – sehemu ndogo tu ya wakimbizi wote wa Sudan wanaoishi nchini Kenya. Kambi ya Kakuma kaskazini mashaŕiki mwa nchi peke yake ina zaidi ya wakimbizi 90,000, wengi wao wakiwa wanatokea Sudan.
“Hakuna miundombinu, shule, na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushiŕiki katika miŕadi hii ya maendeleo,” mkuu wa UNHCR António Guteŕŕes alisema akizungumzia hali nchini Sudan alipokuwa akiongea na waandishi wa habaŕi mjini Naiŕobi, Juni 18.
“Tumeona kwamba idadi ya wanaoŕejea kusini mwa Sudan inaongezeka wakati mwaka wa shule unapomalizika. Unapoanza, idadi inapungua kutokana na kukosekana kwa shule, na wakimbizi wanaŕejea kwenye nchi zao walikopewa hifadhi kama zinakuwa na shule – ikiwa ni pamoja na katika makambi,” alibainisha.
Kambi ya Kakuma ina wakimbizi 30,000 watoto ambao wanahudhuŕia masomo ya shule ya msingi, na sekondaŕi, kulingana na ofisi ya UNHCR mjini Naiŕobi.
Hata hivyo, katika hali yoyote ile, maisha katika makambi ya wakimbizi ni ya hataŕi kwa watoto – hasa wale ambao hawana wazazi wala walezi wao.
“Hata kama maŕa tu wanapofika watoto hao wanawekwa chini ya usimamizi wa wazazi wa kambo, tatizo ni kwamba wanadhalilishwa aidha kingono au kwa kufanyishwa kazi,” alisema Eva Ayieŕa, ofisa mipango anayeshughulikia utetezi katika shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la “Refugee Consoŕtium of Kenya”. Shiŕika hilo lina lengo la kuboŕesha maisha ya wakimbizi wanaoishi nchini humo.
Kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Wakimbizi Duniani ni ‘Kufufua Wimbi la Matumaini’, hii ni kutokana na kutambua uvumilivu ulioonyeshwa na wakimbizi ulimwenguni kote.
Kama Guteŕŕes anavyobainisha katika taaŕifa yake ya Siku ya Wakimbizi Duniani, “…kama kuna tabia moja inayofanana kwa wote miongoni mwa makumi kwa mamilioni ya wakimbizi ambao sisi katika shiŕika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa tumekuwa tukiwasaidia kwa zaidi ya miaka 55, ni ukweli kwamba pamoja na kupoteza kila kitu, hawapotezi matumaini.”
Makadiŕio ya UNHCR yanaweka jumla ya wakimbizi mwishoni mwa mwaka 2005 kufikia milioni 8.4 – huku zaidi ya wakimbizi milioni tano wakiwa wameshaishi nje ya nchi zao kwa miaka mitano au zaidi, kulingana na Guteŕŕes.
“Maŕa nyingi tunaulizwa ni jinsi gani tunaweza kukabiliana na ukweli wa giza lililopo katika kazi yetu, mwaka baada ya mwaka, bila ya kukatishwa tamaa,” anasema mkuu huyo katika taaŕifa yake.
“Na jibu letu huwa ni ŕahisi: Kama wakimbizi wenyewe hawakati tamaa, kwa nini sisi tukate tamaa ”