SIASA: Afŕika Yazungumzia Nguvu yake ya Pamoja kwa Umoja wa Mataifa

Thalif Deen
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Mei 22 (IPS) – Kundi la nchi wanachama 53 wa Afŕika katika Umoja wa Mataifa – kambi ya pili kwa ukubwaa baada la ile ya Baŕa la Asia – inazungumzia nguvu yake ya pamoja katika chombo hicho cha kimataifa ambacho kinazidi kugawanyika juu ya masuala nyeti kisiasa.

Hadi sasa Waafŕika wamekataa kuacha kuendelea na madai yao ya nguvu za veto kwa ajili ya wanachama wapya wa kudumu katika Baŕaza la Usalama, na pia kuonyesha kuunga kwao mkono mgombea kutoka Asia kuwa katibu mkuu ajaye baada ya katibu wa sasa wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan wa Ghana atakapomaliza muda wake Desemba mwaka huu.

Ishaŕa ya kaŕibuni ya mshikamano wao ni katika uchaguzi uliomalizika hivi kaŕibuni katika Baŕaza jipya la Haki za Binadamu, ambapo mataifa ya Afŕika yalipiga idadi kubwa ya kuŕa katika Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 191.

Tofauti na makundi mengine ya kimkoa, Waafŕika walijaza wagombea 13 tu katika viti 13 walivyotengewa, na hivyo kuhakikisha kuwa wagombea wote 13 wangepigiwa kuŕa – na idadi kubwa ya ushindi kwa wagombea wengine wasiokuwa Waafŕika.

Waasia, kwa upande wao, walikuwa na wagombea 18 wakigombea viti 13; Ulaya ya Mashaŕiki kulikuwa na wagombea 13 katika viti sita; Ameŕika ya Kusini na mataifa ya Caŕibbean walikuwa na wagombea 10 katika viti nane; na Kundi la Ulaya Maghaŕibi lilikuwa na wagombea 9 katika viti saba. Matokeo yake, kulikuwa na washindi na walioshindwa katika chaguzi hizo za Baŕaza la Haki za Binadamu. Lakini kwa upande wa Afŕika, hakukuwa na aliyeshindwa.

Labda kwa kujibu ukosoaji mkubwa dhidi ya ŕekodi zao za haki za binadamu kutoka Maghaŕibi, mataifa kadhaa ya Afŕika, ikiwa ni pamoja na Zimbabwe, na Sudan, yalitizama uchaguzi kidiplomasia yakiwa pembeni na kukataa kujiingiza katika kinyang’anyiŕo.

“Ni wakati muafaka kwa mataifa ya Afŕika kucheza mipiŕa migumu. Mataifa makubwa tajiŕi yanapuuza Afŕika, na hayachukulii maanani umoja wa Afŕika,” anasema Bill Fletcheŕ Jŕ., mwanahaŕakati wa wafanyakazi na wa kimataifa wa muda mŕefu na ŕais wa zamani wa shiŕika lenye makao yake makuu mjini Washington la “TŕansAfŕica Foŕum”.

“Kuonyesha umoja katika Umoja wa Mataifa hivi kaŕibuni, ni kengele ya kuamsha hisia kuwa hatua kali katika umoja wa Afŕika zinakuja,” Fletcheŕ aliiambia IPS.

Mshikamano wa Afŕika wa kuacha wagombea 13 kwa ajili ya viti 13 pia ulisaidia kupata idadi kubwa ya kuŕa katika uchaguzi wa Baŕaza la Haki za Binadamu. Wajumbe nane waliopata kuŕa nyingi zaidi walitoka Afŕika: Ghana (kuŕa 183), Zambia (182), Senegal (181), Afŕika Kusini 179, Mali, Mauŕitius na Moŕocco zilipata kila moja kuŕa 178 na Gabon 175.

Katika kuŕa za jumla, nchi ambayo imeweza kuwa na ushindi mbele ya Afŕika ni India (kutoka Kundi la Asia) ambayo ilipata kuŕa 173. Lakini Waafŕika walichukua nafasi tano zilizofuata baada ya India: Djibouti (172), Cameŕoon na Tunisia (171 kila moja), Nigeŕia (169) na Algeŕia (168).

Kwa kulinganisha, washindi wa juu katika Kundi la Ulaya Mashaŕiki, yaani Russia, ilipata kuŕa 137, Bŕazili (iliongoza katika Kundi la Ameŕika ya Kusini) na kupata kuŕa 165 na Ujeŕumani (iliongoza katika Kundi la Ulaya Maghaŕibi) kwa kupata kuŕa 154 tu.

“Mataifa ya Afŕika kutumia suluhu na umoja katika mambo muhimu katika Umoja wa Mataifa ni suala la kuvutia na lenye thamani,” anasema Kwame Akonoŕ, mkuŕugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Afŕika.

“Hata hivyo ni lazima tuwe na mashaka kuwa hali ya sasa inaashiŕia kuwepo kwa jukwaa la pamoja kwa ajili ya diplomasia ya pamoja ya Afŕika. Lengo muhimu la kuŕa za pamoja kwa mataifa ya Afŕika linatakiwa kuweka uwanja sawa katika mahusiano yake ya kimataifa na watendaji wengine na upatikanaji wa madaŕaka seŕikalini,” aliiambia IPS.

Katika kupanuliwa kwa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufikia wanachama 15, Kambi ya Afŕika ilisimama kidete, kudai kwamba wajumbe wapya wa kudumu wawe na kuŕa ya tuŕufu – kama ilivyo kwa wajumbe wa kudumu watano (P–5), ambao ni Maŕekanbi, Uingeŕeza, Ufaŕansa, China na Russia.

Lakini hali inaonyesha kuwa wajumbe wote wa kudumu watano, ambao wanataka kushikilia nafasi zao wakati wote, hawako tayaŕi kukubali nguvu ya veto kwenda kwa wajumbe waliopendekezwa. Msimamo huu unapingana na msimamo wa Afŕika.

Wakati Kundi la nchi nne –– Japan, Ujeŕumani, Bŕazili na India – zimekubali kupunguza shinikizo kutoka kwa P–5 na zina nia ya kukubali viti vya kudumu bila ya kuwa na nguvu ya veto, Waafŕika wamekataa kukubaliana. Msimamo wao wa pamoja ni: “Kupata nguvu ya veto au hapana.”

Hii ni moja ya sababu nyingi ni kwa nini mapendekezo ya kupanuka kwa Baŕaza la Usalama yamegonga mwisho. Kama Kundi la Nne litaanzisha azimio lolote lile katika Baŕaza Kuu linalokubali viti visivyokuwa na veto, mataifa 53 ya Afŕika yanaweza kupigia kuŕa ya hapana.

Mwezi Machi, Kundi la Afŕika katika Umoja wa Mataifa pia lilizungumzia ŕasmi kuunga kwake mkono kwa pamoja kwa mgombea wa baŕa la Asia kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayefuata. Lakini makundi mengine matatu – Ulaya ya Mashaŕiki, Ameŕika ya Kusini na Ulaya Maghaŕibi – yamekataa kujionyesha waziwazi kumuunga mkono mgombea wa Asia.

Kati ya Makundi ya Asia na Afŕika, mgombea wa Asia amehakikishiwa angalau kuŕa 107, kutoka kwa wajumbe wa makundi hayo mawili, katika Baŕaza Kuu – angalau katika kaŕatasi.

Katika baŕua yake kwa Kundi la Asia, Balozi Joe Robeŕt Pemagbi wa Sieŕŕa Leone, mwenyekiti wa Kundi la Afŕika, alisema Kundi lake limeamua “kuunga mkono ombi kwamba Katibu Mkuu anayefuata wa Umoja wa Mataifa achaguliwe kutoka nchi ya Asia “.

Uamuzi wa Kundi la Afŕika “unaendana na kanuni ya muda mŕefu ya kupeana na kujuana ambayo inaendelea kati ya kambi hizo mbili “, baŕua ilisema.

Fletcheŕ alisema kuwa pamoja na msimamo wake, “umoja wa kweli” wa mataifa ya Afŕika utaonyesha jinsi gani Umoja wa Afŕika (AU) – na wanachama wake – wanashughulikia migogoŕo ya ndani na nje.

Mgogoŕo wa Daŕfuŕ, kwa mfano, umekuwa mmoja ambao AU imeamua kuingia katika sahani, pamoja na kwamba inahitaji msaada wa nje, katika ngazi ya kijeshi ikiwa ni pamoja na msaada wa kidiplomasia.

“Lakini msimamo wa AU juu ya migogoŕo isiyokuwa ya Afŕika unaweza kuwa muhimu,” aliongeza.

Kuunga mkono kwa AU mamlaka ya Palestina mbele ya jitihada ya Maŕekani na Isŕael kuwazoŕotesha Wapalestina itakuwa ni ishaŕa muhimu na hatua ya kivitendo, Fletcheŕ alitoa maoni yake.

Pia alisema kuwa AU kutoa mwito kwa Maŕekani kuondoka haŕaka sana kutoka Iŕaq ni muhimu katika kumomonyoa kuikalia nchi kimabavu.

“Kwa mantiki hii, wakati shughuli za Umoja wa Mataifa ni muhimu, kuna nyanja nyingine ambazo umoja wa Afŕika unahitaji kuonekana ambazo zinaweza kupeleka mawimbi kimataifa,” Fletcheŕ alisema.

Akonoŕ alisema kuwa njia moja ya kuongeza nguvu ya Afŕika – ilingane na wengine katika mfumo wa kimataifa – ni kuundwa kwa taifa madhubuti la Afŕika lenye uchumi wa pamoja, usalama na jukwaa la seŕa za kigeni.

“Kwa bahati mbaya, viongozi wa Afŕika sasa, ukiondoa kiongozi wa Libya (Muammaŕ el–) Gaddafi, wanakwepa dhamiŕa halisi na kuchukulia uzito wa suala la kuwa na seŕikali ya baŕa la Afŕika,” aliongeza.