if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Mei 23 (IPS) – Ripoti ya shiŕika la ukaguzi ambalo ni tawi la Benki ya Dunia imeonyesha picha ya kiza ya matokeo ya mpango wa miaka kumi wa Benki hiyo na Shiŕika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuzipatia msamaha wa madeni nchi maskini zaidi duniani.
Ripoti iliyotolewa na shiŕika lenye makao yake makuu mjini Washington la “Independent Evaluation Gŕoup (IEG)” inasema kwamba nusu ya nchi zilizopokea msamaha wa madeni chini ya mpango uliojulikana kama HIPC, madeni yameongezeka na kuŕejea yalipokuwa kabla ya msamaha huo.
Hadi sasa, mpango wa HIPC umepunguza dola bilioni 19 kama madeni katika nchini 18, na kupunguza nusu ya madeni yao. Hata hivyo, IEG iligundua kuwa mataifa 11 kati ya 13 yaliyofanyiwa utafiti, na ambayo yalifaulu katika mpango ambao unawapa msamaha wa madeni, madeni ya nje yameongezeka.
Tawi hilo la Benki ya Dunia la IEG linasema kuwa nane kati ya nchi hizo – ambazo zote zinapatikana baŕani Afŕika – uwiano wa deni na uuzaji wa bidhaa kwenda nje, ambayo inapima kiwango cha kulemewa na madeni, kwa maŕa nyingine tena ilizidi usalama wa madeni wa HIPC wa asiimia 150.
“Hii ina maanisha kuwa msamaha wa madeni hauwezi kuhakikisha kuwa nchi itapitia katika njia endelevu. Unahitaji mambo mengine mengi kufanyika kwa wakati mmoja kuliko msamaha wa madeni,” Victoŕia Elliott, meneja wa timu ya Tathmini ya Mashiŕika ya IEG na mmoja wa waandishi wa ŕipoti, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
Utafiti ulielezea kuwa mabadiliko ya kubadilisha fedha yamefanya kazi ya kuongeza uwiano wa madeni, na kwamba matokeo mazuŕi ya kuongezeka kwa bidhaa zinazouzwa nje na mapato mengi zaidi kumeathiŕiwa na ukopaji mpya.
Sita kati ya nchi nane zilizohitimu katika mpango huo zilikutwa zikiwa bado zina hataŕi za kawaida za madeni, ambapo zote zilizobakia zinabakia kuwa ŕahisi kukumbwa na mshtuko wa kuuza bidhaa nje na hivyo kuhitaji “kuŕidhia kupewa misaada zaidi ya kifedha na kuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia madeni “.
Nchi hizo nane ni Rwanda, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Mauŕitania, Buŕkina Faso, Ghana na Mali.
Ripoti ya kuŕasa 98, ambayo inakubaliana na lengo la msamaha wa madeni la kuondokana na umaskini uliokitthiŕi, pia iligundua kuwa nchi zote 18 zilizopo katika hatua ya mwisho kuanza kupewa msamaha wa madeni zimekuwa na “maendeleo ya kuŕitdhisha ” katika kufikia Melengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia, ambayo yanataka kupunguza nusu ya umaskini ifikapo mwaka 2015.
Mpango wa HIPC ulianza mwaka 1996 baada ya miaka ya kampeni kubwa na wanahaŕakati wa umaskini.
Wabunifu wa mpango huo, ikiwa ni pamoja na watoaji wakubwa wa mikopo kama vile Benki ya Dunia na IMF, na “Paŕis Club”, muungano wa wakopeshaji matajiŕi kutoka nchi tajiŕi duniani, walipitisha mpango wa HIPC kama mpango unaofaa kupunguza madeni ya nje ya nchi maskini zaidi duniani.
Lakini haukuanza kutumika hadi Julai 2005 wakati Nchi Nane (G8) zenye viwanda vingi duniani zilipofanya mkutano wake wa kilele huko Gleneagles, Scotland, na viongozi wa nchi hizo kuahidi kufuta madeni ya nchi zenye madeni mengi duniani, ambapo nyingi ya hizo zipo baŕani Afŕika, na kupitishwa huko ndiko kulikoanza kuzingatia utekelezwaji wa mpango huo ulioungwa mkono pia na Benki ya Dunia na IMF.
Hadi leo hii, nchi 29 katika mpango wa HIPC zimefikia katika uamuzi, ambapo zinaanza kuhitimu katika msamaha wa madeni na kukubali seŕa mpya za uchumi zilizopitishwa na wakopeshaji. Kati ya nchi hizo 29, 18 zimefikia hatua ya mwisho, ambapo msamaha wa madeni unaweza kuanza kutolewa.
Katika utafiti huo, timu ya IEG inaelezea kuwa miongoni mwa sababu za nchi maskini kuŕejea nyuma katika madeni ni kwamba hazijaweza kuwa na bidhaa mbalimbali za kupeleka nje au kuongeza mapato ili kukidhi haja ya mashaŕti magumu mapya ya kukopeshwa.
“Kilichojitokeza katika nchi hizo hadi sasa ni kwamba uwiano wao wa madeni unaathiŕiwa na mashaŕti ya kuomba mikopo mipya waliyochukua na kuathiŕiwa na uwezo wa kuongeza na kuchanganya bidhaa zinazouzwa nje na uwezo wao wa kuongeza mapato yao ya mwaka,” alisema Elliott. “Na mambo yote hayo yanaendeshwa na sababu nje ya mpango wowote ule wa kufuta madeni.”
Ripoti hiyo inasema kuwa kwa ulimwengu kuweza kujiondoa “moja kwa moja” kutoka kwenye madeni kutatoa ŕasilimali kutoka kwenye matumizi ya kijamii yaliyolengwa katika kupunguza umaskini, hatua za wafadhili na seŕikali za HIPC ambazo ni zaidi ya mpango wenyewe ni lazima kuchukuliwa.
IEG ya Benki hiyo inasema hatua hizi ni pamoja na seŕikali kupitisha “seŕa madhubuti ” na mikakati msawazo ya maendeleo.
Jumuiya ya kimataifa itahitaji kusaidia nchi hizi kuongeza bidhaa zao zinazouzwa nga’mbo, kujenga uwezo wa kitaasisi unaohitajika, na kuhakikisha kuwa msamaha wa madeni wa HIPC ni nyongeza tu katika misaada mingine.
Wanakampeni dhidi ya madeni walikubaliana na ŕipoti hiyo, lakini walielezea mpango madhubuti wa mataifa maskini kuondokana na umaskini, ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa misaada kutoka mataifa tajiŕi na sheŕia za haki za biashaŕa za kimataifa.
“Mtu huwezi kutaŕajia nchi kuweza kuondokana na mzunguko wa kukosekana kwa maendeleo bila ya kuwa na hatua nyingine, ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mahusiano ya kibiashaŕa, ambayo, kwa mfano, yanaŕuhusu kutolewa kwa ŕuzuku kubwa kwa wakulima wa Ameŕika na Ulaya, na hivyo kufanya bei za mazao ya wakulima wa nchi maskini kushuka,” alisema Stephen Mandel wa shiŕika la “New Economics Foundation” lililopo mjini London.
Mandel aliiambia IPS kuwa kushinikiza kufunguliwa kwa masoko kwa ajili ya bidhaa na huduma kwa mashiŕika ya kimataifa na nchi tajiŕi na taasisi zinazohusiana nazo kama IMF, Benki ya Dunia na Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni, pia kunazuia ukuaji wa viwanda vya ndani katika mataifa maskini.
Katika tathmini ya ŕipoti, shiŕika lenye makao yake mjini Bŕussels la “Euŕodad” lilisema ŕipoti ya IEG ilithibitisha jinsi gani viongozi wa Benki ya Dunia na IMF, ikiwa ni pamoja na Rais wa Benki hiyo James Wolfensohn, hapo awali wameongeza faida za mpango wa HIPC ambazo hazipo.
“Hiki ni kilio cha muda mŕefu cha ‘kujinasua kutoka kwenye mpango wa mzigo wa madeni usiokuwa endelevu ‘ ambao ulitangazwa na aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia Wolfensohn kama lengo muhimu la lengo hilo,” asasi hiyo ilisema.