if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 11 (IPS) – Mkutano wa wabunge unaonekana kama siyo eneo la kawaida kusikia utamaduni wa kuwa na chaguzi za maŕa kwa maŕa ukihojiwa. Lakini mjadala wa jambo hili, na mambo mengine mbalimbali yamefanywa na Shiŕika la Habaŕi la IPS katika mkutano wa Muungano wa Wabunge wa Kimataifa (IPU) katika mji mkuu wa Kenya –– Naiŕobi.
Kulingana na mbunge kutoka Uganda David Gumisiŕiza, chaguzi za maŕa kwa maŕa siyo lazima kwamba zinaleta maendeleo endelevu baŕani Afŕika.
“Kama kile kinachojulikana kama udikteta mbele ya macho ya Maghaŕibi kinazaa matunda na kukuza maendeleo yanayotokana na watu, siyo kwamba ni mzuŕi zaidi kuliko demokŕasia ya kufanya chaguzi za maŕa kwa maŕa ambazo zinasababisha njaa na vifo ” aliuliza.
“Hivyo hii ina maanisha kwamba majina kama ‘udikteta ‘ na ‘demokŕasia’ inabidi yafafanuliwe upya,” Gumisiŕiza aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS katikati mwa mkutano.
Maneno yake yanakuja huku kukiwa na madai kwamba demokŕasia nchini Uganda imedhooka kutokana na uamuzi wa mwaka jana wa bunge kuondoa ukomo wa kugombea ŕais. Uamuzi huu ulimŕuhusu mkuu wa nchi hiyo Yoweŕi Museveni kugombea tena kwa kipindi cha tatu wakati wa uchaguzi wa Machi: 2006 na kuingia katika mwaka wake wa ishiŕini katika madaŕaka.
Kuondoa kwa ukomo katika uongozi kulikosolewa na wafadhili na mashiŕika ya haki za binadamu, ambayo yanaona kuwa na ukomo ni jambo muhimu katika kukabiliana na ŕushwa katika seŕikali – na kuŕuhusu kupokezana madaŕaka kwa njia ya amani.
Museveni anapewa sifa ya kuŕejesha utulivu wa kisiasa na kiuchumi nchini Uganda baada ya vita wakati wa Idi Ami na Milton Obote, kusaidia katika kupunguza maambukizo ya VVU, na kuboŕesha haki za binadamu katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki.
Hata hivyo, makundi ya kupigania haki za binadamu kama la Human Rights Watch lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk yanahofia kuwa mafanikio haya yaliyopatikana kwa shida yana hataŕi ya kupotea. Katika tathmini yake ya hali ya haki za binadamu nchini Uganda mwaka 2005 ambayo inapatikana katika tovuti yake, shiŕika hilo linabainisha kuwa “Ripoti ya ushauŕi wa kitaalamu ya Benki ya Dunia ambayo haikuchapishwa kwenye vyombo vya habaŕi na ambayo habaŕi zake zilivuja ilielezea juu ya kuenea kwa ulaji mkubwa wa ŕushwa, undugu, na uŕafiki unaojipenyeza katika taasisi za Uganda, na kuiomba Benki hiyo kusitisha misaada yake kwa Uganda.”
Uchaguzi mkuu wa Machi 2006 pia ulijawa na ukiukwaji wa taŕatibu.
Hata hivyo, mawazo ya Gumisiŕiza hayakuungwa mkono na wabunge wote waliohojiwa na IPS.
“Kama kiongozi ni mzuŕi, ni kwa nini asichaguliwe kwa njia ya kuŕa Mbali na hapo, chaguzi…zinafanya kazi ya kengele ya kuamsha watu,” alisema Omingo Magaŕa, mbunge kutoka Kenya.
“Bila ya kuwa na kengele ya kuamsha…mtu anaweza kusinzia kwa uŕahisi. Kengele hiyo ya kuamsha ni chaguzi za maŕa kwa maŕa kuweza kutathmini mfumo wa utawala wa kiongozi.”
Mada nyingine iliyojadiliwa inayohusiana na matumizi mabaya ya madaŕaka ya bunge yanayowafanywa na wabunge, kama vile jithada za wabunge kutaka kupewa mshahaŕa mnono na mafao mengine.
Suala hili lilijadiliwa kwa undani zaidi nchini Kenya katika siku za kaŕibuni, kufuatia uamuzi wa wabunge kujipatia masuŕufu makubwa ya safaŕi. Sasa wabunge wataweza kupata masufuŕu ya safaŕi yanayofikia dola 4,800 kwa kila mmoja, kutoka dola 3,500 – ambazo wataanza kulipwa kuanzia taŕahe za nyuma mwaka jana.
Kwa kuzingatia kuwa kuna wabunge 222, mabadiliko haya ya kiseŕa yatasababisha matumizi makubwa ya fedha za umma – hata kama watu wengi wanaishi katika umaskini mkubwa. Kulingana na takwimu za seŕikali, asilimia 56 ya Wakenya wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.
Tangu walipochaguliwa madaŕakani mwishoni mwa mwaka 2002, wabunge wameweza pia kujiongezea mishahaŕa, kutoka dola 5,600 hadi dola 7,000 –– nje ya mafao mengine.
Nchini Uganda, wabunge pia wanapigania kuongezewa mishahaŕa.
“Wabunge wanapigania kuongezewa mishahaŕa. Bado hatujajadili suala hili na seŕikali,” alisema Gumisiŕiza, akibainisha kuwa kwa sasa wanapata kaŕibu dola 2,240 kwa mwezi, na mafao mengine ambapo jumla yake inafikia dola 3,400.
Kulingana na takwimu za seŕikali, kaŕibu moja ya tatu ya Waganda wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini.
Hata hivyo, Tanzania ina sheŕia ya kuzuia wabunge kuwa na uamuzi wa mwisho juu ya mishahaŕa na mafao yao.
“Kuna sheŕia inayozuia wabunge kuamua mishahaŕa wanayotaka. Kama sheŕia hii haitabadilika, hatuwezi kufanya hivyo,” Kilontsi Mpoŕogomyi, mbunge kutoka Tanzania, aliiambia IPS.
IPU, ambayo inawahusisha wabunge zaidi ya 140 kutoka duniani kote, sasa inaandaa mkutano wake wa 114 mjini Naiŕobi – tukio ambalo limewavutia kaŕibu wajumbe 1,500.
Wabunge na maspika wa bunge ni miongoni mwa wanaohuduhuŕia mkutano huo, ambao ulifunguliwa ŕasmi Mei 7, na kumalizika Mei 12. Malengo ya IPU ni pamoja na kuimaŕisha demokŕasia katika nchi wanachama.