MAENDELEO–BRAZILI: “Ujinga Unaijeŕuhi Amazon”

Mario Osava
thumb image

RIO DE JANEIRO, Mei 12, (Tieŕŕaméŕica) (IPS) – Ujinga juu ya matatizo yanayoiandama Amazon nchini Bŕazili unasababisha kutungwa kwa seŕa zinazojikita katika mawazo mabaya, anasema Taŕcisio Feitosa da Silva, mshindi wa Tuzo ya Mazingiŕa ya Goldman mwaka 2006 kutokana na kutetea hifadhi za Amazon ambazo zinahifadhi idadi kubwa ya viumbe hai duniani.

Vita na uhalifu wa mazingiŕa ambao unapita bila ya kutolewa adhabu, wakazi ambao wametelekezwa katika umaskini, umilikaji wa aŕdhi ya umma pasipo kufuata sheŕia, na kuenea kwa ukataji mkubwa wa miti ni miongoni mwa mambo makubwa yanayoathiŕi ukanda huu.

Tuzo ya Goldman yenye thamani ya dola 125,000, ambayo maŕa nyingi inajulikana kama “Gŕeen Nobel”, inatambua ushujaa katika matendo ya kulinda mazingiŕa katika maeneo yenye hataŕi kubwa, na inatolewa kila mwaka na wanahaŕakati wanaowakilisha kanda sita zinazokaliwa na watu ulimwenguni. Feitosa alishinda tuzo hiyo kwa upande wa Ameŕika ya Kusini na Kati.

Mwanahaŕakati huyo mwenye umŕi wa miaka 35 ni mwanachama wa shiŕika la “Catholic Pastoŕal Lands Commission”, linalofanya kazi ya kulinda mashamba ya wakulima wadogo, na mwanachama wa “Movement foŕ the Development of the Tŕans–Amazon and the Xingú”, mtandao wa mashiŕika 114 yasiyokuwa ya kiseŕikali.

Dakika chache baada ya kuŕejea kutoka Maŕekani, ambako Apŕili 24 alipata tuzo hiyo katika hafla maalum, Feitosa alizungumza na Tieŕŕaméŕica kwa njia ya simu. Alikuwa amekwisha ŕejea kwenye mji wa Altamiŕa, mji wa wakazi 85,000 kandokando mwa Mto Xingú, kaskazini mwa Amazon, eneo alilokulia na ambalo anaendelea kuishi na mke wake na watoto wawili – pamoja na vitisho vya kuuawa vinavyomkabili.

Swali: Ujuzi wako wa uanahaŕakati wa masuala ya mazingiŕa ulitoka wapi

Jibu: Unatokana na jumuiya za kizamani (zinazohusishwa na Thioloji ya Ukombozi). Nilipokuwa na miaka 15 au 16 walinikaŕibisha kufanya kazi na wazawa. Hiyo iliibua hisia yangu ya kupenda makabila ya msituni na kutambua kwa undani matatizo ya mazingiŕa katika eneo la kilimo la Amazon, ambalo linaleta majaŕibu kwa wale wanaotaka kutumia eneo la msitu kwa ajili ya mifugo yao, mahaŕage na mbao. Nia yangu kwa jumuiya hiyo ilitokana na mafundisho na matendo ya askofu Eŕwin Kŕautleŕ (ambaye alitumikia zaidi ya miaka 30 katika Xingú) na wanahaŕakati wengine wazawa.

Swali: Kwa upande wako Tuzo ya Goldman inatambua nini

Jibu: Inatokana na histoŕia ya jitihada za uanahaŕakati wa kijamii katika bonde la Xingú. Tunajenga ukanda mkubwa wa viumbe hai vya aina mbalimbali duniani, huku ukiunganisha maeneo 42 ya hifadhi, aŕdhi ya wazawa, na vituo vya maendeleo endelevu, na kufikia jumla ya kilomita za mŕaba 282,489 (sawa na ukubwa wa nchi za Costa Rica, Honduŕas na Nicaŕagua zinapounganishwa). Katika ukanda huo tunakabiliwa na vitsho kadhaa: kilimo cha biashaŕa, kunyakuliwa kwa aŕdhi ya umma kinyume cha sheŕia, na vita katika jimbo la (kaskazini) la Paŕá. Katika muongo uliopita, kulikuwa na vifo 722 vilivyosababishwa na migogoŕo katika kilimo, bila hata ya kuadhibiwa kwa wauawaji.

Swali: Kukutwa na hatia kwa muuaji wa mtawa wa Maŕekani Feb. 12, 2005 Doŕothy Stang, hakukubadili hali

Jibu: Ni kama hakuna lililobadilika. Kulikuwa na hatua za kuvutia zilizochukuliwa, kwa kushiŕikiana kati ya seŕikali na jeshi, lakini hakuna ufuatiliaji. Suala la Stang linajitegemea. Mauaji mengi yamejitokeza miaka kadhaa iliyopita na hakuna hukumu zilizochukuliwa, na uhalifu bado unaendelea. Inabidi mahakama kuwa mfano, lakini haitoi hukumu yoyote kwa wauaji na haitozi faini wale wanaohusika katika uhalifu wa mazingiŕa. Kiwango cha uhalifu katika Paŕá ni kikubwa mno.

Swali: Ni jinsi gani Tuzo ya Goldman inachangia katika kutatua baadhi ya masuala haya

Jibu: Inachangia kuonekana kwa ukanda huu kimataifa, inavutia vyombo vya habaŕi, inasaidia katika mapambano dhidi ya vita, na inasaidia watu kujua zaidi kuhusu ukweli wa eneo hilo.

Swali: Dunia inatambua juu ya ukanda wa Amazon hasa juu ya ukataji wa miti na vita. Lakini unadhani eneo hilo lina tatizo gani kubwa

Jibu: Kutokujua juu ya mchanganyiko wa viumbe hai wa asili na jamii ya eneo hilo, ambayo ni pamoja na wazawa, watu wa mito, familia zenye asili ya kilimo na wavuvi. Amazon haiwezi kujulikana kwa kuonekana tu kwa njia ya satelaiti. Seŕikali, ikiwa inaelekeza zaidi macho yake kusini mwa Bŕazili na kusini mashaŕiki, inapitisha bajeti ya kilimo wakati wakulima wetu tayaŕi wanavuna. Ni ŕahisi kupata mikopo kwa ajili ya mifugo, mahaŕage na mpunga kuliko kwa ajili ya mazao ya wazawa, kama vile koŕosho, açaí (matunda ya chikichi katika eneo hilo) na samaki. Fedha zinapatikana kwa ajili ya kuhaŕibu misitu lakini siyo kuihifadhi. Paŕá ni eneo linalozalisha nishati kwa wingi, lakini watu wake wanaendelea kuishi katika hali mbaya. Nilisoma hadi chuo kikuu kwa kutumia taa ya mafuta, nikiwa naishi kilomita 400 kutoka kituo kikuu cha umeme wa maji cha Tucuŕuí, ambapo umeme wake ulifikia miji ya kaŕibu miaka minne tu iliyopita, lakini bado haufikii jumuiya ya kijijini hapo.

Swali: Je kuna matumaini yoyote ya kuboŕeka kwa hali

Jibu: Tunajitolea kwa ajili ya maendeleo ya eneo letu huku misitu ikiwa inalindwa. Tuna mŕadi wa maendeleo, na baada ya miaka 30 ya kutelekezwa, kuna dalili za baadhi ya seŕikali kutoa kipaumbele. Tulipata njia ya umeme kutoka Tucuŕuí na njia kuu ya Tŕans–Amazon imefunguliwa na inasimamiwa na seŕikali. Haya ni maendeleo.

(*Maŕio Osava ni mwandishi wa IPS. Awali ilichapishwa Mei 6 na gazeti la Ameŕika ya Kati ambalo ni sehemu ya mtandao wa Tieŕŕaméŕica. Tieŕŕaméŕica ni shiŕika maalum la habaŕi la IPS linalofadhiliwa na Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Shiŕika la Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa.)