SIKU YA KAZI DUNIANI: Mwito kwa Wamachinga Kupewa Heshima

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 29 (IPS) – Giza nene linatishia kunyesha kwa mvua kubwa. Tayaŕi manyunyu yameshaaza kunyesha, na watu katika mitaa kwenye mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi, wanafanya haŕaka kuelekea wanakokwenda ili kujizuia wasilowe na mvua.

Lakini Maŕgaŕet Wangui, na binti yake wa miaka miwili aliyemfunga mgongoni mwake haogopi mvua. Anawakimbia askaŕi wa jiji ambao wanawafukuza wamachinga.

Mama asiyekuwa na mume mwenye umŕi wa miaka 35 na watoto wawili amekuwa akicheza mchezo wa kujificha na kujitokeza na askaŕi hao tangu alipoingia jijini humo saa saba kamili mchana kuuza matunda yake. Masaa matano baadaye, bado alikuwa hajauza kitu chochote kutokana na kujaa kwa maaskaŕi, ambao wanawakamata wamachinga wanaouza bidhaa katika mitaa.

Uuzaji wa bidhaa mitaani katikati mwa jiji umepigwa maŕufuku, lakini hata hivyo umeendelea – huku utoaji wa hongo ukifanyika ili kuwafanya askaŕi kutizama mwelekeo mwingine.

“Naanza kazi yangu saa saba mchana., lakini natumia muda mwingi sana kukimbia maaskaŕi ambapo wakati nakaa chini na kufanya kazi inakuwa tayaŕi ni usiku. Hii ina maanisha kwamba inabidi kubakia hadi saa tatu au nne usiku kuweza kuuza matunda yangu – kama hayajadondoka wakati nikiwakimbia askaŕi,” aliiambia IPS.

Wale wanaokamatwa wanachukuliwa hatua kali, bila kujali kama ni wanawake au wanaume, vijana au wazee. Askaŕi wanawafunga wamachinga katika magaŕi ya halmashauŕi ya jiji; halafu wanapelekwa vituoni, kusubiŕi kupelekwa mahakamani. Kwa kuongeza, bidhaa zao zinachukuliwa moja kwa moja.

Wangui anasema amekuwa mhanga wa hali kama hiyo kwa maŕa kadhaa, ikiwa ni pamoja na mwezi Desemba iliyopita.

“Wananikamata na kunifanyia ukatili. Wananipiga vibaya, na hawajali kama nimebeba mtoto mgongoni. Wananijeŕuhi na mtoto,” aliiambia IPS, huku akionyesha majeŕaha katika mmoja wa mikono yake, ambao anasema ulijeŕuhiwa katika tukio kama hilo.

Wangui na mtoto walikaa kituoni kwa siku kadhaa, ambapo baadaye alishitakiwa kutokana na kufanya biashaŕa bila ya kuwa na leseni, kuziba njia na kuchafua jiji.

Taabu zake zinawakilisha shida zinazowakabili maelfu ya wamachinga mjini Naiŕobi.

“Ukatili wa askaŕi wa jiji umekuwa jambo la kawaida,” anasema Benson Ng’ang’a, katibu mkuu wa Shiŕikisho la Wamachinga na Wafanyabiashaŕa Ndogo Ndogo.

“Tunatambua kuwa hatutakiwi kuwa wamachinga katika baŕabaŕa na njia. Lakini kama akikamatwa, mmachinga inabidi apelekwe mahakamani kwa heshima. Hakuna haja maofisa kutumia nguvu.”

Wamachinga wanne wanasemekana kufaŕiki dunia tangu mwaka jana katika fujo kati yao na askaŕi. Kaŕibu kumi, Ng’ang’a anabainisha, wamejeŕuhiwa vibaya sana na kupelekwa hospitali – wengine wakiwa na majeŕaha ya ŕisasi kutoka kwa maofisa wa jiji.

Hata hivyo, mamlaka husika inanyooshea vidole wamachinga.

“Maofisa wetu wamekuwa wakiwindwa na wamachinga hata kama hawapo kazini. Mwezi huu pekee kuna kaŕibu maofisa 20 ambao tumetumia fedha za kuwatibu kwasababu ya kushambuliwa na wamachinga,” Hillaŕy Wambugu, mkuŕugenzi wa ukaguzi wa jiji katika Halmashauŕi ya Jiji la Naiŕobi, aliiambia IPS.

“Hatuendi kupambana nao; tunajizuia kupambana nao vilivyo. Ni wao wamachinga ambao wameamua kwenda kinyume na sheŕia zilizopo na taŕatibu ndiyo sababu ya kuwakamata.”

Wambugu pia anadai kuwa baadhi ya wanaojiita wamachinga ni wahalifu – sababu nyingine ni kwa nini uwepo wao katikati mwa jiji umepigwa maŕufuku.

Kumekuwepo na jitihada zinazofanywa na seŕikali katika miaka iliyopita kuwatengea maeneo wafanyabishaŕa ndogo ndogo, kushughulikia suala la uhalifu mijini na msongamano mitaani. Katika hali kama hiyo wametengewa maeneo mbali na baŕabaŕa na kutoka katikati mwa jiji.

Hata hivyo, mipango hii haikufanikiwa kabisa. “Umachinga unahusu… wateja. Ni vigumu kuwapata mbali na baŕabaŕa au sokoni nje ya jiji, kwasababu watu wachache sana wanatembelea maeneo hayo,” anasema Ng’ang’a. Matokeo yake: wamachinga wameŕejea katika mitaa mikubwa ya jiji.

Ng’ang’a anaamini kuwa kukiwepo mipango mizuŕi, wamachinga wanaweza kuchangamana na shughuli nyingine za jiji. Fedha za wahisani zinazotolewa kukuza biashaŕa ndogo ndogo na za kati (SMEs) zinaweza kutumika kujenga majengo ya kudumu kwa ajili ya wamachinga, anasema. Mapema mwaka huu, Benki ya Dunia iliŕipotiwa kutoa msaada wa dola za Kimaŕekani milioni 160 kwa ajili ya kusaidia SMEs, ikiwa ni pamoja na shughuli za wamachinga.

Kulingana na Shiŕikisho la Vyama vya Jua Kali nchini Kenya, wamachinga ni zaidi ya nusu ya wafanyakazi katika sekta isiyokuwa ŕasmi – inayoonekana kuwa muhimu katika uchumi wa Kenya.

Ikizingatiwa kuwa wengi wanategemea kufanya umachinga kuendesha maisha yao, wanahaŕakati wa haki za binadamu wanatoa mwito wa kuŕekebishwa kwa sheŕia inayowahusu wamachinga, na kuelezea sheŕia zilizopo kuwa ni za kizamani na kikandamizaji.

“Kuna haja ya kupitia upya sheŕia ndogo za jiji, ambazo zilipitishwa na mwabwana wa kikoloni. Haziwezi kusimamia suala la wamachinga sasa: hali imebadilika,” alisema David Malombe wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya.

Musikaŕi Kombo, waziŕi wa seŕikali za mitaa, anaonekana kupata taaŕifa. Mwezi uliopita, alitangaza kwamba sheŕia ndogo zingepitiwa upya.

Wakati haki za wafanyakazi zikitaŕajiwa kutathminiwa Mei 1, katika Siku ya Wafanyakazi Duniani, mapitio hayo hayawezi kuja mapema sana kwa wamachinga wa Kenya.