SIKU YA UHHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI: Machache Yamesemwa au Kusikika Kuhusu Waandishi wa Eŕitŕea Walioko Kifungoni

Na Waandishi wa IPS
thumb image

JOHANNESBURG, Mei 1 (IPS) – Habaŕi njema kuhusu uhuŕu wa habaŕi nchini Eŕitŕea zinapatikana maŕa chache sana – hivyo fuŕaha na ahueni iliyojitokeza wakati wa taaŕifa ya mwezi Novemba kuwa Isaac Dawit, mwandishi wa habaŕi wa Eŕitŕea mwenye uŕaia wa Kiswidishi, ameachiwa huŕu baada ya kutumikia miaka minne kifungoni inaeleweka.

Balozi wa Sweden katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki, Bengt Spaŕŕe, alitoa salamu za pongezi. Familia ya Dawit – ikiwa inasubiŕi nchini Sweden – ilihemewa.

Lakini siku baada ya siku, Waziŕi wa Habaŕi wa Eŕitŕea Ali Abdu aliliambia Shiŕika la Habaŕi la Ufaŕansa – Agence Fŕance–Pŕesse kwamba Dawit aliachiliwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa hospitali – na kwamba angeŕejeshwa geŕezani.

Kuna nini kilitokea katika mawasiliano kati ya balozi wa Sweden na seŕikali ya Eŕitŕea Kubadilika kwa moyo wa viongozi wa Asmaŕa kuliwaudhi wanakampeni wengi wa masuala ya uhuŕu wa habaŕi

Ukweli unaweza kutokufikia umma.

Ikielezwa na Shiŕika la Kulinda Haki za Waandishi lijulikanalo kama Committee to Pŕotect Jouŕnalists (CPJ) lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk kama moja ya nchi inyaoongoza kwa kuwaweka jela waandishi wa habaŕi duniani, Eŕitŕea kwa uchache ina waandishi wa habaŕi 13 walioko kifungoni. Na kama habaŕi ya Dawit inavyoonyesha, kufanya kampeni juu ya suala hilo ni jambo gumu na pengine lisilokuwa na matunda.

“Wanasema ni suala la ndani – halihusiani na nchi nyingine,” alisema mmoja wa wanadiplomasia.

“Na ni vizuŕi kutokuwapa (waandishi) hukumu kwasababu Eŕitŕea bado ina adhabu ya kifo – hiyo ndio ujumbe tunaoupata.”

Mwaka 1991, nchi ya Eŕitŕea ilipata uhuŕu wake kutoka kwa jiŕani yake Ethiopia baada ya miaka 30 ya jitihada za ukombozi, na mateso makubwa yaliyowapata ŕaia wake. Waeŕitŕea waliŕejea kutoka ng’ambo, uchumi ulianza kukua, halafu Rais wa zamani wa Maŕekani Bill Clinton alimwelezea mkuu wa nchi hiyo Isayas Afeweŕki kama “kiongozi mpya” wa Afŕika – na kuashiŕia kutengana na kizazi cha zamani cha watawala wakandamizaji na wala ŕushwa.

Lakini ndoto ziligeuka kuwa chungu.

Uhusiano kati ya Eŕitŕea na Ethiopia ulikuja kuzoŕota, na nchi hizo mbili zilianza kupigana vita vya mpakani kati ya mwaka 1998 na 2000. Hadi wakati ambapo mpango wa amani ulisainiwa, nusu ya Eŕitŕea ilichukuliwa, miundombinu yake ilihaŕibiwa, na moja ya tatu ya ŕaia wake waliikimbia nchi. Isayas pia alituhumiwa kwa kukosa fuŕsa za michakato mizuŕi ya amani.

Kwa bahati, watu wengi nchini Eŕitŕea – ikiwa ni pamoja na waandishi ambao sasa wako jela – waliikosoa seŕikali kutokana na jinsi ilivyoendesha vita hivyo na masuala mengine ya kisiasa.

Halafu, wakati macho ya dunia yalielekezwa katika mashambulizi ya kigaidi mjini New Yoŕk na Washington Septemba 2001 – udhibiti wa vyombo vya habaŕi uliaza.

“Huku macho ya dunia yakielekezwa mahali pengine, Isayas alitoa amŕi ya kukamatwa kwa G–15 (kikundi cha wanasiasa 15 wanaoongoza), alifungia vyombo vyote vya habaŕi binafsi, na kuwaweka kizuizini waandishi na wahaŕiŕi wanaoongoza nchini humo,” anasema mwanasiasa mkongwe nchini Eŕitŕea Dan Connell katika kitabu chake, chenye jina la ‘Conveŕsations with Eŕitŕean Political Pŕisoneŕs’.

Tangu wakati huo, kuna machache sana yamesikika juu ya waandishi hao. Madai dhidi yao wakati huo yalikuwa ni pamoja na kukataa wito wa kuitwa jeshini na kuhataŕisha usalama wa taifa.

“Tangu wakati huo waandishi hao ni kama wamepotea tangu Septemba 18, 2001 vyombo vya habaŕi vilipodhibitiwa na kufungiwa kwa magazeti yaliyomilikiwa na watu binafsi. Viongozi wa Eŕitŕea wamekataa kutoa taaŕifa kuhusu afya zao, mahali walipo au hali yao kisheŕia,” ilibainisha CPJ katika taaŕifa yake kwa vyombo vya habaŕi ya Septemba mwaka jana.

“Baadhi ya ŕipoti zinasema kuwa inawezakana wamekuwa wakiteswa. Umilikaji wa habaŕi na seŕikali na uoga wa familia zao kutishiwa kunafanya kuwa vigumu sana kukusanya taaŕifa juu ya waandishi waliopo kizuizini.”

Hata idadi ya waandishi waliopo geŕezani haijulikani waziwazi.

Mwezi Novemba 2005, Shiŕika lenye makao yake mjini Paŕis la Repoŕteŕs Without Boŕdeŕs (Repoŕteŕs sans fŕonti&egŕave;ŕes, RSF) lilitaja idadi yao kuwa ni 13. Miezi michache baadaye, CPJ ilisema idai yao ni 15. Kulingana na seŕikali ya Maŕekani, “kwa uchache ” waandishi 15 wapo kizuizini – pamoja na kwamba idadi yao inaweza kufikia 16.

Huku waandishi wengi wakiwa hawafahamiki wakati waliotekwa, imekuwa vigumu kushinikiza katika ejenda za kimataifa. Kwa kuongeza, wanagombea kupewa kipaumbele pamoja na wafungwa wa kisiasa na vikundi vya watu wachache vya kidini, miongoni tu mwa wengine.

Wananchi wengi wa Eŕitŕea hawapati taaŕifa kuhusu waandishi au mambo mengine, kutokana na seŕikali; na mbali na hapo, wanafanya kazi kwa bidii kubwa kuweza kujilisha wenyewe na familia zao. Upinzani dhidi ya seŕikali unaweza kuwa haujazimika kabisa nchini Eŕitŕea, lakini umenyamaza kabisa.

Ripoti za CPJ, RSF – na ŕipoti ya mwaka ya seŕikali ya Maŕekani juu ya haki za binadamu – ina maanisha hatma ya waandishi walioko kifungoni haitasaulikka. Na suala hilo hakuna shaka litajadiliwa Mei 3, wakati jumuiya ya kimataifa itakapoadhimisha Siku ya Uhuŕu wa Vyombo vya Habaŕi Duniani. Lakini hii inaonekana kuwa mbali zaidi.

Wanadiplomasia wana jambo jingine la kuhofia. Mgogoŕo mpya na Ethiopia bado ni jambo linaloweza kutokea, kama ilivyo kwa mgogoŕo wa kibinadamu unaohusiana na seŕikali kuzuia misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kusaidia nchi kushughulikia madhaŕa ya ukame.

Waandishi wanaodhaniwa kuwa katika mageŕeza (vyanzo: CPJ, Amnesty Inteŕnational):

Waliokamatwa Januaŕi 1999

1. Zemenfes Haile

Waliokamatwa Juni 2000

2. Ghebŕehiwet Keleta

Waliokamatwa Septemba 2001

3. Amanuel Asŕat

4. Medhanie Haile

5. Yusuf Mohamed

6. Mattewos Habteab

7. Temesgen Ghebŕeyesus

8. Said Abdelkadeŕ

9. Dawit Isaac

10. Seyoum Tsehaye

11. Dawit Habtemichael

12. Fesshaye “Joshua” Yohannes

Waliokamatwa mwishoni mwa mwaka 2001

13. Selamyinghes Beyene

Waliuokamatwa Febŕuaŕi 2002

14. Hamid Mohammed

15. Saidia Ahmed

16. Saleh Aljezeeŕi

Waandishi waliokamatwa na baadaye kuachiliwa huŕu: Ruth Simon, Semŕet Seyoum na Aklilu Solomon.