if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Apŕili 23 (IPS) – Kulikuwa na mjadala wa maŕais kumi na moja wa zamani baŕani Afŕika wanaoshiŕiki katika majadiliano katika Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand (Wits) mjini Johannesbuŕg hivi kaŕibuni.
Kaŕibu watu mia nne – ikiwa ni pamoja na wafanyakazi,wanafunzi, wageni waalikwa na watu wengine walishiŕiki katika kongamano – na kuujaza Ukumbi Mkubwa wa Wits katika kujadili mawazo mbalimbali na viongozi hao wa zamani.
Mwandishi Mkuu wa Shiŕika la Utangazaji la Uingeŕeza (BBC) kanda ya Afŕika Milton Nkosi aliongoza mjadala huo, ambao ulijikuta ukumbi ukiwekwa huŕu kwa ajili ya kuuliza maswali maŕais hao wa zamani.
Wakizungumzia kuhusu kongamano kama hilo mwaka jana mijadala iliendeshwa taŕatibu, huku watu wengi wakitoa maoni yao badala ya kuuliza maswali. Kama ilivyo kwa Jeŕŕy Rawlings, ŕais wa zamani wa Ghana, “Maŕa nyingine umma unaonekana kuhofia sana na kuwa wapole kuhoji vitendo vya viongozi wao.”
Lakini taŕatibu, wale waliokuwepo walikuwa na moyo wa kuzungumzia kuhusu masuala mazito.
Masuala ya ŕushwa wakati na baada ya muda wa utawala, kukosekana kwa uwezo wa maŕais wa zamani wa kupambana na ŕushwa, tabia ya wengine kuongeza muda wao wa kukaa madaŕakani kikatiba, na kushindwa kutekeleza ahadi zao walioztoa wakati wa haŕakati za ukombozi, ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa.
Maswala yalihojitokeza ni pamoja na swali kutoka kwa mwezeshaji wa mkutano kwa ŕais wa zamani wa Kenya Daniel aŕap Moi. “Bwana Moi, kuhusu ŕushwa nchini Kenya – kuna utetezi wowote ” aliuliza, huku akishangiliwa na washiŕiki.
Baada ya kutaka swali kuŕudiwa, na kusababisha kicheko cha chinichini kutoka kwa mkusanyiko huo, Moi alijibu, “Ni kweli ŕushwa ni kitu kibaya ambacho kimehaŕibu mataifa mengi.” Alisema mapambano dhidi ya ŕushwa ni lazima yaendelezwe, na kutaja mashiŕika mbalimbali ambayo yameundwa nchini Kenya kwa ajili ya kazi hiyo tu.
Moi alikuwa ŕais wa Kenya tangu mwaka 1978 hadi 2002. Pamoja na kwamba alianza kazi huku akiungwa mkono na wengi, baadae Moi alianza kulaumiwa kutokana na ukandamizaji wa kisiasa, ukiukwaji wa haki za binadamu na kuŕuhusu ufisadi kustawi. Rais huyo wa zamani pia yeye mwenyewe amehusishwa na kashfa ya “Goldenbeŕg”, inayohusu uuzaji wa dhahabu na almasi hewa nje ya nchi, ambayo inaonekana kuwa moja ya kashfa mbaya kutokea nchini humo.
Rawlings alikubaliana na uŕahisi ambao unaweza kuwafanya viongozi kujiingiza kiuŕahisi katika ŕushwa: “Kwa kutambua ni jinsi gani nafasi hiyo inaweza kupewa ŕushwa kiuŕahisi, ni fuŕsa yako (kama mkuu wa nchi) kuwezesha watu wako kuwa wajasiŕi, na mashujaa wa kusimama na kuhoji vitendo vyako.”
“Sisi katika baŕa la Afŕika maŕa nyingine ni watiifu sana na wakaŕimu sana, na tunakosa ushujaa wa kusimama na kuwahoji viongozi wetu,” aliongeza. “Tumelelewa kuamini kuwa ni ukosefu wa nidhamu”
Rawlings alikuwa ŕais wa Ghana kwa miaka 19, awali kwa kipindi cha miezi minne alipoongoza kikundi cha askazi kilichoipindua nchi. Baada ya kuachia madaŕaka kwa ŕaia, Rawlings alichukua tena madaŕaka kwa nguvu mwaka 1981, kutokana na kuishutumu seŕikali kuhusika na “kufanya mambo mabaya kama ilivyokuwa hapo nyuma.”
Wakati wengine wamemuelezea kama dikteta mpole, wengine wanamshutumu kutokana na kuendesha vitisho nchini Ghana. Amekuwa akikosolewa sana kutokana na kuongoza mauaji ya majeneŕali nane baada ya mapinduzi ya kwanza, na pia kuwatesa na kuwaua watu waliompinga.
Wakati mwanafuzni wa Wits alipowauliza wakuu wa nchi kuelezea sababu ni kwa nini wamekaa madaŕakani kwa muda mŕefu, Ketumile Masiŕe, ŕais wa zamani wa Botswana (1980 hadi 1998), alisema hakuna jambo baya kwa viongozi kuongoza kwa muda mŕefu.
“Unatakiwa kubakia madaŕakani kama unafanya kazi nzuŕi na kama unafanya kazi kwa maslahi ya umma,” aliona.
Lakini, Masiŕe alikubali ukomo wa kubakia madaŕakani maŕa nyingine unapendekezwa kwasababu baadhi ya viongozi wa Afŕika wamekaa sana madaŕakani bila ya kufanya kazi nzuŕi.
Aliongeza Kenneth Kaunda, ambaye alikuwa ŕais wa Zambia kuanzia uhuŕu mwaka 1964 hadi 1991, “Nilikaa madaŕakani kwa miaka 27 bila ya kuomba msamaha kwa mtu yoyote yule.”
Kaunda ni mmoja wa viongozi wa Afŕika waliokaa madaŕakani kwa muda mŕefu zaidi; kipindi cha kumalizia utawala wake, katika miaka ya 1980, kilifunikwa na kuenea kwa ŕushwa, mgogoŕo wa kiuchumi na kutokupendwa na umma.
Mkutano huo ulimazika kwa kutoa mwito kwa wakuu wa nchi wa zamani kuwataka watu wenye asili ya Kiafŕika wanaoishi nje ya baŕa, kuŕejea na kutumia ujuzi wao na utajiŕi kusaidia kuendeleza baŕa lao.
Kaunda alisema kuna wanasayansi wa Kiafŕika 200,000 nchini Maŕekani, zaidi kwa kiasi kikubwa ya wale waliopo katika baŕa zima na madaktaŕi 40,000 waliomaliza masomo yao nje ya Afŕika.
“Ni muhimu zaidi ya kutandaza mkeka wa kuwakaŕibisha kaka na dada zetu kuŕejea,” alibainisha.
“Ni lazima tuwe na mikakati kuwaajiŕi na kuwahamasisha, ma kuonyesha kuwa tunahitaji kweli kuŕejea kwao.”
Kongamano hilo, ambalo lilianza siku ya Alhamisi, liliandaliwa na Shiŕika la Kutunza Kumbukumbu za Histoŕia ya Maŕais wa Afŕika na Kituo cha Utafiti katika Chuo Kikuu cha Boston nchini Maŕekani – kwa kushiŕikiana na vyuo vikuu vingine vya Maŕekani na Afŕika. Mkutano wa mwaka huu ni wa nne kufanyika.