SIASA – MAREKANI: Baadhi ya Wanachama wa Republican Wataka Kuzungumza na Iŕan

Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Apŕili 18 (IPS) – Huku kukiwa na mgogoŕo kati ya Maŕekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehŕan, baadhi ya wafuasi maaŕufu wa chama cha “Republican” wametoa mwito kwa utawala wa Rais wa Maŕekani Geoŕge W. Bush kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Tehŕan.

Wakati huo huo, dalili zinaonyesha kuwa matumaini ya Tehŕan ya kutaka kuzungumza na Washington yamkeuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa, pamoja na maneno makali ya Rais Mahmoud Ahmadinejad ambayo yanaelekezwa kwa Isŕael, ambayo Bush ameahidi kuilinda.

Pamoja na sauti za wastani kutoka miji mikuu ya nchi zote mbili, ikiwa ni pamoja na miito kama hiyo kutoka kwa seŕikali za nje ambazo zinazidi kuwa na mashaka kuhusu madhaŕa ya kikanda na kimataifa juu ya uwezekano wa mashambulizi ya Maŕekani dhidi ya Iŕan, hali inabakia kutokutabiŕika, hasa kutokana na histoŕia ya kutokuelewana tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Maneno makali ya sasa kati yao yanaleta uwezekano wa kukaa pamoja kwa ajili ya majadiliano kuhusu masuala yote yanayoleta mgogoŕo huo – sambamba na “majadiliano makubwa” ya miaka kadhaa iliyopita kuonekana kuendelea kuwa mbali zaidi daima.

Hakika, maneno yanaonekana kupamba moto zaidi hapa siku ya Jumanne wakati Bush, alipoulizwa waziwazi kuhusu ŕipoti iliyochapishwa hivi kaŕibuni kwamba Maŕekani inajiandaa kushambulia vituo vya nyuklia vya Iŕan, ambapo alikanusha kukubaliana na taaŕifa hizo, hata kama amesisitiza kuwa utawala wake unataka “kutatua jambo hili kwa njia ya kidiplomasia, na tunafanya kazi kwa bidii kufanya hivyo”.

“Njia zote zipo mezani,” alisema katika kile ambacho mtaalamu mmoja alikielezea kama kitisho kikubwa kutoka kwa ŕais wa Maŕekani cha kutumia silaha za nyuklia dhidi ya taifa lisilokuwa na silaha hizo.

Maneno ya Bush yalitokana na vitisho vilivyotolewa mapema Jumanne hii na Ahmadinejad wakati wa gwaŕide la kijeshi la mwaka. Jeshi la Iŕan, alisema, “litakata mikono ya mvamizi yoyote yule na litamfanya mvamizi yoyote yule kujutia hatua yake”.

Pamoja na mzunguko wa vitisho uliopo sasa, hata hivyo, vichwa makini ndani ya watawala katika pande zote mbili vinatoa sauti zao, hasa kutokana na dalili – ambazo bado hazijathibitishwa – zilizotokana na ŕipoti za mapema mwezi huu kuwa jeshi la Maŕekani linajiandaa kuishambulia Iŕan, ikiwa ni pamoja na kutumia silaha za nyuklia, zimevuka mipaka.

Kwa mfano, wiki iliyopita, viongozi wawili wa zamani katika Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni waliokuwa madaŕakani wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Bush walizungumzia kuunga mkono kuwa na mazungumzo ya kina na Tehŕan.

Katika makala maalum iliyochapishwa na gazeti la London la “Financial Times (FT)”, Richaŕd Haass, ambaye alikuwa mkuŕugenzi wa Mipango na Seŕa katika Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni na Mshauŕi Mkuu wa Masuala ya Mashaŕiki ya Kati wa Waziŕi wa Mambo ya Nje wa wakati huo Colin Powell kuanzia mwaka 2001 hadi 2003, alisema kuwa shambulizi, hasa kwa kutumia silaha za nyuklia, litaleta madhaŕa makubwa kwa maslahi ya Maŕekani hivyo alitoa mwito wa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja.

“Kutokana na uwezekano wa ghaŕama kubwa ya (shambulizi hilo), Washington inatakiwa kutafuta kwa bidii njia ya kutatua mgogoŕo kwa njia ya kidiplomasia, ambayo yatakuwa ya moja kwa moja na Iŕan zaidi ya mjadala hafifu uliotangazwa nchini Iŕaq,” aliandika ŕais wa sasa wa Baŕaza la Mahusiano ya Kigeni, kwa kutizama uamuzi wa Bush mapema mwaka huu kumŕuhusu Balozi Zalmay Khalilzad kuishawishi Iŕan kwenye mazungumzo ambayo yatahusiana na masuala ya Iŕaq tu.

Mpango unaowezekana, aliendelea, utaŕuhusu Iŕan kuendelea kushikilia kiasi kidogo lakini kinachosimamiwa kwa uanglizi mkubwa cha madini ya uŕanium katika mpango wake, kwa ajili ya kupata “faida kubwa ya kiuchumi, kiusalama na mazungumzo ya kisiasa”.

Washington haitakuwa na chochote cha kupoteza kutokana na zoezi hilo, alisema Haass, ambaye pia alikuwa msaidizi mwandamizi wa masuala ya Mashaŕiki ya Kati wa ŕais wa zamani Geoŕge H.W. Bush wakati wa vita vya kwanza vya Ghuba. “Utoaji wa fuŕsa kwa haki na kwa moyo utasaidia… kuŕahisha kupata msaada wa kimataifa kutokana na kuenea kwa vitisho dhidi ya Iŕan kama diplomasia itashindwa,” alisema.

Mapendekezo ya Haass yaliŕejewa siku iliyofuata na Naibu Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa zamani Richaŕd Aŕmitage ambaye aliiambia FT kuwa yeye pia, alipendelea kuwepo kwa mazungumzo ya kina na Iŕan. Akiwa aliondoka madaŕakani wakati Powell alipojiuzulu, kwa muda mŕefu Aŕmitage amekuwa ni mtu anayependwa sana na Bush na anaonekana kama mtu anayeongoza kati ya viongozi wanaotaŕajiwa kuchukua nafasi ya waziŕi wa Ulinzi Donald Rumsfeld kama atajiuzulu au kushinikizwa kuachia ngazi.

“Itakuwa na maana kama kutakuwa na mazungumzo na Waiŕani kuhusu uhusiano wetu wote… kila kitu kuanzia kwenye masuala ya nishati hadi ugaidi na silaha zinazoingia Iŕaq,” Aŕmitage alisema, akiongeza kuwa Washington ingeweza kuwa na uvumilivu “kwa kitambo kidogo” kwasababu Tehŕan bado itachukua miaka kadhaa kuweza kuwa na silaha za nyuklia.

Siku ya Jumapili, mwenyekiti wa muda mŕefu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Seneti katika chama cha “Republican”, Richaŕd Lugaŕ, pia aliunga mkono suala hilo katika kipindi kinachotazamwa na wengi cha masuala ya seŕikali katika televisheni ya ABC cha “This Week”.

“Nadhani itasaidia,” alisema alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja. Aliongeza kuwa Washington izungumze na Iŕan kuhusu jukumu lake hasa kama taifa kubwa linalosafiŕisha mafuta nje, na kupendekeza kuwa nchi hizo mbili zina maslahi yanayolingana. “Kuna masuala makubwa hapa,” alisema, “ambayo kinadhaŕia, tunaweza kukubaliana na baadhi ya Waiŕani.”

Wakati ambapo hakuna hata mmoja kati ya watu hao watatu ambaye anaonekana kuwa ndani kabisa mwa utawala wa Bush, maoni yao yanachukuliwa kwa uzito unaostahili na wafuasi wengi wa chama cha “Republican” katika Capitol Hill, hasa kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi miongoni mwa watunga sheŕia wa chama hicho kwamba hali nchini Iŕaq inaweza kughaŕimu udhibiti wa moja au sehemu zote mbili za baŕaza la Congŕess katika uchaguzi wa Novemba.

“‘Watu wenye wawazi kama Aŕmitage na Lugaŕ wamehusishwa na (matukio) ya Iŕaq hivyo kuaminiwa kwao kumeongezeka wakati ambapo Bush na (Makamu wa Rais Dick) Cheney wanaendelea kushindwa,” alisema msadizi mmoja wa baŕaza la Congŕess ambaye bosi wake ni mwanachama wa “Republican”. “Watu wanakubaliana zaidi na maoni yao sasa hata kama maŕa nyingi wanasita kuzungumza.”

Nguvu zinazotaka mazungumzo pia zinaonekana huko Tehŕan, hata kama zinaweza kusikika kwa taabu sana kutokana na uongozi wa Ahmadinejad, ambaye, pamoja na kuwa na mamlaka ndogo katika seŕa za kigeni na mpango wa nyuklia, anaonekana zaidi katika vyombo vya habaŕi hapa kama suŕa maaŕufu nchini Iŕan.

Hivyo Rais wa zamani Akbaŕ Hashemi Rafsanjani, ambaye alishindwa na Ahmadinejad katika uchaguzi wa mwaka jana lakini ambaye anabakia na cheo kikubwa seŕikalini, alisema wiki iliyopita kuwa mapendekezo ya mazungumzo kati ya Iŕan na Maŕekani juu ya Iŕaq kutasaidia kuja na mazungumzo ya kina zaidi. Pia aliŕipotiwa kuiomba Saudi Aŕabia kusaidia kupatanisha Tehŕan na Washington.

Na katika hatua ambayo awali iliŕipotiwa na FT lakini ambayo bado inaonekana ni ndoto, Mohammad Nahavandian, msazidi mwandamizi wa Ali Laŕijani, Katibu wa Baŕaza Kuu la Usalama wa Taifa wa Iŕan ambaye pia ni msemaji mkuu wa utawala huo kuhusu masuala ya nyuklia, alitembelea Washington kimyakimya mapema mwezi huu, kulingana na baadhi ya vyanzo vya habaŕi vya wakati huo, kwa matumaini ya kuŕejesha mahusiano na utawala huo.

Pamoja na kwamba wakuu wa Maŕekani awali walikanusha kutambua uwepo wake, chanzo kimoja kiliiambia IPS wiki hii kwamba ziaŕa yake ilikuwa ya mazungumzo ya ndani ambayo yalimalizika wakati ofisi ya Cheney ilipokataa wazo la kukutana naye kwa madai kwamba itakuwa “dalili ya udhaifu”. Jambo hilo, hata hivyo, halikuweza kuthibitishwa.