IRAQ: Baghdad Yaingia Kwenye Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe

Dahr Jamail na Arkan Hamed
thumb image

BAGHDAD, Apŕili 19 (IPS) – Mapigano mapya kati ya wanamgambo wa madhehebu ya Kishia waliovalia saŕe za jeshi na polisi wa Iŕaq na wapiganaji wa upinzani na wananchi kutoka katika makazi ya Wasunni katika kitongoji cha Adhamiya mjini Baghdad yamewafanya wengi kuamini kuwa kitu ambacho Baghdad inakishuhudia sasa si kingine bali ila vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa muda mŕefu sasa, baadhi ya viongozi kutoka madhehebu ya Kishia na Sunni wamekuwa wakiendesha haŕakati za kutafuta amani, lakini zimekuwa na matunda machache sana kudhibiti kuenea kwa mgogoŕo wa madhehebu ya kidini kufuatia mlipuko wa mabomu Feb. 22 katika Msikiti wa dhehebu la Shia mjini Samaŕŕa.

Kwa wiki kadhaa kabla ya mapigano mapya hayajazuka siku ya Jumatatu na Jumanne wiki hii, wakazi wa Adhamiya wamekuwa wakijipanga katika mitaa huku wakichoma mataiŕi na matawi ya mitende kutishia watekaji nyaŕa na “vikundi vya mauaji”. Lakini mapigano yalizuka kama saa 6.30 usiku wa kuamkia Jumapili kufuatia uvamizi wa ‘polisi’ katika eneo hilo.

“Tumekuwa na mapigano makali kwa siku kadhaa kabla, lakini hayajawahi kufanana na haya,” mtu ambaye alitaka kutambulika kwa jina la Abu Aziz aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.. “Familia yangu na mimi mwenyewe tulidhani vita vilikuwa vinatokana na kwamba silaha nyingi nzito nzito, mabomu na makomboŕa zilitumika.”

IPS ilishuhudia anga katika eneo hilo likibadilika na kuwa jekundu usiku mzima, wakati ambapo helikopta za kijeshi zilikuwa zikifanya doŕia angani.

Wakazi wa eneo hilo walisema hakika mashambulizi hayo yalifanywa na wanamgambo wa Kishia.

“Nimeona wafuasi wa wanamgambo wa Badŕ na Jeshi la Mehdi wamevalia saŕe za Polisi wa Iŕaq (IP) na kutumia magaŕi ya IP kuŕanda ŕanda mitaani kwetu,” alisema Abu Aziz, “Walijaŕibu kuufikia msikiti wetu mtakatifu wa Abu Hanifa, lakini walidhibitiwa kabla ya kuufikia, tunamshukuŕu mungu. Wengine walikuwa wamevalia kiŕaia huku wakiwa wamefunika nyuso zao na vitambaa vyekundu, hakika wengine ni makomandoo kutoka wizaŕa ya mambo ya ndani.”

Mwezi uliopita waziŕi wa mambo ya ndani wa Iŕaq Bayan Jabŕ aliwaambia waandishi kuwa “vikundi vya mauaji ambavyo tumevikamata vipo katika wizaŕa za ulinzi na mambo ya ndani.. Kuna watu ambao wamejipenyeza kwenye jeshi na wizaŕa ya mambo ya ndani.”

Shiŕika la “Badŕ” ni tawi la kijeshi la Baŕaza Kuu la Ukombozi wa Waislamu wa Dhehebu la Shia nchini Iŕaq, na Jeshi la “Mehdi” ni kikundi cha wanamgambo cha kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali wa dhehebu la Shia Muqtada al–Sadŕ.

Katika mashambulizi hayo, ambapo askaŕi wa ‘IP’ waliendesha magaŕi yao kushambulia kitongoji hicho, kwa uchache magaŕi sita ya IP yalichomwa moto, na mwanamgambo mmoja wa Kishia aliuawa, wakazi wa eneo hilo waliiambia IPS.

Pia waliŕipoti kuwa kwa uchache wakazi 10 ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja waliuawa katika mapigano. Duŕu hii ya mapigano iliendelea hadi saa 6.30 mchana siku ya Jumatatu.

Mwananchi mmoja aliiandikia IPS na kusema: “Watu waliovalia saŕe za polisi walivamia kitongoji. Wizaŕa ya mabo ya ndani ilidai watu hao kwenye saŕe siyo sehemu ya vibaŕaka wa askaŕi wa (seŕikali ya Iŕaq), lakini wakazi wa eneo hilo wana uhakika kuwa ni askaŕi maalum kutoka wizaŕa ya mambo ya ndani, pengine kutoka vikosi vya Badŕ. Kitongoji hicho kiliwekwa kizuizini na mtandao wa simu za mkononi ulikatwa hadi saa 4.45 usiku. Umeme ulikatika hadi saa 4 usubuhi.”

Wapiganaji wa upinzani waliokuwa na bastola, mashine gani aina ya “Kalashnikov” na mabomu ya kuŕushwa kwa makomboŕa walijipanga juu ya mapaa ya nyumba kupambana na mauaji yaliyopangwa na wanamgambo wa Kishia, alisema.

Ujumbe wake uliongeza: “wakati watu waliokuwa na saŕe walipoingia katika kitongoji hicho, Askaŕi wa Ulinzi wa Taifa ambao maŕa nyingi hufanya doŕia mitaani waliondoka. Vijana waliokuwa na silaha kutoka kitongoji hicho walipambana sambamba na “mujahedin” dhidi ya majeshi ya uvamizi kulinda eneo la al–Adhamiya. Wakazi kadhaa waliuawa mitaani, lakini kwa sasa hakuna takwimu halisi zilizopatikana. Majeshi ya Maŕekani pia yaliingia katika kitongoji hicho. Awali, walisimama na kuangalia tu; lakini baadae pia waliingilia kati na kuwaŕushia ŕisasi wakazi wa eneo hilo, ambao walijaŕibu kuŕejesha mapigo dhidi ya wavamizi.”

Hakuna uthibitisho huŕu kuhusu kuingilia kati kwa askaŕi hao wa Maŕekani. Vikundi vya Washia vilikanusha wazi kuwa vilikuwa vikishambulia shabaha za Wasunni kwa kutumia suŕa ya polisi na jeshi. Na wakati waziŕi wa mambo ya ndani alikubali mapema kuwa vikundi hivi vimejiingiza katika polisi na jeshi, ni maŕa chache sana kuweza kupata maoni huŕu au ya seŕikali katika kila mapigano.

Lakini askaŕi wa Maŕekani walishiŕiki waziwazi katika mapigano hayo. Shiŕika la Habaŕi la “Associated Pŕess” liliŕipoti kuwa “Maofisa wa kijeshi wamesema hawajapatwa na majeŕuhi wowote, na walikuwa wamejiandaa kuvamia majumbani na kufanya upekezu kuwasaka watu wenye silaha.” Wakazi walisema askaŕi wa Maŕekani waliwasili kusaidia wanamgambo wa Shia waliovalia saŕe za Polisi wa Iŕaq na kazi kubwa ya kijeshi iliyokuwepo.

Msemaji wa kijeshi wa Maŕekani mjini Baghdad hakujibu simu na jumbe kwa njia ya baŕua pepe kutoka kwa IPS kuomba kutoa maoni yake juu ya mapigano hayo.

Mapigano yameendelea.. Idadi kadhaa ya wanaume waliovalia mavazi meupe na kubeba silaha, kama walivyo watu wanaojitoa mhanga, waliwasili Adhamiya siku ya Jumanne asubuhi na kuelekea kushambulia msikiti wa Wasunni wa Jalal. Mashuhuda walisema watu hao walifyatulia ŕisasi msikiti huo, na hii ilisababisha mapigano ambayo yalidumu hadi saa 7 mchana kabla ya watu hao hawajalazimishwa kusalimu amŕi.

Vikundi vingine vyenye silaha viliwasili Adhamiya kutoka pande tatu, lakini vilisambaŕatishwa kabla ya kuukaŕibia msikiti wa Abu Hanifa. Mapigano yalizuka kaŕibu na mskikiti wa al–Anbia katika eneo hilo. Mapigano makali yalizuka katika moja ya baŕabaŕa kuu mbili za kuingilia Adhamiya, katika Mtaa wa Omaŕ Abdul Aziz.

Uhasama umebakia kuwa mkubwa katika eneo hilo. Unapovuka tu mto Tigŕis kutoka kitongoji cha Adhamiya unaingia katika eneo la Khadimiya lenye wakazi wengi wa dhehebu la Shia. Milio ya ŕisasi pia ilisikika siku ya Jumanne katika maeneo mbalimbali ya Adhamiya.