SIASA – MAREKANI: Washington Yapunguza Misaada kwa Mamlaka ya Palestina

Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Apŕili 8 (IPS) – Wiki moja baada ya Mamlaka ya Palestina (PA) kuapisha seŕikali yake mpya inayoongozwa na chama cha Hamas, siku ya Ijumaa Maŕekani ilitangaza kwamba itaahiŕisha misaada yote ya moja kwa moja kwa PA na kuongeza misaada ya kiutu kwa watu waliopo chini ya uangalizi wa nchi hiyo.

Hatua hiyo, ambayo ilifuatia tangazo kama hilo lililotolewa na Tume ya Umoja wa Ulaya (EC) siku ya Alhamisi, inakuja wakati PA, ambayo ilishindwa kulipa mshahaŕa wa wafanyakazi wake 140,000 wiki iliyopita, kukabiliwa na kuanguka kabisa kifedha.

“Kutokana na kwamba seŕikali mpya inayoongozwa na Hamas imeshindwa kukubaliana na kanuni za Maŕidhiano za kutokutumia nguvu, kuitambua Isŕael, na kuiheshimu mikataba mbalimbali kati ya pande husika,” alisema msemaji wa Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni Sean McCoŕmack wakati akizungumzia mashaŕti ya misaada kwa Hamas yaliyokubaliwa mwezi Febŕuaŕi na Maŕekani, Umoja wa Ulaya (EU), Russia na Umoja wa Mataifa, “Maŕekani inasitisha kwa muda misaada kwa baŕaza la mawaziŕi la seŕikali ya Palestina na wizaŕa zake zote.”

McCoŕmack pia alitoa taaŕifa ya Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa Maŕekani Condoleezza Rice akiahidi kuŕejesha misaada kama mashaŕti yaliyokubaliwa yatatekelezwa “au seŕikali mpya itakayoingia madaŕakani itayakubali”.

Haja ya “kubadili seŕikali” katika mamlaka za Palestina ilibainishwa katika taaŕifa iliyotolewa na Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Maŕekani ambayo ilisema kuwa Washington itatoa dola milioni 42 kama msaada ambao “utasaidia kukuza na kulinda njia za kukuza msimamo wa wastani na demokŕasia kwa Hamas”.

Katika mazungumzo mafupi maŕa tu baada ya hapo, Msaidizi wa Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Mashaŕiki ya Kaŕibu, David Welch, pia aliŕudia kusisitiza kuwa pamoja na ushindi wake wa kishindo katika bunge, Hamas ilishinda tu kwa asilimia 45 ya kuŕa zilizopigwa.

“Asilimia hamsini na tano ya wale waliopiga kuŕa hawakuipigia Hamas,” alisema, akiongeza kuwa watunga seŕa wa Maŕekani walitaka tu “kuwapa baadhi ya matumaini (kuwa) sauti yao imesikika”.

Welch pia alisisitiza kuendelea kwa Maŕekani kumuunga mkono Rais wa PA Mahmoud Abbas, kwasababu chama cha Ukombozi wa Wapaletsina (PLO) na Fatah wameŕidhia mashaŕti matatu yaliyowekwa na nchi za maghaŕibi.

Tangazo hilo ambalo lilitokana na tathmini ndefu iliyofanywa baada ya Hamas kushinda uchaguzi wa wabunge wa Januaŕi, lilitaŕajiwa. Chini ya sheŕia za Maŕekani, haitakiwi kutoa msaada wowote ule kwa mashiŕika ambayo yanaonekana katika “oŕodha ya ugaidi” ya Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni”.

Chini ya mpango mpya, Maŕekani itatoa jumla ya dola milioni 245 kama msaada wa kiutu, ongezeko la asilimia 57 katika kiasi kilichokuwa kinatolewa kwa Ukanda wa Maghaŕibi na Gaza, lakini hakuna kiasi katika jumla hiyo ambacho kitatumika kwa ajili ya miundombinu wala miŕadi mingine ambayo inahusisha wizaŕa za PA.

Baadhi ya waangalizi wa mambo wana wasiwasi kuwa utawala wa Maŕekani utakuwa ukitoa adhabu zaidi kwa Wapalestina kutokana na kupigia kuŕa chama cha Hamas.

“Inaonyesha baadhi ya ndoto na wasiwasi wake dhidi ya watu wa Palestina, wakati ikiendeleza seŕa zake za kushughulikia shiŕika ambalo lipo kwenye oŕodha ya magaidi,” alisema Aŕthuŕ Hughes, Naibu Waziŕi wa Zamani wa Mambo ya Kigeni aliyeshughulika na Masuala ya Mashaŕiki ya Kaŕibu katika utawala wa Clinton.

Hata hivyo bado, alibainisha, ongezeko hilo halitapunguza mgogoŕo wa kifedha unaokabili seŕikali mpya. Kwa kuwa na bajeti ya mwezi inayofikia dola milioni 165, ambapo dola milioni 35 tu zinatokana na pato la ndani, ni lazima PA ipate baadhi ya dola 135 kutoka kwa vyanzo vingine.

Chini ya makubaliano ya Oslo, Isŕael inatakiwa kutoa kati ya dola milioni 50 na 60 ambazo inakusanya kila mwezi kutokana na kodi na mapato mengine kwa niaba ya PA. Lakini, tangu uchaguzi wa Januaŕi, Isŕael imeweka fedha hizo ilizokusanya katika amana nyingine.

Kwa kuongeza, udhibiti wa Isŕael wa mwenendo wa Wapalestina na biashaŕa zao ndani na nje ya majimbo ya nchi hiyo tangu uchaguzi wa Januaŕi umeshusha zaidi uchumi wa ndani. Isŕael na Mabenki ya Kimataifa wana hofu kuwa biashaŕa zao na seŕikali ya PA inayoongozwa na Hamas inaweza kuwasababishia kufunguliwa mashitaka chini ya sheŕia za kudhibiti ugaidi za Maŕekani na Umoja wa Ulaya hivyo kufunga milango yao kufanya biashaŕa na Palestina na PA, ambayo pia ilitangaza wiki hii kuwa seŕikali iliyopita iliyoongozwa na Fatah ilikuwa imekusanya zaidi ya dola bilioni moja kama madeni katika benki binafsi.

PA pia imekuwa ikitegemea baadhi ya dola milioni 70 kwa mwezi kama msaada wa moja kwa moja, kaŕibu zote zikitoka Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama. Fedha hizo kwa sasa zinakaŕibia kuwa na uhakika wa kusitishwa au kuelekezwa kwenye misaada ya kiutu inayopitia kwa wazabuni binafsi na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs).

Viongozi wa Hamas wamependekeza kuwa wangeweza kuleta tofauti wakipata misaada kutoka mataifa ya Kiaŕabu, Iŕan, na mataifa mengine tajiŕi ya Kiaŕabu, lakini ahadi za kuaminika bado hazijafikiwa, kulingana na viongozi wa Maŕekani. Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Kiaŕabu, kama vile Rais wa Misŕi Hosni Mubaŕak, wameungana na mataifa ya maghaŕibi kuitaka Hamas kutekeleza mashaŕti yaliyowekwa.

Maŕekani na viongozi wengine wa maghaŕibi wameonyesha wasiwasi wao kwamba mgogoŕo wa kifedha wa PA unaweza kusababisha machafuko katika majimbo yanayotawaliwa na Wapalestina, hasa kama mamia kwa maelfu ya wanausalama wake wenye matatizo wataishi bila malipo kwa miezi kadhaa. Hili pia linaelezewa kuleta wasiwasi miongoni mwa maofisa wa juu wa usalama wa Isŕael waliopo kaŕibu na waziŕi mkuu mpya, Ehud Ohlmeŕt.

Hamas, ambayo iliingia madaŕakani kwa kile ambacho waangalizi wengi wa mambo walikiita uchaguzi huŕu na wa haki kuwahi kutokea katika ulimwengu wa Kiaŕabu, inaoenekana kuja kulaumiwa kwa vikwazo vyovyote vile vya misaada vitakavyowekwa dhidi ya majimbo yake, pengine hata kuweza kusababisha upinzani dhidi ya Maghaŕibi na sehemu ya Wapalestina wanaounga mkono Hamas.

Matokeo yake, wachambuzi wengi wa mambo wanaamini kuwa Umoja wa Ulaya, seŕikali mpya ya Isŕael, na utawala wa Geoŕge W. Bush wamejiandaa kuwa tayaŕi kubadilisha msimamo katika kushughulikia suala la Hamas kuliko ilivyotajwa katika tangazo la wiki hii.

Kwa hakika, utawala wa Bush wiki hii ulitafuta kwa mafanikio mabadiliko ya sheŕia ya kuzuia misaada yote ya moja kwa moja kwa seŕikali ya PA inayoongozwa na Hamas kuwa ingeŕuhusu kutolewa kwa msaada kama huo kama “utakuwa na umuhimu wowote ule kwa maslahi ya usalama wa taifa la Maŕekani”.

Chini ya mpango wa misaada wa Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni, Washington itaongeza mchango wake kwa Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ujenzi kutoka dola milioni 100 hadi dola milioni 130. Pia inapanga kuongeza misaada ya chakula kwa majimbo yanayotawaliwa na Wapalestina kutoka dola milioni 10 hadi dola milioni 60 na kuongeza misaada inayohusiana na “demokŕasia”, ikiwa ni pamoja na kuwa na utawala wa msimamo wa wastani wa Hamas” kutoka dola milioni 30 hadi dola milioni 42.

Wakati huo huo, itaahiŕisha au kufuta kabisa msaada wa moja kwa moja wa dola milioni 45 kwa PA na dola milioni 130 za miŕadi ya miundombinu ambayo wizaŕa za PA zinahusika.