Maendeleo ya ICT Inatarajiwa kusaidia katika Kupambana na Ugonjwa wa Banana Nchini Rwanda

Aimable Twahirwa
thumb image

Katika Rwanda ugonjwa wa ndizi BXW, ni hatari kwa mazao na ina madhara makubwa yasiyo kwa wakulima pekee, pia kwa usalama wa chakula na lishe ya familia zao na wale wanaomtegemea mazao kama chanzo cha chakula. Picha ya Alejandro Arigón/IPS


Tekesohore Ruzigamanzi, mkulima wa shamba ndogo kijijini Rwanda Mashariki, alipogundua madoadoayenye rangi ya manjano kwa mazao yake kabla yaanze kukauka, hakuyazingatia vile ilivyohitajika.

“Nilidhani ilikuwa hali ya pepo kame isiyo ya kawaida, iliyokuwa ikiharibu mazao yangu,” Ruzigaanzi, mwenyeji wa Rwimishinya, kijiji kilicho Kayonza Rwanda mashariki, aliambia IPS.

Lakini kwa ukweli, ilikuwa ugonjwa wa bakteria.

Mazao ya Ruzigamnzi yaliambukizwa na ‘Banana Xanthomonas Wilt’ (BXW), ugonjwa was bakteria inayoambukiza aina zote za ndizi na inayojulikana nchini kama Kirabiranya.

Hapa, katika nchi hii mashariki mwa Afrika, BXW hudhuru mazao na husababisha shida nyingi si tu kwa wakulima, lakini pia kwa usalama wa chakula na lishe ya familia zao na wale wanaotegemea mazao kama chanzo cha chakula.

Ndizi ni zao muhimu Afrika mashariki na kati mwa, nchi kadha kandani zikiwa kati ya wafanyizaji wa juu duniani, kulingana na ‘Food and Agrriculture Ornization Corporate Statistical Database’.

Kulingana na utafiti wa kaya wilayani Tanzania, Burundi na Rwanda, ndizi ni asilimia 50 ya chakula cha kaya katika theluthi ya nyumba za Rwanda.

Lakini, kulingana na utafiti, sababu ya juu inayoathiri uzalishaji wa ndizi katika nchi zote tatu ni BXW.

Watafiti wameonyesha kuwa BXW inaweza kusababisha hasara asilimia 100 ya sahani za ndizi, isipodhibitiwa vizuri.

Utulivu na ukosefu wa habari huchangia kueneza ugonjwa.

Ugonjwa wa BXW si mpya nchini. Ripoti ya kwanza ilitokea 2002. Tangu wakati huo, kampeni nyingi za elimu zimefanywa na mamlaka ya kilimo na wadau tofauti, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali.

Wakulima katika mkoa wa Ruzigamanzi wamefundishwa na timu ya watafiti kutoka Bodi ya Kilimo ya Rwanda na  wataalam wa ukulima mitaani kuhusu BXW. Lakini Ruzigamanzi, baba wa watoto sita, alikuwa mmoja wa wakulima ambao hawakupatwa na kampeni ya ufahamu na ni kwa sababu hakuwa na elimu ya kutambua ugonjwa huo.

Kama angenjua ugonjwa huo, na kulingana na hali ya maendeleo ya mmea, ingekuwa lazima Ruzigamanzi aziondoe mimea za dalili, kuzikata kwa kiwango cha udongo mara moja baada ya uchunguzi wa kwanza wa dalili. Ikiwa ugonjwa haitibiwi kwa muda mrefu, angehitaji kuondoa mimea yote kutoka kwenye mizizi.

Na hivyo ndivyo alivyofanya wiki mili ilipopita wakati mtaalam wa ukulima kutoka kijijini alipoangalia mimea.

Mwishowe hakuwa na wakati wa kuokoa mimea zake na Ruzigamanzi alilazimishwa kutoa mmea yote kutoka mizizi hadi shina.

Hadithi ya Rungamizi si ya kipekee. Kwa kweli, wakulima wengi sana wa shamba nogo kwa vijii vya umbali wamekuwa wakipuuza ama hawajui dalili za hii ugonjwa ya bakteria ya ndizi. Imeongeza hatari ya kueneza hii ugonjwa kwa mikoa mpya na urejeshi mahali ambapo ulikuwa umepunguzwa. Wilaya kadhaa katika Rwanda mashariki wameathirika na hii ugonjwa kwa miaka zilizopita hivi karibuni.

 

Mwandishi wa mradi wa ICT4BXW akifanya tathmini ya Banana Xanthomonas Wilt, ugonjwa wa bakteria, na hali yake katika wilaya ya Muhanga, Rwanda. Kwa hisani ya Julius Adewopo/ International Institute of Tropical Agriculture.
Mwandishi wa mradi wa ICT4BXW akifanya tathmini ya Banana Xanthomonas Wilt, ugonjwa wa bakteria, na hali yake katika wilaya ya Muhanga, Rwanda. Kwa hisani ya Julius Adewopo/ International Institute of Tropical Agriculture.

 

Kutumia teknolojia kuiumarisha wakulima shambani na kuzuia uenezaji wa BMX

Mwanzo wa 2018, ‘Taasisi ya Kilimo ya Kitropiki Kimataifa (International Institute of Tropical Agriculture – IITA)’ pamoja na ‘Biodiversity International’, ‘Leibiz Taasisi ya Maendeleo ya Ukulima kwa Uchumi Zinazobadilika, na Bodi la Ukulima la Rwanda, walianzisha jitijadi za ushirikiano kukabiliana na uginjwa huu kwa kutumia teknolojia. Wanasayansi wa IITA wanatafuta njia tofauti za kusaidia wakulima kufuatilia na kukusanya data kuhusu hii ugonjwa. Taasisi hii inajulikana kwa kubadilisha ukulima wa kiafrika kwa utumizi wa maarifa na mabadili, na juzi ilitangazwa kama mshindi wa Tuzo la Chakula Kiafrika mwaka wa 2018.

Mradi mpya utakayoendelea kwa miaka tatu (inayoitwa ICT4BXW), uliyoanzishwa na uwekezaji wa euro milioni 1.2 kutoka ‘German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development’, utachunguza matumizi ya simu za mkononi kama zana za kuzalisha na kubadilishana habari za sasa kuhusu BXW.

Mradi huu hujengea juu ya urahisi wa kupata simu za mkononi nchini Rwanda. Kulingana na data kutoka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma Rwanda, matumizi ya simu nchini inakadiriwa kuwa asilimia 79 katika nchi ya watu milioni 12, na idadi kubwa ya watu vijijini kumiliki simu ya mkononi.

“Jitihada zetu za kuendeleza, kupima, na kuanza programu za simu ya muhimu au ya kawaida ni hatua muhimu kuelekea ufuatiliaji na udhibiti wa ufanisi wa ugonjwa huo,” Julius Adewopo anasema, anayeongoza mradi ya BXW kwa IITA. Aliendelea kueleza kwamba, “Wakulima wa ndizi Rwanda wanaweza saidika na ubunifu ubunifu ambacho hutokea teknolojia iliyopo na matumizi ya simu za mkononi kuongezaka nchini.”

Muhimu katika mradi huo ni mbinu ya sayansi ya wananchi, inyoamaanisha wadau kijijini, kama wakulima wa ndizi na wanaosaidia wakulima na kueneza kazi yao, wanfanya kazi muhimu sana katika kukusanya na kuwasilisha data juu ya uwepo wa BXW, ukali na maambukizi. Aidha, wadau watashiriki katika maendeleo ya programu na jukwaa, yatakayotumuwa kubadilishana data na habari.

Takribani wakulima 70 kutoka wilaya nane tofauti katika kaskazini, magharibi, kusini na mashariki watafundishwa kutumia programu ya simu ya mkononi. Watashiriki katika kukusanya na kuwasilisha data kwa mradi – kuhusu matukio na ukali wa BXW katika kijiji chao – kwenye jukwaa. Mradi unatarajia kufikia wakulima hadi 5,000 kwa kushirikiana na wakulima na simu za mkononi.

Zaidi, data kutoka kwa mradi itatafsiriwa katika habari kwa watafiti, NGOs na watunga sera kuendeleza mifumo ya usaidizi na ufanisi. Vile vile, data inayotokana itatumiwa katika mfumo wa onyo la mapema ambayo inapaswa kuwajulisha wakulima kuhusu kuzuka kwa magonjwa na ufumbuzi bora kwao.

Mfumo halisi wa kutoa taarifa juu ya ugonjwa huo

Ingawa programu ya kitaifa ya utafiti wa ndizi katika rwanda imezingatia maeneo tano muhimu ya hatua na mikakati iliyotumiwa katika kudhibiti au usimamizi wa magonjwa ya mimea, ufumbuzi uliopendekezwa wa simu za mkononi unaelezewa kama chombo cha ubunifu ambacho kinaweza kupanuka kwa urahisi na rahisi kwa matumizi au ushirikiano na majukwaa mengine ya habari na teknolojia ya mawasiliano au programu.

Tunazingatia mapungufu katika upatikanaji wa data zinazofaa na habari zinazohusiana na uambukizi wa magonjwa, ukali wa kuzuka, na athari za hatua za udhibiti,” Mariette McCampbell, mwanafunzi wa utafiti ambaye anasoma ubunifu na kukua wa ICT kwa mradi was ICTBXW, aliambia IPS. “Pia tunahitaji uchumi na utamaduni wa kijamii nzuri ambayo inaeza kusaidia wakulima kufanya maamuzi na mfumo wa onyo wa mapema.

Mfumo mpya wa kutoa taarifa unatarajia kujiendeleza kukuwa mfumo wa onyo wa mapema ambao utaruhusu serikali ya Rwanda kujaribu kupuliza kuenea ugonjwa wa BXW, pia inalenga kuanzisha ushirikiano kati ya wadau kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa ndizi nchini.

“Hii ubunifu [ICT] ina uwezo wa kuwezesha tathmini halisi wa ukali wa ugonjwa huo na udhibiti wa msaada,” Adewopo alieleza.

Timu ya mradi sasa inafanya kazi ili kuendeleza jukwaa, na wakulima na washauri. Kwa robo ya pili ya 2019, vipimo na toleo la kwanza la jukwaa litaanza katika wilaya nane ambapo programu inafanya kazi.

Timu ya mradi tayari imebainisha chaguo tofauti za kukua kwa jukwaa la mafanikio. “Shida na Banana Xanthomons Wilt haziishi Rwanda, wala si ugonjwa wa mazao wa kipekee ambao huwahimiza wakulima. Kwa hivyo, Lengo letu la muda mrefu ni kukabiliana na programu kama hiyo ambayo inaweza kutumika katika nchi nyingine au kwa magonjwa mengine au mazao mengine,” McCampbell alieleza.

Kulingana na Adewopo, “maono ya mafanikio ni kuendeleza na kuzindua zana na jukwaa za kazi, ambazo watumiaji watahitaji na kwa nia ya kuimarisha taasisi husika, kama Rwanda Agricultural Board, kugawa rasilimali kwa ufanisi ya kudhibiti na kuzuia BXW kupitia programu ya demokrasia ya ICT, kulenga na utoaji.”

Kuna haja ya kuongezeka kwa uangalifu na kasi zaidi wa hatari ambazo zina uzalishaji mdogo katika mifumo ya kilimo.

Kwa kutambua tishio la mwisho la BXW kwa mazao ya ndizi, hakuna shaka kwamba matumizi ya zana za ICT huleta matumaini mapya kwa wakulima, na inaweza kuwasaidia kwa kifedha kupitia upatikanaji bora wa ushauri, bila kujali jinsia, umri au hali ya kijamii – bora wana uwezo wa kupata simu wa mkononi.