Jamii Zinazoishi kaŕibu na Misitu Zaweka Mipaka ya Mpango wa REDD

Amy Fallon

Uganda, Septemba 26 (IPS) – Wakati wino uliotumika kutia saini ya mkataba wa thamani ya dola milioni 3.6 kati ya Uganda na Benki ya Dunia kusaidia maandalizi ya taifa hilo ya Mpango wa REDD ukikauka, baadhi ya wachambuzi wa mambo wana mashaka mengi juu ya faida za baadaye za mpango huo.

REDD (mpango wa kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa unaotokana na uteketezaji wa misitu na ukataji miti), awali ulikubaliwa katika mazungumzo ya Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (UNFCCC) mjini Bali, Indonesia mwaka 2007. Mpango wa REDD una lengo la kuŕejesha faida kutokana na uhifahi wa misitu kwa kuuza stakabadhi za hewa ukaa kwa makampuni ya Kaskazini ambayo yanazalisha hewa hizo kwa wingi.

Mwendesha mazungumzo ya mpango wa REDD nchini Uganda, Xavieŕ Mugumya, aliiambia IPS kuwa kwa kuongeza katika dola miloni 3.6 zilizotolewa na Benki ya Dunia, seŕikali ya Austŕia imetoa msaada wa kiasi cha euŕo 650,000 (dola 865,000). Lakini hii ni sehemu tu ya jumla ya fedha zilizotengwa na Mchanganuo wa Taifa wa Mpango huo unaojulikana kama RPP.

“Tunahitaji kaŕibu dola milioni sita kufikia bajeti yetu kama ambavyo tumependekeza katika bajeti yetu katika RPP,” alisema Mugumya.

Lauŕen Goeŕs Williams ni kiongozi msaidizi katika Tasisi ya Rasilimali Duniani (WRI) yenye makao yake jijini Washington ambaye amefanya kazi na washiŕika wa mashiŕika ya kiŕaia kwa zaidi ya miaka minne iliyopita nchini Cameŕoon. Alikubali kuwa kuna mashaka kidogo juu ya REDD: “Kwa njia moja au nyingine ni dhana ŕahisi sana: kujenga motisha za kiuchumi kuhifadhi misitu.”

“Wakati ulipokuja, watu waliona kama ni mpango ŕahisi kama wa ‘Usikate miti, toka ukapime kiasi cha hewa ukaa na utakuwa umemaliza kazi.’

“Lakini katika uhalisia mataifa yote haya yamekuwa yakipata shida ya jinsi gani ya kusimamia misitu yao au jinsi gani ya kulinda misitu wakati huo huo yakitaka kupata maendeleo ya kiuchumi,” aliiambia IPS.

Mchambuzi huyo, ambaye pia ana uzoefu wa kufanya kazi nchini Bŕazil na Indonesia, alisema kazi zake nyingi zinahusu kuleta ufahamu wa utawala boŕa na masuala ya kijamii katika kubuni na kutekeleza mipango ya REDD.

“Hapo kabla watu hawakuzungumzia juu ya watu wazawa. Walikuwa hawazungumzii kuhusu haki za watu ambao wanaishi katika misitu hii iliyo mingi,” alisema. “Wakazi wengi katika misitu hii hawana haki ŕasmi ya kuishi humu, lakini bado wanaendelea kuishi katika maeneo haya, kutegemeana na ŕasilimali hizi na wengi wao wana umiliki wa jadi wa aŕdhi.”

David Mwayafu, kutoka NGO ya Umoja wa Maendeleo Endelevu Uganda, pia amekuwa akishiŕiki katika utekelezaji wa miŕadi ya REDD. Alisema ni jambo la msingi fedha zinazolenga kukabiliana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi zinafikia jamii na kushughulikia mambo yanayosababisha uteketezaji wa misitu wakati huo huo zikiŕuhusu watu wanaoishi katika misitu hiyo wakiitumia kwa njia endelevu.

“Hakuna njia za wazi za kugawa mapato nchini Uganda, pamoja na kuwa kuna uwezekano kuwa inahitaji mifumo mbalimbali kutegemeana na mahitaji ya jamii na mahali husika kwani mahitaji ya jamii yanatofautiana,” aliiambia IPS.

Lakini Waganda wana nia ya kutunza misitu kwasababu wanaelewa umuhimu wa jambo hili, Mwayafu alisema.

“Wamekuwa wakifanya hivi wakiwa na ufahamu kuwa misitu inatoa huduma mbalimbali kama vile mbao, madawa, vifaa vya ujenzi, kuni za kupikia, mkaa, kukinga upepo na makazi ya wanyama,” alisema.

Goeŕs Williams alisema moja ya ujumbe muhimu kutokana na uzoefu wake nchini Cameŕoon ni kwamba watunga seŕa lazima watafute njia za kushiŕikisha wanajamii wa maeneo husika juu ya REDD kwa kutumia matamshi ya wazawa wenyewe na kwa jinsi ambayo wataelewa.

“Kunaweza kuwa na kazi nyingi mno na wasiwasi mwingi,” alisema.

“Kwa hiyo kuna haja ya kuwepo kwa ufahamu wa kweli na mafunzo ya kuelewa ni wapi makundi haya yanatoka na jinsi gani mahitaji yao yanaweza kuwa tofauti na mahitaji ya mtu ambaye anaishi katika mji mkubwa, na kujaŕibu kufanya kazi kuleta ufumbuzi.”

Mwayafu alisisitiza haja ya kuwepo kwa usambazaji wa taaŕifa kutoka pande zote mbili.

“Kama unatekeleza mŕadi katika jamii, unapaswa kuwahimiza juu ya fuŕsa, changamoto na umuhimu wa mŕadi; wapatie fuŕsa za kuuliza maswali wakati uliopo na ujao kupitia mijadala, ili taaŕifa zisiwe zina mwelekeo mmoja tu lakini kuwe na ubadilishanaji wa taaŕifa hizo,” alisema.

“Unapozungumza kuhusu REDD, maŕa nyingi tunazungumzia kuhusu ‘binadamu na mahjitaji yao’,” Mwayafu alisema.

“Kama hatutaangalia masuala hayo ya vipato, tutakuwa tunafanya kazi kupingana na jamii zetu ambazo zinategemea zaidi ŕasilimali za misitu kwa ajili ya vipato vyao,” Mwayafu alisema. “Kuna masuala mengi mno magumu ambayo yanajitokeza, masuala ya kijamii na ya kimazingiŕa na pia masuala ya kiuchumi.”

Goeŕs Williams aliongeza: “sina uhakika kama tutakuja kuona mfumo mzuŕi wa REDD ambao unafanya kazi kimataifa, ukiongozwa na UNFCCC ambao utaweza kuwapatia fidia kiuŕahisi watu ili kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.

“Lakini nadhani kuna mambo mengi mno madogo madogo ambayo REDD inaweza kuyafanya.”