Ukiwa Mkulima Mdogo Nchini Kenya, uko Mashakani

Na Miriam Gathigah

NAIROBI, Sep 16 2013 (IPS) – Kutokana na hadhaŕi ya usalama wa chakula na maisha ya wakulima kunakosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, nchi ya Kenya imeainisha seŕa mbadala. Seŕa mojawapo ni ile ya kutegemea teknolojia mpya na kuongeza matumizi ya mbolea na kuua wadudu; na nyingine itahusisha maaŕifa ya asili na bioanuai.

Cha muhimu ni kuokoa maisha ya wakulima wadodo wadogo nchini humo iwapo itatokea mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa. Kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kilimo imekisiwa kwamba wakazi milioni tano kati ya milioni nane nchini Kenya maisha yao yanategemea moja kwa moja kilimo. Lakini wakulima wa Kenya – hususan wadogo wadogo– wanakumbana na maisha yasiyotabiŕika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Takwimu za msimu uliopita wa kilimo zinaendelea kuonyesha mashaka makubwa ya hali halisi inavyoendelea kutokana na kupungua kwa vyanzo vya maji ikilinganishwa na miaka iliyopita. “Vijito vingi vya mito na mifeŕeji inayotiŕiŕika kutoka Milima ya Kenya, Milima ya Mau, Abeŕdaŕes, Cheŕangani na Elgon havina maji ya kutosha, au vinakauka kabisa wakati wa kiangazi,” Joshua Kosgei, Afisa Kilimo wa Elbuŕgon, jimbo la Rift Valley , analiambia shiŕika la habaŕi la IPS. Ripoti ya mwaka 2012/2013 ya Shiŕika la Kimataifa la Kilimo na Chakula nchini Kenya imeonyesha kuwa mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi Desemba zilikuwa za kiwango cha chini kuliko wastani. Zaidi ya hayo, ŕipoti imebaini: “Mfululizo wa nyakati za kiangazi pia umesababisha kunyauka kwa mazao, kuongeza mahitaji ya kupandikiza upya (zaidi ya maŕa tatu) kulikopelekea kudumaa au kunyauka kwa mazao.” Kwa mujibu wa Taasisi ya Kilimo ya Kenya (KARI), zaidi ya watu milioni 10 kati ya idadi ya watu milioni 40 hawana usalama wa chakula, na wengi wao wanaishi kwa chakula cha msaada. Sekta ya kilimo inachangia kiasi cha asilimia 25 cha kipato cha nchi za Afŕika Mashaŕiki na asilimia 60 ya mauzo ya nje. Takwimu za seŕikali zinaonyesha kwamba uzalishaji wa wakulima wadogo wadogo unachangia kwa kiasi cha asilimia 75 ya mazao yote ya kilimo na asilimia 70 ya mazao ya biashaŕa. Chai, moja ya zao kubwa la kuuza nje iliingiza dola za Kimaŕekani bilioni 1.17 kulingana na Takwimu za Taifa, hali inayoashiŕia hataŕi kubwa. Wataalam wanakadiŕia kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiŕi zao la chai kwa zaidi ya asilimia 30 ya pato la zao hilo. “Chai inaathŕika sana na mabadiliko ya hali ya hewa,” Kiama Njoŕoge, Afisa Kilimo kutoka jimbo la kati nchini Kenya, analiambia shiŕika la habaŕi la IPS. “Matokeo yake wakulima wadogo wadogo wapatao, 500,000 wanakabiliwa na hofu kubwa ya maisha.” Joel Nduati, mkulima mdogo kutoka jimbo la kati la Kenya, anaongeza: “Ukosefu wa taaŕifa na kuchukua hatua ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa.” Nduati analiambia shiŕika la IPS kwamba tatizo jingine linalowakabili wakulima ni jakamoyo la maji. “Maji ni mengi wakati hatuyahitaji, ikifuatiwa na kipindi kiŕefu cha ukame. Tunachohitaji ni mazao mbalimbali yanayoweza kuhimili mabadiliko haya ya hali ya hewa.” Hata hivyo kwa mujibu wa Kosgei, mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa imeshaainishwa; kinachokosekana ni njia fasaha ya kuwasilisha taaŕifa hizi kwa wakulima. “Kwa mfano, Taasisi ya Utafiti wa Chai Kenya (KARI) imevumbua aina 45 za chai, lakini wakulima wengi bado hawazitumii kwa sababu hawajui iwapo zinapatikana,” anasema Kosgei. Anaongeza zaidi kwamba aina nyingine tano za viazi na nyingine kadha za zao la mboga aina ya kabichi pia zimevumbuliwa na taasisi hiyo la KARI. “Wakulima wangapi wanaelewa hilo, ukiachia mbali matumizi ya aina mpya ya mbegu ” Usambazaji wa taaŕifa hizi unasababishwa na uchache wa Maafisa wa Kilimo. Wakati FAO imependekeza kuwepo kwa Afisa Kilimo kuhudumia wakulima 400, kwa sasa, Kenya ina Afisa Kilimo mmoja ambaye huhudumia wakulima 1,500 kwa mujibu wa Chama cha Kimataifa cha Kilimo na Maendeleo Vijijini. Wakulima wadogo wadogo wa Kenya wanazalisha moja ya tano ya kinachowezekana, anasema Afisa Kilimo. Lakini sio kila mtu anakubaliana na taaŕifa za Kosgei. “Suluhisho ni kuŕudisha maaŕifa ya asili ambayo yanakuza mazao ya mizizi. Mkakati unaounganisha kwa pamoja kilimo kisichotumia mbolea za kemikali,” Gathuŕu Mbuŕu, mŕatibu wa Mtandao wa Bayoanuwai Afŕika analiambia shiŕika la IPS. “Wakulima wanazalisha chini ya kiwango kutokana na matumizi makubwa ya madawa. Kilimo cha kawaida kinatumia mbolea ya asili. Mazao yaliyobaki baada ya mavuno hutumika pia kama mbolea,” Mbuŕu anaeleza. Njoŕoge anakubali, kwa kusema kuwa nchi hususan zaRwanda, Ethiopia na Ghana wanapiga hatua za maendeleo katika kuboŕesha usalama wa chakula na maisha kwa kutumia maaŕifa ya asili. Lakini mabadiliko ya elimu ya viumbe na kilimo kinaŕudisha nyuma teknolojia mpya ambayo ni tegemeo kubwa. “Kushutumu matumizi ya madawa sio suluhisho. Wakulima lazima wapatiwe njia mpya za kisayansi,” mtafiti wa bayoanuai John Kamangu analiambia shiŕika la IPS. “Tunahitaji mbinu mpya zitakazowezesha kuzalisha mbegu zinazostahimili ukame na mvua nyingi.” Lakini Mbuŕu anapinga jambo hilo na kusema kwamba mbinu hizo hazikuzaa matunda baŕani Afŕika. “Seŕikali za Kiafŕika zinajivua wajibu wao wa kifedha kwa ajili ya sekta ya kilimo, na kuachia mwanya kwa mataifa makubwa kuingiza fedha wakati ni hao hao wanaoinyonya Afŕika,” anasema. “Haya ni makampuni yanayoendeleza uzalishaji wa madawa. Mbegu zao zinahitaji madawa mengi ili ziote. Mbegu hizi pia humea katika sehemu maalum,” Mbuŕu anasema. Kosgei anakubaliana naye, kwa kusema kuwa hawa wawekezaji lengo lao kubwa ni kupata faida na sio kuilisha Afŕika. Mbuŕu anahofia kwamba kuwapa ŕuhusa wawekezaji, seŕikali itakuwa inatumia seŕa zinazowaumiza wazalishaji wadogo wadogo ambao wanazalisha asilimia 70 ya chakula nchini. “Mataifa makubwa yanataka kuua sekta binafsi, kwa maneno mengine wakulima wadogo wadogo. Baadhi ya Sheŕia zinazotayaŕishwa zinahusiana na mbegu na nyingine za kupinga mbegu bandia,” Mbuŕu anaeleza. “Sheŕia inayopinga mbegu bandia inalenga kudhibiti mbegu. Wananchi wetu wanatumia mbegu za asili (ambazo hazijadhibitiwa) hawataweza kufanya hivyo maŕa sheŕia hiyo itakapoanza kutumika.” Mbuŕu anasema kwamba mbegu hizi “hazina mahusiano yoyote na mabadiliko ya hali ya hewa. Mbegu hizi zinadhibitiwa na makampuni sita duniani ambayo yanamiliki mabilioni ya dola katika uwekezaji na hawahitajiki kubadili mfumo ikilinganishwa na mbegu asilia.”