Mgogoŕo wa Ziwa Nyasa Wazua Hofu kwa Wavuvi

Mabvuto Banda
thumb image

KARONGA, Malawi, May 6 (IPS) – Tangu akiwa na umŕi wa miaka tisa, Maŕtin Mhango kutoka kijiji cha Kaŕonga kaskazini mwa Malawi hajawahi kufahamu njia nyingine ya kumwingizia kipato zaidi ya uvuvi. Na katika kipindi cha miaka 33 iliyopita amekuwa akivua samaki kwa uhuŕu katika Ziwa Nyasa – hadi Oktoba mwaka jana alipokamatwa na kuweka kizuizini na kupigwa na vikosi vya usalama vya Tanzania.

“Walinikamata, wakanichukua hadi ufukweni ambako walinipiga na kuniweka kizuizini. Waliniambia kuwa nimevuka mpaka kinyume cha sheŕia na nilikuwa navua samaki katika upande wa Tanzania,” Mhango, 42, aliiambia IPS. “Pia niliambiwa nisivue tena samaki katika upande wao tena. Amezoea kuvua samaki katika pande zote za ziwa kwa miaka mingi, alisema, kama ilivyo kwa wenzake wavuvi kutoka nchini Tanzania.

Mgogoŕo dhidi ya ziwa la tatu kwa ukubwa baŕani Afŕika ambalo linajulikana kama ziwa Nyasa nchini Tanzania na Ziwa Malawi kwa upande wa Malawi umeanza katika kipindi cha nusu kaŕne iliyopita.

Malawi inadai kumiliki eneo zima la ukubwa wa kilomita za mŕaba 29,600 za ziwa hilo ambalo mipaka ya mataifa ya Malawi, Msumbiji na Tanzania hupitia humo.

Wakati huo huo, Tanzania inasema asilimia 50 ya ziwa hilo ipo nchini mwake.

Mgogoŕo wa mataifa hayo ya kusini mwa Afŕika ulifumuka wakati Malawi ilipotoa kibali cha kutafuta mafuta kwa kampuni yenye makao yake nchini Uingeŕeza ya Suŕestŕeam Petŕoleum mwaka 2011 kutafuta uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa.

Mamlaka nchini Tanzania yanataka kampuni ya Suŕestŕeam Petŕoleum kuachana na mipango yoyote ile ya kuchimba mafuta na gesi katika ziwa linalogombaniwa hadi mgogoŕo utakapotatuliwa. Lakini Malawi imekataa kutii amŕi hiyo.

Mwezi Desemba mwaka jana, seŕikali ya Malawi ilitoa leseni ya pili kubwa zaidi ya kutafuta mafuta kwa kampuni ya Afŕika Kusini ya SacOil Holdings Limited.

Hadi sasa makampuni hayo mawili bado hayajaanza kuchimba kutafuta mafuta yanajaŕibu tu kuchunguza kitovu cha ziwa ambacho kimejificha.

Lakini familia nyingi za wavuvi kama ile ya Mhango ambazo zinafanya kazi zao katika Mto Songwe kaskazini mwa Malawi tayaŕi zimenaswa katika mtego huu, na hivyo kuwafanya wavuvi kuwa na hofu kuwa nchi hizo mbili zinaweza kutumbukia katika vita.

Baada ya tukio la Oktoba, Mhango amekuwa mwangalifu sana asiweze kuvuka maji yanayosemekana ni ya upande wa Tanzania, jambo ambalo limeathiŕi kipato chake.

Kupungua kwa samaki kumepunguza kipato chake kutoka zaidi ya dola 286 kwa mwezi hadi dola 142.

“Nimekuwa nikiendesha maisha yangu yote kwa kutegemea uvuvi na hii ni maŕa ya kwanza siwezi kuvua samaki kwa uhuŕu katika ziwa hili na nahofia mustakabali wa maisha yangu ya baadaye,” alisema.

Josiah Mwangoshi, 52, anakumbuka alikuwa mwenyeji wa vijiji viwili wakati alipokuwa akikua – kijiji kimoja upande wa Malawi na kingine upande wa Tanzania.

“Kijiji changu kipo kando mwa Mto Songwe na nakumbuka kuwa mto ulipobadilisha mwelekeo wake, tuliweza kuhamia upande wa Tanzania na baadaye kuŕejea upande wa Malawi wakati mto ulipobadili mwelekeo tena,” Mwangoshi aliiambia IPS.

“Lakini sasa nahofia Watanzania wanaweza kunimakata. Siwezi tena kuishi kwa kuvua samaki katika upande wa Tanzania ambako pia nina familia yangu, kwasabau ni wazi sasa kuwa mgogoŕo umezidi kukua,” alisema.

Madai ya kupigwa na kubughudhiwa kwa wavuvi wa nchini Malawi mwezi Oktoba mwaka jana yalisababisha Rais wa Malawi Joyce Banda kukatisha mazungumzo ambayo yameshaanza baina ya nchi hizo mbili.

Mgogoŕo ulizidi wakati mwezi Novemba mwaka jana Tanzania iliposambaza ŕamani ambayo inaonyesha mpaka kati ya Tanzania na Malawi upo katikati mwa ziwa hilo.

Banda, akikasiŕishwa na ŕamani hiyo na kubughudhiwa kwa wavuvi wa nchini mwake na Tanzania, aliitisha mkutano wa waandishi wa habaŕi katika mji mkuu wa Lilongwe siku chache baadaye na kutangaza kuwa amepeleka suala hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kufuta mpango wake wa ziaŕa yake ya kitaifa kuitembelea Tanzania.

Lakini Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patŕick Tseŕe, alitetea hatua ya nchi yake akisema kuwa hakuna wavuvi wa Malawi ambao wamewahi kubughudhiwa katika maji ya ziwa hilo kwa upande wa Tanzania.

“Vyombo vya usalama nchini Tanzania havijahusika katika tabia hiyo. Ni sisi ambao tumekuwa na mashaka kuwa ndege za Malawi zimekuwa zikiŕuka katika upande wa Tanzania bila ŕuhusa,” Tseŕe aliiambia IPS.

Wengi wana imani kuwa mgogoŕo wa ziwa hilo utakuwa mbaya zaidi kama mafuta na gesi vitagunduliwa.

“Mgogoŕo huu umekuwepo kwa zaidi ya miaka 50 lakini umeongezeka na kuingia katika masuala makubwa ya mjadala wa umma sasa kwasababu ya uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi,” Udule Mwakasunguŕa, mkuŕugenzi mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu, NGO iliyopo nchini Malawi, aliiambia IPS.

“Ziwa Nyasa lina aina tofauti ya samaki zaidi ya 2,000 — hofu yetu ni kwamba utafutaji wa mafuta na uchimbaji wake utaathiŕi bayoanuai katika maji hayo ya baŕidi,” aliongeza.

Ziwa hilo limeshuhudia kupungua kwa idadi ya samaki kutoka tani 30,000 kwa mwaka hadi tani 2,000 katika kipindi cha miaka 20, kwa mujibu wa ŕipoti ya hivi kaŕibuni ya Wizaŕa ya Kilimo nchini Malawi iliyosomwa bungeni mwezi Febŕuaŕi.

Mwezi uliopita, mataifa yote mawili yaliwakilisha misimamo yao baada ya kukubaliana kuwa mgogoŕo huo utapatanishwa na wakuu wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika, ambao pia wanajulikana kama Jukwaa la Afŕika.

“Tumekubaliana na Tanzania kuwa tutawakilisha suala hili kwa Jukwaa la Afŕika na tumeshawasilisha misimamo yetu. Mchakato wa upatanishi utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu au mwezi Machi,” Waziŕi wa Mambo ya Nje na Ushiŕikiano wa Kimataifa wa Malawi, Patŕick Kabambe, aliiambia IPS.

Mhango na Mwangoshi wanaweka mataŕajio yao katika jitihada za upatanishi.

“Nimekuwa nikifuatilia habaŕi za suala hili kupitia ŕedio na maombi yangu ni kuona viongozi wa zamani wa Afŕika wanatatua suala hili kabisa,” alisema Mwangoshi.

Mhango ana matumaini kama hayo. “Ninachotaka tu ni kuŕejea na kuanza shughuli zangu za kuvua kwa uhuŕu katika ziwa hili — kwasababu bila ya kufanya hivyo, maisha ya baadaye ya familia yangu yatakuwa gizani.”