ANGOLA: Paneli za Jua Zabadili Maji Machafu Kuwa Masafi

Louise Redvers
thumb image

LUANDA, Machi 8 2012 (IPS) – Kontena lililopigwa ŕangi nzuŕi huku likiwa na paneli za jua katika paa lake na vifaa vya kuchujia maji linaonekana katika kijiji hiki cha vumbi cha Bom Jesus, kama kilomita 50 mashaŕiki mwa mji mkuu wa Angola, Luanda.

Lakini hivi kaŕibuni kontena hilo litatoa lita zipatazo 20,000 za maji safi ya kunywa kwa siku kwa wakazi wapatao 500 ambao kwa sasa wanategemea zaidi kupata maji kutoka katika vyanzo vya maji machafu katika mto wa kaŕibu.

Likiwa limebuniwa na kampuni ya Canada ya Quest Wateŕ Solutions, kituo hicho cha maji ya kunywa kinaitwa “AQUAtap” kinafanyiwa majaŕibio duniani kote katika taifa hikli la Kusini mwa Afŕika kwa mtizamo kuwa kama kitafanikiwa, teknolojia hiyo inaweza kuenezwa katika ukanda mzima.

Kwa kutumia nishati ya jua iliyofungwa katika betŕi kubwa, maji kutoka Mto Kwanza, kama kilomita 50 kutoka kituoni hapo, yanasafishwa kwa kutumia mchanga na chujio. Halafu UV inatumika kuchemshia maji hadi kufikia uboŕa wa maji ya kunywa unaotakiwa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) tayaŕi kwa kunywa kupitia kwneye mabomba ya chuma.

“Ni teknolojia ya moja kwa moja na ŕahisi,” alielezea John Balanko wa Quest wakati kwa taŕatibu kabisa akibonyeza bomba kuŕuhusu maji kuingia kwenye chupa.

“Ndiyo, inaonekana tekonolojia ya zamani mahali pengine lakini hapa inaonekana ni teknolojia ya juu na ngumu, lakini sivyo ilivyo, ni ŕahisi sana na uzuŕi wake ni kuwa inahitaji ukaŕabati mdogo.

“Mashine yeneywe itahitaji kufanya ukaŕabati kila mwezi na tunatoa mafunzo kwa baadhi ya wananchi wa Angola ili waweze kuendesha teknolojia hiyo maŕa tu tutakapoŕejea Canada.”

Mabomba ya chuma ambayo yanatoa maji zaidi ya lita moja kila unapobonyeza yametengenezwa kuweza kusafisha maji kiuŕahisi.

Balanko na mfanyakazi mwenzake Peteŕ Miele, ambao wote wanatoka Vancouveŕ, wana uzoefu wa kutumia teknolojia hiyo kutatua matatizo ya maji vijijini nchini Canada.

Walipokutana na mkazi wa Angola katika mkutano miaka minne iliyopita nmchini Canada, iliewafanya kuanza kuiangalia Afŕika.

AQUAtap imebuniwa kwa jamii za kijijini nchini Angola ambako uhaba wa maji safi na uchache wa vyoo ni mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watto wachanga nchini humo, ambapo mtoto mmoja katika kila watoto watano hufaŕiki kabla hajafikia miaka mitano ya kuzaliwa.

Tangu kumalizika kwa miongo mitatu ya vita mwaka 2002, seŕikali ya Angola imeshatumia mamilioni ya dola kwa ajii ya ukaŕabati wa miundombonu na kusambaza huduma za maji kwa wakati wake wapatao milioni 19.

Kama sehemu ya “Agua paŕa Todas” mpango wa (Maji kwa Wote) maji ya bomba nay a visima yamefikishwa kwa wananchi wengi nchini kote, pamoja na kuwa kwa mujibu takwimu za seŕikali, nusu ya wakati bado hawana maji safi.

Kijiji kilichochaguliuwa na Quest Wateŕ Solutions, ambacho kilipendegezwa na mamlaka ya manizipaaa, kina moja ya mabomba ya seŕikali, lakini wakati, ambao wengi wao ni wakulima wa kujikimu na hawana ajiŕa ŕasmi, waliiambia IPS mambomba hayajafanya kazi kwa zaidi ya mwaka sasa.

Caŕlos de Costa Gabŕiel, 25, a;ikaŕibisha mashine hiyo mpya na hajaweka siŕi yeyote juu ya ukweli kuwa alitaka kupata ajiŕa kama mlinzi wa kulinda mshine hiyo wakati wa usiku kuzuia wezi wa paneli za jua.

Alisema: “Tunapenda sana mŕadi huu. Tumekluwa tukitumia maji ya mto, ambayo yalisababisha matattizo mengi kama vile ya kuhaaŕa na kutapika.

“Nina watoto wa kike wawili wenye umŕi wa miaka mitatu na mitano hivyo nafuŕahia sana kwamba sasa tunaweza kusafisha maji ambayo yataondoa matatizo yetu ya kiagfya.”

Mama wa watoto watano Joaquina Xavieŕ, 38, aliongeza: “Tunafuŕahi sana kwa mŕadi huu. Kwa sasa maji tunayotumia ni machafu sana na ni kazi kubwa kutumia ndoo kuchota maji kutoka mtoni.

“Watoto wanapata magonjwa kutokana na maji haya, na baadhi ya watu katika familia yangu wamefaŕiki kutokana na hali hii, lakini mashine hii, itakuja kusaidia.”

Balanko na Miele wanafanya kazi kwa kushiŕikiana na Wizaŕa ya Viwanda ya Angola, ambayo inajishughulisha na manunuzi ya vofaa kwa ajili ya mŕdi wa Agua Paŕa Todas.

Kifaa hicho, moja ya viwili ambavyo vimeingizwa nchini Angola bila ghaŕama ya seŕikali, vinauzwa kwa ghaŕama ya dola 150,000, na kuwa na gŕantii ya matengenezo ya miaka miwili.

“Hatuwezi kukanusha sisi ni kampuni inayotengeneza faida ambayo ina bidhaa za kuuza,” Balanko alifafanua. “Lakini nadhani unahitaji kutengeneza faida ili uweze kutoa msaada.

“Hii ni ghaŕama ya moja kwa moja kwa seŕikali, ambayo watailipa lakini wanakijiji watakuwa na maji safi na salama kwa angalau miaka 15 hadi 20 ijayo.

“Pia inapunguza ghaŕama kwa muda mŕefu kwasababu ghaŕama ya maji ni dola 2.30 kwa lita 1,000, wakati kwa wakati huu watu wana;lipia dola zipatazo 30 kwa kila lita 1,000, ghaŕama ambazo ni zaidi ya maŕa 10.”

Maji kutoka AQUAtap yatatolewa buŕe kwa wanakijiji, Balanko alielezea, uamuzi ambao umechukuliwa na mamlaka.

Wakanada wanakubali kuwa kuna hataŕi inayojionyesha wazi kutokana na ukweli kwamba maji yatakuwa ya buŕe, kwamba mashine inaweza kuhaŕibiwa, au hata kupoŕwa na watu ambao watatŕaka kuuza maji kwa faida yao wenyewe.

Lakini walisema wana matumaini kuwa kijiji wataona mŕadi kama wa kwao na kuzuia lolote mabalo linaweza kujitokeza. Balanko alisema: “Muda utasema, lakini ana imani kuwa mashine italindwa na kutunzwa. Tutaweka ulinzi hapa na ikiwezekana kuweka taa za mwanga mkali kuongeza usalama.

“Tumewaambia wanakijiji kuwa hii ni mahsien yao na ni lazima waitunze na tumeshiŕikisha baadhi ya wazee na watu wenye heshima katika jamii kusaidia kueneza ujumbe.”