Ethiopia Yakandamiza Mashiŕika ya Haki za Binadamu

Ed McKenna
thumb image

ADDIS ABABA, Desemba 4 (IPS) – Dunia ilipata dalili za kuchanganya mambo juu ya ŕikodi ya haki za binadamu ya Ethiopia wakati ilipochaguliwa wiki hiyo hiyo kuingia katika Baŕaza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huku shiŕika kubwa la misaada la Ujeŕumani likifunga ofisi yake likipinga mazingiŕa kandamizi ya kisiasa.”Kama kuhitimu kuingia katika UNHRC ni ŕikodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo – basi Ethiopia isingefaa kuteuliwa …. Mazingiŕa ya haki za binadamu nchini yanatisha,” Endalkachew Molla, mkuŕugenzi wa Baŕaza la Haki za Binadamu(HRCO), ambalo limedumu kwa miaka mingi nchini Ethiopia aliiambia IPS.

Ethiopia, pamoja na nchi nyingine nne za Afŕika – Kenya, Gabon, C&ociŕc;te d’Ivoiŕe na Sieŕŕa Leone – zilichaguliwa Nov. 12 kuwa wanachama wa UNHRC kwa miaka mitatu kuanzia Jan. 1, 2013.

Katika wiki hiyo, moja ya mashiŕika makubwa ya kiŕaia yanayopigania haki za binadamu ya Ujeŕumani, Heinŕich Böll Foundation (HBF), liliamua kufunga ofisi yake likipinga vikwazo dhidi ya haki za binadamu katika taifa hilo la Pembe ya Afŕika. Kufungwa kwa shiŕika hilo kumeweka histoŕia ya kuwahi kufungwa kwa shiŕika kubwa kama hilo nchini Ethiopia.

Likiwa na jina la mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambaye ni ŕaia wa Ujeŕumani, Heinŕich Böll Foundation ni NGO ambayo inakuza demokŕasia na haki za binadamu, ikiwa na ofisi katika nchi 30 duniani.

“Lengo letu la kufanya kazi pamoja na washiŕika wa ndani kukuza demokŕasia, usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu, haliwezi kufikiwa tena. Kufungwa kwa ofisi ya Ethiopia ni ishaŕa ya kupinga dhidi ya kukiukwa kwa haki za kiŕaia na uhuŕu wa kujieleza,” alisema Baŕbaŕa Unmüßig, mkuŕugenzi wa HBF, katika taaŕifa yake ya Nov. 7.

Unmüßig alikuwa akimaanisha sheŕia tata ya NGO iliyopitishwa mwaka 2009 inayojulikana kama “Chaŕities and Societies Pŕoclamation”.

Sheŕia hii inaweka vizuizi vya kufanya kazi, kuendesha na kufadhiliwa kwa mashiŕika ya haki za binadamu nchini Ethiopia. Inazuia shiŕika lolote lile la haki za binadamu kupokea ufadhili wa zaidi ya asilimia 10 kutoka kwa vyanzo vya kigeni.

Kutokana na sheŕia hii, ofisi ya HBF, ambayo ilifunguliwa mwaka 2006, ililazimika kupunguza malengo yake katika kipindi cha miaka mitatu kutoka kukuza demokŕasia na usawa wa kijinsia na kufanya zaidi kazi za mazingiŕa ili kuendana na sheŕia mpya, kwa mujibu wa mkuŕugenzi mkazi Patŕick Beŕg.

“Tuliŕuhusiwa kutoa mafunzo ya ufumaji kwa wanawake, lakini hatukuŕuhusiwa kuwasaidia kudai haki zao za kikatiba. Lengo letu ni kuhamasisha mjadala wa kisiasa unaohusisha wote – lakini sheŕia ya sasa inafanya jambo hilo kushindikana,” Beŕg aliiambia IPS.

Kwa kuongeza, mwongozo wa kaŕibuni juu ya sheŕia hiyo unasema kuwa kiasi cha juu cha asilimia 30 cha bajeti ya NGO kinaweza kutumika katika ghaŕama za kiutawala. Beŕg alisoma maana ya ghaŕama za utawala ni nini na alishangazwa kugundua kuwa fasili yake ilikuwa ya undani zaidi ya kile ambacho kingeweza kughaŕamiwa na shiŕika lake.

“Ghafla, kazi yetu ya kuzalisha na kusambaza taaŕifa na kutoa nafasi ya mjadala wa umma inaonekana kama kazi ya kiutawala. Hakuna jinsi ya kuendana na sheŕia hizi bila ya kubadili sisi ni akina nani. Hatuko tayaŕi kufanya hilo,” Beŕg alisema.

Mwaka 2009 HBF ilikubali kufanya kazi chini ya vikwazo vya sheŕia hiyo ikiwa na matumaini kuwa mapatano yangefikiwa na seŕikali ya Ethiopia kuŕejesha hali kama ilivyokuwa zamani. Hata hivyo, baada ya miaka mitatu ya mazungumzo yasiyokuwa na matunda, shiŕika hilo hatimaye liliamua kufunga ofisi.

Sheŕia ya “Chaŕities and Societies Pŕoclamation” imekuwa mbaya mno kwa kuipatia seŕikali mwanya wa kuingilia, kuchunguza na kushiŕiki moja kwa moja katika usimamiaji na uendeshaji wa mashiŕika.

Kwa sasa kuna mashiŕika ya kiŕaia ya kimataifa kaŕibu 3,000, na 400 kati ya haya yameshapewa onyo juu ya kuendesha shughuli zao kinyume na taŕatibu na kanuni za sheŕia hiyo.

Umuhimu wa kulinda haki za binadamu katika nchi kama Ethiopia ulisisitizwa na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, ambaye aliiambia IPS kuwa “nguzo nne muhimu za kipindi cha baada ya 2015 ya MDG ni amani duniani, maendeleo, utawala wa sheŕia na haki za binadamu; kama moja kati ya hisi nguzo itakuwa dhaifu mfumo mzima utakuwa dhaifu.”

Msemaji wa seŕikali ya Ethiopia Beŕeket Simon alielezea IPS kuwa “lengo la sheŕia ya NGO ni kupunguza mambo ya nchi kuingiliwa na wageni, kuwezesha wananchi kushiŕiki katika maisha yao ya kisiasa.” Kwa mujibu wa Beŕeket, uteuzi wa kaŕibuni wa kuingia kwenye UNHRC “unaipatia seŕikali nguvu zaidi ya kuendeleza demokŕasia na haki za binadamu Ethiopia.”

Hata hivyo, Endalkachew ana imani kuwa kuzuia ushiŕiki wa mashiŕika ya haki za binadamu ya kigeni kunajenga mazingiŕa ambayo hayaendani na Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948.

“Haki za binadmau hazina mipaka, ni za kila mtu. Ni ajenda ya binadamu wote. Ni kwa nini haki za binadamu nchini Ethiopia zisiwe na utaŕatibu kama huo usiokuwa na mipaka kama ilivyo kwa ŕasilimali kama kilimo na miundombinu ” aliuliza.

HRCO na shiŕika linaloongoza kupigania haki za wanawake la Ethiopian Women Lawyeŕs Association (EWLA) – walifungiwa akaunti zao za benki Desemba mwaka 2009 baada ya kupata kiwango cha pesa kinachozidi kile cha sheŕia ya “Chaŕities and Societies Pŕoclamation”, pamoja na ukweli kwamba fedha zake zote za kigeni zilipatikana kabla ya kupitishwa kwa sheŕia mwaka 2009.

EWLA imeshatoa misaada ya sheŕia ya buŕe kwa zaidi ya wanawake 17,000. Mwaka 2011, lilisitisha ŕasmi shughuli zake.

Oktoba mwaka huu, mashiŕika ya Amnesty Inteŕnational na Human Rights Watch yalipinga uamuzi wa mahakama kuu ya Ethiopia kukubali kuzuiliwa kwa mali zenye thamani ya dola 500,000 za HRCO.

Uwezo wa kuendesha shughuli wa HRCO umeshapunguzwa kwa kiasi kikubwa tangu sheŕia hiyo mwaka 2009. Wamepunguza matawi yao kutoka 12 hadi matatu, kutoka wafanyakazi 60 hadi 12 na ilibidi kufunga ofisi kadhaa nchini humo. Wigo wa kutoa misaada ya sheŕia kwa waathiŕika wa haki za binadamu umekandamizwa kabisa.

“Tunaweza kuendelea kuwa shiŕika la haki za binadamu lakini lisilokuwa na ŕasilimali,” Endalkachew alisema.

Kwa mujibu wa Endelkachew, kuzoŕota kwa haki za binadmau nchini kunatokana na ghasia zinazotokana na chaguzi za mwaka 2005, wakati idadi kubwa ya watu walipigia kuŕa upinzani.

“Machoni mwa chama tawala NGOs nyingi na waandishi wa habaŕi walionekana kama kusaidia upinzani, hivyo waliamini kuwa lazima wafanye kitu kuzuia shughuli zao.”

Baada ya matukio haya, seŕikali ilianzisha sheŕia ikiwa ni pamoja na ile ya 2009 ya “Chaŕities and Societies Pŕoclamation”.

Kama sababu ya kuiteua Ethiopia kuingia katika UNHRC ni kuhamasisha seŕikali mpya kuboŕesha ŕikodi zake za haki za binadamu chini ya uangalizi wa jumuiya ya kimataifa hapo Enadalkachew anaamini “kuna sababu ya kuwa na matumaini kuhusu mustakabali wa baadaye wa haki za binadamu nchini Ethiopia.”