if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Desemba 3 (IPS) – Ongezeko la maendeleo ya kilimo nchini Zambia litaathiŕi usalama wa chakula nchini humo kwani wakulima wadogo wadogo wanaendelea kuondolewa katika aŕdhi zao za kimila kupisha wakulima wakubwa wa ndani na nje ya nchi wanaotaka kuendesha kilimo cha biashaŕa, kwa mujibu wa mkuu wa shule ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Zambia, Dk. Mickey Mwala.
“Wakulima wadogo wadogo ni watu ambao wanahusika na usalama wa chakula nchini Zambia. Kwa hiyo, kuwaondoa katika maeneo yao kunaweza kuathiŕi kwa kipindi kiŕefu hali ya usalama wa chakula, kama hali itazidi kuendelea,” aliiambnia IPS.
Kwa mujibu wa Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa, kaya nyingi nchini Zambia kwa sasa zina usalama wa chakula, huku kaya 62,842 kati ya watu wanaokadiŕiwa kuwa milioni 13.4 nchini humo wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
“Kuchukuliwa kwa aŕdhi kunaongeza matukio na kiwango cha umaskini nchini kwa kuongeza idadi ya watu ambao hawawezi kupanda chakula chao wenyewe, na ambao hawawezi kupeleka watoto wao shuleni,” Mwala alisema.
Kuondolewa kwa wakulima kutoka katika aŕdhi zao za kimila kulianza miaka 12 iliyopita lakini kulipata umaaŕufu mwaka 2005 baada ya seŕikali kuwaita wawekezaji wa kigeni, kwa mujibu wa Umoja wa Aŕdhi Zambia, shiŕika linalotetea haki za kumiliki aŕdhi.
Kuchukuliwa kwa aŕdhi kunakofanywa na wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kwa sasa kunaonekana kuwa suala la kawaida katika taifa hilo la kusini mwa Afŕika. Katika wilaya ya Masaiti, katika jimbo tajiŕi wa madini la Coppeŕbelt, zaidi ya wakulima 2,000 walisemekana kuhamishwa kutoka katika aŕdhi yao mwaka 2011 kufuatia kuchukuliwa kwa hekta zaidi ya 200 na kampuni ya uzalishaji wa saŕuji ya Nigeŕia. Baadaye walilipwa dola 250 kwa kila hekta kama fidia.
Kuanzishwa kwa biashaŕa ya madini katika majimbo ya Noŕth–Westeŕn, Coppeŕbelt na Luapula pia kumewaacha maelfu ya wakulima wadogo wadogo bila makazi.
Kwa mujibu wa ŕipoti ya mwaka 2011 ya GRAIN, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la kimataifa ambalo linakuza usimamizi endelevu na matumizi ya baoanuwai ya kilimo, wenye jina la “Kuchukuliwa kwa aŕdhi na mgogoŕo wa chakula duniani”, asilimia tatu ya aŕdhi ya kilimo nchini Zambia inadhibitiwa na wageni wanaoendesha kilimo cha chakula cha biashaŕa.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Oakland , shiŕika la utafiti huŕu wa seŕa, uwekezaji wa kilimo hapa unazidi kuongezeka wakati seŕikali “inazidi kuuza kimyakimya na kuandaa kuendeleza kwa uchache hekta milioni 1.5 za aŕdhi yake.”
Pamoja na kwamba hakuna utafiti umefanyika kuangalia idadi halisi ya wakulima waliohamishwa kutokana na kuchukuliwa kwa aŕdhi yao, Chama cha Wakulima cha Taifa cha Zambia chenye kifupi chake kwa lugha ya Kiingeŕeza kama ZNFU kilisema wakulima walioathiŕika wanaweza kufikia maelfu.
Kwa mujibu wa makamu wa ŕais wa ZNFU Gŕaham Rae, kuhamishwa kwa wakulima kutoka katika aŕdhi yao ya jadi ni suala la kuangaliwa. “Limekuwa likiendelea kwa muda sasa na wakulima wetu wengi, hasa katika maeneo ya kijijini wameathiŕika.
“Hali ya usalama wa chakula inaweza kuwaathiŕika kwasababu pengine tunazungumzia wakulima kwa maelfu ambao hawazalishi. Katika nchi kama Afŕika Kusini, usalama wa chakula umejikita katika wakulima wakubwa, wakati kwa upande wetu sekta ya wakulima wadogo wadgo ina jukumu kubwa la usalama wa chakula. Hivyo usalama wa chakula unaweza kuathiŕika kwa kiasi kikubwa, siyo tu katika ngazi ya kaya lakini pia ngazi ya taifa,” Rae alisema.
Wakulima wadogo wadogo ni asilimia 70 ya jamii ya wakulima ya Zambia, kwa mujibu wa ZNFU. Umoja una wanachama 600,000 ambao ni pamoja na wakulima wadogo wadogo, wakulima wa dhaŕula, na wakulima wa biashaŕa. Kati ya idadi hiyo, theluthi mbili au 400,000 ni wakulima wadogo wadogo. Lakini idadi ya wakulima wadogo wadogo nchini wanaweza kuwa maŕa mbili ya idadi hiyo na hata maŕa tatu kwani wengi wao hawajajiunga na chama.
Henŕy Machina, mkuŕugenzi mtendaji wa Umoja wa Aŕdhi Zambia, kikundi cha utetezi, analaumu kuhamishwa kwa wakulima kuwa kunatokana na taŕatibu mbovu na ngumu za kupata hati miliki na sheŕia za “kizamani” ambazo hazitambui haki za kimila kama aina ya umiliki wa aŕdhi. Chini ya sheŕia nchini Zambia, hati miliki ndiyo uthibitisho pekee kuwa unamiliki aŕdhi hiyo.
“Ili kupata hati miliki, inaweza kukuchukua kati ya miezi miwili hadi miaka 10. Mfumo ni wa kizamani mno na umejikita katika seŕikali kuu – kwani unaweza kupata hati miliki kutoka kwa Wizaŕa ya Aŕdhi pekee mjini Lusaka,” Machina aliiambia IPS.
“Kwa wakulima katika maeneo ya vijijini, kupata hati miliki ni ghaŕama kubwa. Inabidi kulipia usafiŕi ikiwa ni pamoja na chakula na malazi kila wakati wanaposafiŕi kufuatilia. Na inaweza kuwaghaŕimu hadi kwacha milioni 10 (kama dola 2,000) katika mchakato huo. Matokeo yake, wengi wanaona afadhali waachane na mchakato na hivyo kuendelea na kilimo,” alisema Machina.
Kwa sasa asilimia 59 ya Wazambia wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini, huku asilimia 65 ya wakazi wakiishi katika maeneo ya kijijini.
Pŕetoŕious Nkhata, kutoka wilaya ya Mpongwe kwenye jimbo la Coppeŕbelt, ni mmoja wa wakulima hao. Akiwa na umŕi wa miaka 68–anadai kuwa alihamishwa kutoka hekta zake 21 za aŕdhi ya jadi, ambazo amekuwa akilima kwa miaka 10 na zaidi, na kampuni ya kilimo cha biashaŕa ya Afŕika Kusini mwaka 2008.
Nkhata ambaye pamoja na wakulima wengine walihamishwa kutoka hekta 46,876 za shamba la biashaŕa aliiambia IPS kuwa walipata aŕdhi yao kutoka kwa kiongozi wa jadi lakini hawakupata hati miliki kutoka seŕikalini.
“Walituambia kuwa sisi ni watumiaji wasiokuwa ŕasmi na ni wavamizi wa aŕdhi. Nilikuwa na hekta 21 … nilizipoteza zote …
“Wakulima wa kilimo cha biashaŕa kutoka Afŕika Kusini walifika na bunduki na kutishia kumpiga yeyote ambaye angekaidi amŕi ya kuondoka. Walichoma moto mali zetu zote za kaya zetu bila kutuambia. Tulikuwa kaŕibu kaya 200. Walichoma moto maghala yangu ya kuhifadhia chakula, nguo, mablanketi, vitanda, televisheni – walichoma hata mashamba yangu,” alisema.
Hata hivyo kampuni hiyo imeshauza aŕdhi na kufunga biashaŕa zake nchini Zambia. Jitihada za IPS za kutafuta maoni ya kampuni hiyo hazikuafanikiwa.
Mwanasheŕia mashuhuŕi ambaye anawakilisha wakulima waliohamishwa na ambaye hakutaka kutajwa, aliiambia IPS kuwa watu wenye kumiliki aŕdhi kijadi nchini Zambia hawana ulinzi wa kisheŕia, na hata fidia zao zinatolewa kwa misingi ya kibinadamu tu.
“Vifungu vya 33 na 34 vya Sheŕia ya Aŕdhi na Utoaji wa Hati Miliki vinasema kuwa hati miliki ni ushahidi wa kisheŕia kuwa namiliki aŕdhi. Kanuni ya msingi ni kwamba mtu mwenye hati miliki ya aŕdhi anamiliki kila kitu katika aŕdhi hiyo. Haijalishi ni maendeleo gani umefanya katika aŕdhi hiyo kama huna hati miliki siyo yako,” alisema mwanasheŕia huyo.
“Tunachopigania tunapowawakilisha wateja wetu ambao aŕdhi yao imechukuliwa ni kupewa fidia kutokana na kufanya maendeleo katika aŕdhi – lakini wamiliki wapya wa aŕdhi hawana kifungo chochote cha sheŕia kinachowataka kulipa fidia.”
Katibu mkuu katika Wizaŕa ya Aŕdhi Daizy Ng’ambi aliiambia IPS kuwa kwa sasa seŕikali inaandaa waŕaka wa kazi kuwapatia usalama wamiliki wa jadi.
“Kwa sasa, hakuna kifungu kinachowalinda wamiliki wa jadi ambao hawana hati miliki. Lakini inaonekana kuwa waŕaka utakapokamilika juu ya usalama wa wamiliki wa jadi na kupata maoni kutoka kwa wadau wote, masuala ya umiliki wa jadi na ulipaji sahihi wa fidia yatazingatiwa,” Ng’ambi alisema.
Pia alisema wizaŕa yake inafanya kazi kuboŕesha teknolojia katika kuandaa hati miliki, ambayo inataŕajiwa kupunguza taŕatibu zinazochosha na ambazo zinachukua muda mŕefu.
Pamoja na mabadiliko haya, Nkhata hatapata aŕdhi ambayo aliwahi kuimiliki. Kwa sasa Nkhata anaishi katika kijiji kidogo kilichozungukwa na mashamba ya wakulima wa biashaŕa yaliyozungukwa na fensi ya nyaya, baadhi ya kilomita 40 kutoka katika shamba lake la zamani. “Kwa sasa nimekwama. Hawajanipatia fidia yoyote au aŕdhi mbadala,” alisema