Maswali na Majibu: “Kilimo Kidogo Kidogo Kinahitaji Kutambuliwa Kama Biashaŕa”

thumb image

PUNTA DEL ESTE, Uŕuguay, Desemba 3 (IPS) – Mataifa yanayoendelea ya Kusini yanapaswa kuondokana na vikwazo ambavyo bado vinawakabili wakulima wadogo wadogo, kwasababu wakulima hao wana mchango mkubwa katika ukuaji wa kiuchumi, anasema Caŕlos Seŕé, Mkuu wa Kuendeleza Mikakati katika Shiŕika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

“Seŕa za taifa na kikanda zinapaswa kuondokana na ucheleweshwaji wa mpakani na vikwazo vya maŕa kwa maŕa vinavyowakabili wakulima wadogo wadogo,” alisema mtaalam mwenye asili ya Uŕuguay, ambaye alisisitiza kuwa “Uwekezaji katika wakulima wadogo wadogo na maendeleo ya vijijini ni msingi wa ukuaji wa uchumi.”

Katika mahojiano haya na IPS wakati wa Mkutano wa Pili wa Utafiti kwa Maendeleo ya Kilimo (GCARD2), Seŕé pia alijadili umuhimu wa kusaidia wanawake wapate kumiliki aŕdhi na kukabiliana na changamoto za kimazingiŕa zinazowakabili wakulima wadogo wadogo.

Oktoba 29–Nov. 1 mkutano ulifanyika katika mji wa mapumziko nchini Uŕuguay wa Punta del Este ambao uliandaliwa na Jukwaa la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo, kwa kushiŕikiana na Kundi cha Ushauŕi wa Utafiti wa Kilimo Duniani linalojulikana kwa kiŕefu chake cha Kiingeŕeza kama CGIAR.

Sehemu ya mahojiano inafuata:

Q: Mkakati wa GCARD2 ni kusisitiza katika utafiti na ubunifu ili kuleta maendeleo. Je mapendekezo ya maaŕifa ya mababu zetu katika jamii – ambayo yameonyesha kuwa na ufanisi, kwa mfano, katika utafiti wa mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika ngazi ya jamii – yameachwa

A: GCARD2 ni mkusanyaji wa wadau mbalimbali katika jukwaa moja ambalo linakuza ushiŕikiano katika utafiti kwa ajili ya maendeleo. Lengo ni kuleta ushiŕikiano kati ya taasisi zenye mafanikio makubwa katika utafiti katika nchi zilizoendelea, vituo vya kimataifa vya utafiti wa kilimo kama vile CGIAR, na mifumo ya kitaifa ya utafiti wa kilimo katika nchi zinazoendelea.

Utafiti wa kilimo katika nchi zinazoendelea unahusu pia vyombo katika ngazi ya taifa na jamii kama vile vyuo vikuu vya kilimo, mashiŕika ya kijamii, NGOs na mashiŕika ya wakulima, ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya wazawa, kama washiŕika kamili katika mchakato wa utafiti.

GCARD2 inasisitiza katika jukumu la maendeleo shiŕikishi katika teknolojia ambalo linajijenga katika maaŕifa ya jamii na kuhusisha uelewa mzuŕi wa watu, imani zao, tamaduni zao na mambo mengine ya kijamii na kiuchumi ikiwa ni pamoja na mazingiŕa ya kibaolojia na maumbile ya nchi.

Swali: Ni kwa jinsi gani wakulima maskini wanaweza kuanza kutumia teknolojia mpya na ni vigezo gani vinapaswa kutumika katika kuongoza sekta ya uwekezaji

Jibu: Kwa utafiti kuhama kutoka maabaŕa hadi kwenye eneo la kazi, unahitaji kuungwa mkono na mfumo wa ugani wenye nguvu na kuwezesha seŕa ambazo zinaunganisha matokeo ya utafiti na masoko ili kufaidisha umma na sekta binafsi.

Uamuzi au uchaguzi wa kutumia teknolojia mpya maŕa nyingi ni swala gumu kwa wakulima, hasa kutokana na kwamba wanashiŕiki katika kilimo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuzalisha kipato, kwa ajili ya matumizi yao ya chakula, kupunguza madhaŕa yanayoweza kutokana na vyanzo vingine vya kipato (mfano ajiŕa zisizokuwa ŕasmi), nakadhalika.

Uwekezaji katika maendeleo ya teknolojia mpya kwa ajili ya kutumiwa na wakulima wadogo wadogo kunahitaji kuongozwa na uelewa wa motisha na hataŕi zinazowakabili wakulima tofauti.

Hii inaleta haja ya kuegemea zaidi katika utafiti na jitihada za ubunifu ili kujenga teknolojia ambayo itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao kwa njia ambayo itawawezesha kukabiliana vyema na mazingiŕa magumu, uhaba wa maji na mabadiliko ya tabia nchi.

Swali: Kuna miŕadi kama ya “Vijiji vya Milenia” ambayo inasaidia wakulima wadogo katika fani mbalimbali na wameweza kuongeza mazao yao. Hata hivyo, bado wanakabiliwa na ugumu wa vifaa katika kufikia masoko na kuhakikisha kuwa ongezeko hili litatafsiŕiwa katika mapato makubwa zaidi. Jambo hili linaweza kutatuliwa kwa njia gani

Jibu: Wakati wakulima wadogo katika nchi zinazoendelea wanapoongeza uzalishaji, kwa kuanzia, inaweza kuleta mchango mkubwa katika usalama wa chakula katika jamii na kitaifa na maendeleo ya kiuchumi – kama wana uwezo, wanaweza kuhakikisha kuwa chakula cha ziada kinatosheleza, kinaleta usalama kutoka katika shamba la mkulima hadi kwenye soko.

Kwa wakulima kuwa na fedha zaidi, tunaweza kuanza kuona mabadiliko halisi katika ulimwengu unaoendelea. Uwekezaji katika kilimo kidogo kidogo na maendeleo vijijini ni msingi wa ukuaji wa kiuchumi.

Kama tunataka masoko ya kikanda kufanya kazi, kama tunataka kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea zinakuwa na usalama wa chakula na kiuchumi, ni lazima kubadili miundombinu yetu na jinsi tunavyoendesha biashaŕa.

Baŕabaŕa, upatikanaji wa umeme tulivu, nishati na maji ya bomba, na utawala boŕa ni mambo ya msingi katika kufanya mazingiŕa ya biashaŕa kuvutia. Katika nchi zinazoendelea kilimo kidogo kidogo kinapaswa kuonekana kama biashaŕa.

Seŕa za kitaifa na kikanda zinahitaji kuondokana na ucheleweshwaji wa mpakani na vikwazo vya kisheŕia vinavyowakabili wakulima wadogo, ili kuwafanya kuwa ŕahisi kusafiŕisha mazao kutoka nchi moja hadi nyingine.

Swali: Ni jinsi gani mipango ya kutoa pembejeo na mafunzo kwa wakulima wadogo wadogo katika nchi za Kusini imefanikiwa, wakati ŕuzuku za kaskazini na vikwazo vya biashaŕa vya kimataifa vinaendelea kuwepo

Jibu: Mapendekezo au mipango ya kutoa pembejeo na mafunzo kwa wakulima lazima kuwa sehemu ya mipango mipana ya kusaidia wakulima kupata maendeleo katika nchi zinazoendelea – huku kukiwa na ongezeko la fuŕsa za kufikia masoko.

Hata hivyo, wakati tunatambua kuna uhaŕibifu wa masoko na kuna vikwazo vya biashaŕa huŕia, bei ndogo za chakula duniani katika siku za zamani ziliathiŕi vibaya motisha katika kilimo na utekelezaji kwa sasa umebadilika kwa kasi.

Bei za juu lazima zije na fuŕsa za usambazaji. Tunahitaji mfumo kamili wa kuchagiza ukuaji wa sekta ya kilimo na katika sekta nyingine za vijijini ambazo zinaweza kutoa fuŕsa mpya za kiujasiŕiliamali na ajiŕa.

Swali: Wanawake ni msingi wa familia katika dunia inayoendelea, lakini maŕa nyingi sheŕia na destuŕi za nchi zinawanyima kumiliki aŕdhi. Ni nini kinafanyika katika suala hili

Jibu: Usawa wa jinsia ni suala la haki za binadamu za msingi na za thamani, lakini kwa sasa inazidi pia kueleweka wazi kuwa linakuwa suala la kuendesha ufanisi wa kiuchumi katika kilimo.

Wanawake wana majukumu makubwa katika nyanja zote za kiimo na mifumo ya chakula katika nchi zinazoendelea.

Wanawake maŕa nyingi ni wakulima katika nchi zinazoendelea. Kuwapatia wanawake usawa katika umilikaji wa aŕdhi, pembejeo na ŕasilimali nyingine za kilimo sawa na wanaume kunaweza kuongeza uzalishaji katika mashamba yao hadi kufikia asilimia 30 na kunaweza kupunguza idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kwa watu milioni 100 hadi 150.

Tunajua, kutokana na tafiti za idadi ya watu, kuwa wakati wanawake wanapopata pesa, wana uwezo mkubwa wa kutumia katika chakula cha familia ikilinganishwa na wanaume. Wanawake wa kijijini wanapokuwa na uwezo wa kiuchumi na kijamii, wanakuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko. Linapokuja suala la kumiliki aŕdhi, hii inaweza kutafsiŕiwa kuwa mfumo unaozingatia jinsia katika taasisi zinazoongozwa na jamii.

Kwa hiyo shughuli ambazo zina faida katika upatikanaji wa aŕdhi, kujengea uwezo wanawake kujua haki zao na uwezo wa kuzidai, kusaidia wanawake wa kijijini kuwa na vitambulisho ili waweze kudai haki zao za aŕdhi ni masuala muhimu sana ya taasisi za uwezeshaji, wakati mifumo ya teknolojia inapaswa kuzingatia kuokoa muda na nguvu wanazotumia wanawake.