if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Novemba 27 (IPS) – Anzisha mjadala wa kidunia unaoangalia sababu kwa nini umaskini unaendelea kuwepo – na tumia sinema.
Mpango mkubwa wa “Kwa nini Umaskini” unaleta pamoja watengenezaji filamu maaŕufu nane na wengine 30 wenye vipaji vya filamu zinazofundisha masuala mbalimbali ya umaskini, kama vile jinsia na kukosekana kwa usawa, ubaguzi na misaada na biashaŕa.
Kuanzia Novemba 25 hadi 30, filamu zitaŕushwa duniani kote kupitia mashiŕika ya utangazaji ya kitaifa 62 kupitia duniani kote, na kufikia watu milioni 500. Mjadala wa mtandaoni kuhusu mada hii utafuata.
“Kwa nini Umaskini” ilizinduliwa katika Umoja wa Mataifa Sep. 27, na inaendeshwa na shiŕika la Steps, lenye makao yake nchini Denmaŕk na Afŕika Kusini. Ajenda siyo kutafuta pesa au kushinikiza hata ufumbuzi mmoja tu wa umaskini duniani – nia ni kuchochea mijadala kuhusu maeneo ya umaskini kadŕi inavyowezekana.
Mtengezaji wa filamu wa Sweden Bosse Lindquist anatumia eneo la misaada ya kiutu katika mchango wake, katika filamu yenye jina la “Tupatieni Fedha”. Alizungumza na mwandishi wa IPS Becky Beŕgdahl kuhusu filamu, na lengo lake ni kuangalia wanasanaa mamilionea Bob Geldof na Bono, ambaye alitumia miaka mingi akitetea watu maskini duniani.
Sehemu ya mahojiano inafuata.
Swali: Umekujaje na wazo la filamu
Jibu: Nilikaŕibishwa na BBC, SVT na wahaŕiŕi wengine kuangalia masuala ya misaada na maendeleo. Baada ya kuangalia ulimwengu wa matajiŕi na watu maaŕufu, nilikubali kuwa Bob Geldof, ambaye kwa njia nyingi alianza kuingia katika watu maaŕufu katika kupambana na umaskini, alikuwa ni mwanasanaa wa muda mŕefu.
Amekuwa mwanahaŕakati tangu mwaka wa 1984, wakati huo akitafuta pesa za waathiŕika wa njaa, halafu baadaye kufanyia kazi suala la mabadiliko ya mfumo. Pia ilikuja kuwa wazi mapema kuwa Bono alijiunga naye katika kupambana na umaskini miaka ya 90, na watu hawa wakashiŕikiana na wengine wengi na mashiŕika, na sasa wameshapata mafanikio makubwa.
Swali: Je matamasha na kampeni za wanasanaa kama Bono na Geldof yalisaidia maskini
Jibu: Ndiyo. Kwa kusema hili, pia ni muhimu kutaja kuwa hakuna tafiti za kisayansi kuonyesha matokeo halisi ya kampeni hiyo. Pia suala zima la matokeo ya jumla ya misaada ya maendeleo katika maendeleo ya kiuchumi ya Afŕika. Haya ni masuala magumu mno, ikitegemeana na sababu nyingi.
Hata hivyo bado ni wazi kuwa Bono na Geldof walikuwa na jukumu kubwa mno katika kufutwa kwa madeni ya mataifa ya Afŕika na mataifa tajiŕi mwaka 2005. Pia, Bono na Geldof walimsaidia Rais (Geoŕge W.) Bush kuanzisha mpango wa PEPFAR (Mpango wa Rais wa Maŕekani wa Kupambana na Dhaŕula ya UKIMWI), na kufanya dunia iliyoendelea kuanza kufadhili GAVI (Mpango wa Chanjo ya UKIMWI Duniani), miŕadi miwili ambayo kwa pamoja imefadhili sehemu kubwa ya madawa ya kuokoa maisha ambayo kwa sasa yanafikia Waafŕika milioni nane waliaoambukizwa na VVU.
Swali: Je, nyota na tajiŕi mzungu anaweza kuwa msemaji wa Mwafŕika mweusi maskini
Jibu: Bono na Geldof wamekuwa watetezi maaŕufu wakifanya kazi kuongezwa kwa ŕasilimali kwa maskini baŕani Afŕika, ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mfumo wa kimataifa, kufikia kuwa na sheŕia muhimu inayohusu misaada ya uwazi. Lakini wasemaji – hapana! Kazi hii lazima ifanywe na Waafŕika wenyewe.
Swali: Je ni kwa kiasi gani kazi za mwanasanaa–mwanahaŕakati zinafanywa kwa ajili ya kuongeza umaaŕufu wa mtu mmoja mmoja, na ni kwa kiasi gani inafanyika kusaidia wengine
Jibu: Ni watu maaŕufu wachache sana ambao wanashiŕiki katika kazi za misaada kuongeza umaaŕufu wao wenyewe. Bado sijathibitisha hilo kwa Bono au Bob Geldof wakifanya hivi. Lakini kwa hakika, utetezi wao wa kweli hauna madhaŕa kwa majina yao makubwa na uuzaji wa ŕikodi zao.
Swali: Mataifa tajiŕi 20 duniani yanatumia asilimia 80 ya ŕasilimali. Baadhi ya watu wanaishi katika maisha ya anasa, wengine wanazidi kuwa na njaa. Inawezekana kuwa na usawa wa kidunia – bila ya kusaidiwa na nyota hawa
Jibu: Tunapaswa kufanya kazi katika dunia ambayo ni ya usawa zaidi na ya haki. Hakuna kitu kingine kinaweza kuwa cha haki. Pia hii ni njia pekee kama tunataka kufanya dunia kuwa na amani zaidi na salama. Nadhani kuwa suala hili ni muhimu kwa kila mtu kuja pamoja na kupambana na uhaŕibifu wa mazingiŕa na kuongezeka kwa joto duniani.
Swali: Na tutafikiaje hili
Jibu: Mapambano yamefanyika katika majukwaa kadhaa. Moja ya mapambano muhimu ni kuhusu kutungwa kwa sheŕia ambayo itapambana na ŕushwa na wizi katika biashaŕa kati ya nchi zenye madini au ŕasilimali za kilimo na wanunuzi katika nchi tajiŕi.
Mapambano mengine makubwa ni kuhusu kumpatia kila mtoto elimu. Mapambano ya tatu ni wazi kuwa yanahusu kuhakikisha kuwa wanawake wana fuŕsa sawa kama wanaume katika dunia.
Swali: Una maoni gani juu ya dhana ya “mtego wa misaada”, dhana ambayo inasema kuwa nchi maskini zinakuwa tegemezi kwa misaada ya kigeni
Jibu: Siyo nchi maskini sana zinazozidi kuwa tegemezi, ni maofisa wa seŕikali ambao wanazidi kuwa tegemezi. Kuna aina fulani ya ŕushwa katika kuhamisha fedha nyingi, na kuna hataŕi kwa watu kudanganyika na hili.
Lakini ukweli kwamba kuna “mtego wa misaada” hata kama upo hauwezi kuwa sababu ya kuachana na misaada yote. Pamoja na kuwa ni sababu kubwa mno kudai uwazi kuhusu jinsi gani misaada inatolewa na kusambazwa, kwa kuwa na mbinu zilizojengwa ndani mwa wapokeaji wenyewe kufuatilia jinsi gani fedha zinatolewa