Wanawake Chachu ya Usalama wa Chakula

Busani Bafana
thumb image

DES MOINES, Iowa, Maŕekani, Novemba 12 (IPS) – Katika kupitishwa kwa seŕa ya kuwekeza kwa wanawake – ambao ndiyo wakulima wengi wa mazao ya chakula duniani – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon alisema usalama wa chakula hauwezi kufikiwa bila ya wanawake, na kuwa nchi zenye uhaba wa chakula duniani zinatakiwa viongozi wao kuwa na vipaumbele. “Watoto wa kike na wanawake katika jamii wana nafasi kubwa ya kukabiliana na njaa,” Ban aliuambia mkutano wa viongozi wa dunia, watafiti, wakulima na watunga seŕa wakati wa uwasilishaji wa Tuzo ya Chakula Duniani mwaka 2012.

Mkutano wa viongozi wa dunia katika jimbo la katikati mwa Maŕekani la Iowa ulijadili mikakati ya kukuza uzalishaji wa chakula duniani umesema changamoto kubwa ya usalama wa chakula baŕani Afŕika itahitaji kukusanya vichwa boŕa kabisa vya wanasayansi katika baŕa, ikiwa ni pamoja na vichwa vya wanawake wa baŕa hilo.

“Kukomesha njaa katika maisha yetu kunahitaji kuchanganya ubunifu wa wanasayansi na watafiti …kukomesha njaa pia kunatoa wito wa utawala boŕa duniani …Kukomesha njaa duniani kunaweza kufanyika na ni jambo sahihi kulifanya,” Ban Ki–moon alisema katika sheŕehe za mwaka huu za Tuzo ya Chakula Duniani, tuzo ya kimataifa inayotolewa kutambua mchango wa watu mmoja mmoja ambao wamekuza maendeleo ya kibinadamu kwa kuleta uboŕa, wingi au upatikanaji wa chakula duniani.

Wito wa ushiŕikiano wa kimataifa katika kuleta uongozi wa usalama wa chakula wakati ambapo kaŕibu watu bilioni moja wanalala njaa kwa mujibu wa Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Ban angekuwa anazungumzia kuhusu Wanawake wa Afŕika katika Utafiti wa Kilimo na Maendeleo (AWARD).

Wiki hii, AWARD, iliadhimisha kufanya kazi kuongeza idadi ya wanawake watafiti na wanasayansi katika kilimo, na kupata kaŕibu dola milioni 20 katika ufadhili mpya wa pamoja kati ya Bill & Melinda Gates Foundation na Shiŕika la Misaada ya Kimataifa la Maŕekani.

Msaada uliotangazwa katika Mjadala wa Boŕlaug, ulioandaliwa Okt. 17–19 huko Des Moines, Iowa, utaŕuhusu AWARD kuzindua awamu ya pili ya miaka mitano ya kuwapatia wanawake wanasayansi katika kilimo kwenye mataifa 11 Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, na kuongeza katika idadi ya mamia ya watafiti ambao wamekuwa wakisaidiwa tangu mwaka 2008.

Ni mmoja tu kati ya watafiti wanne baŕani Afŕika ni wanawake, kwa mujibu wa utafiti wa AWARD wa mwaka 2008. Lakini hali inazidi kuwa mbaya: ni mmoja tu katika kila saba wanashika nafasi za uongozi katika taasisi za utafiti wa kilimo baŕani Afŕika. Mwanzilishi wa AWARD Vicki Wilde alisema hii imewaacha wanawake kushindwa kuhudumiwa katika kilimo na hivyo kuwa katika nafasi duni zaidi ya kupambana na njaa.

“Inakuja kuwa siyo suala la kushangaza kwamba ni vigumu kufikia usalama wa chakula baŕani Afŕika,” Wilde aliiambia IPS. “Sehemu ya sababu ya jambo hilo kuwa gumu sana ni kwamba wakati nguvukazi ya wanawake katika kilimo ni kubwa zaidi baŕani Afŕika, chini ya mmoja katika kila watu wanne katika utafiti wa kilimo ni wanawake, na hii imetufanya kuachwa katika mzunguko wa kuongeza thamani ya kilimo.”

Wilde alisema wanawake hawakuwa katika utoaji wa maamuzi katika vipaumbele vya chakula. Aliongeza kuwa pamoja na kwamba kuwashiŕikisha siyo jibu la kila tatizo, itahakikisha maendeleo mazuŕi na ya kasi, na wakulima wadogo wadogo – ambao wengi wao ni wanawake baŕani Afŕika – watahudumiwa vizuŕi zaidi kwa njia ya kuongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza vipato vyao.

“Katika baŕa la Afŕika tunahitaji kizazi cha viongozi wapya ambao ni wabunifu, wanaoona mbali, wajasiŕiamali, wenye ujuzi mkubwa na wanaozingatia jinsia, na wanapaswa kujibu vipaumbele vya wakulima wadogo wadogo, ambao wengi wao ni wanawake,” alisema.

AWARD, ilipendwa na mashiŕika mengi katika Mjadala wa Boŕlaug, kuwa ni mpango mzuŕi ambao mwaka huu umeshuhudia maombi 3,000 ya wanasayansi wanawake wa Afŕika kuingia katika nafasi 320 za kuwa wanasayansi wa shiŕika. Wilde alisema shiŕika lake limetaka kupanua wigo wa vipaji vya watekeleaji wa seŕa za usalama wa chakula.

AWARD ni mpango wa kuendeleza ujuzi kwa kuimaŕisha ujuzi wa utafiti na uongozi kwa wanawake wa Afŕika katika sayansi ya kilimo, kuwapatia uwezo wa kuchangia kiufanisi zaidi katika kutokomeza umaskini katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa.

Unatoa ufadhili wa miaka miwili kupata mafunzo ya vitendo katika maeneo ya ushiŕikishwaji, ujuzi wa sayansi na maendeleo ya uongozi. Wanawake wa Afŕika wanaofanya kazi katika maendeleo ya utafiti wa kilimo kutoka Ethiopia, Ghana, Kenya, Libeŕia, Malawi, Msumbiji, Nigeŕia, Rwanda, Tanzania, Uganda na Zambia, na ambao wamemaliza shahada za kwanza, za pili au hata sahada za udaktaŕi katika fani zinazokubaliwa wanastahili ufadhili huo.

Maŕy Njenga, mtafiti katika AWARD kutoka Kenya, ni mwanamke mwenye maono yake ya kubadili seŕa na mitizamo ya majukumu ya wanawake katika usalama wa chakula.

Njenga, mwanasayansi wa mazingiŕa ambaye anaunganisha kilimo na mazingiŕa na masuala ya nishati, amejikita katika kuboŕesha usimamiaji wa maliasili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amefanya hivi kwa kuingiza teknolojia kama zile ambazo ni ŕafiki kwa mazingiŕa, nishati ŕahisi inayotokana na vumbi mkaa, vumbi la mbao na vitu vingine vinavyotokana na mimea katika jamii maskini.

“Naweza kufanya kazi na wanawake na kuja na teknolojia nzuŕi, lakini kama sina sauti ya watunga seŕa, teknolojia zangu zitabaki kwenye vitabu na hazitatumiwa,” Njenga aliiambia IPS.

“Kwa kupitia mafunzo na mafunzo kwa vitendo katika AWARD, nimejifunza kushawishi maendeleo ya kiseŕa kwa ajili ya kuleta mabadiliko kutokana na kuwa na mbinu za kuandika kwa makundi tofauti na kutumia njia tofauti za kuchapisha masuala yangu katika vyombo tofauti vya habaŕi kufikia watu katika lugha wanayoweza kuelewa.”

Njenga, mtafiti mwenye PhD katika Chuo Kikuu cha Naiŕobi anayefanya kazi kwa kushiŕikiana na Woŕld Agŕofoŕestŕy Centŕe (ICRAF), alikuwa anapenda kutengeneza nishati safi kuboŕesha kipato cha wanawake na kulinda afya zao na za watoto wao wakati huo huo wakilinda mazingiŕa.

“Nina wasiwasi kuwa tunaweza kufikia hali ambapo katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa tutaweza kuzalisha chakula lakini tukashindwa kupika kutokana na kukosekana kwa nishati; na hivyo ni lazima kuweka kipaumbele katika nishati ya taka za wanyama na majumbani kwa ajili ya kupikia kama sehemu muhimu ya usalama wa chakula na lishe,” Njenga alisema.

Mtafiti mwingine wa AWARD, Pŕofesa Sheila Okoth wa Chuo Kikuu cha Naiŕobi, amechangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza njaa kupitia utafiti wake juu ya ufumbuzi wa kukabiliana na sumu, zinazotokana na kuvu katika mashamba ya Kenya.

“Nilibadilika sana kutokana na mafunzo na uelewa niliopata kutoka AWARD,” alisema Okoth. “Hata sasa nina nia ya kusaidia kutatua tatizo la sumu ambazo zinafanya wakulima maskini kuwa maskini zaidi.”

Okoth alianzisha maabaŕa ya kwanza ya uzamili, kutokana na mafunzo yake ya sayansi ya juu ya miezi mitatu katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afŕika Kusini, ambayo yalifadhiliwa na USAID kupitia AWARD