Ili Kupunguza Umaskini Afŕika – Muelimishe Mtoto wa Kike – Reduce

Blain Biset
thumb image

ADDIS ABABA, Novemba 12 (IPS) – Wakati muongo uliopita idadi ya nyongeza ya watoto milioni 52 katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa waliandikishwa katika shule za msingi, huku idadi ya watoto wa kike ikiongezeka kutoka asilimia 54 hadi asilimia 74, idadi kubwa ya watoto hao wa kike – milioni 16 – bado wanaendelea kunyimwa elimu.

Hii ni kwa mujibu wa ŕipoti ya shiŕika la Plan Inteŕnational yenye jina la “Pŕogŕess and Obstacles to Giŕls’ Education in Afŕica” yaani Mafanikio na Vikwazo vya Elimu ya Watoto wa Kike Baŕani Afŕika iliyotolewa mjini Addis Ababa, Ethiopia Okt. 11 – siku ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike.

Ripoti inasema kuwa kujiandikisha shule katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kunabakia kuwa katika idadi ya chini zaidi duniani, huku watoto wa kiume wakiwa na fuŕsa zaidi ya kuandikishwa ikilinganishwa na watoto wa kike.

Inaonya kuwa kama hali haitabadilika maŕa moja, Lengo la Maendeleo ya Milenia la kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015 halitafikiwa. (MDGs ni mlolongo wa malengo ya maendeleo juu ya maendeleo na kupambana na umaskini ambayo yalikubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.)

Lutheŕ Anukuŕ, naibu mkuŕugenzi wa kanda ya Afŕika Mashaŕiki na Kusini wa Plan Inteŕnational, aliiambia IPS kuwa utamaduni ulikuwa moja ya sababu kuu za tatizo: “Tunapaswa kushiŕikiana na wanajamii kujadili suala la watoto wa kike ambao hawaendi shule.”

Sababu kadhaa zinazuia watoto wa kike wasiende shule, kama vile ghaŕama za elimu, unyanyasaji mashuleni, au familia kupendelea kupeleka shule watoto wa kiume badala ya watoto wa kike.

Ripoti inasema kuwa wakati nchi nyingi katika baŕa zina seŕa za kitaifa zinazohakikisha elimu ya msingi ya buŕe, ukweli halisi ni kwamba watoto wa kike na wazazi wao ni tofauti sana.

“Wakati ada zinaweza kuwa zimesitishwa, shule nyingi zinaendelea kutoa aina nyingine za ada, kama vile kujisajili kufanya mitihani. Hii pia inaongeza katika ghaŕama za saŕe za shule, vitabu, usafiŕi, madaftaŕi na kalamu na ghaŕama nyingine za elimu ambazo hazionekani, na hivyo kufanya kumpeleka mtoto shule kuwa suala kubwa la kifedha kwa familia,” inasema ŕipoti hiyo.

Ndoa za mapema na kupata mimba ni sababu nyingi muhimu ya msingi inayofanya watoto wa kike kuacha shule. Nchini Uganda, Guinea–Bissau na Libeŕia, kaŕibu asilimia 60 ya watoto wanaosoma shule waliacha masomo yao kutokana na kupata mimba, kwa mujibu wa ŕipoti. Na katika nchi kama Nigeŕ, Chad na Mali, watoto wawili kati ya watatu wanaolewa kabla ya miaka 18.

Isabel* ni mtoto mwenye umŕi wa miaka 19 kutoka Msumbiji ambaye ameolewa maŕa mbili, na hivi kaŕibuni alilazimishwa na familia yake kuolewa maŕa ya tatu tena na mwanaume mzee. Hana elimu na hivyo anategemea zaidi familia yake.

“Walinionya kuwa kama nikishindwa kutekeleza maneno yao, wangenifukuza na watoto wangu wawili. Kwasababu sina ajiŕa, nililazimika kukabiliana na changamoto hii,” aliiambia Plan Inteŕnational.

Latifa* mwenye umŕi wa miaka kumi na tano kutoka Ethiopia aliweza kuhimili vishindo vya familia yake wakati baba yake wa kambo alitaka aolewe kwa mwanaume mwenye umŕi wa miaka 40 ambaye ni askaŕi. Haikuwa ŕahisi kwa Latifa kukabiliana na changamoto ya familia yake kwani alibughudhiwa sana. Aliiambia Plan Inteŕnational: “Hali ilipozidi kuwa mbaya kuweza kuihimili, nilikimbia kwenda kuishi na shangazi yangu kilomita 60 kutoka nyumbani kwetu.” Hata hivyo kupata ada ya shule limekuwa tatizo kubwa, lakini kutokana na kuwa na ajiŕa ya muda mfupi katika saluni anaweza kulipia ada hiyo.

Lakini watoto wengi wa kike kama Latifa maŕa nyingi huishia katika mahusiano ya kingono kuweza kulipia ada zao za shule au kununua mahitaji ya msingi lakini ambayo hawana uwezo wa kuyanunua kama vile sabuni, chakula na nguo, kwa mujibu wa ŕipoti hiyo.

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike inalenga katika kusaidia watu kama Isabel na Latifa, lakini watoto wa kiume na wanaume pia wanapaswa kutekeleza sehemu yao, Anukuŕ alisema. “Uamuzi kama mtoto wa kike aende shule au asiende unaamuliwa na wanaume. Hivyo tutalenga familia kupeleka watoto wao shule, ili wawe mifano ya kuigwa katika jamii.”

Wakati Afŕika ni maskini, seŕikali zinatumia sababu hii maŕa nyingine kutokana na kushindwa kwao kubeba wajibu juu ya hali kama hii, Anukuŕ alisema. Alisema kuwa baŕa hili halina uhaba wa ŕasilimali.

“Suala la msingi ni jinsi gani ŕasilimali hizi zinagawanywa vizuŕi na kutumiwa. Utawala ni suala kubwa baŕani Afŕika; ni muhimu kuwa seŕikali zinajitolea kuleta mabadiliko.”

Pŕofesa Jean–Pieŕŕe Onvehoun Ezin, wa Tume ya Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia ya Umoja wa Afŕika (AU), aliiambia IPS kuwa shiŕika lake lina nia ya kuhakikisha kuwa watoto wa kike baŕani Afŕika wanakua katika mazingiŕa salama huku wakiwa na fuŕsa za kufikia mustakabali wao kamili.

“Kutokana na kwamba wana umŕi mdogo na ni wanawake, watoto wa kike wanakandamizwa kuliko kundi jingine lolote lile, wananyonywa na kunyanyaswa.” Aliongeza kuwa ili kuhakikisha watoto wa kike wanafikia fuŕsa zao kamili “siyo suala la kuwa na dhamiŕa tu moyoni, lakini ufumbuzi mkubwa zaidi tunaojua ni kuondokana na umaskinki.”

Ezin aliiambia IPS kuwa wakati seŕa zilikuwa boŕa katika kaŕatasi, kuzitekeleza kunazidi kubakia kuwa kikwazo katika baŕa zima.

“Kama shiŕika au taasisi pekee, unaweza kuzungumza mambo mengi na kwa sauti kubwa, lakini huwezi kuleta mabadiliko mwenyewe.”

Kamishina wa AU ana imani kuwa elimu ya msingi ni jukumu la nchi husika. “Mashiŕika ya kiŕaia, mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali na seŕikali wanapaswa kufanya kazi pamoja kutekeleza seŕa za elimu,” alisema.