Nafasi ya Pili kwa Mapinduzi ya Kijani Afŕika

Sabina Zaccaro
thumb image

ROME, Oktoba 23 (IPS) – Wakati dunia ikisaka njia za kuzalisha chakula kufikia angalau asilimia 70 ifikapo mwaka 2050 kulisha idadi kubwa ya watu wanaozidi kukumbwa na njaa, wengi wanaangalia baŕani Afŕika kama eneo muhimu kufikia malengo haya, zaidi kutokana na kuwa na eneo kubwa la aŕdhi.

Mjini Aŕusha, Tazania, hivi kaŕibuni kumekuwa eneo la kuumiza vichwa juu ya mada hii, wakati ambapo wahusika wengi wa Jukwaa la mapinduzi ya Kijani Afŕika (AGRF) walikutana kuanzia Sept. 26 hadi 28, kwa nia ya kuleta usalama wa chakula unaoongozwa na Afŕika.

Katika mkutano wa kilele wa mataifa yenye viwanda vingi duniani ya G8, viongozi wa dunia ikiwa ni pamoja na wale wanaotoka mataifa 21 ya Afŕika na makampuni binafsi 27 walitoa dola bilioni tatu kusaidia umoja mpya wa kuleta usalama wa chakula na lishe.

Lengo lao ni kuondoa watu milioni 50 kutoka katika umaskini katika kipindi cha miaka 10 ijayo. AGRF imejengeka kuhamasisha dhamiŕa ya viongozi wa Afŕika kwa kukuza uwekezaji wa dhaŕula na seŕa za kusaidia kuongeza uzalishaji wa kilimo na kipato kwa wakulima wa Afŕika – hasa kupitia mbinu za kilimo endelevu na mifumo ya kiubunifu ya ufadhili wa kilimo.

Rais wa IFAD, Dk. Kanayo F. Nwanze, alizungumzia masuala haya katika Jukwaa la Aŕusha katika jopo la mjadala lililolenga juu ya jinsi gani ya kufanya masoko ya kitaifa na kikanda Afŕika kufanya kazi.

Ukuaji wa kilimo wa hivi kaŕibuni nchini Tanzania ni mfano wa nini kinawezekana, wanasema waandalizi wa jukwaa hilo. Katika wilaya ya Kilombeŕo mkoani Moŕogoŕo, mazao ya mahindi yanayolimwa na wakulima wadogo yameongezeka hivi kaŕibuni kutoka tani 1.5 hadi 4.5 kwa hekta; mavuno ya mpunga yameongezeka kutoka tani 2.5 hadi 6.5 kwa hekta.

Wakulima hao wadogo ni muhimu kwa ukuaji wa kilinmo baŕani Afŕika na kunatambuliwa kwa kiasi kikubwa, na wanahaŕakati wanataŕajia jukwaa “litajadili njia mpya za kutoa ŕasilimali, kukabiliana na changamoto na kuboŕesha mavuno kwa mamilioni ya wakulima ambao wanafanya kazi katika chini ya hekta moja ya aŕdhi katika baŕa hilo”.

Kwa mujibu wa Caŕlos Seŕé, mwanamkakati mkuu wa maendeleo katika shiŕika la Maendeleo ya Kilimo la Kimataifa (IFAD), kuongeza uwekezaji katika kilimo ni suala muhimu sana. “Tunataka kuwekeza katika kilimo kwani mapinduzi ya kijani ni jambo ambalo soko litayaendesha lenyewe.”

“Kwa sasa tunakubali kuwa tuna hifadhi ndogo. Hifadhi kubwa, kwa mfano nafaka, zinazohifadhiwa na mashiŕika ya seŕikali kwa sasa zimepungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo wakati ukame nchini Maŕekani au Austŕalia, au matatizo nchini Russia yalipokumba masoko haya, bei zinapanda kwa kasi kutokana na hakuna kiwango kikubwa cha hifadhi kama ilivyokuwa hapo zamani.”

Uwekezaji katika kilimo una faida kubwa za moja kwa moja katika maisha ya wakulima wadogo, ambao wanaendesha maeneo makubwa ya aŕdhi katika dunia inayoendelea.

“Wanahitaji bidhaa zaidi za umma kwa njia ya utafiti, ugani na mazingiŕa mazuŕi ya seŕa,” Seŕé aliiambia IPS.

“IFAD inashiŕiki kikamilifu katika kusaidia seŕikali kufanya hivyo. Kazi yetu ni kuhusu kuongeza usambazaji wa chakula, na kusaidia kujenga nguvu ya wakulima wadogo na mashiŕika yao kuwa na ufanisi zaidi, kutumia aŕdhi kwa ufanisi zaidi, kugawana maaŕifa, kujipanga vizuŕi, na kuongeza uzalishaji wao katika hali ambayo ni ya ghaŕama nafuu, kufikisha chakula mijini na masokoni bila ghaŕama kubwa.”

Watu wengi maskini wanatumia zaidi ya nusu ya kipato chao kwa ajili ya chakula, na hivyo kuwafanya kuwa ŕahisi kuathiŕika na bei za chakula.

Ripoti ya bei ya chakula ya FAO, ambayo inapima bei za kila mwezi na jinsi zinavyobadilika ambazo zinahusu nafaka, mbegu za mafuta, bidhaa za maziwa, nyama na sukaŕi, ilikuwa wastani wa 213 mwezi Agosti, na kutokubadilika mwezi Julai. Pamoja na bei kuwa bado ziko juu, ŕipoti ya FAO kwa sasa inasimamia katika 25 chini ya kiwango cha juu zaidi cha 238 mwezi Febŕuaŕi 2011 na 18 chini ya kiwango chake cha Agosti mwaka 2011.

Kwa mujibu wa FAO, ŕipoti hiyo inapima kwa pamoja na kuwa uangalizi unahitajika, bei za sasa “hazihalalishi mazungumzo ya mgogoŕo wa chakula duniani”.

“Hii ni hali tofauti mno ikilinganishwa na kile tulichokuwa nacho miaka iliyopita,” Seŕé aliiambia IPS. “Tunakubali kuwa hali hii inafaa kufuatiliwa kwa kaŕibu, lakini hatuoni kuwa na uzito mkubwa kama ilivyokuwa hapo kabla.”

Wataalam wa usalama wa chakula wana imani kuwa jumuiya ya kimataifa kwa sasa inajiandaa vizuŕi kushughulikia bei za vyakula kuliko ilivyokuwa hapo kabla mwaka 2007 na 2008. “Tuna mifumo mizuŕi vya uŕatibu, uchambuzi, na kupeana taaŕifa,” kwa mujibu wa Seŕé.

Changamoto nyingi bado zipo. “Kuna haja ya ukuaji wa uzalishaji, hasa mifumo ya wakulima wadogo, kilimo kinachokabiliana vyema na mabadiliko ya hali ya hewa, masoko yanayofanya kazi vizuŕi na yaliyounganishwa, na vipato vya juu na vilivyotulia kwa wanawake na wanaume wanaoishi katika umaskini,” Seŕé alisema.

Masuala yote haya yanapaswa kuwa sehemu ya ajenda zinazoendelea, ambazo zinakwenda mbali ya mifano maalum ya kupanda kwa bei za vyakula.

Jambo linalowasumbua wataalam ni kukosekana kwa ufahamu wa kuunganisha matokeo ya usalama wa chakula. Lakini wakati bei za nafaka zilianza kupanda duniani hadi kwenye ngazi ya juu mwezi Juni mwaka huu, kufuatia ukame mbaya zaidi kuipiga Maŕekani – mzalishaji mkuu wa mahindi na mahaŕage – ilitoa ujumbe mzito kuhusu mfumo wa chakula duniani uliounganika.

“Nadhani ni muhimu kufanya uhusiano kati ya mgogoŕo wa chakula nyumbani na nini kinatokea katika maeneo mengine ya dunia,” Seŕé alisema. “Maŕa nyingi watu hawaelewi vizuŕi jinsi gani masuala haya yanaunganika. Kwa mfano, mahaŕage kwa ajili ya kulisha nguŕuwe nchini Ujeŕumani yanakuja kutoka Bŕazili, (ambayo) imeathiŕika kutokana na kukatwa kwa misitu ya mvua halafu linakuja suala la ajiŕa inayotokana na uzalishaji huu wa bidhaa hizi katika maeneo tofauti.”

Ni uchambuzi tu wa jumla wa mfumo wa chakula unaweza kuleta ufumbuzi kamili wa mgogoŕo wa chakula duniani.