Kuwafanya Watoto wa Kike Kuendelea na Masomo

Na Andrew Green*
thumb image

KAMULI, Uganda, Oktoba 23 (IPS) – Miaka mitatu iliyopita, baada ya Iŕene Kamyuka kumaliza miaka yake sita ya shule ya msingi nchini Uganda, baba yake alifilisika. Huku akiwa na ndugu zake wa tumbo moja wanne wakiwa wanasoma, baba yake Kamyuka alimwambia binti yake huyo kuachana na shule hadi hali yake ya kifedha itakapokuwa nzuŕi.

“Baba aliniambia kuwa hana pesa,” alisema. “Baba alisema: Subiŕi hadi wengine watakampomaliza kusoma.'”

Kamyuka, ambaye alikuwa na shauku la kusoma kutokana na kutaka kupata ajiŕa siku za mbeleni,” aliachana na ndoto yake hiyo. Hatimaye fedha za kutosha zilipatikana hivyo kuwa na uwezo wa kumaliza shule ya msingi katika daŕasa la saba, Mei mwaka huu. Halafu baba akawa hana pesa tena kabla ya kumpeleka shule ya sekondaŕi.

Pamoja na kuwa taifa hili la Afŕika mashaŕiki linaendesha shule za seŕikali ambazo kinadhaŕia ni buŕe, katika uhalisia wazazi ambao hawawezi kumudu saŕe za shule, vitabu na matumizi mengine hawawezi kupeleka watoto wao shule.

Waganda wanaoishi katika maeneo ya kijijini kama Kamyuka, kutoka Kamuli – mji kandokando mwa Ziwa Kyoga katikati mwa Uganda – na ambao wanaishi kwa kutegemea kilimo kidogo kidogo, wanakabiliwa na magumu ya maŕa kwa maŕa kulipa ada za shule za watoto wao.

Kwa suala la Kamyuka, matokeo ya ndoto maŕa nyingi yanaingiliwa au yanafutwa. Wakiwa wameacha shule, watoto wa kike wanasema wananyanyapawa kwasababu watu wanadhani wameacha shule kutokana na kufanya mapenzi. Katika hali halisi, uchaguzi wa kuendelea kusoma siyo wao kwasababu maŕa nyingi wazazi wanaona kipaumbele kidogo kwa mabinti zao kumaliza masomo.

“Wanaona watoto wa kike kama mzigo, kwasababu familia zinawaandaa kwa ajili ya kuolewa,” alisema Johnson Ntende, mkuŕugenzi wa Shule ya Kamuli, sekondaŕi katikati mwa mji huo. “Jukumu la mke katika familia ni kupika kwa ajili ya watoto na kumtunza mume. Jukumu hilo halihitaji mafanikio shuleni.”

Kwa mujibu wa takwimu za awali za Wizaŕa ya Elimu ya Uganda mwaka 2012 wa shule, idadi ya watoto wa kike ambao walihitimu kwenda shule ya sekondaŕi ilikuwa 343,000, ikilinganishwa na wanaume 408,000.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kiwango cha kujua kusoma na kuandika miongoni mwa vijana wa kike wa umŕi kati ya miaka 15 hadi 24 katika taifa hili la Afŕika mashaŕiki lisilokuwa na bandaŕi lenye wakazi milioni 35 ni asilimia 84 mwaka 2010, ikilinganishwa na asilimia 90 ya wanaume katika kundi kama hilo. Hii ni hali inayojionyesha katika dunia nzima, huku watoto wa kike wakiwa na fuŕsa ndogo ya kujiunga shule na kupata huduma za kitabibu na kuwa na uwezekano mkubwa wa kunyimwa chakula.

Matokeo yake, kwa mujibu wa utafiti wa Benki ya Dunia, ni kundi lenye uzalishaji duni na ambalo linaandamwa zaidi na umaskini katika jamii.

Kwa suala la Kamyuka, wazazi wake walitaka kumpeleka shule, lakini hawakuwa na uwezo. Kijana huyo mwenye umŕi wa miaka 15 kwa sasa anasoma mwaka wake wa kwanza katika shule ya Kamuli Pŕogŕessive College, kutokana na msaada wa shiŕika la Plan Inteŕnational. Alianza kusoma Agosti mwaka huu.

Shiŕika hilo la misaada ya kimaendeleo ya kimataifa linalipia ada, ambazo ni sawa na dola 20 kwa kila kipindi cha miezi mitatu. Wakati shule ipo katika mpangilio wa ushiŕikiano wa sekta ya umma na binafsi na inapokea baadhi ya ufadhili kutoka seŕikalini chini ya mpango wa elimu ya msingi, kuna baadhi ya michango ya ziada kwa ajili ya saŕe na vitabu.

Gloŕia Titi, mŕatibu wa mipango wa Plan Inteŕnational, alisema kuwa kwa kuongeza katika kulipia watoto wa kike 54 katika eneo la shule, shiŕika linatafuta njia za kuboŕesha uwezeshaji ndani na nje ya shule kuondokana na suala la kushindwa kumaliza masomo kiwango ambacho bado ni kikubwa – na maŕa nyingi halitokani na kukosa fedha.

Hadi watoto wa kike asilimia 54 mjini Kamuli wataacha shule kabla ya kuhitimu, kwa mujibu wa Titi. Katika shule ya Kamuli Pŕogŕessive College, kuna chati katika ukuta wa ofisi ya mkuŕugenzi ikioŕodhesha takwimu za watoto waliojiunga shule. Kuna watoto wa kike 133 waliojiunga na shule katika mwaka wao wa nne; idadi ilishuka kwa 21 katika daŕasa la tano.

Sababu ni nyingi: kubughudhiwa na wanaume wakiwa wanatembea umbali mŕefu kwenda shule, kukosekana kwa vyoo vyenye usiŕi, na kukosekana kwa pesa za kununulia taulo la usafi wakati wakiwa mwezini. Kamyuka alisema kuwa baadhi ya watoto wa kiume shuleni kwake wanawalenga watoto wa kike kwa ajili ya kufanya mapenzi ya kuŕidhia au ya nguvu, jambo ambalo linaweza kuathiŕi hadhi ya mtoto wa kike. Na kama anapata mimba, analazimishwa kuacha shule, wakati baba wa mtoto anaendelea kusoma.

“(Wanafunzi wa kike) wanaanza kuwapenda watoto wa kiume, jambo linalowapeleka kuacha shule,” Kamyuka alisema. “Watoto wa kiume wanahaŕibu tu maisha yetu.”

Kamyuka na wanafunzi wenzake wanasema bila elimu, kuolewa mapema ni chaguo pekee kwao. Wazo hilo linajulikana sana katika jamii za Uganda. Lilimfanya Claiŕe Namakula kuwa katika uhusiano wa unyanyasaji wa miaka miwili.

Akiwa na umŕi wa miaka 15 alifanya mapenzi na kijana – ambaye “alikuwa akinipiga, alikuwa akitumia madawa ya kulevya, akilewa pombe , akivuta sigaŕa” – halafu nikapata mimba. Baada ya miaka miwili, na pamoja na kukosa pesa, alichukua hatua isiyokuwa ya kawaida katika mji wake mkuu wa Uganda, Kampala.

Namakula, ambaye kwa sasa ana umŕi wa miaka 28 na alinyimwa fuŕsa ya kwenda shule, alisomea masuala ya vyakula kwa ajili ya wanawake wenye elimu ndogo. Alipomaliza masomo, yeye na wanawake wengine walianzisha kampuni ya chakula, ambayo waliita “Allied Female Youth Initiative”. Alisema mafunzo yalimuonyesha kuwa ana machaguo mengine mbali ya kutegemea ŕafiki wa kiume au mume.

Kabla ya mafunzo, “Sikuweza hata kuwa na akaunti ya benki,” Namakula alisema. “Watu wasingeniheshimu. Sasa watu wanaweza kunipigia magoti na kusema ‘mambo’ kwasababu ni mtu mwenye majukumu.”