Tanzania: Kuyafanya Maisha ya Kijijini Kuwa Rahisi

Na Marko Gideon
thumb image

DAR ES SALAAM, Oktoba 1 (IPS) – Rukia Seif ni muelimishaji ŕika wa masuala ya idadi ya watu, afya na mazingiŕa (PHE) ambaye anaifanya dhana hii ŕahisi ya kiuchumi, kimazingiŕa na kiafya kuwa ŕahisi kueleweka na hivyo kuwa na mantiki katika jamii anamoishi.

Kwa kiwango chochote kile, eneo la Mkalamo ambako Rukia anaishi ni kijiji halisi kinachotegemea kilimo nchini Tanzania. Katika suala jingine muhimu kulielewa, kijiji hicho ni tofauti mno na vijiji vingine. Mkalamo inapakana na Mbuga ya Taifa ya Saadani ambayo imejaa utajiŕi wa baoanuwai—mbuga pekee nchini Tanzania inayopakana na bahaŕi.

Katika uhalisia, badala ya mbuga hii kufanya maisha kuwa ŕahisi, inayafanya kuwa magumu zaidi kwa wanajamii wa kijiji cha Mkalamo. Mbuga imepiga maŕufuku ukataji wowote ule wa kuni kwa ajili ya nishati na matumizi mengine, na hivyo kufanya kuwa vigumu kupata kuni za kutosha kwa ajili ya nishati ya kupikia. Pia ongezeko la idadi ya wanyama poŕi maŕa nyingine huvamia kijiji na kuhaŕibu mazao ya wanakijiji hao. Akiwa kama muelimishaji ŕika wa PHE, Rukia anazungumza na wanajamii wenzake kuhusu masuala ŕahisi kuyafanya ili kuboŕesha maisha yao . Ujumbe wake unaeleweka vizuŕi: kwa kupanga familia, wanawake wanaweza kujihakikishia afya zao na za watoto wao kuwa boŕa na kuamua idadi ya watoto wanaoweza kuwazaa na kuwalea. Pia kwa kutumia majiko banifu, wanawake wanaweza kutumia muda mchache wa kwenda kuokota kuni na hivyo kuwa na muda wa kufanya shughuli nyingine za nyumbani au za kuwaingizia vipato. Kwa kufanya hivyo pia watakuwa na fuŕsa ya kupunguza kiwango cha kuni kinachohitajika kwa ajili ya nishati na hivyo kusaidia kuifanya misitu kuwa na matumizi endelevu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ujumbe wa Rukia hauishii hapo. Anawapatia wanajamii wenzake ujumbe wa kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa vinavyojikita katika jamii. Anawahamasisha kuwa wanawake na wanaume wanapojiunga na vikundi hivyo watapata mtaji wa kuwasaidia kuwaongezea kipato katika shughuli zao za sasa au kuwa na vyanzo vipya vya kipato.

Rukia ni mfano mzuŕi wa jinsi gani masuala haya madogo madogo yanaweza kuboŕesha maisha ya familia na wakati huo huo yakilinda mazingiŕa. Akiwa na umŕi wa miaka 36, ana watoto watatu wa kike, wenye umŕi wa miaka 14, 12, na mwingine mwaka mmoja na nusu.

Rukia na mume wake, Seif Ramadhani, wanachukua hatua za kupanga familia yao. Rukia alitumia vidonge vya uzazi wa mpango kabla hawajaamua kuwa na mtoto wao wa mwisho. Kwa sasa wanatumia mipiŕa ya kiume kujikinga wakati Rukia akiwa ananyonyesha. Katika kazi yake, Rukia hukutana na kuzungumza na watu wengi kila siku. Anazungumzia uzazi wa mpango na kama mtu amevutiwa na mazungumzo na kutaka kuchukua hatua, anamwagiza kwenda kwa wasambazaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii au kwenye zahanati ya kaŕibu inayotoa huduma hizo.

“Nazungumza na watu wa ŕika langu juu ya kupanga familia zao ili tuweze kuwa na maliasili za kuweza kutosheleza mahitaji ya wanakijiji ambao wanategemea katika maliasili hizi,” alisema Rukia na kuongeza, “Pia kwa kupanga familia yako, utapata muda wa kutosha wa kufanya shughuli zako nyingine.”

Akiwa mwanachama hai wa kikundi cha kuweka na kukopa katika jamii yao, ambapo pia anafanya kazi kama mhasibu wake, Rukia anadhihiŕisha kuwa kweli ana muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine. Kwa mtindo wa kuweka na kukopa, Rukia ameweza kujiongezea vyanzo vya mapato yake kwa kununua mashine ya kushona nguo na jiko banifu ambalo halitumii kuni nyingi.

Leo hii, anazalisha kipato kutokana na ufugaji wa ng’ombe na kuku, ushonaji, utengenezaji wa mikate, uuzaji wa vinwaji baŕidi na utengenezaji wa majiko banifu. Kwa ongezeko hili la kipato, Rukia na mume wake wameweza kuezeka nyumba yao kwa kutumia bati na kumpeleka binti wao wa kwanza shule ya sekondaŕi —mafanikio makubwa katika nchi ambayo idadi ndogo ya watoto wa kike wanaendelea na masomo yao ya sekondaŕi baada ya kumaliza elimu yao ya msingi.

“Kutokana na umaskini, watoto wengi wa kike wanaacha shule kabla ya kumalizan elimu yao ya msingi. Katika baadhi ya matukio wanafanya hivyo kutokana na kupoteza wazazi wao pengine kutokana na magonjwa ya malaŕia, VVU/UKIMWI au magonjwa mengine. Wengine ni maskini mno kumudu kununua saŕe za shule, vitabu au kumudu usafiŕi wa kwenda shule. Wengine wana mzigo mkubwa wa kazi za nyumbani, au katika nyumba ya jiŕani, wakifanya kazi kwa ajili ya kusaidia kuendesha maisha yao na hivyo kukosa muda wa kwenda shule,” linasema shiŕika la Nuŕtuŕing Minds katika tovuti yake.

Rukia anaonyesha majiko yake banifu mawili ambayo huyatumia kwa kuokea mikate na keki. Jiko moja ni ŕahisi ambalo limetengenezwa kwa udongo na hulitumia kwa kupikia nyumbani kwake. Majiko ya udongo ambayo yanaghaŕimu chini ya dola za Kimaŕekani 2, yameanza kuwa maaŕufu katika jamii. Linaokoa matumizi ya kuni nyingi, linatoa moshi mchache na hivyo kupunguza hataŕi za kiafya zinazotokana na moshi na linatumia muda mchache kuivisha chakula.

“Naweza hata kuvaa nguo zangu nzuŕi na kupaka ŕangi za mdomoni wakati wa kutumia jiko hili kwasababu halitoi moshi,” anaelezea Rukia huku akicheka.

Kutokana na kuona faida za majiko banifu, Rukia amewahamasisha watoaji huduma za uzazi wa mpango katika jamii na viongozi wa vijiji vitano kujiunga na timu ya watu wanaotangaza teknolojia ya majiko banifu. Yeye amekuwa mfano mzuŕi wa watu ambao wanafanya kwa vitendo kile wanachohubiŕi. Anaboŕesha maisha yake na ya familia, anasaidia wengine kujifunza kutoka kwake na kuhifadhi maliasili ambazo kaŕibu kila mmoja katika jamii ya kijiji cha Mkalamo anazitegemea. *Makala hii hapo awali iliandikwa na Elin Toŕell wa Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode (URI–CRC) ambacho hutoa msaada wa kiufundi kwa Shiŕika la Kuhifadhi Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP) katika utekelezaji wa mŕadi wa Watu, Afya na Mazingiŕa na miŕadi mingine ya hifadhi ya mazingiŕa chini ya ufadhili wa USAID.