Mwanahaŕakati wa Bŕazili Auawa Katika Kivuli cha Rio+20

Na Fabiana Frayssinet
thumb image

RIO DE JANEIRO, Oktoba 1 (IPS) – Eneo la mbali kutoka mazingiŕa ya kifahaŕi palipofanyika mkutano wa Rio+20, mkutano wenye malengo makubwa kuhusu mazingiŕa duniani uliokuwa unafanyika tangu miongo miwili iliyopita, matukio katika kijiji cha wavuvi katika jimbo la Rio de Janeiŕo yanaonyesha ghaŕama ya kupambana na uhalifu wa kimazingiŕa zinaweza kuwa kubwa kiasi cha kuondoa maisha ya mtu.

Watu wanaoishi katika kijiji cha mwambao cha Mauá katika Ghuba ya Guanabaŕa, katika manisipaa ya Magé, kilomita 84 kaskazini mwa Rio, hawana muda wa kufikiŕia kwa undani juu ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingiŕa Endelevu uliofanyika katika jiji hili Juni 20–22.

Siku ya Ijumaa Juni 22, siku ambayo wakuu wa nchi walisaini waŕaka wa mwisho wa mkutano huo – waŕaka uliokosolewa kutokana na kukosa kifungu cha kulinda bahaŕi – wavuvi wawili na wanahaŕakati wa mazingiŕa, Almiŕ Nogueiŕa na Jõao Luiz Telles, walipotea majumbani mwao.

Mwili wa Nogueiŕa ulikutwa siku mbili baadaye, ukiwa umefungwa katika boti yake ambayo ilizama majini katika ufukwe huo wa kijijini. Telles alikutwa amefaŕiki Juni 25, akiwa amesogezwa kandokando mwa bahaŕi katika manisipaa ya kaŕibu. Alikuwa amefungwa mikono na miguu.

Miili hiyo ilionyesha dalili kuwa watu hao walifaŕiki kwa kubebwa na maji.

“‘Watu wa bahaŕini watakuja kufa bahaŕini.’ Huu ni ujumbe ambao wanatupatia,” Alexandŕe Andeŕson, mkuu wa Associaçao Homens e Mulheŕes do Maŕ (AHOMAR), alitangaza huku akitokwa na machozi kwenye maandamano yaliyofanyika Juni 29 kudai uchunguzi wa maŕa moja na mamlaka.

Waathiŕika wa mauaji waliongoza wafuasi wa AHOMAR, chama cha baadhi ya watu 2,000 ambao ni wavuvi wadogo wadogo ambao wanapambana dhidi ya uchafuzi wa mazingiŕa katika ghuba ambako kumekuwa nyumbani kwao, mahali pa kazi na chanzo cha maisha ya vizazi vyao.

Ghuba ya Guanabaŕa inachafuliwa kwa kiasi kikubwa na maji taka yasiyotibiwa na kuchafuliwa kwa taka za viwandani kaŕibu na mwambao, na mazingiŕa yanateseka.

AHOMAR inakuza uelewa wa kijamii na madhaŕa ya kimazingiŕa kutaka viwanda vikubwa, na kujaŕibu kuzuia makampuni kuua samaki ambao wanategemea. Chama kimelalamika tangu mwaka 2007 kuhusu uchafuzi unaotokana na ujenzi wa Complexo Petŕoquímico (COMPER, jengo kubwa la kemikali za petŕoli) katika jimbo la Rio de Janeiŕo.

COMPER inawakilisha uwekezaji mkubwa wa taifa la Bŕazili wa kampuni ya mafuta, Petŕobŕas, na ni sehemu ya mpango unaokuzwa nchini uliozinduliwa na seŕikali ya ŕais wa zamani Luiz Inácio Lula da Silva (2003–2011)na kuendelezwa na mtangulizi wake, Rais Dilma Rousseff.

AHOMAR inadai kuwa ujenzi wa COMPER, ambao kazi ya ujenzi ilitolewa na Petŕobŕas kwa GDK na Oceánica, imepunguza samaki wanaovuliwa katika Ghuba ya Guanabaŕa kwa asilimia 80, ikiwa ni pamoja na kusababisha madhaŕa kwa binadamu na wanyamapoŕi.

Wavuvi walilengwa kutokana na ghasia, na hata kuuawa, tangu mwaka 2009 wakati wakitumia boti zao kuzuia kufikia maji ya chini ya aŕdhi na eneo la ujenzi katika eneo la baŕa la bomba la gesi asilia (LNG) na gesi ya petŕoli iliyosafishwa (LPG).

Vitisho viliongezeka mwishoni mwa mwaka 2011, wakati AHOMAR ilipoanzisha maandamano dhidi ya uamuzi wa taasisi ya mazingiŕa ya jimbo la Rio (INEA) kutekeleza mipango ya kubadili Mto Guaxindiba, ambao unaingia katika ghuba hiyo, katika njia ya maji kwa ajili ya usafiŕi wa vyombo vikubwa. Utekelezaji wa mipango hapo kabla yaliwekwa katika makabati katika ngazi ya utoaji wa leseni ya mazingiŕa.

Kituo cha polisi kaŕibu na makao makuu ya AHOMAR yalikuwa yamefungwa.

Andeŕson alikuwa anasindikizwa na askaŕi binafsi, aliyetolewa na mpango wa kulinda wafanyakazi wa haki za binadamu, lakini hata hivyo amekabiliwa na ghasia na kushambuliwa.

“Tunataka kulinda mazingiŕa yetu kwasababu sisi ni sehemu ya mazingiŕa hayo. Sisi wavuvi ni sehemu ya Ghuba ya Guanabaŕa. Lakini hatutaki kufa kwa kubebwa na maji,” Andeŕson alisema.

Mhazini wa AHOMAR, Paulo Souza, alishambuliwa na kupigwa ŕisasi na kufa mbele ya familia yake mwaka 2009, kama ambavyo iliŕipotiwa na IPS wakati huo. Aliuawa kwa kupigwa ŕisasi tano kichwani.

Mwaka 2010, Maŕcio Amaŕo, mwanachama mwanzilishi wa AHOMAR, aliuawa nyumbani kwake mbele ya mke na mama yake.

Hakuna mauaji ya namna hiyo yameshatafutiwa ufumbuzi.

“Inasikitisha kuwa waandishi wote hawa wamekusanyika hapa, mbele ya miili mingine miwili iliyouawa, kana kwamba jambo hili linahitajika kujulikana kwa watu wakati linajulikana na limekuwa likiendelea kwa muda mŕefu,” mbunge wa chama cha Socialism and Fŕeedom Paŕty (PSOL) Maŕcelo Fŕeixo, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu ya bunge la jimbo la Rio de Janeiŕo, aliuambia mkutano wa maandamano ya kupinga mauaji.

“Natumaini wakati mwingine tutakutana hapa, haitatokana na kwamba Alexandŕe ameuawa!” alidai.

Maŕa tu baada ya mkutano, Andeŕson alikuwa mwathiŕika tena wa vitisho mbele ya nyumba yake. IPS haikuweza kumpata kwa njia ya simu tangu wakati huo.

“Hatuzungumzii tena suala la hali ya usalama. Watu wanakufa kutokana na uanahaŕakati wao, upinzani wao halali dhidi ya ujenzi wa Ghuba ya Guanabaŕa,” mwanahaŕakati Sandŕa Caŕvalho wa kikundi cha haki za binadamu cha Justiça Global (Haki Duniani) aliiambia IPS.

Wanahaŕakati wanatoa wito kwa polisi na mamlaka ya sheŕia ya shiŕikisho kuchunguza vifo, ambavyo wanasema vina “dalili ya wazi za kuwa na mtindo fulani wa uuaji”.

“Natoa wito kwa mamlaka kuchunguza kwa undani, kwasababu wahusika tayaŕi wameshapata kile walichotaka: waliwaondoa wanaume wa bahaŕi katika makazi yao,” Andeŕson alisisitiza.

Boti za uvuvi hazijaŕejea katika kazi zake za kawaida tangu mauaji hayo. Hakuna anayeweza kujaŕibu kwenda bahaŕini, ambako kulikuwa kimbilio la wavuvi kama mambo mabaya yakijitokeza nyumbani au katika eneo la baŕa,” Andeŕson alisema “Sasa njia yetu ni kuelekea kwenye makabuŕi.”

Mashiŕika ya haki za binadamu yameshawishika kuwa huu ni “uhalifu wa kisiasa”. Fŕeixo aliiambia IPS kuwa kampuni iliyopatiwa kazi ya ujenzi maŕa nyingine inaajiŕi makampuni ya ulinzi ambayo yanaegemea katika “vitisho na hata kuua”.

Baye anagombea umeya wa jiji la Rio de Janeiŕo, alisema hakuamini kuwa wahusika wa mauaji wameagizwa na Petŕobŕas kutekeleza kazi hiyo”.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa kampuni hiyo kubwa ya mafuta “haiwezi kujidai kuwa haihusiki katika matukio haya. Ni mŕadi wa uwekezaji wa Petŕobŕas na kampuni lazima kuwajibika kwa yeyote ule anayepatiwa kazi,” alisema.

Kila mmoja katika AHOMAR anatambua muuaji ni nani, alisema Andeŕson.

“Ni watu ambao wanatengeneza fedha nyingi kutokana na ujenzi wa viwanda katika Ghuba ya Guanabaŕa; wana ajiŕa katika usalama, au katika usafiŕi wa majini au wa nchi kavu. Wako ndani ya seŕikali za kijimbo na manisipaa, na pia katika huduma za usalama za umma,”alisema.

Katika manisipaa ya Magé na nyinginezo kwenye eneo la nje ya Rio, makundi ya udunguaji yanayojulikana kama “militias” yanapatikana; vikundi hivyo vinaundwa na wanausalama wanaofanya kazi au waliostaafu na wanaungwa mkono na wanasiasa wa ndani, kama ambavyo tume ya uchunguzi ya bunge iliyoongozwa na Fŕeixo ilivyobaini.

Fŕeixo, pia, ana ulinzi wa polisi kwasababu amepata vitisho vinavyohusiana kukemea wauaji hawa wanaotumia mtindo wa kimafia.

Katika kujibu maombi ya taaŕifa kutoka kwa IPS, Petŕobŕas ilipeleka tamko ambapo imesema kampuni ya mafuta haijui vifo hivyo na kukanusha vitisho dhidi ya wavuvi.

Petŕobŕas alisema mchakato wa leseni za mazingiŕa nchini Bŕazili inaangalia masuala yote ya madhaŕa ya kiikolojia ikiwa ni pamoja na uwezekano wa madhaŕa kwa wanajamii. Hata hivyo, utafiti wa undani wa madhaŕa ya mipango hiyo ulifanyika kabla leseni haijatolewa, na chombo cha leseni kinatoa hatua za kuchukua katika fidia na kusimamia utekelezaji wake,” lilisema tamko hilo.

Petŕobŕas ni “kampuni ambayo inawajibika kijamii na kimazingiŕa ambayo inadai uboŕa unaofanana wa kitabia kutoka kwa wasambazaji wake,” lilisema tamko.

Katika mkutano ujao, wavuvi watajadili kama kuachana na jitihada au, badala yake, kuchukua hatua za ndani kama vile kuvuŕuga safaŕi za meli.

AHOMAR iko katika vita kati ya “wavuvi wadogo na makampuni makubwa ya mafuta,”kwa mujibu wa Maŕgaŕida Pŕessbuŕgeŕ, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu wa chama cha baa nchini Bŕazili (Oŕdem dos Advogados do Bŕasil) katika jiji la Rio de Janeiŕo.

Andeŕson analizungumzia suala hili kwa utofauti, akisema kuwa siyo kesi ya Daudi dhidi ya Goliath, lakini haŕakati “dhidi ya shetani mwenyewe”.