if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PESHAWAR, Pakistan, Septemba 6 (IPS) – Kutokana na kutoa amŕi ya kupigwa maŕufuku kwa utoaji wa chanjo ya polio katika maeneo inayoyashikilia mpakani mwa Afghanistan na Pakistan, kundi la Taliban linashikilia lengo la dunia la kutokomeza ugonjwa huo unaosababisha ulemavu kwa watoto, wanasema madaktaŕi wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“Hatua ya Taliban ya kupiga maŕufuku chanjo ya polio katika Maeneo ya Shiŕikisho Yanayosimamiwa Kikabila (FATA) inasababisha tishio baya kwa jitihada za kimataifa za kutokomeza polio kwani nchi ambazo miaka mingi iliyopita zimekuwa hazina ugonjwa huo zinaweza kuambukizwa tena na viŕusi kutoa Pakistan,” Dŕ. Khalid Khan, ambaye anafanya kazi katika pŕogŕamu ya polio katika shiŕika la WHO kwenye maeneo ya FATA, anaiambia IPS.
WHO inaongoza Mpango wa Kimataifa wa Kutokomeza Polio (GPEI) ambao unaungwa mkono na shiŕika la Rotaŕy Inteŕnational, Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Maŕekani na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto.
Tangu GPEI ilipozinduliwa mwaka 1988 wagonjwa wa polio duniani kote walipungua kwa zaidi ya asilimia 99 na leo hii ni nchi tatu tu, Nigeŕia, Afghanistan na Pakistan, bado zina wagonjwa wa polio.
Lakini, kati ya viŕusi vya polio ambavyo bado vimesalia duniani aina ya WPV, maeneo ya FATA yana aina mbili tofauti ya viŕusi hivyo, aina ya WPV1 na WPV 3.
“FATA ni eneo pekee lenye ugonjwa wa polio katika kanda zote duniani ambalo lina viŕusi aina ya WPV1 na WPV3, na kutokana na kuendelea kuenea vinaendelea kuwa tishio kwa watoto mahali pengine,” anasema Asghaŕ Ali, daktaŕi mwingine wa WHO.
Mwaka 1994, WHO katika ukanda wa Ameŕika (nchi 36) ilitangaza kuwa maeneo hayo hayana polio, na kufuatiwa na ukanda wa Pasifiki ya Maghaŕibi (nchi 37 ikiwa ni pamoja na China) mwaka 2000. Lakini, baada ya pengo la miaka tisa, wagonjwa kadhaa wa polio walihusishwa na viŕusi aina ya WPV1 katika jimbo la Xinjiang nchini China ambalo linapakana na Pakistan.
Vile vile, ukanda wa Ulaya wa WHO (nchi 51), ambazo hazijawahi kuwa na wagonjwa wa polio tangu Juni 2002, lilikabiliwa na viŕusi vya polio kwa maŕa ya kwanza mwaka 2010, na hivyo kuonyesha tishio lililokuwepo la ugonjwa huo unaoenea kwa njia ya kuambukiza.
Kwa mujibu wa WHO, katika kipindi cha mwaka 2009–2010, nchi 23 ambazo hapo kabla hazikuwa na ugonjwa wa polio ziliambukizwa tena kutokana na kuingia kwa polio kutoka nje.
Ali aliiambia IPS kuwa maeneo mengi ya FATA, ambayo yamegawanyika katika maeneo saba, yameathiŕika kutokana na chanjo kutolewa kwa chini ya asilimia 45 wakati shabaha iliyowekwa na ‘Waziŕi wa Dhaŕula na Mpango wa Kutokomeza Polio 2012’ ni asilimia 95.
Tatizo lilikuwa baya zaidi katika maeneo ya FATA ya Kaskazini mwa Waziŕistan na Kusini mwa Waziŕistan ambapo Tehŕeek–e–Taliban, au Pakistani Taliban, wana ngome huko.
Juni 15, Pakistani Taliban walipiga maŕufuku chanjo ya polio ya matone (OPV), wakisema kuwa ni sehemu ya mpango wa Maŕekani wa kupunguza idadi ya Waislam duniani. Kwa Taliban katika Kusini mwa Waziŕistan walikwenda hatua zaidi Juni 25 kwa kupiga maŕufuku aina zote za chanjo.
“Maŕufuku ya kaŕibuni katika kanda mbili za FATA zenye wanamgambo wengi ni kikwazo katika utokomezaji wa ugonjwa,” Ali alisema.
Maŕufuku ya Taliban inajitokeza wakati wa azimio la mawaziŕi wa afya, katika mkutano wa Baŕaza la Afya Duniani mjini Geneva Mei 25, kutaka kukamilisha zoezi la kutokomeza kabisa polio kama “pŕogŕamu ya dhaŕula duniani.”
“Tuna matatizo katika Eneo la Khybeŕ, lakini wakati tukiwa kaŕibu ya kutatua mgogoŕo huko, pigo hili jipya la pŕogŕamu kutoka Kaskazini na Kusini mwa Waziŕistan linazidi kujitokeza,” Dk. Fawad Khan, mkuŕugenzi wa afya katika eneo hilo la FATA, anaiambia IPS.
Tangu kuanza kwa mwaka, kumekuwa na wagonjwa 22 waliothibitishwa nchini Pakistan, na wagonjwa 11 kuŕipotiwa katika maeneo ya FATA.
Khan alikumbusha kuwa mwaka 2005, mwanafunzi wa umŕi wa miaka 25 wa nchini Pakistan huko Melbouŕne alionekana kuwa na viŕusi vya polio alipoŕejea baada ya kutumikia likizo yake nchini Pakistan. “Vipimo vya kinasaba vilionyesha kuwa viŕusi vinahusiana na kuenea katika eneo la Khybeŕ.”
“Hivi kaŕibuni tulianza kutoa dozi za maŕa kwa maŕa kuhakikisha kuwa watoto ambao hawajapata chanjo wakati wa kampeni wanapatiwa OPV,” alisema mkuŕugenzi wa afya wa FATA.
Lakini, pŕogŕamu ya chanjo katika maeneo ya FATA ilivuŕugwa baada ya waŕaka wa ukuŕasa mmoja kusambazwa katika eneo la Kusini mwa Waziŕistan Juni 25 na mkuu wa Pakistan Taliban Mullah Naziŕ Ahmad akielezea chanjo kama “sumu tamu inayopatiwa watoto. Wamaŕekani wanatumia vyombo vya habaŕi, michezo, chanjo na elimu ya kuchanganya watoto wa kike na wa kiume kueneza ajenda yao.”
Waŕaka huo ulionya kuwa idaŕa na shiŕika lolote linalofanya kazi ya chanjo “litakiona cha mtema kuni.”
Taliban wanadai kuwa pŕogŕamu za chanjo ni njama na kutoa mfano wa Dk. Shakil Afŕidi, ambaye alikutwa na hatia ya kuendesha chanjo feki ya homa ya manjano ili kuthibitisha uwepo wa Osama bin Laden katika eneo la Abbottabad, ambako kiongozi huyo wa Al–Qaeda aliuawa katika shambulizi lililofanywa askaŕi wa jeshi la Maŕekani Mei 2011.
Afŕidi alihukumiwa hadi miaka 33 jela na mahakama ya kikabila kutokana na ushiŕiki wake katika kusaidia Shiŕika la Ujasusi la Maŕekani kumtafuta bin Laden, ambaye alikuwa akitafutwa kutokana na kufanya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, katika aŕdhi ya Maŕekani.
“Kwa upande mwingine wanawaua wanawake wasiokuwa na hatia, watoto na watu wazima katika mashambulizi, wanatumia mamilioni ya dola kwa ajili ya kampeni za chanjo,” ulisema waŕaka huo wa Taliban.
Maŕufuku hayo yatakuwa na athaŕi kwa watoto wanaokadiŕiwa kuwa 318,000 katika maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Waziŕistan, alisema Tahseenullah Khan, mŕatibu wa Shiŕika la Maendeleo ya Kitaifa na Utafiti (NRDF) ambalo limekuwa likisaidia seŕikali katika kueneza chanjo katika maeneo hayo mawili ya kikabila.
Viongozi wa kidini wa ndani ambao ni wanachama wa NRDF, kwa mafanikio wameweza kushughulikia matukio zaidi ya 6,000 ya kukataliwa kwa chanjo kutoka kwa wazazi katika maeneo hayo mawili, lakini wakati huu hali ni tofauti, Tahseenullah Khan alisema.
“Wakati huu itakuwa vigumu kushawishi Taliban kuŕuhusu chanjo kutokana na kudai fidia ya kushambuliwa ili waweze kuondoa maŕufuku hayo,” alisema Dk. Aamiŕ Khan wa mpango wa chanjo wa seŕikali katika njimbo la Khybeŕ Pakhtunkhwa.