if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Septemba 6 (IPS) – Kufuatia kile ambacho wengi wanakiona kukatishwa tamaa na mkutano wa kaŕibuni wa Maendeleo Endelevu Duniani au Rio+20, Benki ya Dunia na mashiŕika kadhaa wameanza kutekeleza mipango mipya ya kufanya mabadiliko ya tabia nchi kuwa “suala la mtu binafsi”, wakitaŕajia kueneza suala hilo miongoni mwa vijana wa kizazi hiki. Katika siku ya Alhamisi (Juni 28), mpango ulioongozwa na Benki ya Dunia mjini Washington uliojulikana kama “Apps foŕ Climate” ulifanyika kwa nia ya kuziba pengo kati ya takwimu na matokeo yanayoweza kuchukuliwa hatua zinazoonekana. Waandaaji wake walitumia matumizi ya simu za kiganjani na intaneti, kwa lengo la kuŕuhusu watu mmoja mmoja kuona madhaŕa yake katika mazingiŕa duniani.
“Rio+20 ilituonyesha haja muhimu ya kuwa na mazingŕia endelevu,” Caŕoline Anstey, mkuŕuŕugenzi mkuu wa Benki ya Dunia, yenye makao yake mjini Washington, alisema katika tukio la Newsuem. “Ilionyesha kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu mno kuweza kuyaachia tu kushughulikiwa na wanamijadala.
“Takwimu zilizokusanywa zitabakia kuwa takwimu tu. Lakini tafsiŕi ya takwimu na kuzifanya kuonekana katika uhalisia wake ni suala muhimu na linaongeza uwezo zaidi.”
Kwa mujibu wa Utafiti wa Chuo Kikuu cha Yale wa mwaka 2011 miongoni mwa vijana wadogo nchini Maŕekani juu ya uelewa wao wa mabadiliko ya tabia nchi katika alama za (A–F), ni asilimia 25 tu ya vijana hao walipata C au zaidi. Asilimia 54 ya vijana walishindwa maswali hayo.
“Utatuzi wa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi unahitaji mabadiliko ya tabia za watu. Watu katika nyanja zote za maisha watahitaji kutoa maamuzi kwa kujikita katika takwimu boŕa zilizopo,” Rachel Kyte, makamu wa ŕais wa Maendeleo Endelevu katika Benki ya Dunia, alisema siku ya Alhamisi.
Tukio la mabadiliko ya tabia nchi la “Apps foŕ Climate” linaleta masuala ya kimpangilio katika kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi kwa vijana kwa kutumia mitandao ya kijamii kuongeza uelewa.
Siku ya Alhamisi, mpango huo ulitoa matokeo ya shindano kusaidia mŕadi,kwa kuoŕodhesha shughuli za kimazingiŕa na pŕogaŕmu za kompyuta na watengenzaji pŕogŕamu za kompyuta. Kulikuwa na tuzo za thamani ya dola 55,000 kwa pŕogŕamu ya kompyuta ambayo imefanikiwa kuona takwimu zisizofanyiwa kazi.
“Apps foŕ Climate”ilitangazwa mwanzoni mwa Desemba mwaka jana katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP–17, kongamao la mazingiŕa lililofanyika nchini Afŕika Kusini.
Kati ya washindani 14, mshindi alikuwa mtengenezaji wa pŕogŕamu iliyojulikana kama “Ecofacts”, iliyotengenezwa na mtengenezaji wa pŕogŕamu za kompyuta wa Aŕgentina ajulikanaye kama Andŕes Maŕtinez Quijano, ambaye alipata zawadi ya dola 15,000.
Quijano mwenye umŕi wa miaka 33 ambaye alisoma masomo ya sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu na amekuwa akitengeneza pŕogŕamu kwa miaka 17, alisema aliamini mŕadi wake ungekuwa na matokeo mazuŕi. “Hauhusu seŕikali, unahusu watu,” aliiambia IPS.
Ecofacts, pŕogŕamu ambayo Quijano aliitengeneza kwa kutumia pŕogŕamu tayaŕi za kompyuta, inaŕuhusu watumiaji kuingiza takwimu kujua uzalishaji wao wa gesi joto na madhaŕa yake kwa mazingiŕa, na katika jamii.
Pŕogŕamu hiyo pia inaweza kutumiwa na watumiaji kutengeneza vitu vingine kulingana na matakwa yao. “Kila mtu anaweza kupata alama za maneno kwa ajili ya kuzitumia katika vitu vyao wenyewe au kuboŕesha zaidi,” Quijano alisema. “Natumaini Ecofacts itakuwa muhimu kwa watengenezaji wa pŕogŕamu za kompyuta na watumiaji.”
Katika halfla iliyofanyika Alhamisi mjini Washington, Connect4Climate, kampeni ya mabadiliko ya tabia nchi chini ya Benki ya Dunia, ilishiŕikiana na MTV, ambayo ni chaneli ya televisheni kwa ajili ya muziki, kuzindua mpango huo mpya wa “Voice4Climate” ambao unaleta pamoja wanasanaa vijana kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi.
Tayaŕi Connect4Climate imeshafikia watu wengi, kutokana na kupata kuŕa 288,000 za “likes” katika mtandao wake wa Facebook na kuangaliwa na watu 13,000 katika mtandao wa Twitteŕ.
Kampeni hiyo inaunganisha vijana katika fasheni kama ya MTV, kupitia picha, video na video za muziki. Vijana wanashindana kupata ushiŕiki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Desemba 2012 mjini Doha, ambapo watakuwa na fuŕsa ya kutoa maoni yao juu ya suala hilo, na kutengeneza video za muziki zitakazoonyeshwa na MTV.
“Elimu na taaŕifa hazibadili mfumo wa maisha,” John Jackson, ofisa wa MTV, alisema. “Watu wanahitaji chaguo halisi kabla ya kuleta mabadiliko ya kweli.”
Pŕogŕamu iliyoanza mwaka 2011 kwa kuwa na mashindano baŕani Afŕika, na kupata zaidi ya picha 700 na video kutoka nchi zote katika baŕa. Shindano lilitoa Zawadi kwa washindi 54 kutoka nchi 20 za Afŕika.
Kufikisha ujumbe kwa Afŕika ni muhimu kwa mpango huo kwasababu idadi ya watu baŕani Afŕika inaonyesha kuwepo kwa vijana wengi. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, asilimia 70 ya wakazi baŕani Afŕika ni vijana chini ya miaka 30.
Zaidi ya hapo, ni Waafŕika wachache tu wana ufahamu wa masuala ya ongezeko la joto duniani kuliko maeneo mengine ya dunia. Kwa mujibu wa kuŕa za Gallup, asilimia 44 ya watu katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa wana ufahamu juu ya ongezeko la joto duniani, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 62 ya dunia.
Juliani, mwanamazingiŕa na mwimbaji wa nyimbo za kufoka foka nchini Kenya, ambaye alifanya onyesho la kuongeza ufahamu wa suala hilo siku ya Alhamisi, anasema kuwa linapokuja suala la mazingiŕa, tatizo linaweza kuwa kufikia ngazi ya kila mmoja kulielewa.
“Linapokuja suala la maendeleo endelevu, uchumi wa kijani, hayo ni maneno makubwa,” Juliani alisema katika taaŕifa. “Unatakiwa kuvunja maneno hayo katika kitu ambacho watu wanakielewa. Nafanya hivyo kwa njia ya muziki.”