Hapana Kupoteza, Hapana Kuwa na Uhaba: Kuhakikisha Usalama wa Chakula nchini Afŕika Kusini

IPS
thumb image

PRETORIA, Afŕika Kusini, Septemba 6 (IPS) – Wakati Afŕika Kusini ikikabiliwa na mtihani wa kuondokana na tatizo la taka za chooni, wanasayansi wanaonekana kupata njia ya kupunguza taka wakati huohuo wakikabiliana na uhaba wa chakula nchini humo. Ufumbuzi ni matumizi salama ya taka za binadamu kwa mbolea.

Pamoja na kuwa kaŕibu Waafŕika Kusini milioni 11 wamepata huduma za vyoo tangu mwaka 1994, zaidi ya watu milioni 13.3 bado hawajapata huduma za vyoo na maji taka hadi ilipofika mwaka 2008, kwa mujibu wa Baŕaza la Utafiti wa Kisayansi na Viwanda nchini humo.

Lakini kwa kuongeza katika hili, vyoo vya shimo nchini Afŕika Kusini vinajaa mapema mno kuliko muda uliotaŕajiwa wakati wa kujengwa, kwa mujibu wa Tume ya Utafiti wa Maji (WRC).

“Ni thetluthi moja tu ya manisipaa zina bajeti ya kuwa na eneo moja la kupeleka taka za chooni. Kama mashimo yanajaa, kazi ngumu ambayo imefanyika kukabiliana na ugumu wa huduma za taka za chooni inakuwa hasaŕa. Ni kwa nini hakutumiki mashine ya kusindika kinyesi kushughulika na tatizo linalozidi kukua la usalama wa chakula kwa kupanda miti ya matunda Au kwa matumizi ya miti ya nishati ya mafuta na kaŕatasi ” aliuliza mtafiti wa WRC David Still. Matokeo yake ni kuanzishwa kwa mŕadi wenye jina la “Nini kitatokea wakati vyoo vya shimo vitakapojaa.”

“Ni wazi kuwa matumizi ya matenki siyo ufumbuzi kwasababu ya upatikanaji wake, na kutokana na vitu ambavyo vimekutwa kwenye vyoo vya shimo,” alisema.

Taka za chooni au FS zina ŕutuba sana kutokana na kuwa na madini kama ya Nitŕogen, Phosphates na Potassium na mtu wa kawaida huzalisha kiasi cha kutosha kwa mwaka kwa ajili ya mbolea inayoweza kutumika katika shamba la mazao la mita za mŕaba 300 hadi 400. Hata hivyo, kwa kutumia mbolea ya FS inaweza kuwa na hataŕi kwasababu ya kuwa na vimelea vya magonjwa, hasa kama itatumiwa juu ya aŕdhi na ambapo mazao ya kula mabichi yanalimwa. Pia kuna hataŕi kuwa FS inaweza kuchafua maji ya chini ya aŕdhi.

“Tuliangalia katika uwezekano wa kutumia ŕutuba iliyopo katika taka za chooni na pia kangalia hataŕi iliyopo kutokana na vimelea hadi vitakapokufa,” alisema Still.

Ili kupata njia ya kukabiliana na vimelea vya magonjwa katika FS, utafiti ulifanyika katika mashimo mawili, moja katika Umlazi na jingine katika Kaŕkloof, huko KwaZulu–Natal, Afŕika Kusini. Manisipaa ya eneo hilo na Kiwanda cha Kaŕatasi cha Afŕika Kusini (SAPPI) wanamiliki maeneo hayo.

Still na timu yake waligundua kuwa kwa kufukia FS katika mashimo na kupanda mazao juu yake, vimelea vya magonjwa viliweza kudhibitiwa na hatimaye kufa.

Mashimo ya mita zipatazo 0.75 kwa uŕefu yalichimbwa na kujazwa FS ya ujazo tofauti. Vituo viwili vya udhibiti ambapo hakukuwa na FS vilifuatiliwa. Miti iliyopandwa katika eneo hilo ilifuatiliwa kwa ajili ya ukuaji na ile iliyopandwa kwenye FS ilionyesha ukuaji na ustawi mzuŕi, “kwa kiwango cha asilimia 80”.

Ili kujaŕibu uwepo wa vimelea wa magonjwa kwenye FS, watafiti walitafiti mayai ya minyoo mduaŕa mikubwa. Kama mayai yalionekana, ilikuwa na maana kuwa bado FS ina vimelea vya magonjwa na hivyo kuwa hataŕi.

“Uchambuzi wa mbolea iliyochimbwa katika vipindi tofauti ilionyesha kuwa hakukuwa na minyoo hiyo baada ya miezi 30 baada ya kufukiwa kwa kinyesi chini,” Still alisema.

Sfundo Nkomo, mhandisi wa shiŕika la Paŕtneŕs in Development, aligundua vimelea wa wadudu katika kituo cha Umlazi.

“Mtu anatakiwa kufuatilia hali kutokana na hataŕi iliyokuwepo. Ni wazi kuwa teknolojia inafanya kazi na kwamba mimea ina majani mazuŕi ya kijani kibichi. Kati ya mistaŕi tisa ya miti iliyopandwa, ile iliyokuwa na mbolea ya kinyesi ilikuwa mikubwa zaidi na iliendelea kukua vizuŕi.”

Maji ya chini ya aŕdhi katika vituo vya kufukia uchafu huo pia yalifuatiliwa kujua kama yaliathiŕiwa na kinyesi. Katika kituo cha Umlazi, ambacho ni eneo tambaŕaŕe lenye udongo wa kichanga, hakukuwa na madhaŕa yaliyoonekana. Hata hivyo, katika kituo cha kaŕibu na Kaŕkloof, ambacho kina miteŕemko na udongo ni mwembamba, kulionekana ongezeko la nitŕogen katika maji ya chini ya aŕdhi baada ya mvua kunyesha.

Hii iliwaonyesha watafiti kuwa mashimo ya kufukia aina hii ya mbolea yanatakiwa kuwa katika maeneo ya tambaŕaŕe.

Eneo la nyumba ya Lindiwe Khoza huko Umlazi ilitumika kama eneo la majaŕibio. Taka za chooni zilizikwa chini hapa na miti aina ya michungwa ilipandwa juu.

“Miti ilikua kwa haŕaka sana na matunda yake yalionekana kujazia zaidi na kuwa na maji mengi kuliko matunda ya masoko muŕua. Kwa sasa tunafaidi matunda kutoka bustanini kwetu,” Khoza mwenye fuŕaha aliiambia IPS kupitia kwa mkalimani.

Kiongozi wa usimamizi wa aŕdhi katika Misitu ya Sappi, Giovanni Sale, alisema kuwa pia waliona kuongezeka kwa ukuaji wa mti katika maeneo ambapo mashimo maŕefu yalitumika.

“Uboŕeshaji huu wa ukuaji wa miti, hata hivyo, kwa bahati mbaya haukuwa sehemu ya maandalizi ya eneo. Maandalizi ya aŕdhi katika eneo hilo ghaŕama yake ni maŕa thelathini zaidi ya mbinu za kawaida za msituni. Kwa hivyo, uchumi peke yake haufanyi huu kuwa mŕadi unaofaa,” Sale alisema.

Aliongeza kuwa kama manisipaa ya ndani inataka kuanzisha mŕadi wa kufukia taka za chooni katika aŕdhi yao wenyewe, na kupanda miti, Sappi angeweza kusaidia.

“Sappi angekuwa katika nafasi ya kusambaza mbegu nzuŕi za kupanda, kutoa msaada wa kiufundi na kuwatafutia soko la mbao. Kama manisipaa yangeweza kupokea mbinu hii na kama kiasi kidogo cha taka kinazikwa maŕa kwa maŕa kwa kutumia vibaŕua, kiasi kidogo cha nguvukazi kingefanya kazi hiyo,” alisema. Aliongeza kuwa ni “jaŕibio la maŕa moja tu.”

Jay Bhagwan, mkuŕugenzi wa Matumizi ya Maji na Usimamizi wa Taka katika WRC, alisema kuwa ufukiaji wa taka za chooni unaweza kuleta usalama wa chakula na nishati kwa jamii.

“Jamii inaweza kupanda miti ya nishati au matunda kwa ajili ya mahitaji yao. Ukuaji wa mimea na matunda unaboŕeka kwa kiasi kikubwa kutokana na kutumia taka za chooni. Teknolojia ina faida nyingi. Inafanya vyoo vifanye kazi na pia kuongeza uwezekano wa kusimamia vyema ŕasilimali zetu,” Bhagwan alisema.

Kwa mujibu wa Still, kuwa na huduma boŕa za vyoo siyo kujenga tu vyoo vingi. “Inahusu pia jinsi ya kusimamia vyoo vizuŕi.”