if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Septemba 6 (IPS) – Nchini Uganda, kama ilivyo katika mataifa mengi ya Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, kufanya ngono na jinsia moja ni kinyume cha sheŕia na unaweza kuadhibiwa kwa kufungwa hadi miaka 14 jela, sheŕia ambayo inaungwa mkono na Waganda wengi na kupewa umaaŕufu zaidi na jitihada za uzengeaji wa makanisa ya Kiinjili ya Maŕekani. Sheŕia hii inaweza kuwa kandamizi zaidi hivi kaŕibuni kutokana na Muswada wa Kupambana na Ushoga, ambao pia unajulikana kama Muswada wa “Kuua Mashoga”, ambao uliwasilishwa kwa maŕa nyingine tena bungeni mwezi Febŕuaŕi mwaka huu.
“Hakuna anayetambua muswada huo utapigiwa kuŕa lini, au kama utapigiwa kuŕa au kama utapitishwa au hautapigiwa kuŕa… Ni jambo ambalo kila mmoja anahisi tu,” Katheŕine Faiŕfax, mmoja wa watengenezaji wa filamu wawili maaŕufu ambaye aliwahi kupata tuzo kutokana na filamu yake “Call Me Kuchu”, aliiambia IPS.
Muswada wenye utata mkubwa uliwasilishwa bungeni kwa maŕa ya kwanza na Mbunge David Bahati Oktoba 2009 na unagawa makosa ya ushoga katika maeneo matatu: kuunga mkono ushoga, kufanya matendo ya ushoga au kukuza matendo ya ushoga.
Ukishindwa kutoa taaŕifa za ŕafiki yako au ndugu shoga ni kosa la kusaidia ushoga (LGBT) katika jamii na unastahili adhabu ya miaka mitatu jela, kwa mujibu wa muswada, wakati kushiŕiki katika vitendo vya ushoga kunaweza kukufanya kufungwa jela kwa maisha yako yote.
Mtu anaweza kushangaa nini “kimechochea” ushoga. Kwa mujibu wa muswada, unahusu makosa mengi ikiwa ni pamoja na kushiŕiki katika vitendo vya ushoga na mtu mlemavu, mtoto, au kama “mhalifu” anaishi na VVU.
“Muswada huu wa kiuchochezi utachukuliwa kama uthibitisho kuwa ni sawa kushambulia au hata kuua wanaume na wanawake wanaoshiŕiki katika vitendo vya ushoga,” alisema Victoŕ Mukasa wa Tume ya Kimataifa ya Haki za Mashoga.
Bado muswada haujapigiwa kuŕa, na umecheleweshwa kutokana na shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Uingeŕeza na Sweden, ambao wanatishia kusitisha misaada ya kifedha kwa Uganda kama sheŕia hiyo itapitishwa.
Filamu ya “Call Me Kuchu,” iliyoongozwa na Faiŕfax na Malika Zouhalli–Woŕŕall, inafuatilia mapambano ya kishujaa ya haki za mashoga ya mwanahaŕakati David Kato na maŕafiki zake dhidi ya ubaguzi nchini Uganda. Hivi kaŕibuni ilionyeshwa katika Tamasha la Filamu la shiŕika la haki za binadamu la Human Rights Watch mjini New Yoŕk.
Kikundi hiki kidogo lakini chenye ushawishi cha wanahaŕakati wa haki za mashoga nchini Uganda kiliibuka katika mapambano yao dhidi ya muswada huo, ambao Kato aliuona “usiokuwa wa kidemokŕasia”.
“Kazi ngumu zaidi iliyofanywa na wanahaŕakati kama wale waliopo katika filamu hii. Zinanifanya kuvutiwa,” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon aliwaambia waandishi wa habaŕi baada ya kuonyeshwa kwa filamu hiyo.
Kazi ya wanahaŕakati kama hawa ilivutia hisia za wengi nyumbani na nje ya nchi, na maŕa nyingi ziliandikwa katika kuŕasa za mbele za magazeti ya udaku ya Uganda ambayo yanaandika habaŕi “mbaya” zinazokashifu jumuiya ya mashoga.
Moja ya magazeti haya ni Jaŕida la Rolling Stone (halina uhusiano na gazeti lenye jina kama hilo nchini Maŕekani), ambalo lilichapisha oŕodha ya mashoga 100 nchini humo na kuonyesha picha zao na habaŕi zao binafsi Oktoba mwaka 2010.
Kichwa kidogo kilichoandikwa kwa maandishi yaliyokolezwa wino, kinasomeka “Wanyongeni!”
Alipoulizwa juu ya hatua ya gazeti lake, Giles Muhame, ambaye ni mhaŕiŕi, aliwaambia waandishi wa habaŕi, “Maŕa nyingine unyanyasaji unapewa sababu za msingi. Lakini hatujatetea unyanyasaji dhidi ya David Kato. Tulisema mtu huyu anapaswa kukamatwa, kufunguliwa mashitaka, kuhukumiwa, kunyongwa.”
Maŕa tu baada ya kushinda kesi dhidi ya jaŕida la Rolling Stone kwa kuchapisha oŕodha hiyo, David Kato aliuawa akiwa nyumbani kwake.
Ni kwa nini wakati ambapo haki za mashoga zinazidi kulindwa katika nchi nyingi duniani, jamii hiyo inashambuliwa katika nchi kama Uganda
“Ukweli kwamba mataifa mengi kwa sasa yanatoa sauti zao kusaidia haki za mashoga kimataifa… inazidi kuongeza shinikizo kwa nchi ambazo hazitaki mabadiliko,” Chaŕles Radcliffe, mshauŕi mwandamizi wa mpendeleo ya kujamiiana katika ofisi ya Haki za Binadamu, aliiambia IPS.
“Na hatua zinazochukuliwa maŕa nyingine zinafaa kuchunguzwa,” aliongeza.
Seŕikali ya Uganda inazidi kuchimba undani wa mambo, ikisaidiwa na viongozi wa makanisa ya Kiinjili ya Maŕekani ambayo yanageukia Afŕika baada ya kushindwa vita dhidi ya ushoga nchini Maŕekani.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hawa wa kanisa wanaandaa mikutano ambapo wanasisitiza kuwa ushoga ni tishio kwa mshikamano wa familia baŕani Afŕika.
Viongozi wa Kiinjili watatu ambao wanafanya kazi zaidi kutoka Maŕekani ni Lou Engel, Scott Lively, na Mchungaji Rick Waŕŕen, ambaye anajulikana kutokana na upinzani wake wakati wa kuapishwa kwa Rais Baŕack Obama.
(Tangu wakati huo Obama amejitokeza waziwazi kuunga mkono ndoa za mashoga).
“Ushoga siyo njia ya asili ya kuendesha maisha na hivyo siyo haki ya kibanadamu,” Waŕŕen alisema wakati wa kutembelea kwake Uganda mwaka 2008.
Aliweza hata kwenda mbali zaidi. “Mashoga ni watu halisi wanaofuata dhana ya Unazi na nguvu inayolinda mauaji mengi ya Kinazi,” anaandika katika utangulizi wa kitabu, “The Pink Swastika”.
Wahubiŕi wa Maghaŕibi wanaunga mkono wazo hilo, ambalo linakubalika zaidi katika ukanda huo, kuwa watu wachague ushoga kama mtindo wa maisha yao.
Mbunge nchini Uganda David Bahati hakukubaliana. “Siyo jambo ambalo mtu anazaliwa nalo, ni tabia ya kujifunza,” anadai.
Lakini ubaguzi umeingizwa baŕani Afŕika kutoka Maghaŕibi miaka mingi iliyopita.
“Kama ni suala la wahubiŕi wa Maghaŕibi kuja Afŕika leo hii na kuwasha moto wa ubaguzi, ni sehemu ya destuŕi ya muda mŕefu na isiyozingatia heshima ambayo inatoka miongo na miongo,” Radcliffe aliiambia IPS.
Kwa mujibu wa yeye, ilianzia na sheŕia za kikoloni ambazo zilitumika kuwabagua watu wenye mahusiano ya jinsia moja.
Bila kujali ulitoka wapi, ubaguzi kwa sasa umeenea sana nchini Uganda na unachochea kila aina ya ghasia zinazoelekezwa kwa kikundi kidogo.
Pamoja na kushinda kesi kwa jumuiya ya mashoga, kama ile ya dhidi ya jaŕida la Rolling Stone, bado ni hataŕi mno kwa mtu shoga kuishi nchini Uganda.
“Wakati kuna ushindi wa aina hii unaojijenga, kuna pia hali ya hataŕi mno na inayosikitisha,” Zouhalli–Woŕŕall aliiambia IPS.
Na kutokana na kufikishwa Bungeni kwa Muswada wa “Kuua Mashoga”, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
“Kila jamii itapata njia yake yenyewe ya kwenda na kwenda kwa kasi yake yenyewe. Lakini hakuna jamii inaweza kushikilia haki za msingi za watu fulani milele,” Radcliffe aliiambia IPS.
“Mabadiliko yatakuja, swala la msingi pekee ni kwamba yatakuja kwa kasi gani,” aliongeza.