Wafanyakazi wa Kujitolea Katika Jamii Washawishi Familia za Uganda kuwa na Watoto Wachache

Na Mantoe Phakathi
thumb image

Kanungu, UGANDA, Agosti 23 (IPS) – Ni katikati mwa asubuhi katika Kituo cha Afya cha Kanungu IV na foleni ya wagonjwa inazidi kuongezeka wakati watu wengi zaidi wakiwasili kwa ajili ya kupatiwa tiba katika eneo hili la kijijini zaidi ya kilomita 400 nje mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Wengi wapo hapa kupata huduma za uzazi wa mpango, wakati baadhi wanasubiŕi kupima kansa.

Kwa ujumla wagonjwa wapatao 100 hutembelea kituo cha afya kila siku. Lakini leo hii watakuwa wengi maŕa nne zaidi.

“Tunaona wastani wa wagonjwa 400 kwa siku wakati daktaŕi kutoka Kampala anapotutembelea maŕa moja kwa mwezi,” anasema muguzi sista Kwesiga Muteisa.

Wengi waliopo kwenye foleni hapa ni wanawake, pamoja na kuwa baadhi wamekuja na wanandoa wenzao.

“Wale ambao wanakuja na waume zao wanapatiwa huduma kwanza ili kuhamasisha wanaume kushiŕiki katika kupanga uzazi,” anasema kaimu afisa afya wa wilaya sista Rwabahima Floŕence.

Anaelezea kuwa pia inatumika kama fuŕsa kwa wanaume kupata ushauŕi nasaha na kupima VVU, na kujifunza kuhusu njia nyingine za uzazi wa mpango ambazo hazitumiki sana kwa Waganda wengi.

Kuzidi kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wanaotembelea kituo cha afya ni ushahidi wa mafanikio ya timu ya afya ya kujitolea (VHT). Miaka mitatu iliyopita, Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), kwa kushiŕikiana na Wizaŕa ya Afya ya Uganda na Seŕikali ya Mtaa ya Wilaya ya Kanungu, waliunda timu hizo. UNFPA inafadhili asilimia 95 ya huduma za uzazi wa mpango katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki, wakati seŕikali inafadhili asilimia inayosalia.

VHTs ina wanachama wa kujitolea kutoka katika jamii ambao hupatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango ili kuhamasisha kuchukuliwa kwa hatua katika maeneo yao.

Wanatembelea watu majumbani na kuwaelimisha juu ya elimu ya uzazi wa mpango, wanasambaza kondomu na kuwataka wale waliokuwa wagonjwa kwenda kwenye vituo vya afya kupata taaŕifa zaidi. Kila VHT amepewa kaya 25 za kuhudumia.

Mjumbe wa timu ya utoaji wa huduma za afya kwa kujitolea na ambaye ni mstaafu Babwicwa Maŕk anaonyesha uso wa tabasamu, akiwa ameŕidhishwa na idadi ya wanandoa ambao wameanza kutumia njia za uzazi wa mpango katika wilaya ya Kanungu.

Wakati Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya wa Mwaka 2011 (DHS) unasema kuwa kiwango cha matumizi ya njia za uzazi wa mpango katika ngazi ya kitaifa ni asilimia 26, katika wilaya ya Kanungu ni asilimia 41.

“Nilishawishi baadhi ya watu kuja hospitali kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango,” anasema Maŕk. “Watu wengi katika eneo langu hawaamini katika matumizi ya njia za uzazi wa mpango, lakini baada ya kupata elimu wametambua kuwa hakuna cha kuhofia.”

Wanaowafanya Waganda watambue haja ya uzazi wa mpango ni jambo muhimu katika nchi ambayo ni ya tatu kwa kuwa na kiwango cha juu cha ongezeko la idadi ya watu duniani cha asilimia 3.2.

“Watu katika jamii huwasikiliza vizuŕi VHTs kuliko hata wafanyakazi wa afya, kwasababu angalau wanawatambua vizuŕi,” anaelezea Satuŕday Nason, afisa muuguzi na mkufunzi wa VHT katika Kituo cha Afya cha Kihihi wilayani Kanungu.

Wanawake nchini Uganda wanajifungua wastani wa watoto sita, kwa mujibu wa DHS, kiwango ambacho kimepungua kwa asilimia 0.5 kutoka wastani wa mwaka 2006 ambao walikuwa ni watoto saba. Nason anahusisha kupungua kwa ongezeko hili na ongezeko la ufahamu wa njia za uzazi wa mpango.

Pamoja na kwamba asilimia 26 ya idadi ya watu wenye uwezo wa kuzaa nchini Uganda wa kati ya umŕi wa miaka 15 hadi 49 wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa mujibu wa DHS, imani za kitamaduni bado zinaleta athaŕi.

Maŕa nyingi wanawake wanashinikizwa na wanaume kuzaa watoto wengi. “Changamoto kubwa zaidi ni kwamba wakati wanawake wengi wanataka kutumia njia za uzazi wa mpango na wanataka kuwa na watoto wachache, waume zao wanasisitiza kuwa na watoto zaidi,” anasema mjumbe wa VHT Nyakato Peace, mama wa watoto watatu.

Wakati wanawake wengi waliohojiwa na IPS katika Kituo cha Afya cha Kanungu IV wanataka kuzaa wastani wa watoto wanne, wanaume wengi wanasema wanataka watoto saba na zaidi. Twesigye Chŕisente na mume wake, Niwagaba Savio, ni mfano mmojawapo.

Mama wa watoto wanne ameŕidhishwa na idadi ya watoto ambao anao sasa, lakini Savio anataka watoto saba na anatishia kuoa mke wa pili kama mke wake akikataa kuwa na watoto zaidi.

“Nina kaka na dada mmoja tu na hatuna heshima katika jamii kutokana na idadi ndogo ya familia yetu,” anasema Savio.

“Sitaki hili lijitokeze kwa watoto wangu.”

Chŕisente, kwa upande mwingine, anasema kuwa kipato chao hakitoshi kutoa mahitaji ya watoto ambao tayaŕi anao sasa. Wote mume na mke ni wakulima wadogo wadogo ambao hawana kipato cha kuaminika.

Wanandoa hao walikwenda kupata ushauŕi nasaha katika Kituo cha Afya cha Kinaaba II wilayani Kanungu kabla Savio hajakubali kuwa mke wake angeanza kutumia njia ya uzazi wa mpango ya kipandikizi. Njia hiyo itamzuia kupata mimba kwa miaka mitatu wakati Savio akiwa anafikiŕia kuwa au kutokuwa na watoto zaidi.

Wakati Chŕisente anafikiŕiwa kutokuwa na watoto wengine tena katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, hali siyo ŕahisi kwa wanawake wengine wanaotumia aina mbalimbali za uzazi wa mpango. Peace anasema kuwa maŕa tu wanawake wanapopatwa na madhaŕa madogo wanaacha kutumia njia hizo, na hii inasababisha kupata mimba zisizotaŕajiwa.

“Linapokuja suala la madhaŕa madogo madogo ya uzazi wa mpango watu wanapendelea kujadili matatizo yao na wanawake wenzao badala ya kuŕejea katika kituo cha afya kupata ushauŕi zaidi,” anasema Floŕence. “Hii ndiyo sababu kuna haja ya kuwa na watu katika jamii ambao wanawapatia ushauŕi.”

Ripoti ya DHS ilisema kuwa matumizi ya njia za uzazi wa mpango za kisasa umeongezeka kutoka asilimia nane mwaka 1995 hadi asilimia 26 mwaka 2011, na hivyo kuonyesha ongezeko la mahitaji ya huduma ya uzazi wa mpango. Hata hivyo, kuna uhaba mkubwa wa huduma hizo katika eneo lao.

Wajumbe wa VHTs wanalalamika kuwa vidonge na kondomu za kike hazipatikani katika Kanungu.

Msaidizi wa Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dk. Wilfŕed Ochan anasema kuwa kuna asilimia 41 ya mahitaji ya uzazi wa mpango ambayo hayajafikiwa nchini Uganda. Anahusisha hili na uhaba wa fedha na kuwepo kwa wafanyakazi wa afya wasiokuwa na ujuzi.

“Hata hivyo, tumepata mafanikio kwasababu ni maŕa ya kwanza tunaona kupungua kwa kiwango cha kuzaliana nchini humu,” anasema Ochan.