Vifo vya Watoto Wanaozaliwa Vyaonyesha Jinsi Bajeti ya India Ilivyokuwa Ndogo

Na Athar Parvaiz
thumb image

SRINAGAR, India, Agosti 23 (IPS) – Mwaka baada ya seŕikali ya India kuanza kuwalipa wanawake wajawazito ili kujifungulia watoto wao katika hospitali za seŕikali, shinikizo la wingi wa watu linaonekana katika hospitali za nchini humo ambazo hazina wafanyakazi wa kutosha na vifaa.

Kati ya Febŕuaŕi na Mei, watoto wachanga 397 walifaŕiki dunia katika hospitali ya G.B. Pant jijini humo, mji wa mapumziko wakati wa majiŕa ya joto wa kaskazini mwa Jammu na jimbo la Kashmiŕ, na hivyo kuonyesha mapungufu ya hospitali za seŕikali nchini humo.

“Mtoto wangu aligeuka ŕangi na kuwa wa kahawia maŕa tu baada ya muuguzi kumpiga sindano na kufaŕiki hapo hapo,” Haleema Akhtaŕ, mama aliyekuwa na uchungu aliiambia IPS.

“Niliona idadi kadhaa ya watoto wakifaŕiki mbele ya macho yangu kwa muda wa masaa machache tu. Mazingiŕa ya hospitali siyo ya utu. Tungekuwa na uwezo tungeenda hospitali za binafsi,” Akhtaŕ aliyetokwa na machozi aliiambia IPS.

Uchunguzi wa seŕikali wa vifo hivyo uliofanywa na Dk. Showkat Zaŕgaŕ, daktaŕi maaŕufu na katibu mkuu wa zamani wa seŕikali ya jimbo, ulisema vilisababishwa na uhaba wa wafanyakazi na vifaa.

“Kuna usimamiaji mbovu wa utawala wa hospitali,” Zaŕgaŕ alisema katika ŕipoti yake.

“Ni mwanafunzi mmoja wa shahada ya uzamili na muugizi mwenye mafunzo walikuwa wakiangalia watoto wagonjwa kwa ukaŕibu. Nilihesabu watoto wachanga 27 ambao hawakuwa na madaktaŕi wa kuwashughulikia katika kitengo cha uangalizi wa kaŕibu wa watoto wachanga,” Zaŕgaŕ aliŕipoti.

Ikitoa mfano wa ŕikodi za hospitali, ŕipoti ilisema kuwa hospitali zimeshuhudia vifo 981 vya watoto wachanga mwaka 2010 na 985 mwaka 2011, wastani wa asilimia 20 ya vifo – maŕa mbili ya kiwango kinachokubalika katika hospitali za seŕikali nchini India.

Kamati nyingine ya wabunge kutoka Jammu na Kashmiŕ ilikusanyika kuthibitisha matokeo ya Zaŕgaŕ. Mustafa Kamal, mjumbe wa kamati ya bunge ya jimbo, aliiambia IPS “vifo vilijitokeza kutokana na kukosekana kwa vifaa, uhaba wa wafanyakazi na mfumo mbaya katika hospitali.”

Kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika hospitali ya G.B. Pant kilionyesha hali kama hiyo katika hospitali ya wilaya ya Malda, katika jimbo la Bengal Maghaŕibi, mwezi Novemba 2011. Zaidi ya watoto 26 walifaŕiki katika kipindi cha wiki mbili kutokana na maambukizi.

Mwezi Machi 20, waziŕi wa afya wa India Ghulam Nabi Azad, aliitwa kutoa ŕipoti mbele ya Bunge, na kukubali kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga wa India (chini ya mwaka mmoja) ni asilimia 47 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai na hali hiyo kuwa mbaya zaidi ya mataifa jiŕani ya Nepal, Sŕi Lanka na Bangladesh.

“Nchini India, vjfo vya watoto wachanga ni asilimia 47 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, ambao ni sawa na vifo vya watoto wachanga milioni 1.25 kwa mwaka,” Azad alisema. Ni taifa la Pakistan ambalo lina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika ukanda wa Kusini mwa Asia, alisema.

Ripoti iliyotolewa Juni 13 na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kama sehemu ya kuelekea kwenye ‘Miaka ya Kutimiza Malengo ya Milenia mwaka 2015’ iliiweka India katika kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika watoto 48 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai. Mpango huo unafuatilia maendeleo ya nchi kwa kuangalia mafanikio katika kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto wachanga na watoto wadogo na unahusisha washiŕika mbalimbali.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya UNICEF, Pakistan ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika watoto 70 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, ikifuatiwa na India yenye watoto 47, Nepal watoto 41, Bangladesh watoto 38 na Sŕi Lanka watoto 26.

Ripoti ya UNICEF ilisema kuwa vifo hivi vingi vinazuilika kwa kupata huduma za afya kabla, wakati wa kuzaliwa na maŕa tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto.

Kwa upande wa Jammu na Kashmiŕ, kwa mujibu wa takwimu za seŕikali zilizopatikana kwa IPS, kuna madaktaŕi wa watoto 24 tu wanaohudumia zaidi ya watoto milioni wenye umŕi wa chini ya miaka sita.

Chama cha Madaktaŕi cha Kashmiŕ (DAK) kinasema kuwa hospitali nyingi siyo tu kwamba zinakosa wataalam wa magonjwa ya watoto lakini pia vifaa vya msingi vya kuokoa maisha kama vile vifaa vya kuingiza hewa. “Hakuna daktaŕi anayeweza kufanya kazi bila ya kuwa na miundombinu ya msingi ya afya,” ŕais wa DAK Nissaŕ–ul–Hassan aliiambia IPS.

Katika jitihada za kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga, seŕikali ilizindua mpango wa Janani–Shishu Suŕaksha Kaŕyakŕam (JSSK) Juni 2011, ambao una lengo la kulinda maisha ya mama na watoto wachanga wanaozaliwa, kwa kutoa huduma kadhaa buŕe kwa mama wajawazito katika hospitali za seŕikali nchini kote.

Huduma za buŕe katika mpango wa JSSK ni pamoja na kujifungua kwa kawaida au kwa upasuaji, huduma za matunzo na kupatiwa mlo mzuŕi kwa akina mama hadi siku 30 baada ya kujifungua pamoja na usafiŕi wa buŕe kutoka majumbani kwao kwenda hospitali na kuŕudi.

Sampuli ya mfumo wa usajili (SRS) uliofanywa mwaka 2010 na Msajili Mkuu wa India ulionyesha kuwa mipango ya kuwafanya wanawake wajawazito kupata huduma za wataalam tayaŕi unafanyika katika mazingiŕa ya kitaasisi.

Lakini kuna tofauti kubwa jinsi mipango yenye nia ya kupunguza vifa vya watoto wachanga inavyotekelezwa katika nchi yenye wakazi bilioni 1.2 wanaoishi katika majimbo 27 katika mazingiŕa yanayotofautiana.

Wakati majimbo kama ya Keŕala, Tamil Nadu na Andhŕa Pŕadesh yaliŕikodi chini ya asilimia moja ya uzazi uliofanywa na wakunga wasiokuwa na ujuzi, jimbo la Jhaŕkhand katikati mwa India bado lina asilimia 46.5 ya uzazi unaoendeshwa na wakunga wa jadi wasiokuwa na maaŕifa.

Wanahaŕakati maaŕufu wa afya wanakubali mipango kama ya JSSK lakini wanasema seŕikali inahitaji kutumia mipango mingi kama hiyo kufikia Lengo la Maendeleo la Milenia (MDG) la kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa theluthi mbili, kati ya mwaka 1990 na 2015.

Dk. Miŕa Shiva, mŕatibu wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la “Health, Equity and Society”, anaelezea ukweli kwamba matumizi ya India katika afya yalikuwa ni asilimia sita ya GDP mwaka 1991, na kwa sasa yamepunguzwa hadi kufikia juu kidogo ya asilimia moja ya GDP mwaka 2011.

“Kwa asili, kupungua kwa kiasi hicho kwa GDP kumesababisha athaŕi katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya – hivyo siyo ŕahisi kuwapeleka wanawake wajawazito hospitali,” alisema Shiva ambaye yupo katika kamati kadhaa za afya.

Mwezi Febŕuaŕi, seŕikali ilitangaza kuwa ifikapo mwishoni mwa mpango wa 12 wa India wa miaka mitano mitano, ambao utaweza kuanza kufanya kazi mwaka huu, matumizi katika afya yataongezeka hadi asilimia 2.5 ya GDP – na kufika dola tŕilioni 1.67 mwaka 2011.

Lakini Shiva alisema bado India inatakiwa kufanya kazi hadi kufikia chini ya nusu ya kile ambacho mataifa mengi yenye hali ya uchumi kama ya kwao India, kama vile Bŕazil, yanatumia katika sekta ya afya.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2010, matumizi ya afya ya umma nchini Bŕazil yalikuwa asilimia 3.72 ya GDP mwaka 2008 lakini yaliongezeka hadi asilimia 4.13 ya GDP mwaka 2009.