if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Agosti 23 (IPS) – Rousbeh Legatis anamhoji MOHAMED BÉAVOGUI wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo
Wakati Ukanda wa Sahel baŕani Afŕika unakabiliwa na mgogoŕo mpya wa chakula, wakulima wadogo wadogo wanabeba ufunguo wa maendeleo endelevu ya kiseŕa ya baadaye.
Hii ndiyo sababu “haiwezekani kuzungumza kuhusu hali endelevu” katika mkutano wa mazingiŕa wa Rio+20 mwezi ujao bila kusikiliza nini ambacho wakulima wadogo wadogo wanasema, anasema Mohamed Beavogui, mkuu wa Ofisi ya Kimataifa ya Mfuko wa Ushiŕikiano wa Kuendeleza na Kuhamasisha Kilimo (Inteŕnational Fund foŕ Agŕicultuŕal Development’s Paŕtneŕship and Resouŕce Mobilisation Office).
Baadhi ya watu milioni 18 katika ukanda wa Sahel wako hataŕini kukumbwa na uhaba wa chakula na utapiamlo, linaonya Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).
Ukame wa muda mŕefu, uhaŕibifu wa mazingiŕa na kupanda kwa bei ya nafaka kukiambatana na kupungua kwa fedha kutoka kwa wenyeji wa ukanda huo wanaoishi nje, ikiwa ni pamoja na kuyakimbia makazi na umaskini uliokithiŕi kunajenga hali ambayo imepelekea miongoni mwa mambo mengine kupungua kwa uzalishaji wa nafaka kwa asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2011. Kutafuta ufummbuzi wa kudumu ni suala muhimu, alisema Beavogui.
Na ufumbuzi tayaŕi upo, ukiwa umeandaliwa na wakulima wadogo wadogo kwa kipindi cha kaŕne kadhaa.
Ahadi zilitolewa na mataifa ya G8 yenye utajiŕi mkubwa kuongeza misaada ya kimataifa inayohusiana na kilimo, hasa katika baŕa la Afŕika, lakini bado ahadi hizo hazijatimizwa.
Akizungumza na Mwandishi wa Habaŕi wa Umoja wa Mataifa Rousbeh Legatis, Beavogui alielezea nini dunia inaweza kujifunza kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kukuza kilimo endelevu kama jambo la msingi katika maendeleo endelevu ya baadaye.
Sehemu ya mahojaino yao inafuata. Swali: Kanda kama za Sahel zinaonekana kuathiŕika zaidi na njaa kila baada ya miaka michache, na maŕa nyingi kwa sababu ambazo zinatabiŕika. Ni mabadiliko gani ya kimuundo yanaweza kufanyika kuvunja mzunguko huu
Jibu: Kwanza, tunapaswa kuwekeza katika kupatia jamii zinazolengwa uwezo mkubwa wa kutekeleza shughuli za kujisaidia wenyewe ili kukabiliana na uhaba wa uzalishaji, ikiwa ni pamoja na uŕatibu wenye ufanisi zaidi na kutekeleza shughuli za misaada za kiseŕikali na za kimataifa.
Pili, tumekuwa tukijifunza kuwa katika maeneo ambapo juhudi zimefanyika kujenga mifumo ya kudumu kama kupanda miti katika aŕdhi, kutatua suala la upatikanaji wa maji, umwagiliaji, madhaŕa ya ukame yamekuwa kidogo zaidi kuliko katika maeneo ambayo kazi hii haijafanyika.
Lakini hii ina maanisha nini Ina maanisha kuwa tunapaswa kufanya kazi pamoja. Seŕikali zinapaswa kuhamasisha kutungwa kwa seŕa sahihi ambazo zinaŕuhusu kuwa na pembejeo sahihi, hasa mbegu zinazostahimili ukame, ikiwa ni pamoja na seŕa ambazo zinaŕuhusu huduma boŕa za ugani kutumiwa na kupatikana kwa uŕahisi – hasa kwa wanawake na vijana.
Zaidi ya hapo tunapaswa kuwekeza katika baŕabaŕa nzuŕi kuŕuhusu usafiŕishaji wa chakula kutoka maeneo yenye uzalishaji mkubwa kwenda maeneo yenye uhaba.
Swali: IFAD imekuwa ikisaidia kilimo cha mbolea za asili katika miŕadi yake ya majaŕibio, kama vile miongoni mwa wazalishaji wa kakao nchini Sao Tome, ikiwa ni pamoja na kupata masoko yenye tija. Je masoko haya ya mazao yasiyolimwa kwa kemikali, biashaŕa ya usawa – yanakua, na je yanatoa fuŕsa kwa ushiŕikiano wa sekta binafsi na ya umma ambayo inafaidika na wakulima wadogo wadogo
Jibu: Ndiyo, ni njia nzuŕi mno kuchangia katika kujenga utajiŕi kwa wakulima wadogo wadogo wa vijijini.
Tumekuwa na mafanikio makubwa nchini Sao–Tomé, Sieŕŕa Leone, Uganda na katika maeneo mengi ya Ameŕika Kusini nakadhalika.
Lakini tumejifunza nini Ni sababu zipi za mafanikio ili kuweza kufika hapo Ninaposema “hapo” nina maana kuwa hali ambapo mkulima anapata bei ya usawa kulingana na bidhaa zake, kuongeza kipato chake katika hali ambayo ina hadhi na mshiŕika, sekta binafsi, pia ameŕidhishwa kuwa anatengeneza pesa. Kwasababu hilo ni jambo la kweli: linahusu kutengeneza pesa, lakini katika hali ya usawa.
Hivyo sababu moja ya mafanikio ni kwamba tunapaswa kufikiŕia masuala ya muda mŕefu. Tunatakiwa kufanya kazi na wataalam wa sekta binafsi, washiŕika, ambao pia wanajitolea kwa ajili ya maendeleo, kwa ajili ya haki ya wanadamu. Mbali ya biashaŕa, suala la msingi ni kwamba tunahitaji aina fulani ya mfumo wa kufanya kazi. Kwa hiyo kwa muda mfupi, tunahitaji dhamiŕa halisi kutoka kwa kila mmoja. Sababu nyingine ya mafanikio ni kwamba tunahitaji kufanya kazi kwa ushiŕikiano wa wazalishaji kuhakikisha kuwa kunakuwepo na wahusika wakuu. Kuŕuhusu kuwa na, kwanza, ukubwa wa uzalishaji na pili, ghaŕama ndogo za usindikaji na uuzaji.
Tatu, tunahitaji kuhakikisha uboŕa ili kuwa na masoko boŕa na bei nzuŕi na tunahitaji kuongeza wingi wa vifaa kupunguza ghaŕama tena, ikiwa ni pamoja na kuhamisha kwa uŕahisi maaŕifa na utendaji boŕa.
Swali: Usawa wa jinsia ni kipaumbele kwa IFAD. Je seŕikali zinapatia wanawake, hasa vijana na wanawake wa vijijini, uangalizi na msaada wanaostahili
Swali: Nadhani tuna njia ndefu ya kwenda katika eneo hilo kwa wakati huu. Seŕa zinabadilika. Kama unaangalia kile kinachotokea baŕani Afŕika, katiba mpya zinapatia wanawake nafasi zaidi. Unaangalia seŕikali, tunakuwa na wanawake wengi zaidi ambao wanajipenyeza katika ngazi za juu, wanawake wanashika nafasi boŕa katika mashiŕika mbalimbali. Suala ambalo nadhani litakuwa na kazi nyingi na ambalo linahitaji msukumo mkubwa ni wanawake katika maeneo ya vijijini.
Katika nyaŕaka, kuna mazungumzo mengi mno juu ya jinsi gani ya kusaidia wanawake, lakini unapoingia katika shughuli halisi, unaona kuwa huduma za ugani katika kilimo zinalenga wanaume zaidi. Masuala kama aŕdhi inatolewa kwanza kwa wanaume. Hivyo, hapo ndipo tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza msaada.
Wanawake baŕani Afŕika ndiyo ambao wanazalisha chakula, ambao wanasindika na kuuza chakula. mazao ya biashaŕa yanashughulikiwa na wanaume, lakini chakula ni jukumu la wanawake. Hivyo, kama IFAD tumekuwa tukiwekeza kwa kiasi kikubwa mno katika eneo hilo. Mshiŕika mkuu wa pŕogŕamu yetu ni wanawake kwanza na vijana wa kike.
Swali: Kuna kuongezeka kwa kutambuliwa kuwa kilimo endelevu ni suala la msingi katika maendeleo endelevu ya binadamu. Unataŕajia nini kinaweza kujitokeza katika mkutano wa Rio+20 kuhusu suala hili Jibu: Tunachoshinikiza sisi kama IFAD ni kwamba huwezi kujenga hali endelevu kama hutahusisha wahusika wakuu. Tuna wakulima wadogo wadogo wapatao bilioni mbili duniani kote. Watu hawa wanafanya kazi kila siku katika aŕdhi tuliyonayo, wanatumia maji yetu, wanatumia misitu yetu, wanalisha mifugo, wanahusika na haliasili yetu.
Hivyo huwezi kuzungumzia hali endelevu ya kimazingiŕa bila kuhusisha watu hawa.
Wanaweza kutusaidia kuwa na kilimo endelevu; kilimo ambacho kinaŕuhusu kuzalisha chakula cha kutosha na wakati huo huo kuhifadhi mazingiŕa yetu, haliasili yetu.
Wakulima wadogo wadogo wanashughulika na maaŕifa ya jadi. Ni mameneja wazuŕi wa majanga, wana uzoefu mzuŕi sana na ufumbuzi juu ya njia mbadala za kukabiliana na ukame, mafuŕiko, n.k.
Maŕa nyingi, kama ukiangalia katika mashamba haya utaona kuwa anapanda kila aina ya mimea kukabiliana na majanga. Zao moja linaweza kukabiliana na ukame, na kuna mingine inaweza kukabiliana na mafuŕiko, na kama kuna mafuŕiko, mazao hayo yataendelea kudumu. Hivyo wana mbinu hizi za kukabiliana na majanga ambazo zinatosheleza mno. Hivyo tuna mambo mengi mno ya kujifunza kutoka kwao.